Jina gani hutaki kulisikia linalokuumiza kimapenzi?

Hahahahahah, dah nasikitika kukwambia hao wanafunzi ishirini wana michezo mibaya sana ama watakuja kuwa wanoma
So far sijaona baya kwao, maybe mpaka pale mtakapowavuruga nao wakaamua kuvaa roho ya kuwatesa.

Kama ambavyo mnadai mmekuwa katili kwa wanawake kwasababu tu mlitendwa na wanawake wengine basi ukute nae alikuwa katili kwako kwasababu alitendwa na mwanaume mwingine.
Tujifunze kusamehe na kulet go ili tuwe na mahusiano healthy, lasivyo tutaendelea kulaumiana hivi hivi na kamwe hatutofikia muafaka.
 
Hao akina Mary dont try aisee, mama angu ana miaka 60 siku nkawa natania Tu, nipo mama mchumba wangu anaitwa Mary, hapo hapo akasema mmh akina mary ni wajinga Na wahuni mno lkn sikubisha ila nikaumia sana, kwa nini? Kwa sababu mama yangu ni mwalim af walimu ni mafundi Wa saikolojia!!! Yan baada ya wiki mbili tu nilipigwa kibuti... Nakumbuka sana maneno ya mama yangu kwa yule boya!!!
 
Mkwe unafundisha nursery nini, maana kama ni primary hao la 6 tu wanaanza kazi
 
Take it mkuu,mwanaume hatulii mpaka atulizwe,mwanamke hatulizwi mpaka atulie. Wanaume sisi si chochote kwa wanawake na asilimia kubwa sisi ndio tunaachwa kuacha hatujui.
 
Uzi huu unafurahisha sana,yaani kila mtu anatoa povu tu hapa kwa X wake!Inanikumbusha kwa wenzetu Nchi ya Malkia yaani unakuta wametenga eneo kwaajili ya kutoa hasira kama umekasirika sana,yaani unakuta ni mwendo wa kuvunja Tv,Makabati na vyombo mbalimbali ili kupunguza hasira(Anger free zone).
Hongera JF kwa hili!
 
Mkwe unafundisha nursery nini, maana kama ni primary hao la 6 tu wanaanza kazi
Nafundisha sekondari, na kama wameanza si nyie ndio mmewaanzishia. Mnawatenda weeeh alafu wakija kuwatenda mnalalamika!!

Tangu nitambue kuwa mimi ni binadamu na sijakamilika hivyo vile ambavyo ninawadisapoint watu ndivyo hivyo hivyo nitegemee dissapointment kutoka kwa wengine naishi maisha fresh tu.
Sitegemei kuhold grudge against anybody. Nakupuuza maisha yanaendelea.
 
Take it mkuu,mwanaume hatulii mpaka atulizwe,mwanamke hatulizwi mpaka atulie. Wanaume sisi si chochote kwa wanawake na asilimia kubwa sisi ndio tunaachwa kuacha hatujui.
Haya, subiri utatulizwa.
 
Nilikuwa najiandaa nikutaje na povu la hatari ila kwakua umeomba msamaha nimetulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…