Jina la mwanangu limezua vita ya kifamilia

Jina la mwanangu limezua vita ya kifamilia

Mimi wa kwangu alikaa wiki bila kupewa jina hadi nilipoambiwa na mama yake kuwa tunasubiria jina la mtoto nikalitamka likawa hilo hadi kesho. The same kwa mtoto wa kike same same nashangaa huyo mwanamke wako anachogombania nini basi kuna siri nzito usipuuze hakuna kitu mwanamke anachobishania kwenye mahusiano kisichokuwa na sababu za nyuma kwake.
Joseph
 
Anayeacha kodi ya meza ni Nani?, anayelipia bills mbalimbali ni Nani?, Mwenye mkia wa mbele hapo ni Nani kwani?, Anayehakikisha ulinzi na ustawi wa familia ni Nani kwani?

Kama jibu ni wewe basi una haki ya kubariki jina la mwanao kwa maana ya kulitoa Kama utapenda ww Kama baba , majina pia yana maana kiroho...mama mkwe tayari ashamaliza kazi yake ya kutoa majina ya watt wake.
 
Kiukweli majina yana maana kubwa sana. Ila haya mambo next time kwa ushauri simple tu mkuu..discuss kwanza kwamba baby akija tumpe jina gani na yawe na option za gender zote mbili....ili kuepusha migogoro ya kishubwada kama hii.

Umoja huleta utajiri..msiposhikana kama familia kisa mere things kama hizi mtafeli mapemaaaa... Wengine sisi wazazi wameshatuambiaga mapemaa tusiwape wajukuu majina yao hata kama wametuzaa na kutulea sisi. Sisi kuwa na amani katika ndoa tumewapenda na kuwaheshimu inatosha.

Tutafute majina ambayo mbingu imeyaleta kama tuitwavyo na Bwana Mungu wetu.
NB: Unaweza kumuuliza Roho Mtakatifu na akakupa jina. Ni wewe tu kuamini.

#kamaunakataapitahivi#
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 dah kuna watu wana shida nyingi sana. Hata jina la mtoto mgogoro? Nilishawahi kusema mimi ukisikia nina mgogoro na mtu au polisi ujue chanzo ni pesa tu sio ujinga mwingine
Je mwanamke akiforce jina?
 
Wakuu nipo njia panda ya kuchagua upande. Haya mambo yasikie tu kwa wengine.

Wakati anazaliwa mwanangu huyu mama yake mzazi mwenzangu ndio alisimamia jambo hili ukizingatia kuwa hiyo ndio ilikua taaluma yake.

Sasa jamaa alipozaliwa tu huyu mama akampa jina dogo tuseme jina Y maana ndio alikua mtu wa kwanza kumbeba na kumhudumia wakati mama wa mtoto bado akiwa katika usingizi.

Sasa baada ya hapo tukakaa na Mzazi mwenzangu kujadili official name ya dogo. Tukakubaliana Jina X . hili likashika kasi na likakubalika kwetu.

Sasa tunataka kupata cheti cha kuzaliwa . Tangazo la Kuzaliwa linamtambua dogo kwa jina Y ila ipo option ya kubadili.

Sasa upande wangu wakagundua kuwa kuna jina jingine la dogo analotambulika ambalo lipo katika tangazo la kuzaliwa.

Binafsi mimi sina matatizo na jina lolote so long as huyu dogo anabeba DNA yangu either mimi ndio nimempa au mtu mwingine yeyote.

Historically hata mimi mzee wangu hakunipa jina langu familia nzima walipewa karatasi kura nyingi zikaangukia jina langu. So nimepata jina kwa kura.

Ila sasa naona watu wanaanza kununiana tu nani mwenye haki ya kuchagua jina na jina lipi litumike.

Nilichoamua ni kuwa majina x na y yote yaandikwe kwenye cheti. Yaani aitwe YX ...... I hope kila upande utaridhika na vita itakwisha.
Mambo mengine mnayataka wenyewe , mtoto wako unataka kumshirikisha kila mtu ! kuzaliwa siyo kama msiba , watoto wako ni wa kwako tu , labda kama mna mila za kishirikina .

Quran inasema hivi , " WAPENI WATOTO WENU MAJINA MAZURI MYAPENDAYO NYINYI " Wala hawakusema subiri mama mkwe ampe jina .
 
Mambo mengine mnayataka wenyewe , mtoto wako unataka kumshirikisha kila mtu ! kuzaliwa siyo kama msiba , watoto wako ni wa kwako tu , labda kama mna mila za kishirikina .

Quran inasema hivi , " WAPENI WATOTO WENU MAJINA MAZURI MYAPENDAYO NYINYI " Wala hawakusema subiri mama mkwe ampe jina .
😀😀😀wanaume wa siku hizi. Yaani mtoto wako watu wengine ndio wajadili jina la mwanao.

Erythrocyte sasa uelewe hawa watani zetu aina ya maisha na akili walizo nazo🤣🤣🤣
Ni aina ya irresponsible fathers ambao ni KKBs
 
Huku kwetu mwenye jukumu la kutoa jina ni baba wa mtoto peke yake, hao wengine ni washauri tu, ila jina huwa tunatoa sisi baba.

Hata mabibi au mababu huwa wanatulia na unapigiwa simu baba mwenye mtoto kama uko mbali au vipi, utoe jina huko huko.

Sisi wengine huwa tuna majina yetu tayari, na wake zetu huwa wanajua kama tukijaliwa mtoto wa kike au wa kiume ataitwa fulani.
mwita,chacha,robi,wankulu,koku,,,katunzi,ruta,,,,yaani safi sana.
 
Data
X= ?
Y=!
If the NAME =XY
Find the values of ? and ! if the NAME is YX ?
 
Kuna sababu ya baba kuwa ndio muhusika mkuu wa kutoa jina. Unaweza kuta huyo bibi katoa jina la mchepuko wake au njemba aliyemkata utepe.

Anataka kuenzi ujana wake kupitia watoto wa wenzie.

Hata mke wangu hana haki ya kutoa jina. Yeye ni mshauri tu.
 
Back
Top Bottom