Stroke ukishakua mzazi kuna mambo yanakuhusu wewe kama mzazi na sio ya bibi babu au nani....
Jina la mtu ni kitu kikubwa sana kwenye maisha yake.
Jina linabeba roho ya baraka, laana, mafanikio, mizimu..... kutokana na ni nani alimpa mtu hilo jina na alikua na maana au nia gani wakati anampa jina Hilo.
Kumbuka baraka sio Mali au pesa ila ni Maneno
Na laana au uchawi pia ni maneno
Sijui imani yako lakini toka maandiko matakatifu ya biblia kuna watu Mungu alishindwa kuwabariki kabla ya kuwabadili majina yao. Sababu ni kwamba yale majina yalikua yamebeba roho zilizozuia baraka zao either kwa maagano yaliyonenwa au kufanywa wakati wanapewa hayo majina au laana na hatia walizorithi kupitia hayo majina
MWANZO 17
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
15 Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.
16 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.
MWANZO 32
24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.
Hadi mtu alete vita sababu ya jina la mtoto wako lazima ujiulize anapata faida gani kwa hicho anachopigania
Ongeza neno
Jasmoni Tegga