Jina la mwanangu limezua vita ya kifamilia

Asha Rose
 

Stroke ukishakua mzazi kuna mambo yanakuhusu wewe kama mzazi na sio ya bibi babu au nani....

Jina la mtu ni kitu kikubwa sana kwenye maisha yake.
Jina linabeba roho ya baraka, laana, mafanikio, mizimu..... kutokana na ni nani alimpa mtu hilo jina na alikua na maana au nia gani wakati anampa jina Hilo.

Kumbuka baraka sio Mali au pesa ila ni Maneno
Na laana au uchawi pia ni maneno

Sijui imani yako lakini toka maandiko matakatifu ya biblia kuna watu Mungu alishindwa kuwabariki kabla ya kuwabadili majina yao. Sababu ni kwamba yale majina yalikua yamebeba roho zilizozuia baraka zao either kwa maagano yaliyonenwa au kufanywa wakati wanapewa hayo majina au laana na hatia walizorithi kupitia hayo majina

MWANZO 17
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,

5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.​

15 Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.​

16 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.​



MWANZO 32
24 Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo.

28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.​

29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.

Hadi mtu alete vita sababu ya jina la mtoto wako lazima ujiulize anapata faida gani kwa hicho anachopigania

Ongeza neno Jasmoni Tegga
 
Hii kitu ilishawahi kutokea kwangu ,,Mama mkwe akaleta ubabe kumpachika mwanangu jina ...tukajadili na wife nikaona ngoja niendelee na utafutaji was hela tu.
 
Mimi nasoma hapa taratibu na kujifunza haya madini yako, mama D

Fantastic!
 
Ilinikuta hii, mwanang kazaliwa mwezi wa Ramadhan, Baba mkwe anaitwa ramadhan pia ni wife kajifungulia nyumban kwake! Wajukuu zake kibao jina Ramadhan! Akasema na mwanangu apewe jina lake! Nilipiga simu Moja tu kwa wife Kua mwanangu aitwe jina Fulani! Na mjadala nimeufunga kwenye Hili. Mwanamme hapangiwi jina ila anependekezewa jina.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mimi jina langu nilipewa na babu mdogo.akajipa jina lake bahati nzuri.
Na babu mzaa baba naye anaitwa jina Hilo hilo la babu mdogo upande wa mama vinginevyo ningekuwa na majina mawili.
Najua babu mdogo asingekubali jina lake lipingwe na baba asingekubali jina la baba yake lipingwe
 
Uliangalia kwa juu juu NI vitu vidogo.
Ila majina kwa watoto.ni muhimu Sana.
Majina yanarithisha na tabia ya mwenye jina.
huyo niliyepewa jina lake ni kichaa Kama Mimi Tena ndugu zangu wanasema nimemzidi
Kazi sana mnahangaika na vitu vidogodogo!
 
Fanya mnada Washindane kumsomesha, atakayekubali kumsomesha kwa kulipia ada stage ya mbali ashinde jina.

Mfano: Atakayesaini kuwa atamsomesha hadi form 4 huku wengine wakiishia darasa la saba basi wa drs la saba anachagua jina.
 
We ni kiazi tena sio cha chips kiazi kitamu unachukulia vtu rahisi rahis unazan ndo dunia iko ivyo acha kufanya vtu kirahisi rahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…