Naamini nyaraka za Abdul na wengine hazikuwa na hata chembe ya UDINI ndani yake. Abdul ameishi na TANU kwa zaidi ya miaka 14( 1954-1968). Hakuandika kitabu wala makala kwenye gazeti pamoja na wewe kumpamba sana kwamba alikuwa na akili nyingi, mtaalamu wa lugha, mwandishi wa hotuba za Mwalimu,..., kwa nini wewe uliamua kuingiza UISLAM kwenye hii historia yako?
WildCard,
Hakika wewe huwezi kutoka hapo ulipo.
Nami sitachoka kukumbusha kuwa mimi sijaandika "udini."
Nimekueleza kuwa maandiko yangu yako chini ya Islam/Politics/History.
Library of Congress hii ndiyo ''classification'' yake.
Hili la kwanza.
La pili mimi sijampamba
Abdul Sykes.
Abdul Sykes kajipamba mwenyewe.
Abdul Sykes kapambwa na Waingereza.
Hebu soma nini Special Branch iliandika kuhusu
Abdul Sykes:
"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":
"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid
Sykes has dispatched letters to all branches asking members for
suggestions under the following heads for a memorandum to be
prepared for the Royal Commission..."
"...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association
who, as reported in last month's summary (paragraph 20) was going
on safari up country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani,
President of the Bukoba African Association, and accompanied him to
Bukoba. Sykes then visited Kampala alone.....on 8[SUP]th[/SUP] March, a secret
meeting was held, attended by leading members of the Mwanza Branch..."
(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada
ya kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa
mtafiti yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.)
Mwaka wa 1942
Abdul Sykes alikuwa anaingia Makerere lakini Waingereza
wakampeleka Burma Vita Vya Pili Vya Dunia.
1953 akapata nafasi ya kuingia Princeton University.
La tatu.
Sijapata popote kusema kuwa
Abdul Sykes alipata kumwandikia
hotuba
Nyerere.
Ukiwa una ushahidi tafadhali ulete hapa wote washuhudie.
Usipoleta nitakuita muongo.
Labda lililobaki kwa nini kitabu changu nimekiita "The Life and
Times of
Abdulwahid Sykes 1924 - 1968 The Untold Story of
the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika?"
Jibu ni kuwa wote walioandika historia ya uhuru wa Tanganyika
wazee wangu waliwekwa nje.
Waliwekwa nje kwa hofu ya mchango wa Waislam katika historia
ya Tanganyika.
Hii ndiyo sababu ya mimi kutoka jina hilo hapo juu kumaliza ubishi.