Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

Nishaelewa sasa kumbe bwana Mohamed Said yupo upande wa kuwawakilisha waislamu wenzanke katika kushiriki kupigania uhuru wa tanzania!!! Sio vibaya ila husiishi kwa uchochezi na kumuhusisha Nyerere juu ya udini

Jilala Gabriely,
Sikulaumu huenda huijiu historia ya Tanganyika.

Msome: Bergen (1981), Sivalon (1992), Njozi (2000) na Ghassany (2010).
Utapata mshtuko.
 
Labda kweli sijaelewa ila kwa jinsi unavyojibu watu waswali yao ndipo nilipokugundua ivyo lakini kama sivyo basi
 
Maandiko yako hasa kwa Mwalimu ni chuki ya ajabu. Umemzulia mengi Mzanaki wa watu kwa kuwa tu alimtia ndani mzee wako kwa udini wake.
Kule Kenya na Uganda EAMWS haikuwako? Nasikia makao yake makuu yalikuwa Mombasa. Iliondokaje kule? Hauwezi kuirudisha sasa?

WildCard,
Niletee hapa JF hicho unachosema nimemzulia Nyerere kila mtu
akione.

Babu yangu Salum Abdallah hakuwekwa kizuizini na Nyerere kwa
ajili ya Uislam.

Yeye na Nyerere ugomvi wao ulikuwa mwingine kabisa na ulihusisha
harakati nyingine kabisa.

Kuwa muungwana, njoo na adabu na uliza kama binadamu
nitakueleza kisa hicho na ukumbi mzima utasisimka.

Kisa hiki cha babu yangu na Nyerere ni kisa muhimu sana katika
historia ya Tanganyika.

Usidhani mimi nimekuja hapa nabwabwanya.

Ninapokuambia wazee wetu wamemtoa Mwingereza Tanganyika
sifanyi utani.

Nikikwambia Abdul Sykes ndiye aliyeasisi TANU usidhani nafanya
mzaha.

Nayajua ambayo wewe huwezi kuyajua.

Wazee wangu walikuwapo na wakashiriki katika kuupigania huu
uhuru wetu.

Ndiyo maana unaona hadi leo hakuna hata professor mmoja wa
Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kathubutu kukigusa kitabu
changu si kwa "review" au hata kusema kuwa wamekisoma.

Jiulize ni kipi kimewafunga mdomo?

Wanagwaya, wanajiuliza imekuwaje sisi hatukuyajua aliyokujanayo
Mohamed Said?

Siwalaumu.

Wao hawakuwapo walikuwa kwao huko bara na vijijini.
Mimi nilikuwa Mtaa wa Kipata, Dar es Salaam.

Hatuwezi kuwa sawa.

Ndiyo maana katika kuadhimisha uhuru wa Tanganyika miaka 50
Abdul na Ally Sykes wakapewa medali - baada ya miaka 50 ya
kupuuzwa na kufutwa katika historia ya TANU.

Jiulize nini kiliwafanya waliotoa medali watoe baada ya nusu karne
kupita?

Hayo ya EAMWS unauliza kejeli nakunyamazia.
 
nimeisoma historia hiyo vizur lakn sioni huo utabiri wa jinamizi la udin zaidi ya kuona udini ulivyotaka pewa nguvu na huyo sheikh Suleiman...***
 
Labda kweli sijaelewa ila kwa jinsi unavyojibu watu waswali yao ndipo nilipokugundua ivyo lakini kama sivyo basi

Jilala Gabriel,
Nenda kasoma hizo rejea utajua mengi.

Kitabu cha Njozi serikali ilikipiga marufuku.
Kitabu cha Bergen kimya kimya hakiagizwi tena.

Kitabu cha Sivalon wachapaji wameacha kuchapa lakini
hakijapungua mitaani kipo siku zote toka 1992.
 
nimeisoma historia hiyo vizur lakn sioni huo utabiri wa jinamizi la udin zaidi ya kuona udini ulivyotaka pewa nguvu na huyo sheikh Suleiman...***

Bilulu,
Jitulize usisome hasira zimekupanda kweli mengi yatakupita
utasema hapa jamvini "huoni utabiri."

Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ulikuwa kama hivi:
Kwanza alimtabiria Nyerere kuwa ni "Mtume wa Afrika," aliyeletwa
na Mungu kuwakomboa Waafrika.

Hili lilikamilika Nyerere alikuja akawa mstari wa mbele kuikomboa
Afrika kutoka kweye ukoloni.

Sheikh Takadir alitabiri kuwa mwisho wa Nyerere na Waislam
hautakuwa mzuri.

Utabiri huu nao vilevile ukakamilika mara tu baada ya uhuru.
Ninazo hotuba nyingi za Sheikh Takadir alizokuwa akitoa katika
kumsifia Nyerere kati ya mwaka 1954 - 1958.

In Sha Allah iko siku nitaziweka hapa tuzijadili.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya kuvutia sana.

Mtu huchoki kuiisikiliza.
 
Sheikh Takadir alitaka Tanganyika iwe Jamhuri ya kiislam halikuwezekana ndio sababu mnapiga makelele.

Bilulu,
Jitulize usisome hasira zimekupanda kweli mengi yatakupita
utasema hapa jamvini "huoni utabiri."

Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ulikuwa kama hivi:
Kwanza alimtabiria Nyerere kuwa ni "Mtume wa Afrika," aliyeletwa
na Mungu kuwakomboa Waafrika.

Hili lilikamilika Nyerere alikuja akawa mstari wa mbele kuikomboa
Afrika kutoka kweye ukoloni.

Sheikh Takadir alitabiri kuwa mwisho wa Nyerere na Waislam
hautakuwa mzuri.

Utabiri huu nao vilevile ukakamilika mara tu baada ya uhuru.
Ninazo hotuba nyingi za Sheikh Takadir alizokuwa akitoa katika
kumsifia Nyerere kati ya mwaka 1954 - 1958.

In Sha Allah iko siku nitaziweka hapa tuzijadili.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya kuvutia sana.

Mtu huchoki kuiisikiliza.
 
Ngongo,
Haikuwa hivyo.

Tatizo lilikuwa kwenye fursa na kugawana madaraka.

Haya nimeyaeleza kwa kina katika kitabu changu.
 
If you did not use them during the colonial times The Scramble for Africa hey days and you did not use them 50 years ago you will never use them again you will continue to pass the relay to you children and grand children generation by generation because your masters in reality never set you free.
For your clue just Search in Facebook for "Bring Back The Empire" teh teh teh.
https://m.facebook.com/profile.php?id=234069788705

I don see any reason for visiting Fb as long as I hv got ua point,its like this we are not the only race suffered by colonialism...if ua an Asian surely u or ua fathers hv tasted also from British.....

Again,what z important ryt now z not to condemn our fore fathers for failing to use their common sense in eradicating colonialism coz am very sure u know all the reasons for their failure though they had an intention...The best we can do now is to unite ourselves n fighting our weaknesses,eradicating high level of poverty we are experiencing,corruption n so to many other setbaks,fortunately b'se we are now in a cool environments.

This is what actually raised the economy n life standards to the most Americans n Asians....Lets don dwell to the poor n painful past that can't help us in the current problems we are experiencing....

Thanks,
 
Sheikh Takadir alitaka Tanganyika iwe Jamhuri ya kiislam halikuwezekana ndio sababu mnapiga makelele.

Ngongo,
Huwa sipendi mimi kutumia baadhi ya maneno.

Kwa nini huandiki kwa kulijua lile uliandikalo?

Unajua mimi unaponijia hivi naona tabu kukuweka katika list Waamerika
wanaita "shit list."

Yaani list ya watu wapuuzi.

Wewe hupendi uwe mtu akiona post yako awe anaikimbilia kuisoma
kwa kuwa atanufaika?

Si lazima uchangie.
Kama huna elimu kaa pembeni uwe msomaji.

Wako wengi hapa hawatii neno wao wanasoma na kujifunza.
Sasa wewe unataka uwe mwanafunzi wangu siku zote niwe nakusomesha?

Nimewasomesha Kivukoni sasa unataka na wewe usomeshwe?

Hujui si uliza utaambiwa?

Mwaka wa 1958 hakukuwa na fikra ya Jamuhuri ya Kiislam ulikuwa wakati wa
"Ahlan Tabu."

Hii ilikuwa kauli mbiu ya Bantu Group kupinga hisia za Uislam kushika hatamu
ndani ya TANU ili Wakristo wasijihisi wageni katika chama.

Waiokuwa wakiendesha hiyo kampeni ni hao Bantu Group chini ya Yusuf Bakis.
Huyu alikuwa Muislam.

Yako mengi.

Ngongo,
Hebu angalia hiyo picha kwa makini sana kisha tafakari nini unakiona hapo:

scan0026.jpg


Hao waliomzunguka Nyerere wanaonekana ni dini gani.
Angalia mavazi yao.

Hii ilikuwa 1955.

Wakati ule hao walikuwa hawachukui amri kutoka kwa Nyerere.
Walikuwa wanachukua amri kutoka kwa Sheikh Takadir.

Jaza mwenyewe hawa vijana nani akiwalipa posho.
Tumia akili yao na njoo na jibu.
 
Sheikh Takadir alitaka Tanganyika iwe Jamhuri ya kiislam halikuwezekana ndio sababu mnapiga makelele.
Dr. Ngongo.

NYEBIBIrecruitingVoters1957.jpg

Kushoto kwa Nyerere ni Sheikh Takadir, soma hapa chini nakupa kisa kiduchu kuhusu Takadir na Nyerere.


[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Sheikh Suleiman Takadir alihofia kwamba mara watakaposhika madaraka hawa Wakristo walioelimishwa misheni wataendeleza sera zile zile za wakati wa ukoloni wakiwa wameegama kupokea amri za makadinali na mababa askofu wakiwa hawana lengo la kuiletea maendeleo nchi wala kuinua hali za Wananchi waliowengi hususan Waislamu.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Sheikh Takadir alikuwa kiongozi wa kwanza wa TANU kuonyesha hatari hii katika Tanganyika na hatimaye Tanzania huru.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Sheikh Haidar Mwinyimvua rafiki mkubwa wa Sheikh Suleiman Takadir, mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU na mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU katika mwaka 1958, anakumbuka jinsi Sheikh Takadir alivyosimama ghafla na kuanza kuweka wazi tuhuma zake dhidi ya Nyerere na wenzake:[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Ilikuwa katika ofisi ya zamani ya TANU tulipokuwa tukisubiri kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Ghafla tu Sheikh Takadir alisimama wima akishikilia bakora yake ya kutembelea na kumuelekezea Nyerere huku akisema, "Huyu mtu katu hatakuja kutujua ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta." Sheikh Takadir alirudia maneno haya mara mbili. Sisi sote katika kile chumba cha mkutano tulishangazwa sana ama kwa maana ya maneno yale. Nilimwona Nyerere akilia. Nyerere alitugeukia sisi na kutuuliza, "Je, Sheikh Suleiman alisema maneno yale kwa niaba yenu ? Tulijibu kwa kwa pamoja hapana na ule mkutano ulivunjika papo hapo."[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Sheikh Takadir alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo waliomjenga Nyerere mpaka akakubalika miongoni mwa Wazee wa kiislamu na alikuwa ameifanyia kampeni TANU kwa nguvu akihutubia mikutano juu ya jukwaa moja na Nyerere. Alikuwa amesaidia kufutilia mbali 'doa' la Ukristo toka kwa Nyerere ili kuwafanya watu mjini Dar es Salaam kuacha kumnasibisha Nyerere na Kanisa Katoliki. Wadhifa wa Sheikh Takadir mwenyewe kama mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU ulikuwa wa heshima kubwa.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Si kwamba wale wote waliokuwemo ndani ya chumba kile hawakuelewa alichodokeza Sheikh Takadir. Walielewa kila neno alilotamka na maana yake hasa kwa uongozi wa TANU.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kile ambacho hawakufahamu, kutambua au kusadiki kilikuwa ule ukweli kwamba Nyerere, kijana wao mpendwa na kiongozi wao iko siku moja atageuka dhidi ya Waislamu. Wakati huo hili lilikuwa wazo lisilokuwa na maana kwao. TANU na mtangulizi wake, African Association, hazikuundwa kwa ajili ya masilahi ya kikundi fulani pamoja na ukweli kwamba Waislamu aghalabu ndio walioanzisha kuundwa kwao (vyama hivyo viwili) na kuchukua majukumu ya utendaji katika uongozi. Sheikh Takadir alikuwa amegusa jambo nyeti. Njia pekee ya kuzuia mgogoro huu mpya kuendelea mbele ilikuwa kwa Nyerere kuthibitisha kwamba wananchi Waislamu watatendewa vizuri na kwamba kutakuwa na haki sawa kwa wote baada ya uhuru kupatikana.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kwa wakati ule, umoja wa watu ulikuwa muhimu kwa ajili ya harakati mbeleni. Hii ikajakuwa ndio hoja Nyerere katika hotuba zake tangu ule mkasa wa Takadir ulioelekea kwenye ule uchaguzi wa kura tatu uliochukiwa.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kwa hiyo HKT-TANU (Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU) iliamua kuunda kamati moja ya upesi upesi bila ya matayarisho ili kwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir katika Mtaa wa Msimbazi kumuuliza kwa nini alimtukana Nyerere.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo walikuwa Idd Faiz, Mwenyekiti wa HKT-TANU (TANU-NEC), Idd Tulio na Jumbe Tambaza. Sheikh Takadir aliiambia kamati hiyo kwamba Nyerere alikuwa akitumia mwavuli wa lile sharti la elimu la uchaguzi wa kura tatu kuwaweka Wakristo wenzake madarakani kwa hoja kwamba wanazo zile sifa za lazima kuchukua majukumu ya serikali. Kisha Sheikh Takadir akarudia tena maneno yale yale aliyomwelezea Nyerere, neno kwa neno, akiongeza kwamba hana majuto yoyote kwa msimamo wake huo. Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Idd Tulio walisimama na kuondoka kimya kimya.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kwa hiyo Sheikh Takadir akafukuzwa toka TANU kwa kuanzisha suala la udini, ambalo lilidhaniwa, lingewagawa watu. Uenyekiti wa Baraza la Wazee ukapelekwa kwa Idd Tulio.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kwa usiku mmoja tu Sheikh Takadir akageuka kuwa mtengwa wa kisiasa. Sheikh Takadir alikuwa dalali na alikuwa akifanya biashara yake hiyo pale nyumbani kwake.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Wakati mmoja pale mnadani kwake palikuwa mahala walipokutana wanachama wa TANU. Walikuwa wakikutana pale kunywa kahawa na kujadili matukio ya kisiasa ya siku zile. Baada ya kufukuzwa kwake toka TANU mahali hapo paliachwa na hakuna aliyekwenda pale.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Sheikh Takadir alipokwenda sokoni Kariakoo kununua chakula, hakuna mfanyabiashara aliyegusa fedha zake au hata kule kumtizama tu. Na aliposalimia watu hakuna aliyemwitikia. Sheikh Takadir alikuwa amefukuzwa katika jamii na TANU na alihisi hasa ule uzito kamili wa kutengwa. Biashara yake ikaanza kuanguka na vivyo hivyo siha yake. Akageuka kuwa mpweke sana na mwenye kufadhaika.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Zimepita zile siku alipokuwa akisoma "surat fat'ha" na kusoma dua kabla ya kumtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam katika mikutano ya awali ya TANU katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Zimepita zile siku wakati Sheikh Takadir akiijenga vyema taswira ya Nyerere akimkweza na kumdadavua kufikia kiwango kisichosemeka.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mara baadaye, Sheikh Takadir alifariki. Lakini kabla ya kufariki aliacha usia. Kikundi cha Waislamu kilikuwa kimekwenda nyumbani kumdhihaki, wakimtukana na kumcheka, wakipiga makelele huku wakiimba kwa sauti kubwa ule wimbo, "Takadir mtaka dini". Kikundi hiki kilimtembelea baada ya kutoka mkutanoni ambako Nyerere alitoa hotuba ya kumshambulia Sheikh Takadir.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Hapa ndipo Sheikh Takadir alipotoa ule usia ambao leo hii ndio kilio cha Waislamu dhidi ya Serikali ya Wakatoliki inayojitokeza kwa sura ya CCM. Mzee Takadiri alitoka nje ya nyumba yake na akawaambia wale Waislamu kwamba, "iko siku mtanikumbuka".[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Gazeti la kila wiki la TANU Mwafrika, chini ya uhariri wa Heri Baghdelleh na Robert Makange, lilichapisha habari za Sheikh Suleiman Takadir katika ukurasa wa kwanza, likitangaza kufukuzwa kwake toka TANU kwa wino mzito, picha yake akiwa amevaa kanzu na kofia akikodoa macho pale gazetini.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Picha ya Sheikh Takadir iliwekwa pale ili wote wauone uso wa "msaliti" aliyetaka kuchelewesha mwenendo wa uhuru kwa kutaka Waislamu wapewe uthibitisho wa mustakabali wao kwa sababu ya mchango wao katika harakati za kudai uhuru."[/SIZE][/FONT]
 
Last edited by a moderator:
Pasco,

Faiza ni mama mtu mzima sana pengine kuliko hata Mzee Mohamed. Kwenye mjadala kama huu huwa anaamua kujilipua tu. Anajua mzee huyu ni MDINI sana na ndio utambulisho wake. Anamsaidia ili apumue kidogo na makombora ya ndani ya JF.
Hapana, usiseme uongo, mimi ni mdogo sana kwa kaka yangu Mohamed Said, nikimuona nnamuamkia.

Halafu hako ka Pasco ndiyo usiseme, katoto kajuzi tu hata kukomaa ki akili hakajakomaa, waliomuingiza mjini na waliomuajiri mwanzoni mimi wananiamkia. Kwangu ni kinyagarakata tu, hakinisumbuwi hata kiduchu.
45 Niliipita zamani sana hiyo, imekuwa ni historia wala si story tena.

Kamuulize bosi wako wa zamani Alioki au Meb Al Haddad wananijuwa fika na wananiamkia wakiniona.

Ukionesha busara japo kiduchu ntakuonesha busara hujawahi kuziona lakini ukija na kubwabwaja na kuhororoja bila mpango ntakupa kavu za uso. Kumbuka hilo.
Shikamoo!, heshima adabu!.

Pasco
 
Sheik Muhammad,This young boy Pasco is a vile being specializing in women harrasment we have a history of him relating his overall view of women and he thinks that he is too a macho man to dhalilisha any woman who opposes his view and he is so vile that his idea on women makes him so disgracefull. Having said that, I don't believe that he ever respected his own mother, and since he does not have a sister and may he doesn't have Mama mudogo or Shangazi too.I recall how he even dared to publish a photo of a famous woman scribe right here in JF.He even dared to boast about having abused his position as a man of press media to get to lure women and does not regret it doing again.Indeed Ms.FF has outwitted many members of The kind of Pasco here in JF and that is what scares him.No wonder Pasco lost his two jobs, his position in his so called 'profession' if real he is a scribe does not give him the right to speak in such manner to Ms. Faiza and to such un-ethical behaviour against women.
Mkuu Punjabi Singi, kama hakuna yoyote humu aliyewahi kukueleza kuwa una matatizo, naomba mimi niwe wa kwanza kukujulisha rasmi kuwa, Mkuu Punjabi Singi una matatizo!.

Maadam ndani ya uzi huu nimeishakubali sasa ni heshima na adabu, sitakuambia matatizo yako humu, ila tukikutana uzi mwingine, labda nitakueleza!.

Pasco
 
heshima adabu!.

Pasco

Mtalaam Pasco mimi nakuheshimu sana lakini naomba jibu swali langu hapo juu au nirudie? Je ni kweli wewe kazi yako ni kudhalilisha wanawake? Nina adabu nyingi kwako lakini kwa ujumla nimeshangazwa sana maana hata mtu anaekujengea ile nyumba yako ya mbezi njia ya massana namfahamu vizuri sana. Na ni jirani yangu huku mtaani kwetu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom