Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir

 
[/QUOTE]

George Jinasa,
Kipi kinachokufanya wewe unitukane kwa kuniita "msomi fake?"
Tujaalie mie si lolote si chochote wala huo "usomi" sina.

Basi ndiyo unitukane kwa ujinga wangu?

Unazungumza amani na upendo...
Isome historia ya wazee wangu utajua wapi tumetoka.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kisha rejea Majlis tufanye mjadala.
Usizungumze somo usilolijua.
 

We jamaa wa Ajabu, badala ya kusema Watanzania unasema Waislam..!?
 
We jamaa wa Ajabu, badala ya kusema Watanzania unasema Waislam..!?
Tamko,
Kuna msemo wa Kiarabu unasema hivi: "Unapoijua sababu ile ajabu huondoka."
Nitashukuru ikiwa utanifahamisha hiyo ajabu.
 
Tamko,
Kuna msemo wa Kiarabu unasema hivi: "Unapoijua sababu ile ajabu huondoka."
Nitashukuru ikiwa utanifahamisha hiyo ajabu.

Mkuu, umejinadi kuwa ni msomi, umetunga VI-tabu lakini umeshindwa kumwelewa hapa?!!!


Kiufupi amepunguza ukali wa maneno.
Ya kwamba MTU anayetaka mapatano na Amani, anaanzaje kusema waislamu badala ya kutamka watanzania ili kujenga ile solidarity. Hii ndio ajabu yenyewe.

Ingependeza zaidi kama angalisema "...unawaKosea watanzania badala ya kusema unawakosea waislamu."
 
2013,
Sijapatapo kujinadi.
Kujinadi hakuwezi kumfanya mtu kuwa msomi.

Usomi huletwa na sifa maalum.
Ikiwa hivyo ndivyo sasa nani hajamuelewa mwenzie?
 
kaka mimi siwezi hata siku moja kukuita msomi fake. Maelezo yangu mimi ni yale ya juu niliyokuwa namjibu Mpinga Shetani katika maelezo yake hapo chini.

George Jinasa,
Kipi kinachokufanya wewe unitukane kwa kuniita "msomi fake?"
Tujaalie mie si lolote si chochote wala huo "usomi" sina.

Basi ndiyo unitukane kwa ujinga wangu?

Unazungumza amani na upendo...
Isome historia ya wazee wangu utajua wapi tumetoka.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kisha rejea Majlis tufanye mjadala.
Usizungumze somo usilolijua.[/QUOTE]
 
Kaka Mohamed hata siku moja siwezi kufungua kinywa change kumtukana mtu yoyote katika ukumbi huu, achilia mbali wewe. Maandiko yangu ni yale yanayoonekana juu nikijibu maandishi ya kaka Adoloy sio Mpingashetani kama nilivyonukuu kimakosa yanayoonekana hapo juu hasa hoja yake kwamba chuki zinatokana na mafunzo ya chuki katika madrasa. Tafadhari tizama vizuri posts zilizotangulia. Toka nijiunge jamii forum sijawahi kumtukana yoyote na nimekuwa nikikemea lugjha za matusi
 
Mdogo wangu George basi tuwiane radhi kukosea ni.sifa yake binadamu.
 
Sasa
2013,
Sijapatapo kujinadi.
Kujinadi hakuwezi kumfanya mtu kuwa msomi.

Usomi huletwa na sifa maalum.
Ikiwa hivyo ndivyo sasa nani hajamuelewa mwenzie?

Mkuu labda hujajinadi kama ninavyotaka kukuelewa Mimi. Lakini jambo moja najua ni kuwa wewe ni msomi.

Kitu cha kuzingatia Mzee wangu.. Ni kuwa elimu yako inathamani sana pale unapotambua tofauti zetu na kuzitumia kutuunganisha. Sio kutugawa. Kwa wewe kuonyesha nani ni bora kuliko mwingine. Haitakubalika kwa gharama yoyote kama utaleta taswira kuwa waislamu ni bora kuliko wasio waislamu kwa hoja za kutafuta Uhuru wa hii nchi. kwenye historia ya uhuru. *Hata kama kuna ukweli.
Japo Nina shuku kuwa hujafanya jitihadi kuja hao watu unaoonyesha walishiriki Uhuru wa nchi hii kwanini walipigwa kihistoria.
Ikiwa waislamu bwana wema wewe ni.msomi na wasio waislamu wakakukataa usomi wako hautakuwa na faida.
Haya yesser Arafat ilimbidi aache ugaidi ili aheshimike kimataifa mpaka kupewa tuzo ya Amani ya Nobel.

Nachotaka kusema itumie elimu yako kujenga solidarity na sio kutugawa watanzania(sio waislamu).
Vitabu vyako viwili vimekula ban nchini, you never know inawezekana ni kutokana na kuwagawa wazalendo wa nchi hii kwa misingi ya dini zao.( I don't know).may be una abuse elimu yako. Au umechots historia ya watu walikuwa na nia ya kuigawa nchi kwa msingi ya udini.

Hitler alithubutu kugawa races, Francis Botha alithubutu lakini haikumsaidia. Haeshimiki kama Mandela.

Ufahamu tu. Wema wa watu hautegemei.dini zao kwa asilimia mia moja.
Watu mashujaa in wale wanaoweza kusamehe na kusahau mabaya waliofanyiwa. Mandela is one of them.

Watu wema wanazaliwa wakiwa wema.
Tunapomsifu Martin Luther Jr kuliko Malcom X hatuangalii dini yake. Hata hivyo malcom aliwahi kukiri kuwa alikuwa mhalifu a
Na akaongeza kuwa uislamu umembadilisha. Anyway....

Tunapomwita nyerere baba wa taifa hatuangalii dini wala kabila Lake.

Tunapomkosoa IDD amin.hatuangalii dini yake, wala taifa lakem hata wewe kukubalika BBC haikuwa kutokana na dini yako.(mawazo yangu lakini)

Mungu sio mkatili. Lasivyo hasingeabudiwa .Watu wakatili sikuzote historia yao hufutika, lakini ukiona mkatili anaheshimiwa utagundua si kwa Uhuru Bali kwa kulazimisha. Naff said mkuu.
 
2013,
Kwanza ningependa kukusahihisha.
Vitabu vyangu viwili havikupigwa ban.

Vitabu hivyo havipendezi.

Kama vile unavyoona mashujaa waliopigania uhuru hawakutajwa
katika historia huwezi kusema wamepigwa ban bali hawapendezi
ndoyo maana wakafutwa katika historia.

Sijapatapo kusema kuwa Waislam ni bora kwa sababu ya mchango
wao katika TANU na kupigania uhuru.

Nilichosema ni kuwa kwa nini mchango wao umefutwa kwa takriban
nusu karne.

Wakujenga solidarity ni yupi.

Ni yule anaekandamizwa na kufutwa kwenye historia au yule mwenye
madaraka akayatumia kumuhujuma dhalili?

Hayo ya ugaidi sijui yana uhusiano gani na uandishi wangu wa historia
ya Tanganyika.

Mengine nimeona sina sababu ya kuyajibu.
Angalia kitabu kilichopigwa "ban" chembilecho.
http://www.mohammedsaid.com/2014/01/the-torch-on-kilimanjajaro-kitabu.html
 
Jembe Pori,
Nifahamishe kama umesoma kitabu changu na kama umemsoma Bergen, Njozi na Sivalon.
 
Mkuu mohamed mimi nilisikiliza kipindi chako radion kuhusu hotuba ya mwl UNO ila nilichojifunza sicho nilichokitarajia maana hakuna cha hotuba yeyote ila niliambulia maneno matupu na story za hapa na pale za yaleyale ya waislam waliosahaulika katika historia ya tanzania....

mi sidhan kama kuna mtu atapinfahilo ila hawa watu waliosahauliwa wapowrngi mno na si rahis kumtaja mmojammoja.....

watu wanamtaja sana nyerere hata kama waislam ndio waliomsaidi sababu waislam waliomsaidia hawakumsaidia sababu ya uislam ama ukristo ila ilisababishwa na uwezo binafsi wa mwalimu nyerere wa kuijua historia na kuielezea vizuri kukiko watanganyika wa kipindi kile......

kila mmoja alishauchoka ukoloni lakin nani alikuwa na uwezo wa kumfunga paka kengele....

ukiachs wasomi kama akina patrick kunambi na wengineo waliokuwa taysri kumyumikia mkoloni, nyerere alikataa kukaa na wasomi wenzake na yeye akaamua kukaa upande wa wanyonge bila kujali dini........

watu wakampenda na kumwamini na mimi naamini hiyo ndiyo ilikuwa sababu..kuhusu historia na picha za washiliki wengine sidhani kams ama nyerere ama watu wengine kuwa walificha kwa makusudi ukweli wote wa washiriki wengine wa kiislqm kwenye harakqti zq uhuru,...

huu ni mfumo wa kawaida tu duniani maana maranyingi kazi kubwa hufanywa na watu wa chini lakini sifa huchukua wakubwa, mfano baba yangu kulasiku analalamika kuwa wslipigana vita uganda lakini waliporud wakaambiwa asante ya mdomo tuu,nimewahi kuangalia documentary ya mtu anayesadikiwa kumuua osama bin laden,bnaye analalsmika hakupewa kitu na serikali............

yan huo ndiyo mmo wa kiutswala duniani na sidhan kama.hao wazee wa TANU kunajipys kwao
nu ishu ya kutafakari tuu na kuelewa.....
 
Ndahani,
Hii ni political history na maandiko yangu yana label hiyo hata
kwenye Library of Congress, Washington.
wewe Mohamed Said huwa unaandika vitu vya msingi watu wavijue lakini tunapopishana mimi nawewe ni kwamba makala zako nyingi ni onesided na ni biased kwanini huwa unaleta majina ya waislam tu katika orodha ya wapigania uhuru inamaana waislam walihusika kuliko watu wengine kuwa balanced bwana .
 
Jembe Pori,
Angalau soma kitabu changu uijue historia ambayo si wengi walikuwa wanaifamu. Ukiijua historia hii utaweza kuchangia vizuri.
 
Pter,
Ukiwa unaona hao Waislam walioko katika historia ya uhuru hawastahili walete hao unadhani wewe kuwa ndiyo wanastahili kuwepo
 
Jembepori,
Ulikuwa ukiyajua kabla hayo uliyoyasikia? Nyerere hakukaa na wanyonge. Alikuwa na Abdul Sykes na mdogo wake Ally. Alikuwa na Dossa Aziz na John Rupia hawa wote watu wenye nafasi zao. Alikuwa na Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate wote hawa walikuwa na uwezo mkubwa. Usizungumze kitu usokijua. Historia hii dunia nzima utaipata kwenye kitabu cha Abdul Sykes. Si Iliffe, Kimambo au Chuo Cha Kivukoni walioandika historia ya TANU wamepita nilipopita mimi. Sasa jiulize imekuwaje hivi?
 
Pter,
Balance utakayo wewe ni ipi?
Kumtoa Idd Faiz katika historia ya TANU?

Au kuficha ukweli kuwa TANU ilikuwa katika fikra ya Abdul Sykes
toka vitani Burma? Au kutotaja kuwa African Association iliundwa
na baba yake?

Balance ni kumfuta Sheikh Hassan bin Amir na Sheikh Suleiman
Takadir?

Vipi mathalan tukaifuta historia hii yangu tukawa na ile ya Chuo Cha
Kivukoni wewe utaridhika?

Unatambua kuwa mkakati wa kuanzisha harakati za kuunda TANU
Abdul alimkusudia kumpa uongozi Chief David Kidaha Makwaia?

Hii ilikuwa 1950/51.

Wewe hupendi kuyajua ninayokunyambulia kutoka mafaili ya wenyewe
waliokuwa katika African Association toka 1929?
 
Kinachofanywa waumie si jambo la kariakoo kuhusu harakati za Uhuru bali ni kwa vile waislam ndio waliokuwa chachu na waanzilishi wa michakato ya kuleta uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…