Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir


Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kwa kisa hiki cha Mzee wako, Sheikh Suleiman Takadir, ila sio kweli kuwa Mzee huyu hatajatwa popote kwenye historia ya Tanu, kwa sababu mimi nimelisikia jina la Sheikh Suleiman Takadir siku nyingi, kabla sijakusoma wewe, hivyo lazima kuna mahali alitajwa hadi mimi kumjua!, na sio kutajwa tuu, nadhani ia kuna namna alienziwa, sikumbuki vizuri, lakini nahisi niliwahi kulisikia jina la Mtaa fulani ukiitwa Takadiri japo sikumbuki vizuri!.

Kama hii ndio ilikuwa sifa kuu ya Sheikh Takadir, "kuongea sana na kupiga 'fatha' kwenye mikutano ya Tanu!, connotation meaning ya para hii ni kuwa Mkiristo Nyerere, alikuwa hawezi kupanda jukwaani kuwahutubia Waislamu wa Tanu, mpaka kwanza Sheikh Takadir atangulie kuwapooza kwa 'fatha'!, jambo ambalo sii kweli!, ili ukweli ni kuwa Maeneo mengi ya Uswahilini, walijaa Waislamu, hivyo hizo 'fatha' ni kikolezo tuu cha kujengea hamasa, kama alivyoakifanya Salum Tambalizeni kwenye mikutano ya CCM, yaani kazi ya uhamasishaji, hivyo inawezekana kwa sasa, usimsikie Tambalizeni ekienziwa popote!, kama ambavyo alivyotoswa Sheikh Takadir!, msingi wa mtu yeyote kuenziwa ni mchango wake kuthaminiwa kwenye jambo fulani!, kama mchanga wake ni uhamasishaji tuu, then alivyothaminiwa hata kwa kutajwa tuu hadi mimi kumfahamu, ni thamani tosha!. Wako wengi walioisaidia sana Tanu, na wengine hadi kufungwa gerezani kuipigania Tanu kama kina Robert Makange na Kheri Bagdelalah lakini sikumbuki kuwasikia ni wapi walienziwa!. Kuna mamia wengine huko mikoani, wamefanya makubwa kwa Tanu, lakini sikupata kuwasikia mfano Dr. Kyaruzi, mimi ndio nimemsikia juzi juzi tuu baada ya kufariki kimya kimya huko kwao Bukoba!. Hivyo kuna wengi waliofanya makubwa kwa Tanu, hawajatajwa, ila wewe unajenga picha kwa Wazee wako tuu kuwa hawajatajwa kwa Uislamu wao!, kitu ambacho sii kweli, na haitakuwa kweli hata siku moja!.[/QUOTE]

Huyu ndiye Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954.Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA.
Huu pia ni urongo, hapa unataka kujenga picha kuwa eti ni Sheikh Takadir ndie aliyemtambulisha Nyerere kwa mara ya kwanza kwa watu wa Dar es Salaam!, sii kweli!, kwenye utambulisho wa Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, naamini unaujua vilivyo!, labda ungesema, Sheikh Takadir pia alipiga ile 'fatha' yake maarufu kwenye mkutano wa kwanza wa kumtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam, ningekukubalia, lakini siye yeye aliyemtambulisha Nyerere kwa watu wa Dar es Salaam!.

Hili pia ni kujazilizia tuu kile Nyerere alichoandikiwa, kama Sheikh Takadir aliyasema haya 1957, alicopy tuu utabiri uliotangulia na kuja kuwa paste hapo kwenye hiyo tafrija ya Taarab, nyota ya Nyerere iliisha anza kung'aa siku nyingi tangu yuko Tabora School, Makerere, Edinburg hadi St. Francis (Pugu) siku nyingi kabla, hivyo utabiri huu wa Sheikh Takadir ilikuwa ni kujazia tuu yaliomo yamo!, usitaka kudanyanga humu eti aliyemtabiria Nyerere ukuu ni Sheikh Takidir!, is just one of them!.

Lakini usuhuba huu ulikuja kuvunjika na watu wawili hawa wakawa mahasimu wakubwa, Sheikh Suleiman kafa hasemi na Nyerere na Nyerere kwa upande wake hakupata hata siku moja kumtaja Sheikh Takadir popote hadi anaingia kaburini.
Huu utakuwa ni urongo mwingine, unless wewe ulikuwa bennet na Mwalimu, 24/7 hadi anaingia kaburini, ndio uweze kulisema hili kwa hakika!.

Hapa sasa ndio the Best of Maalim Mohamed Said!, muogope Mola wako!, huwezi kudaid kuwa Sheikh Takadir alikufa kwa kihoro cha kutoswa!, yaani kisababishi cha kifo chake ni kule kutenwa na jamii!. Uhai umeumbwa, na kifo pia kimeumbwa, Sheikh Takadir alijifia natural death siku yake aliyopangiwa na Mungu ilipowadia!. Kwa msio jua!, Malaika mtoa roho, Israel, anampitia kila mmoja wetu mara sabaini fii sabaa kwa siku, ili kuhakikisha muda wake ukifika asizidishe hata sekunde moja!. Hili ni moja ya bandiko jingine la Maalim Mohemed Said lenye kutoa ilmu adimu, but with "ill motive" behind!, ili ilionekane hata kifo cha Shekh Sulemain Takadir, msababishi ni fulani!.

Pamoja na "the ill motive behind", asante kwa simulizi nzuri,
endelea tuu kuipalilia na kuimwagilia na kuitilia mbolea hii "mbegu", soon itamea vilivyo na tutapata mavuno stahiki muda stahiki ukiwadia, wakati huo huo mimi naendelea kufanya research yangu kwenye urais wa Tanzania, rais akiwa ni Mkristo ni kwanini lazima awe ni Mkatoliki?.
Pasco.
 

nilipoanza kuisoma mwanzo tu nkaelewa serikali inatambaa kwa kutumia mgongo wa waislamu kutimiza malengo yao waislam tunatakiwa kuamka adui sio mkristo
 
Hakuna anayelazimisha huo ndiyo ukweli wa history ya Tanganyika, kwa faida ya JF tufahamishe wewe history ya Tanganyika.

Cc; FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:

Nadana!
Unapokwenda kwa Daktari kwa sababu una maradhi yanayokusumbua anachofanya Daktari Mzuri sio atakutafutia Tiba tu bali atataka kujua Ulipata vipi Huo Ugonjwa au Hayo maradhi.
Na baadabya kujua Chanzo chake ni lzm akupe Ushauri Ili Usije kuugua Tena.

Sasa anachofanya hapa Mzee Mohamed Said Ni Kutuonyesha Sisi watanzania Tusiojua au tunaojifanya hatujui CHANZO CHA Huu ubaguzi wa Udini. Na shukurani nyingi zimuendee mzee Mohamed Said Tumefahamu Mengi mno yaliofichwa na Kukaliwa na Serikali ya huyo Nyerere muasisi wa Mfumo Kristo.

Na kwa taarifa yako ile SRATANI ya Mfumo Kristo aliotuachia bado Inaendelea Kuota Mizizi kila.Kona Ktk Serikali yetu. Na wewe km Una macho Lzm Utakuwa umeshaliona hilo la km huna Basi Wazee wasomi Km Hawa Watakusaidia Kuyaona hayo kupitia Kwenye Macho yao ya Kalamu.

Tushirikiane ktk kutafuta hio Tiba lkn waache wazee km Mohamed Said aendelee kutukumbusha Chanzo cha haya MARADHI ili Sisi kizazi cha sasa tusijerudia makosa aliyo yafanya yule mzee aliekosa Huruma na Imani Mchonga meno wa butiama.
Kafa katuachia balaa huku nyuma.
Mungu amuongeze Adhabu.

Sema amen!
 
Last edited by a moderator:
ninaichukia dini na siasa ni vitu vyepesi ila imara katika kuvunja ama ni..
Tanzania Si nchi salama waislam wanashindana na wakristo na wakristo vivyohivyo..
hatutaishia pazuri.
 
Ghosryder,
Una ushahidi madhubuti kwa tuhuma hizo?

Kama unao ulete hapa.

Haipendezi mtu kuzua maneno kuwatia watu hofu.
 
Demulikuy,
Umekuja na historia ya Kivukoni.

TAA ilichukua mkondo wa siasa 1950 baada ya mapinduzi ya Dk. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes na wakaunda TAA Political Subcommittee.

Kamati hii ndiyo iliyoandika katiba waliyoipendekeza TAA kwa Gavana Twinning.

Nyerere hakuwapo wala hakuna mtu aliyekuwa anamjua.

Habari hii nimeieleza kwa kirefu katika kitabu changu.

Masahihisho haya ya historia ya Tanganyika ndiyo yaliyovutia kitabu changu na kusababisha nipate mialiko mingi ya kuzungumza ndani na nje ya nchi.

Hii si dalili ya mtu aliyefilisika.
 
Pasco,
Mtaa wa Takadiri uko Magomeni ila si kwa ajili ya sheikh.

Ilikuwa mwiko Sheikh Takadir kutajwa...

Kusikika nje ya duara jina likisikika kama vile alivyokuwa
akitajwa Abdul Sykes lakini ndani ya TANU hakuwa akitajwa.

Hivi vitu vikinishangaza sana.
 
Huyo Mzee Takadir alikuwa hafai, badala ya kuuliza Mstakabali wa Watanganyika baada ya Tanganyika huru anauliza mstakabali wa Waislamu? Alikuwa na agenda gani kana kwamba Tanganyika ilikuwa na waislamu pekee. Na huu ni Mfuno Baguzi unaofanywa na Waislamu dhidi ya jamii ya watu wengine wasiyokuwa Waislamu.
 
Pasco,
Sikuzuii kusema ulitakalo.

Mimi nimewaeleza wazee wangu kwa kuwa nawajua.

Sikulazimishi kuniamini.

Sasa Mzee Mbona Maandiko yako hayana hitimisho, tuwafanyie nini hawa waislaam ili kuwalipa fadhira za kupigania uhuru. Tuwafanyie nini ili wao waridhike maana mchango wao ni mkubwa
 
Hata hueleweki. Je ni kwa nini unaleta mada hizi kipindi hiki ambacho watu wanaojinasibisha na uislam wakiwa wanashambulia vituo vya polisi na kutaka kuunda dola ya kiislam, tukuchukulieje? uko upande gani?
Nadhani wewe ndio hutaki kumuelewa! Halafu usichanganye mada, Mzee Mohammed Saidi anaongelea historia, huko unakomoeleka hakuhusiani kabisaa na mada zake.
 
Pasco,
Sikuzuii kusema ulitakalo.

Mimi nimewaeleza wazee wangu kwa kuwa nawajua.

Sikulazimishi kuniamini.

tatizo lako lipo kwenye umimi ktk kuwaelezea wazee wako.. then udini
. Bhaaasi nje ya hapo maandishi yako yangekuwa na maana sana.
 

na Nyerere alikuwa hana masihara na wadini.
 
Tunahitaji hitimisho, sio kutoa history. Tunataka tujue waislaam wanataka nini ili waridhike maana haya malaamiko bila kujua tunafika vip tamati ili wenzetu waridhike maana Tanzania ni ya wote
 
Sasa Mzee Mbona Maandiko yako hayana hitimisho, tuwafanyie nini hawa waislaam ili kuwalipa fadhira za kupigania uhuru. Tuwafanyie nini ili wao waridhike maana mchango wao ni mkubwa

hawa jamaa hawaridhiki hata wakisikilizwa hoja zao nyanya.....ipo siku watasema marufuku kula na kunywa hadharani mwezi wa Ramadhan.....ni rahisi kuishi kwa amani na paganism, hindu, au buddha kuliko watu wa dini hii...
 
Tunaokuomba mzee KINGUNGE Na wewe andika historia ya WAPAGANI Waliopigania UHURU.Tumechoka na HEKAYA HIZI za huyu mzee.
 
Tunajua mna mkakati wa kusilimisha NCHI,Hamtaweza.Tangu huyu mzee apewe AZIMIO LA ABUJA.Kaleta MAJANGA.
 
Tanzania hii, inamchango wa watu wengi katika kuleta uhuru. Wakati ule isingelikuwa rahisi kwa namna yoyote ile wazee wa mji fulani kuleta uhuru wa nchi hii peke yao. Maandiko mengi ya Mzee wetu M. Saidi nimeyasoma. Na hitimisho langu ni kuwa ukiayaangalia kwa jicho la kutokuelemea upande ni kuwa historia inayodaiwa kufichwa haipo, bali kinachoelezwa ni jinsi ya kuwatia hamasa watu wa imani nyingine kujiona kuwa walishiriki kikamilifu, ila sasa wamesahauliwa. Hili si la kweli hata kidogo na halikubaliki.

Tatizo lingine la historia nayoidai mwandishi ni historia ya kuvizia. Akishafariki mtu, basi ndipo maandiko yake huibuka. Kwa kuwa marehemu hana lake hivyo basi inakuwa ni wakati wake wa kujenga hoja za chuki. Wakiwa hai hana muda wa kuwahoji, ila wakifa huwatia maneno vichwani mwao na midomoni mwao.

Utetezi wake ni kuwa maandishi yake yamechapishwa na vyuo na majarida maarufu. Lakini kuchapishwa kwake sio hoja ya kusema ni sahihi.

Kama kweli Mzee. M. Saidi unaipenda sana nchi yetu, basi usingechagua watu katika historia yako kwa misingi ya dini zao. Mfano unaaandika wazee wa dar wa dini fulani, baadae unaenda mikoa ya magharibi na kanda ya ziwa, kule unaandika wazee wa imani hiyo hiyo, kisha unaenda mikoa ya kaskazini unafanya hivyo.

Kisha unamalizia kwa kumlaumu nyerere. Nia yako ni ipi hasa kama sio chuki.
 
NYERERE Itakuwa alijuta kufanyia HARAKATI Huku,watu wanataka Fadhila wawe kundi special kuliko wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…