Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #161
historia ya tz imesahau wengi tu sio waislam peke yao,mbona hao wakristo hujawaongelea nfano oscar kambona aliyeacha chuo uingereza kwajili ya TANU,mtu aliyetuliza machafuko 1962 ambapo nyrere na mkwawa walikimbilia kigambon.mbona hujawah kumuongelea,vip kwakua n mkristo.acha topic za chuki za kidini.tz kuna vitu vingi sana vyakuviandikia ili jamii ijikomboe na sio kidini.af unajikuta mwandishi et vyuo vingi dunian vinakusoma.
Maliedo,
Huna haja ya kuandika kwa ghadhabu,
Ukiandika hivyo unaweza ukanipoteza hata mimi unaetaka kufanya
mjadala nami nikakupuuza.
Kwanza ni kuwa unazungumza jambo usilolijua na hili ni tatizo kubwa.
Kambona hakuacha chuo Uingereza kwa ajili ya TANU.
Soma, tafiti, utajua ukweli kipi kilimfanya akaacha masomo.
Pili hayyo machafuko hayakuwa mwaka wa 1962.
Soma, tafiti, utajua ni mwaka gani yalikuwa machafuko.
Mimi siandiki topiki za dini kama unavyodai.
Nimeshaeleza hili katika post za nyuma tena kwa urefu na ushahidi
wa maktaba kubwa duniani zinazochambua maandiko na maudhui
kisha wakazipanga katika masomo stahiki.
Mwisho nataka nikueleze.
Mimi nilikuwa Mtafiti Msaidizi katika utafiti wa historia ya mapinduzi
Zanzibar nikifanya kazi chini ya mwandishi na mtafiti Dr. Harith
Ghassany ambae kutokana na utafiti ule aliandika kitabu, "Kwaheri
Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).
Katika kitabu kile hayo yote uliyouliza hapa kuhusu Oscar Kambona
yameandikwa na zaidi yake.
Unataka kufanya majadiliano na mimi kuwa na staha na adabu
tutajadiliana na sote tutafaidika.
Mwisho ni kuwa Mkwawa hakuhusika katika mkasa ule.
Tafiti, soma utakuwa mwerevu.
Usikurupuke ukaanza kutupa shutuma huku na huko.
Sasa rudi kwa adabu na niulize kwa uungwana nini unataka kujua
kuhusu Kambona nitakueleza toka alipokuja Makao Makuu ya TANU
1956.