EPISODE 24
“A TRUE STORY BY INSIDER”
“Insider mambo I was very busy ila naomba kuterminate mkataba na wewe mwisho wa mwezi huu.”
Na muda huu nilihisi kuchanganyikiwa mara 2 hata Msomali aliona mabadiliko yangu pale, nilijikuta niko kwenye wakati mgumu sana.”
TUNAENDELEA….
“Bro are you ok?”
“Yes I’M IN let me go.”
Nilijikuta nakubali offa ya Msomali bila hata kufikiria vizuri muda ule, nilikuwa mtu ambaye kama nimechanganyikiwa kwa muda ule.
“Good Bro! ukitoka huko njoo mimi nitakuwa hapa hapa” na alinitajia room No. ili nikitoka huko niende direct.
Baada ya kuachana na Msomali nilitoa gari na nikapark pale nje parking sikutaka kuanza safari muda huo.
Nilimpigia simu Iryn na hakupokea simu zangu kabisa. Nikaamua kuachana naye lakini ule ujumbe hakuwa mzuri kwangu ni kama ulinishtua sana.
Wakati niko pale nje Parking nilitumiwa tena ujumbe mwingine na Iryn,
“Insider nitakulipa Pesa ya mwezi huu hakuna haja ya kuendelea kufanya kazi tena kwa hizi siku zilizobakia, wish you all the best.”
Nilitoka kwenye gari muda huu na nikamuita Masai anisaidie kumwita bodaboda. Sikutaka kupeleka lile bom na gari hivyo niliona bodaboda ni wazo zuri.
Japo nilikuwa bado sijajua exactly mule ndani kuna nini ila nilipatwa na uwoga sana muda huu.
Bodaboda alifika pale na nikamwomba Masai anisaidie kuangalia gari yangu na sisi tukaondoka kuelekea Posta.
Tulifika pale Posta kama taarifa zilizovyokuwa zinaonesha na nikafanikiwa kuiona hiyo nyumba. Cha ajabu baada ya kugonga mtu alitoa mkono getini na nikamkabishi ule Mzigo ni kama alikuwa ananisubiri mimi.
Baada ya kukabidhi Mzigo ule, ndani ya dakika moja nikapata ujumbe kutoka kwa Msomali ukisomeka “Good” na mimi nikaondoka maeneo yale kurudi Seacliff Hotel.
Baada ya kufika maeneo yale nilimlipa bodaboda pesa yake na mimi nikaingia ndani ya gari. Na mudaa huu nilikuwa kwenye mawazo sana ukisikia deep stress bhasi nilikuwa nayo ule usiku. Niliwaza pale niende kwa Msomali au nimkatae muda huu, lakini nilikuwa dilemma maana kuna Roho ilikuwa inaniambia niende nyingine inapingana.
Niliamua kwenda kumsikiliza ana jambo gani maana nilikuwa sijui nifanyaje muda ule. Nilikwenda moja kwa moja mpaka room yake nikagonga mlango na akatoka kunifungulia mlango.
Na tulikwenda kukaa kwa pembeni kidogo ambako kuna kama uwazi ambapo palikuwa na viti na meza.
MSOMALI: “Bro umenifurahisha sana nimeprove uaminifu wako.”
MIMI: “Bro hukunambia exactly kulikuwa na nini mle maana mpaka sasa nina uoga.”
MSOMALI: “Acha uoga Bro, soon utajua.”
MIMI: “Na wewe unajishughulisha na nini?”
MSOMALI: “Mimi na deal na madini yote, ila pia nafanya mishe zingine za pembeni, Bro mimi naangalia Pesa. Tanzania mmebahatika kuwa na nchi ya Amani ila raia zake ni wazembe hawajiongezi acha sisi Wasomali tuwafundishe jinsi ya kupata hela.”
MIMI: “Ni kweli, sasa kuna deal gani unataka kunambia.”
Ukweli ni kwamba Msomali alikuwa anadeal na masuala ya madini ila pia alikuwa akifanya michezo ya hatari sana ambayo inatakiwa uwe na kifua na akili sana. Msomali alinambia nikikubali deal angeniunganisha na masuala ya madini. Pia hizi mishe zingine nisingekuwa nakosa chini ya $2,000 kwa kazi ndogo kwa kazi kubwa ningekuwa naingiza hadi $5,000.
Na alisema nikiwa tayari atanipa mkanda mzima wa hii mishe, hivyo anachotaka ni utayari wangu tu.
Muda huu nilikuwa sielewi elewi ikabidi nimwambie anipe muda wa kufikiri then ningempa majibu. Msomali hakuwa na noma na yeye alitamani sana kufanya kazi na mimi na aliniahidi kunielekeza namba ya kuitumia nyota yangu nikafanikiwa.
Naam, ni maongezi yaliyotumia lisaa pale hotelini na baada ya hapo tuliagana na mimi nikarudi home kulala.
Barabarani niliendesha gari kwa fujo sana maana nilikuwa kwenye mawazo sana, kwanza suala la Iryn na pili suala la Msomali.
Ukweli nilikuwa nahitaji sana pesa kipindi hiki ili nikamilishe ujenzi kufikia level ambayo nilipanga. Ila kila nikikumbuka maneno ya Msomali nilikuwa nakosa nguvu kabisa maana nilikuwa bado sijui ni deal gani japo roho ilikuwa inaniambia ni hatari.
*********
Jumapili nilichelewa sana kuamka ni Mama J aliyeniamsha baada ya kutoka Kanisani ile asubuhi na ilikuwa saa4 tayari.
“Wewe Baba J ulalaji gani huo nimekuacha umelala na nimerudi bado umelala. Amka bhana ukanywe chai mimi ndo nakwenda kukuandalia hivyo.”
Niliamka pale na kucheki Whatsapp nilikuta Prisca amenitext kwamba anaomba badae tutoke out, na mimi sikutaka kumkatalia, niliona ingekuwa ni muda mzuri wa mimi kupunguza stress zangu.
Baada ya kupata breakfast nilirudi tena chumbani kulala na hii siku nilishinda niko chumbani tu maana nilikuwa na mawazo sana. Na muda nikiwa kitandani nilikuwa nikijiuliza mambo mengi sana pale,
“kwanini Iryn akatishe mkataba kwa haraka hivi? au suala la mimi kuwa na mke na mtoto ndo limemuumiza hivi? Hapana Iryn hawezi kuterminate mkataba kwa jambo la kipuuzi kama hili, nikawaza pale maybe kuna kitu Mama J atakuwa alimwambia Iryn. Mama J lazima kuna kitu aliongea kwa Iryn hivyo ameona akae mbali na mimi, ila mbona ile siku walikuwa na furaha na walikuwa wanacheka mpaka tunaachana?. Nitaongea na mama J vizuri nitajua ukweli tu.”
Na muda huu Mama J aliingia chumbani na akaanza kusoma, lakini muda wote macho yalikuwa kwangu na mimi nilikuwa nawaza namna ya kumwingia.
MAMA J: “Baba Junior upo sawa kweli?”
MIMI: “Yeah niko sawa kwani vipi unataka kunipa tunda?”
MAMA J: “Nakuona una mawazo something wrong?”
MIMI: “Hamna nimechoka tu ila niko sawa.”
MAMA J: “Nataka unisaidie kusovu maths week ijayo na test.”
MIMI: “Sawa nakuja tusovu.”
Niliona ndo muda muhafaka wa kumchimba deep na nikapata taarifa nazo taka kuzipata toka kwake.
MAMA J: “Ngoja nikachukue calculator Junior alikuwa anaichezea.”
Baada ya kurudi tulianza kusovu na alikuwa anataka nimfundishe kusovu hesabu za Price index.
MIMI: “Hesabu nyepesi kama hizi ndo nikusaidie unaniangusha swahiba.”
MAMA J: “Sijasema siwezi kuna maswali nataka tusovu magumu.”
Tulianza kusovu pale zile hesabu na zilikuwa zinakwenda vizuri tu na story zilikuwa zikiendelea pamoja na utani wa hapa na pale.
MIMI: “Hivi Mama J ile siku wewe na Iryn mlikuwa mnaongea nini? Niliona mmepatana kwa muda mfupi sana.”
MAMA J: “Baba J ukweli tulikuwa tunaongea masuala mengine kabisa na kipindi unaona tunacheka nilimwambia nikimaliza chuo sitaki kufanya kazi mpaka nikuzalie mtoto wa 2 ili Junior awe na mdogo wake, yeye alisema nikimaliza chuo atanisaidia kunitafutia kazi.”
MIMI: “Una uhakika mmeongea hayo tu? Maana nakujua vizuri sana.”
MAMA J: “Kweli Baba Junior I swear sikuongea mambo yoyote kuhusu wewe kwanza mtu mwenyewe alikuwa mgeni kwangu how should I strusted her?”
MIMI: “Sawa mke wangu haina shida nimekuelewa, mli exchange contacts?”
MAMA J: “Nope mbona unauliza sana? What’s really going on? Unasema ni Bossy wako ila haonekani kama Bossy wako kabisa, Baba J unaweza vumilia kufanya kazi na mwanamke mrembo kama yule bila kuingia tamaa?”
MIMI: “Swahiba huko umeanza kwenda mbali sana hivi unaona mimi nina hadhi ya kutembea na Mwanamke kama yule?”
MAMA J: “Yule dada anakupenda kabisa na sisi wanawake tunajuana vizuri na inaonesha kujua kwamba wewe unamke na mtoto kimemuumiza sana, na kwanini ulimficha hili?”
Nilijikuta naanza kujuta kwanini nilianzisha hii mada maana Mama J alianza kuwaka na kuongea kama radio, japo kwa upande mwingine Nilikuwa nimeshapata tayari baadhi ya taarifa.
MIMI: “I told you siwezi kuwa na mwanamke mwingine zaidi yako au umesahau?”
MAMA J: “Yule malaya wako niliyekuta chats zake najua bado mtakuwa mnawasiliana ila nitajua tu soon, nadhani hunijui vizuri this time nitakavunja vunja vipande, mwambie kabisa this time nitadeal naye na sio wewe.”
MIMI: “Mama J achana na hayo mambo tuendelee na hesabu maana nataka nilale.”
MAMA J: “Mimi nishaelewa tayari, nitajaribu kwa upande wangu badae, formula nimezishika inatosha.”
Mchana Mama wa2 alinipigia simu akanambia mke wangu Pili karudi toka jana na nikamwambia nitakwenda kumsalimia badae, pia kuna mambo nataka tuzungumze ni muhimu.
Niliwaza kuongea na Mama wa2 suala la kunisaidia mkopo maana aliniahidi atanisaidia nikihitaji mkopo kutoka bank. Niliamua kuanza kuseti mambo mapema ili ujenzi uendelee kule Dodoma.
Jioni nilijiandaa vizuri kabisa na nilipendeza maana nilikuwa natoka out pia na Prisca. Nilitoka pale home saa 10 jioni na nilimwaga Mama Junior natoka nitarudi badae
“Ndomana leo umeshinda umelala ili upate nguvu za kutoka usiku na yule Malaya wako sindio?”
Niliamua kunyamaza na kuondoka maeneo yale bila kuongea chochote. Niliondoka na kuelekea kwa mama wa2 na mapema tu nilikuwa pale nimeshafika tayari. Nilipiga honi na dada alitoka kunifungulia geti nikaingia na kupark gari.
Nilikaribishwa ndani na dada, nikaingia seblen na muda huu nilimkuta Rachel akiangalia TV.
“Uncle Insider shikamoo”
“Marahaba, Mama yuko wapi?”
“Mama alikuwa anaoga ngoja nikakuitie”
“Kama anaoga muache.”
“No atakuwa kamaliza ni muda.”
Na muda huu Rachel aliinuka kwenda kumuita mama yake na dada alikuwa kaniletea juice tayari.
Ilimchukua dakika 10 Mama wa2 kutoka ndani na alitoka akiwa amevaa dela na nilikuwa nikiyaona matandamu yake Vizuri.
MAMA 2: “Mkwe nisamehe sana nilikuwa naoga.”
MIMI: “Usijali mimi hapa ni nyumbani nilikuwa napiga story na Rachel, ila mke wangu simwoni.”
MAMA 2: “Pili atakuwa kalala ameshinda siku nzima anaangalia TV, Rachel kamuite dada yako amsalimie Insider.”
MIMI: “Muacheni alale navyoondoka atakuwa kaamka tayari.”
MAMA 2: “Nambie Insider una jambo gani unataka kushare na mimi?”
MIMI: “Nataka kukuoa.”
Na muda huu nilishtuka maana niliropoka bila kujua Rachel yuko pale ila mwenyewe alikuwa busy na mambo yake.
MAMA 2: “Unioe na uzee wangu huu? Uache watoto wabichi na watamu.”
MIMI: “Wewe hata 45 hujafika unawazidi hata mabint wa 2000 mbali sana.”
MAMA 2: “Watasema umeoa lishangazi si unawajua wabongo kwa maneno tena.”
MIMI: “Sasa wewe utasikiliza maneno yao?”
MAMA 2: “Acha utani bhana nambie una ishu gani?”
MIMI: “Mama mkwe nashida na mkopo si unakumbuka nilikwambia na ujenzi? Kuna amount nimekwama utanisaidiaje kwa hili.”
MAMA 2: “Unahitaji mkopo wa kiasi gani?”
MIMI: “Kama million 10 hivi na nitakuwa nalipa kila mwezi million 1.”
MAMA 2: “Haina shida kwa mkopo mdogo kama huo nitafanya maarifa hata usiwe na wasiwasi mkwe.”
MIMI: “Ahsante sana Mama mkwe ilikuwa neema kukutana na wewe.”
MAMA 2: “Usijali hata wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”
MIMI: “Mama mkwe mimi naondoka kuna sehemu nakwenda kama Pili amelala muache nitakuja hata kesho kwaajili yake.”
Niliaga pale na nikaondoka kuelekea kwa kina Prisca maana alikuwa kaanza kunipigia simu kwa fujo. Na habari njema Prisca alikuwa kasajili line mpya kama nilivyokuwa nimemwambia afanye.
Wakati niko njiani nilikuwa nafuraha sana maana Mama wa2 alikuwa kaniahidi kunikopesha pesa, na nikijumlisha na zile pesa nilizopata kwa Msomali jana nakuwa niko vizuri. Hivyo ujenzi ungeenda vizuri kabisa kama nilivyopanga, maana ujenzi ndo ulikuwa unaniumiza kichwa sana kipindi hiki tuache masikhara.
Iryn aliterminate mkataba kwenye kipindi muhimu tena ambacho namuhitaji sana. Lakini nikawaza pale alinikuta nafanya mishe zangu na maisha yalikuwa yanakwenda fresh tu.
“Hiki kipindi natakiwa kuwa na bajeti kali sana na nikawaza pesa ambazo nalipwa na Mama wa2 na Maggy kwa mwezi ni 484,000/= na wale madogo 660,000 kwa mwezi kama mnakumbuka. Jumla hapo ni 1,144,000/= kwa mwezi, nikaplan hii pesa nitakuwa nalipa mkopo wa Bank. Pia niliwaza pale inabidi nipambane sana kufanya kazi kwa bidii ili zipatikane pesa za kodi na matumizi ya nyumbani kwa ujumla, na pia nihakikishe zinapatikana pesa za mafuta na service ya gari.”
Niliwasili kwa kina Prisca na nikafunguliwa geti nikaingia ndani na nikapark gari uwanjani.
Na muda huu Prisca alitoka na akanikaribisha niingie ndani maana wao bado hata hawajiandaa.
MIMI: “Unavyosema hawajajiandaa unamaanisha nini?”
PRISCA: “Insider tunatoka na Mary na Mamdogo Ney”
PRISCA: “Njoo ndani bhasi Insider karibu be free.”
Na mimi nilikubali vivyo hivyo maana nilikuwa sina jinsi muda ule ilibidi niingie tu. Sasa ile nimeingia seblen nikakutana uso kwa uso na mama yao.
PRISCA: “Mama huyu anaitwa Insider ndo tunatoka naye out leo.”
Na muda huu mimi nilimsalimia mama yake pale ndo nilikuwa namjua mama yao kwa mara ya kwanza
“Karibu Mwanangu kaa chini na jiskie upo nyumbani.”
“Ahsante sana mama.”
Mama yao na kina Prisca alikuwa ni wamotoo sio poa na alikuwa kafanana sana na watoto wake, familia yao ilikuwa na watoto 4 afu wote wa kike na walikuwa wako vizuri sana. Afu mama yao hakuwa na noma wala nini na alitoka jikoni akiwa na matunda akavuta stuli na akaniwekea pale.
“Karibu matunda unavyo wasubiri hao na watakuweka sana hapa, mambo yao ni slow sana.”
“Ahsante sana mama, hao waache tu wajiandae taratibu maana muda bado tunao.”
Na mama alikaa pale seblen akiangalia TV na mimi ukweli sikuwa na confidence kabisa ila nilikuwa najikaza kiume tu. Ile nyumba yao ukiacha Mlinzi wa getini wengine wote ambao wanakuwepo ni wanawake.
Na muda huu Mary alitoka akiwa amependeza sana na akaja akakaa pembeni yangu kwenye mkono wa coach na akanisalimia
MARY: “Insider mambo, karibu.”
MIMI: “Ahsante nimekaribia.”
MARY: “Mama huyu anaitwa Insider kama hujatambulishwa, ni mstaarabu sana.”
MAMA: “Hata wewe mnafahamiana kumbe, mimi nilijua ni mgeni wa Prisca.”
MARY: “Prisca naye anakiherehere sana.”
MAMA: “Ndo aliyemkaribisha mgeni na muda wote alikuwa hapa seblen akimsubiri mgeni.”
Na muda huu Mary alikuwa akitaniana sana na mama yake pale na kwa haraka haraka nilihisi Mary zitakuwa zinaiva sana na mama yake.
MARY: “Mama hii nguo imenipendeza eeh imenichora shepu vizuri.” Na muda huu Mary alikuwa akizunguka kwa mapozi, akisubiri mama yake atoe neno.”
MAMA: “Embu na wewe nitokee hapa bhana, unaniboa ujue.”
MARY: “Mama unawivu wewe.”
Na muda huu mamdogo wao alitoka akiwa kawaka pia na baada ya dakika 10 Prisca ndo akatoka pale seblen, na tulikuwa tukimsubiri yeye atoke.
MARY: “Kila siku unakuwaga wa mwisho wewe tu, unatia aibu.”
PRISCA: “Mwanamke una wivu wewe. Nikachofanya uumie ni nini?
MARY: “Sasa kutuchelewesha kote huku ndo nin? na umetoka hovyo tu.”
PRISCA: “Insider eti sijapendeza?”
MIMI: “You look great.”
“Dada Prisca you look great than everyone here”
Ilikuwa ni sauti ya mdogo wake wa mwisho.
PRISCA: “Thanks Ivy hujawai kusema uongo mdogo wangu.”
MARY: “Lets go guys”
Muda huu ilikuwa 19:30 tayari, nilimuaga Mama yao na tukaondoka pale, na uelekeo wetu ulikuwa ni Kidimbwi.
MARY: “Guys msiwe na wasiwasi nilifanya reserve mapema sana.”
Tulifika pale mapema na tulikuta tumeandaliwa tayari sehemu nzuri ya kukaa, tulielekezwa sehemu ya kukaa na mhudumu alikuwa amefika kutuhudumia.
Mimi nilikaa na Mary na upande mwingine Prisca alikuwa na mamdogo wake. Na muda huu nilikuwa niko busy sana na Mary tukiongea na kupiga story mbalimbali huku tunacheka. Kwa upande wa Mamdogo wao tulikuwa tushazoeana tayari na tulikuwa tukipiga story sana.
Mida ya saa4 Mary alitoka na Mamdogo kwenda washroom na muda huu Prisca alihamia kuja upande wangu na akakaa pembeni yangu.
MIMI: “Vipi tunaondoka wote leo?”
PRISCA: “I wish but ni ngumu kwa leo si unaona mazingira?
MIMI: “Nakuzingua tu, but don’t do anything stupid here.”
Na muda huu Prisca wine zilikuwa zimemkolea kisawasawa hata aibu alikuwa hana kabisa. Na alionekana amekaa kimahaba sana kwangu.
PRISCA: “Insider What did you say?”
MIMI: “Nothing”
Mary na mamdogo Ney walikuwa wamerudi tayari na alishangaa kuona Prisca amekuja kukaa kwangu ikabidi akae na Mamdogo, na tuliendelea kuagiza vinywaji vingine.
Kadri muda unavyozidi kwenda Prisca alizidi kuonesha mahaba yake waziwazi kwangu na hata dada zake walihisi something fishy is going on kati yetu. Mary ndo alikuwa akitupiga sana macho muda huu, kwa upande wangu nilikuwa nikijaribu sana kumtuliza Prisca lakini wapi maana alikuwa haelewi kitu.
Kwa upande mwingine Mary alionekana kuwa na hasira sana ni kama alishajua kinachoendelea kati yangu na Prisca. Mudi ya Mary ilionekana kubadilika haraka sana muda ule, na mimi niliona hakuna haja ya kuendelea kubaki pale, nikawaaga nasepa ila wao walisema wataendelea kuwepo.
Prisca ndo alinisindikiza mpaka tulikokuwa tumepark gari na tulijikuta pale nje ya gari tukianza romance. Ndani ya muda mfupi nilishakuwa nimepima saizi ya nazi zake na nimepima oil vya kutosha.
Tulishtuka kumwona Mary akituangalia huku akiwa kama haamini anachoona muda ule pale.
TO BE CONTINUED
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu