EPISODE 42
CONTINUE….
Niliondoka pale home bila hata kuaga na muda huu Mama J na Iryn walikuwa pale seblen. Na mimi niliamua kuondoka na ile Dualis.
Niliamua kwenda kwa kina Prisca baada ya kuona hapokei simu zangu na dizaini kama ananikwepa na mimi nilikuwa na wasiwasi, kwanini hayuko serious kwenye jambo kama hili?.
Ilinichukua dakika 10 tu kufika pale kwao na baada ya kufunguliwa geti niliingia ndani na nikapark gari. Baada ya kushuka kwa gari nilimwona Mary akiwa nje kibarazani amekaa na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka pale.
MIMI: “Nakuona shem wangu unapanga mipango.”
MARY: “Hahahaa Insider mambo?”
MIMI: “Poa tu unaendeleaje lakin?”
MARY: “Niko poa bora umekuja twende hata Kidimbwi nikapunguze mawazo.”
MIMI: “Mke wangu yuko wapi?”
MARY: “Ivy……., muite da Prisca, vipi mna Agenda gani.?”
MIMI: “Anazingua acha leo nimwoneshe mimi ni nani.”
MARY: “Kafanyaje tena?”
Na muda huu Prisca alitoka pale nje kibarazani na mimi nikamshika mkono huku namvuta mkono
MIMI: “Twende kwenye gari.”
MARY: “You guys mna shida gani leo?”
PRISCA: “Insider … subi.. subirii nivae viatu.”
Na muda huu nilikuwa namvuta kwenda kwenye gari kwa nguvu.
MIMI: “Kwanini unanikwepa? na simu zangu hupokei?”
PRISCA: “Insider subiri please.”
Nilifungua mlango wa gari wa mbele na kumuingiza, upande mwingine Mary na Ivy walikuwa wanacheka sana. Na mimi nilikuwa serious sana sikutaka masikhara kabisa maana niliona Prisca ananifanyia mambo ya kitoto acha nimwoneshe mimi ni mhuni.
Niliwasha gari na tukaanza kuondoka pale kwao,
“Insider tunakwenda wapi?”
“Hospital kucheki mimba hiyo.”
“Insider stop, please.”
Na muda huu nilikuwa nishaingia mwaikibaki road tayari. Na akili zangu zilikuwa zinanituma kwenda Rabininsia Hospital.
MIMI: “Nataka twende tukapime afya yako afu unasema nini hapa? Prisca ntakuzingua nadhani hunijui vizuri.”
PRISCA: “Sasa unanipeleka hospital niko peku?.”
MIMI: “Wewe ndo umeyataka ungekuwa unapokea simu hata tusingefika huku.”
PRISCA: “Insider mimba kweli ninayo unakwenda poteza muda wako tu.”
MIMI: “Bado sikuamini tukifika hospital ndo tutajua ukweli.”
PRISCA: “Insider nielewe bhasi I’m serious, tunaenda kupoteza muda huko.”
MIMI: “Siwezi poteza muda kwaajili ya mwanangu.”
Tulikwenda moja kwa moja na Bahari Beach road tukaja kupanda njia panda ya kwenda Tegeta nyuki. Na baada ya kufika pale sokoni nilipark gari pembeni na nikamchagulia sando nzuri ya kuvaa maana alikuwa peku miguuni.
Hatukutumia muda mrefu pale Sokoni na tuliondoka kuelekea Hospital. Baada ya kuwasili pale hospital nilifanya malipo kwaajili ya vipimo vyote muhimu pamoja na Ultra sound.
Baada ya kufika muda wa kuchukua vipimo vya Ultra sound na mimi niliingia ndani kushuhudia mambo. Na kweli vipimo vilionesha Prisca anamimba tayari ya week 4 na maendeleo yake yalikuwa mazuri. Pia Doctor alitumia muda huu kutupa elimu ya Afya kwa mama mjamzito na mambo mengine mengi.
Pia tulichukua vipimo vya damu na majibu yalionekana kuwa safi pande zote mbili, na Prisca alifanyiwa vipimo vingi sana hii siku.
Hapo sasa nikaamini Prisca alikuwa serious kuhusu mimba. Kwa upande wangu sikuwa hata na sauti ya kuhoji ile mimba, maana kama kufanya mapenzi na Prisca tulikuwa tunafanya sana na ubaya nilikuwa sinaga habari na kuvaa condom.
“Hii mimba ni yangu sasa hapa sina ujanja na kutoa hii mimba siwezi hata Prisca hayuko tayari, hili jambo lishakuwa serious tayari hapa itabidi niandae mipango mapema.”
Ukweli ni kwamba nilikuwa na mawazo sana muda huu nikiwa nimekaa pale kwenye bench nikimsubiri Prisca akichukuliwa vipimo. Maana niliwaza mama yangu atalichukuliaje hili suala pale ambapo nitampa taarifa, niliwaza pia na Mama J atanielewaje?.
Ukweli nilikuwa kwenye majuto makuu sana na nilijisemea kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mungu. Huyu mtoto alishapangwa kuzaliwa hivyo sinabudi kuendelea kulaumu kwa jambo lililotokea, kama Prisca alishakubali kuwa mchepuko kulihandle hili suala ni rahisi.
Tulitumia kama saa 1 na nusu pale hospital na muda huu ilikuwa saa moja usiku tayari, hivyo tuliondoka pale na tulikwenda moja kwa moja mpaka Ledger Hotel, Bahari Beach.
Ilibidi nimpeleke pale ili tufanye mazungumzo juu ya ile mimba namna ya kuilea. Baada ya kuwasili pale hotelini tulitafuta sehem nzuri restaurant na tukakaa pale.
Baada ya mhudumu kuja kutusikiliza mimi niliagiza wine na Prisca aliagiza juice ya embe ‘Minute maid”, nilishangaa kwa mara ya kwanza namwona Prisca anaagiza juice.
“Usinambie mimba imekubadilisha tabia haraka hivi.”
“Yeah sahivi mimi na Juice tu.”
“Ni jambo zuri, huko kwenu bado hujashtukiwa tu?.”
“Bado maana nalala na Ivy hajui lolote hata hivyo mimba bado haijaanza kuchanganya kwasasa napata dalili za kawaida tu.”
“Kwanini ulishika mimba wakati unajua hali halisi Prisca.”
“Insider ulishawai hata siku moja kukumbuka kinga?.”
“Hata wewe lilikuwa ni jukumu lako kunikumbusha.”
“Umenipandisha stim tayari nakumbukaje?”
“Ulishasema unataka kunizalia najua umefanya makusudi.”
“One day nitakuambia kwanini nimeamua kufanya hivi ila wewe kuwa na amani mimi sitoingilia ndoa yako ila naomba uwe unamkumbuka mwanao. Na huyu nitakuzalia wa kike atafanana na wewe kwa kila kitu.”
“Wewe unachukulia simple unafikiri wazazi wataelewa binti yao azalishwe tu bila kuolewa?”
“Sidhani kama wazazi wangu watakuwa tatizo wewe ondoa shaka mimi ni mtu mzima tayari.”
“Kwanini umechukua maamuzi ya kijinga hivi Prisca.”
“Sikuwai kukukatalia kutumia kinga ina maana wewe ulifikiri unamwagilia shamba na lisitoe mazao?”
“Sawa bhana ila naomba uwe smart kama tulivyokubaliana hiyo mimba mimi nitaielea na kuitunza.”
“Honey nampango wa kuondoka pale home nikapange ili uwe free kuja kuniona wakati wowote.”
“Unaona hio ni good idea? Home watakuruhusu?”
“Nitawaambia nakwenda hostel.”
“Na umeplan kupanga maeneo gani?”
“Makongo juu au Changanyikeni wewe unaona wapi panafaa.”
“Changanyikeni kuzuri na karibu na chuo usafiri ni bajaji moja tu na ni sehem salama.”
“Sawa nitatafuta huko.”
“Utanambia bajeti zikoje ili tuone tunafanyaje.”
“Suala la kodi niachie mimi, wewe nisaidie kununua baadhi ya vitu muhimu vya ndani.”
“Sawa itabidi utafute na dada wa kazi.”
“Insider acha kuniona mimi laini sana mimba ndogo hii dada wa kazi wa nini kwasasa?, nitakuwa nakaa na Eva.”
“Sawa haina shida ni wewe. Na kilichokuwa kinafanya unanikwepa ni nini?”
“Insider nilikuwa sikuamini nilijua utanifanyia kitu kibaya ila nimegundua una mapenzi ya kweli na mimi.”
“Ulikuwa na utoto unakusumbua”
“Insider mwanao anacheza I can feel it.”
“Acha siasa na wewe mapema hivi mtoto anachezaje?, embu tuondoke”
Tulitoka pale restaurant na tulikwenda parking tulikokuwa tumepark gari na baada ya kuingia kwenye gari Prisca alinivuta na akaanza kunipa makis. Prisca alionesha anataka bakora muda huu, tuliondoka pale na tulikwenda moja ya lodge ya kule Bahari Beach. Ni bakora zilitembezwa humo ndani na kelele za utamu zilikuwa zikisikika muda huu. Mama kijacho alinipa style zote hii siku na ni moja ya sex tamu kupewa na Prisca usiku huu, that night was beautiful.
Baada ya mchezo kuisha Prisca alipitiwa na usingizi maana alikuwa hoi bin taaban. Na muda huu Mary alinipigia simu na nikaipokea
MARY: “You guys mko salama huko maana Prisca hapokei simu.”
MIMI: “We are good usiwe na wasiwasi Prisca amesahau simu kwenye gari.”
MARY: “Nilikuwa na wasiwasi maana mmeondoka kwa shari na mpaka sasa naona Prisca hajarudi.”
MIMI: “Do you really think nitamfanyia kitu kibaya Prisca?”
MARY: “No I just worried ndomana. Mko wapi sasa?.”
MIMI: “Tuko Bahari Beach tutarudi soon.”
MARY: “Hivi unajua mama ameshuhudia lile tukio?”
MIMI: “Mary acha utani Bimkubwa alikuwepo?”
MARY: “I swear to God, sikudanganyi na ameshuhudia mchezo mzima mliokuwa mnafanya.”
MIMI: “Hii ya leo ni noma kwakweli.”
MARY: “Na ametoka kumwulizia hapa kama amerudi nikamwambia bado.”
MIMI: “Kwahiyo tuseme Mama kashajua kinachoendelea kati yetu?”
MARY: “Toka ile siku umekuja ukamkuta alishajua wewe na Prisca ni wapenzi japo Prisca alikuwa anakataa, sasa hii ya leo ndo amegongelea msumari. Usiwe na wasiwasi mama hana shida kabisa kuwa na amani usije ukaanza kuogopa kuja hapa home.”
MIMI: “Haahahaa hamna bhana hapo ni home tu nitakuwa nakuja kama kawaida.”
MARY: “Sawa na vipi kuhusu suala la kwenda Mikumi?”
MIMI: “Kwani ulikuwa bado hujaenda tu maana ulinambia mwisho wa mwezi wa 5.”
MARY: “Weekend inayokuja tunakwenda.”
MIMI: “Ok sawa tutaongea hili sawa?”
MARY: “No problem.”
Ilibidi nimuamshe Prisca sababu muda ulikuwa umekwenda sana na saa yangu ilikuwa inaonesha saa 5 usiku tayari.
Kwa upande mwingine Iryn naye alikuwa ameanza kunipigia simu na mimi sikutaka kupokea simu zake muda huu,na alipiga simu mara 3 nikasema nitamkuta home tutaongea nikirudi.
Tuliondoka pale na Prisca nikamrudisha kwao na mimi nikarudi home. Ukweli ni kwamba hii siku Prisca alioneka kuwa na maongezi ya kiutu uzima sana na alionekana kuwa matured, nilihisi mimba imeanza kumbadilisha tabia tayari.
Sikutumia muda mrefu kuwasili pale nyumbani na baada ya kuingia ndani nilimkuta Iryn akiwa peke yake pale seblen anaangalia movie. Nilimsalimia na akajibu japo hakuonesha furaha ni kama alikuwa kamind hivi.
Niliingia kwanza chumbani nikakuta wife kalala nikarudi tena seblen.
“Mummy are you ok?”
“Where have you been?”
“Nilikuwa naangalia match pale 25.” Ilibidi nimdanganye tu.
“Sawa haina shida, kilichofanya usipokee simu ni nini?”
“Simu nilisahau kwa gari, wakati narudi ndo nikaona missed call zako nikasema haina haja ya kukutafuta maana narudi tutaongea huku, everything is ok?”
“Yeah mimi nakwenda kulala, kesho tutakwenda kuangalia hizo apartments.”
“Sawa haina shida usiku mwema.”
Na mimi wakati niko pale seblen nilikuwa na mawazo juu ya suala la Prisca na muda huu nilikuwa nawaza hili suala litabaki kuwa siri yangu. Niliwaza hata mama yangu mzazi sitomwambia mpaka mtoto atakavyokuwa mkubwa. Kuhusu mama J niliwaza kuja kumwambia badae sana mtoto akishakuwa mkubwa na tumefunga harusi tayari.
Naam ndugu zangu, mpaka sasa nimeprove mwenyewe hospital Prisca ni mjamzito tayari na ninatarajia kupata mtoto wa pili, Junior anatarajia kupata mdogo wake.
EPISODE 43[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu