Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Hivi INSIDER MAN bajaji biashara dogo yule ilkuwaje?
Nataka nione mli manage vipi biashara ya Bajaj .....najifunza Mengi the way unaongelea hizi biashara za vyombo vya usafirishaji aseeh !

Blessed!

Biashara ya Bajaji ni ya Mama Junior mimi ni kama msimamizi tu na bado tunaendelea na yuleyule dogo. Bajaji bado mpya kabisa dogo anaitunza sana, good news kupitia bajaji, Mama J mwezi May alinunua pikipiki so now ana bajaji na Pikipiki.
 
tupe ratiba kiongozi, yani hapa tupo tunachungulia kila mda kama nyumba za uswahilini kuchungulia kama mtu katoka msalani ama laa 🤣🤣
 
Sasa sijui itakuwaje Insider ile Dualis maaana Jane hajui kama ni ya kwake, alafu teyari keshajengewa Nyumba na mzee Pama. Kibongobongo unaweza ukaikaushia kila mtu afe na chake nawaza tu lkn sijui wewe ulifanyaje? maana we mzee wa kuchagua dhambi...kanisani sana alafu unawalamba. any way wacha tuone ilikuaje
Episode 45 Insider man alielezea mzee Pama alishaandika will nadhani ilisomwa kwenye kikao cha ukoo nadhani Dualis itaonekana kwenye wosia kwa Jane.
 
Sasa sijui itakuwaje Insider ile Dualis maaana Jane hajui kama ni ya kwake, alafu teyari keshajengewa Nyumba na mzee Pama. Kibongobongo unaweza ukaikaushia kila mtu afe na chake nawaza tu lkn sijui wewe ulifanyaje? maana we mzee wa kuchagua dhambi...kanisani sana alafu unawalamba. any way wacha tuone ilikuaje
Umewaza kama mimi[emoji2][emoji2][emoji2]
 
ADDITION

IN LOVING MEMORY OF MR. PAMA

Mzee Pama alikuwa na sumbuliwa na ugonjwa uliomtesa kwa zaidi ya miaka 12, mpaka kifo chake kinatokea ilikuwa ni tayari muda umefika. Hata kusurvive kwa kipindi chote hicho ni sababu ya Pesa tu, la sivyo angekuwa alikufa muda sana.

Mzee Pama aliandika waraka toka May na aliandika barua ya Mirathi June week moja kabla ya kifo chake, ni kama alikiona kifo chake mapema.

Mzee Pama alikufa akiwa na watoto watano (5) ambao wote ni mabinti na aliacha mjamzito ambaye ni Jane ambaye alikuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume. Hata waraka ulivyosomwa kuwa Jane atapata mtoto wa kiume watu walionekana kufurahishwa sana na zile taarifa.

Mzee pia aliacha Jina la kuitwa mtoto wake wa kiume akizaliwa na baada ya Jane kujifungua alipewa hilo jina X.

Mzee Pama alikuwa ni mstaafu wa Kampuni moja kubwa tu ya kimataifa inadeal na uchimbaji wa madini hapa nchini. Licha ya kustaafu bado walikuwa wanamtumia kwenye Project zao kwenye nchi nyingi hapa Africa. Pia mzee Pama alikuwa ana kampuni zake za kununua na kuuza madini na alikuwa na vitalu pia so alikuwa ana Pesa balaa.

Siku ambayo alikuwa anaagwa pale kwake Ununio mimi na Mary si tulikwenda kujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio?. Kimbembe ni kwamba ulikuwa unaandika Majina yako, unakotokea, namba ya simu, Mahusiano yako na Marehemu, kiasi chako cha mchango wako na mwisho kabisa ulikuwa una sign.

Mary ndo alikuwa wa kwanza kuanza kuandika na mimi sikuwa siriazi muda ule sasa baada ya kumaliza nilifata mimi. Nilivyofika kwenye mchango nikasema ngoja niangalie wengine wameandikaje kwakweli nilidata maana watu walikuwa wanatoa michango mikubwa balaa.

Niliona watu wameandika michango mikubwa sana hizi milioni 5, 10 zilikuwa kibao kwenye ile page, wa laki walikuwa wakuhesabika. Kabla ya Mary Pesa ndogo ilikuwa ni laki 5 sasa baada ya kuona Mary kaandika laki 2 ilibidi nicheke kimoyomoyo. Mimi ukweli nilichangia laki 5 maana pesa yenyewe nilitoa kwa zile ambazo alikuwa kanitumia Mzee Pama.

Niliwaza muda ule kutoa pesa yote iliyokuwa imebaki milion 4 kwa account maana milion 2 nilikuwa nishaiutoa tayari kule Mbweni. Lakini nikakumbuka Mzee alisema ananipa Pesa kwaajili ya Shukran na kunipa assist nilikokwama niliamua kuchangia laki 5. Na niliwaza pesa itakayobaki nitafanya jambo kwaajili ya ukumbusho wake.

Malipo yalikuwa yanafanyika kwa bank au Lipa namba na zilikuwa palepale kwa daftari. Nilishangaa sana kuona watu wakichanga pesa nyingi vile hapo watu Karibu 500 kasoro walikuwa washajiandikisha tayari.

Mary alishangaa sana alinambia “Insider hata nilikuwa sijui niweke kiasi gani maana niliona watu wanatoa michango mikubwa balaa ikabidi nijivute na mimi sio mbaya”.

Nilicheka sana kwakweli, hapa ndo nikawaza ukiwa maskini utazikwa na maskini ukiwa Tajir utazikwa na matajiri.

Kitu kingine msiba ulisimamiwa na Kikundi cha Mzee Pama ambacho huwa wanasaidiana kwenye shida na Raha. Walisimamia kila kitu mpaka mazishi na bado walitoa rambirambi kwa wafiwa. Yaani ile michango ilikuwa sio kitu tuseme haikutumika kabisa.

Mzee Pama nilifanya naye kazi nyingi na alinisaidia sana kiuchumi kielimu nk. Bado tumetoka sana out kama Samaki Samaki tumekwenda sana. Ni mambo mengi sana ambayo sikuyandika humu, alikuwa ni rafiki, Mzazi na mshauri kwangu.

Mzee Pama alinifundisha sana maisha na jinsi ya kuishi na watu, pia mzee aliniamini na alinipenda sana kama kijana wake. Kitu ambacho kilimkosesha raha Mzee Pama ni kukosa mtoto wa kiume tu.

R.I.P mzee Pama kila June nitaendelelea kukumbuka na kukuenzi kwa yote. Uliniachia task ya kuwa karibu na Jane na sasa ana mtoto wako wa Kiume wa miezi 9 na ana afya tele.

Ni vitu vingi sana vilitokea kwenye huu msiba ikiwemo watoto zake wote kusomeshwa mpaka chuo, siwezi kumbuka vyote.

Kingine June hii tulikwenda Tabora na Jane kulitembelea kaburi lake na kuweka maua. Niliteseka sana baada ya kifo chake nilikuwa na stress sana na nilikuwa nikimwota sana usiku Mzee na ndotoni nilikuwa naona akicheza na mwanae.

Baada ya kifo cha Mzee Pama niliamua
kuachana na Biashara ya Uber/Bolt kama heshima yangu kwake.

Hii ni moja ya kumbukumbu kubwa na mbaya sana ambayo biashara ya Uber iliniachia kwenye historia ya maisha yangu. Kumbukumbu ingine tutaikuta huko mbele kidogo.

R.I.P MZEE PAMA MUNGU AENDELEE KUKULAZA MAHALI PEMA PEPONI.

Romans 14:8
"If we live, we live for the Lord, and if we die, we die for the Lord. So, whether we live or die, we belong to the Lord."

Warumi 14:8
"Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana"

AMEN [emoji120]
R.I.P MZEE PAMA
 
Hii stori chai zimejaa mpaka nimemaliza chapati zote aisee jamaa muongo kinyama yaani yeye Kila mtu ataempa hela hua anatoa kuanzia laki 3 hamna tajiri anaetoatoa hela ovyo ovyo eti nauli tu aisee uongo umejaa sana madereva Uber mnazidisha sana chai aise
Mimi sio tajiri lakini kuwapa jamaa zangu laki 3 au 5 jambo la kawaida sana tu. Kuna rafiki yangu nime msamehe million 2 kwasababu alianza kupunguza mawasiliano na mimi nikajua huyu hataki kulipa tu. Kwahio acha nimsamehe ili urafiki wetu ubaki
 
Sasa sijui itakuwaje Insider ile Dualis maaana Jane hajui kama ni ya kwake, alafu teyari keshajengewa Nyumba na mzee Pama. Kibongobongo unaweza ukaikaushia kila mtu afe na chake nawaza tu lkn sijui wewe ulifanyaje? maana we mzee wa kuchagua dhambi...kanisani sana alafu unawalamba. any way wacha tuone ilikuaje
Tufanye wewe ndio insider vipi utaisalimisha au utabaki nayo ili iwe kumbu kumbu ya kumuenzi mzee pama
 
Mimi sio tajiri lakini kuwapa jamaa zangu laki 3 au 5 jambo la kawaida sana tu. Kuna rafiki yangu nime msamehe million 2 kwasababu alianza kupunguza mawasiliano na mimi nikajua huyu hataki kulipa tu. Kwahio acha nimsamehe ili urafiki wetu ubaki
mh! another KIDUKULILO kwenye ubora wake
 
Hii stori chai zimejaa mpaka nimemaliza chapati zote aisee jamaa muongo kinyama yaani yeye Kila mtu ataempa hela hua anatoa kuanzia laki 3 hamna tajiri anaetoatoa hela ovyo ovyo eti nauli tu aisee uongo umejaa sana madereva Uber mnazidisha sana chai aise
Utasema ivo labda kwasababu haujafanya kazi na watu wa namna hiyo, kwenye kutoa izo ela sina shaka na hii story, kuna muda unazungukwa na watu wanene kupata milioni, laki5 izi, mtu akikupa laki2 anakwambia kanywe soda au hii ni lunch
 
Back
Top Bottom