Who is your favorite character in the story? So far and why?
You my friend. Kwanza Uko vizuri kwenye kupambana.
Pili nilichojifunza zaidi kizuri kwako huna tamaa. Kwa hiyo tamaa inajikuta inakufuata yenyewe baada wewe kuikataa.
Kwanza tukianzia kwenye Ubber katika wateja wako wote uliokutana nao kufanya nao kazi. Hapo vijana wengi wangekuwa wameshaharibu. Iwe kwa kumpiga zaidi ya bei ya kawaida kwenye usafiri,maana kuna muda ulikuwa unaachiwa useme ni kiasi gani ktk mizunguko yenu,lakini mwamba ulikuwa unacheza fair unawaambia nauli ya kawaida bila kuangalia uwezo wa mtu. Kuna muda ulikuwa unawapa fair kabisa kwa kuwaambia leo nauli nimesamehe. Hicho kilikuwa kinawaachia maswali sana. Na kimekutengenezea uaminifu sana.
Mfano mzee Pama,ingekuwa kijana mwingine angekuwa ameharibu kitambo kwa huyu mzee,iwe kwa kumuomba omba hela hasa pale ulipopewa uhuru wa kusema chochote utakacho. Kwa mzee Pama ulicheza sana.
Ukija kwa Iryn hujafanya haraka kabisa kama hutaki vile. Kuna muda amekutega sana iwe kwa pesa kukuangalia au kivingine. Lakini mwamba hukuniangusha,umecheza kama Pele. Pamoja na kujirengesha kila mara,lakini ukawa unamkwepa kila mara. Ukasubiri muda muafaka. Ukasubiri muda yeye mwenyewe atengeneze njia ya wazi na aseme kwa sauti na mwisho amesema hapo ukafanikiwa tena kwa kiasi kikubwa kumfanya awe weak kwako kwa hali. Umejijengea uaminifu mkubwa sana kwake. Hongera sana.
Pia ukija kwa wengine kama Mbotswana, Prisca,Jane,Mary,Sumaiya. Umecheza kwa nafasi yako murua kabisa. Hukuikimbilia kuichagua tamaa. Tamaa ndio ikawa inakutafuta yenyewe.
Kwa ujumla kuna mengi ya kuelezea kuhusiana na hii FILAMU,lakini naona nitawachukulia muda. Kuna mengi sana ya kujifunza
Nasemaje MUNGU anijalie tu nipate maokoto, Hii ni bonge moja la series. BONGE MOJA LA FILAMU.
BIG UP SANA
INSIDER MAN