EXTRA EPISODE 06
BY INSIDER MAN
Kwanini nimemuita Iryn ni Mrembo wa Ajabu?
Kabla ya kuandika hii story nilipata tabu sana kwenye kuchagua kichwa kutakacho beba jina la story, lakini target ya huu uzi ilikuwa ni Iryn.
Ningeweza kuandika heading nyingi tu lakini niliona hii ndo sahihi kutokana na jinsi tulivyokutana na tulivyoishi sababu tulipitia mambo mengi sana.
Kwangu Iryn nilikuwa namuona ni mtu wa ajabu, kwanza namna tulivyo kutana, pili maisha yake kwa ujumla kwangu mimi yalikuwa yananipa maswali sana, tatu utajiri wa wazazi wake na yeye pia, nne uzuri na urembo wake.
Nilikutana na Iryn kimaajabu sana kupitia hiihii bishara ya Uber, ukisoma vizuri wakati nakutana naye ilikuwa ni usiku sana afu nimechoka. Baada ya kupata request yake nilitaka kupiga chini ile request lakini nikaamua kwenda kibishi na ndo yeye kaja kunipa heshima ya kuwa baba mtoto.
Kama ningeipiga chini ile request ina maana nisingekuja kumfahamu mtu anayeitwa Iryn kwenye Maisha yangu, kuna msemo wazungu wanasema “everything happen for a reason.”
Tukija kwenye maisha yetu halisi huenda tunapishana na baraka nyingi na connections nyingi kwa kupuuzia tu, kama wewe dereva wa Uber unapata request ya kwenda Mbagala lakini hutaki kwenda, kumbe ilikuwa ni connection kwako bila kujua.
Iryn ni moja ya mwanamke mzuri na mrembo hapa Duniani na uzuri wake ni natural sio namsifia kumpa sifa ambazo hana, hapana ni moja ya mwanamke mrembo sana na amekamilika kila Idara (Episode ya 7 nilimuelezea kidogo). Hii ilinifanya nimuone Iryn ni moja ya mwanamke wa ajabu kukutana naye kwenye maisha yangu. Kuna muda ile mwanzoni nilikuwa nahisi maybe atakuwa sio kiumbe wa kawaida. Kitu kingine suala la kuwa mtoto pekee kwa mama nalo kilifanya nimuone Iryn wa tofauti sana.
Suala la mali na utajiri ambao familia yake unao kuanzia marehem mama yake, Mzee wake na yeye pia vilikuwa vinanipa maswali sana. Mzee wake Iryn anapesa sana na huko South Africa ana ma apartments kibao anayamiliki na bado ni mfanyabiashara mkubwa.
Nimeplay part kubwa sana ya kumuweka Iryn sawa maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana, kitendo cha kuwa naye close mara kwa mara ndo kilifanya aanze kunipenda kwa kasi ya 5G.
Licha ya kufaham nina familia ila kwake yeye ilikuwa tofauti na aliendelea kunipenda tena ni upendo wa kweli. Tumepitia mambo mengi sana na sikuyaandika yote, niliyoandika ni baadhi tu.
Baada ya Iryn kwenda South Africa hapa katikati mambo mengi sana yalitokea, na yeye alikuwa anakuja Dar kuniona kama alivyo niahidi na ilikuwa ni kwasiri sana na hakuna aliyekuwa anajua hili. Amekuja sana Dar mpaka mimba ilivyokuwa kubwa ndo akaacha kuja na toka aondoke kwenda South Africa hajawahi kuonana na mama J tena.
Pia kuna mambo mengi sana yalitokea na mazito juu ya ujauzito wake na niliishi kwa stress sana ndugu zangu. Kwa upande wake alikutana na pingamizi kubwa sana hasa upande wa ndugu, lakini all kila kitu kilikwenda sawa na mwezi June 2023 alijifungua salama na tulipata mtoto wa kike.
Nilifurahi sana kupata mtoto wa kike japo nilikuwa najua kuwa nitapata mtoto wa kike lakini baada ya kujifungua na kujihakikishia kwa macho nilifurahi sana. Before hajajifungua mwezi wa sita nilikwenda South Africa kwa mara ya pili ili niwepo wakati wa kujifungua na nilikaa kule kwa week 2.
Siku anayojifungua nilikuwa naye hospital nikishuhudia kila kitu kule leba asee kule kama mwanaume unahasira utaishia kuwapiga madoctor[emoji23][emoji23], wanachokonoa sana K kwa mikono. All nashukuru Mungu alijifungua salama kwa kupush, na kama tulivyokubaliana mimi ndo nilimpa jina mtoto.
Mtoto wetu ana miezi 5 kasoro mpaka sasa na anakua vizuri, ana afya nzuri niseme she is so beautiful jamani na nimefanana naye copyright. Pia amefanana sana na kaka yake Junior, yaani siku wakija kukaa pamoja itaonesha ni watoto wa mama mmoja maana wote wamefanana sana na mimi, hata mama J akija kumuona hatauliza mtoto ni wanani kwani tumefanana sana.
Hili suala bado imebaki kuwa siri kwangu hata wazazi hawajui mpaka sasa navyoandika hapa. December hii Iryn atakuja Dar na bado najifikiri niende naye mkoani na mtoto kwa wazazi wamuone au niendelee kuvunga tu mpaka mtoto akue, au niwape taarifa na mtoto wa nje?, hapa bado nakosa majibu.
Iryn anataka kunizalia mtoto mwingine wa pili, amesema yeye anahitaji watoto sababu anaona ndo furaha kwake na jinsi tunavyoishi hata kama tuko mbali anaona mimi natosha kuwa mume wake. Unajua Iryn anajua fika mimi sijampendea kisa pesa zake na anafahamu fika mimi sina habari na pesa zake kabisa na ninamchukulia kama mama watoto wangu.
Niilimpa greenlight kama atapata mtu sahihi awe huru kuwa naye au kuolewa, lakini amegoma kabisa hataki kuzisikia hizi habari. Yeye anasema hakuna mwanaume wa kumpenda kama jinsi mimi navyompenda na hatamani kuwa na mtu mwingine kwa heshima yangu na mtoto, pia ameridhika kuwa mchepuko.
Kwa upande mwingine nilimwambia yeye ni mke mdogo na nimempa hiko cheo na ninaandaa mpango wa kumpeleka home akaijue familia yangu maana analea damu yetu, na yeye ana hamu kubwa sana.
Kipindi alichojifungua ndo nilijihakikishia Iryn sio mtu wa kawaida, unajua walikuja watu wengi sana kumuona kule South Africa, kuanzia friends zake zake wa chuo, ndugu zake wa Ethiopia nknk.
Kwa upande wa mimi na mama J mahusiano yetu yako strong sana kwasasa, japo baada ya Iryn kuondoka kuna mambo yalitokea lakini bado tuko pamoja na familia yetu inazidi kustawi na mwakani tunatarajia kufunga Ndoa rasmi kama Mungu akitujalia uhai.
Kwa upande wa my son Junior yeye kashakua mkubwa tayari na mwakani tunategemea aanze nursery mapema na atakuwa na 2.5yrs by January. Dogo kawa mtundu sana, ni mkorofi sana kupiga watoto wenzie kwake ni kitu cha kawaida ila huji kuta akiwapiga watoto wa kike.
December Iryn atakuja kama nilivyosema awali na tutadiscus mambo mengi sana ikiwemo kuhusu project ya kufanya kule Dodoma, suala lingine nilimwambia nikimaliza chuo nataka kufanya project zangu sitaki kuwa chini yake tena.
Nilimwambia yeye ni mke wangu kuendelea kunilipa mshahara naona kama dharau, so kama vipi tufungue kampuni ya pamoja au mimi nifanye mambo yangu. Baada ya kumpa hizi taarifa naona hajazipenda na amesema yuko tayari kunisikiliza ila hataki nifanye kazi na mtu mwingine kwani bado ananitegemea sana, akija mwezi ujao ndo tutafikia muhafaka.
Plan za Iryn akimaliza chuo anataka kwenda kuishi Ufaransa na mtoto maana kuna project zake mpya anazo kule. Pia hata yeye anapenda sana kuishi Ufaransa.
Mwisho, sikuwahi kuwaza kuja kuchepuka au kuzaa na mwanamke mwingine nje na mama J, nilianza kuchepuka kutokana na kutopewa tendo kwa wakati maana kama mwanaume uvumilivu ulinishinda na kile kitendo cha kuondoka kwenda kwao kisa Prisca na huku sijatembea naye, ukweli kilinikera sana.
NB: Nitaangalia kama nitawapa muendelezo hata mwakani huko lakini siwapi promise kwa hili, nitaangalia kama kuna code zozote zimefunguka kupitia hii story mpaka sasa na kama upepo ni shwari nitaangalia namna ya kuwapa.
“Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.
Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana. (EPISODE 07)