Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EXTRA EPISODE 06
BY INSIDER MAN

Kwanini nimemuita Iryn ni Mrembo wa Ajabu?


Kabla ya kuandika hii story nilipata tabu sana kwenye kuchagua kichwa kutakacho beba jina la story, lakini target ya huu uzi ilikuwa ni Iryn.

Ningeweza kuandika heading nyingi tu lakini niliona hii ndo sahihi kutokana na jinsi tulivyokutana na tulivyoishi sababu tulipitia mambo mengi sana.

Kwangu Iryn nilikuwa namuona ni mtu wa ajabu, kwanza namna tulivyo kutana, pili maisha yake kwa ujumla kwangu mimi yalikuwa yananipa maswali sana, tatu utajiri wa wazazi wake na yeye pia, nne uzuri na urembo wake.

Nilikutana na Iryn kimaajabu sana kupitia hiihii bishara ya Uber, ukisoma vizuri wakati nakutana naye ilikuwa ni usiku sana afu nimechoka. Baada ya kupata request yake nilitaka kupiga chini ile request lakini nikaamua kwenda kibishi na ndo yeye kaja kunipa heshima ya kuwa baba mtoto.

Kama ningeipiga chini ile request ina maana nisingekuja kumfahamu mtu anayeitwa Iryn kwenye Maisha yangu, kuna msemo wazungu wanasema “everything happen for a reason.”

Tukija kwenye maisha yetu halisi huenda tunapishana na baraka nyingi na connections nyingi kwa kupuuzia tu, kama wewe dereva wa Uber unapata request ya kwenda Mbagala lakini hutaki kwenda, kumbe ilikuwa ni connection kwako bila kujua.


Iryn ni moja ya mwanamke mzuri na mrembo hapa Duniani na uzuri wake ni natural sio namsifia kumpa sifa ambazo hana, hapana ni moja ya mwanamke mrembo sana na amekamilika kila Idara (Episode ya 7 nilimuelezea kidogo). Hii ilinifanya nimuone Iryn ni moja ya mwanamke wa ajabu kukutana naye kwenye maisha yangu. Kuna muda ile mwanzoni nilikuwa nahisi maybe atakuwa sio kiumbe wa kawaida. Kitu kingine suala la kuwa mtoto pekee kwa mama nalo kilifanya nimuone Iryn wa tofauti sana.

Suala la mali na utajiri ambao familia yake unao kuanzia marehem mama yake, Mzee wake na yeye pia vilikuwa vinanipa maswali sana. Mzee wake Iryn anapesa sana na huko South Africa ana ma apartments kibao anayamiliki na bado ni mfanyabiashara mkubwa.

Nimeplay part kubwa sana ya kumuweka Iryn sawa maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana, kitendo cha kuwa naye close mara kwa mara ndo kilifanya aanze kunipenda kwa kasi ya 5G.

Licha ya kufaham nina familia ila kwake yeye ilikuwa tofauti na aliendelea kunipenda tena ni upendo wa kweli. Tumepitia mambo mengi sana na sikuyaandika yote, niliyoandika ni baadhi tu.

Baada ya Iryn kwenda South Africa hapa katikati mambo mengi sana yalitokea, na yeye alikuwa anakuja Dar kuniona kama alivyo niahidi na ilikuwa ni kwasiri sana na hakuna aliyekuwa anajua hili. Amekuja sana Dar mpaka mimba ilivyokuwa kubwa ndo akaacha kuja na toka aondoke kwenda South Africa hajawahi kuonana na mama J tena.

Pia kuna mambo mengi sana yalitokea na mazito juu ya ujauzito wake na niliishi kwa stress sana ndugu zangu. Kwa upande wake alikutana na pingamizi kubwa sana hasa upande wa ndugu, lakini all kila kitu kilikwenda sawa na mwezi June 2023 alijifungua salama na tulipata mtoto wa kike.

Nilifurahi sana kupata mtoto wa kike japo nilikuwa najua kuwa nitapata mtoto wa kike lakini baada ya kujifungua na kujihakikishia kwa macho nilifurahi sana. Before hajajifungua mwezi wa sita nilikwenda South Africa kwa mara ya pili ili niwepo wakati wa kujifungua na nilikaa kule kwa week 2.

Siku anayojifungua nilikuwa naye hospital nikishuhudia kila kitu kule leba asee kule kama mwanaume unahasira utaishia kuwapiga madoctor[emoji23][emoji23], wanachokonoa sana K kwa mikono. All nashukuru Mungu alijifungua salama kwa kupush, na kama tulivyokubaliana mimi ndo nilimpa jina mtoto.

Mtoto wetu ana miezi 5 kasoro mpaka sasa na anakua vizuri, ana afya nzuri niseme she is so beautiful jamani na nimefanana naye copyright. Pia amefanana sana na kaka yake Junior, yaani siku wakija kukaa pamoja itaonesha ni watoto wa mama mmoja maana wote wamefanana sana na mimi, hata mama J akija kumuona hatauliza mtoto ni wanani kwani tumefanana sana.

Hili suala bado imebaki kuwa siri kwangu hata wazazi hawajui mpaka sasa navyoandika hapa. December hii Iryn atakuja Dar na bado najifikiri niende naye mkoani na mtoto kwa wazazi wamuone au niendelee kuvunga tu mpaka mtoto akue, au niwape taarifa na mtoto wa nje?, hapa bado nakosa majibu.

Iryn anataka kunizalia mtoto mwingine wa pili, amesema yeye anahitaji watoto sababu anaona ndo furaha kwake na jinsi tunavyoishi hata kama tuko mbali anaona mimi natosha kuwa mume wake. Unajua Iryn anajua fika mimi sijampendea kisa pesa zake na anafahamu fika mimi sina habari na pesa zake kabisa na ninamchukulia kama mama watoto wangu.

Niilimpa greenlight kama atapata mtu sahihi awe huru kuwa naye au kuolewa, lakini amegoma kabisa hataki kuzisikia hizi habari. Yeye anasema hakuna mwanaume wa kumpenda kama jinsi mimi navyompenda na hatamani kuwa na mtu mwingine kwa heshima yangu na mtoto, pia ameridhika kuwa mchepuko.

Kwa upande mwingine nilimwambia yeye ni mke mdogo na nimempa hiko cheo na ninaandaa mpango wa kumpeleka home akaijue familia yangu maana analea damu yetu, na yeye ana hamu kubwa sana.

Kipindi alichojifungua ndo nilijihakikishia Iryn sio mtu wa kawaida, unajua walikuja watu wengi sana kumuona kule South Africa, kuanzia friends zake zake wa chuo, ndugu zake wa Ethiopia nknk.

Kwa upande wa mimi na mama J mahusiano yetu yako strong sana kwasasa, japo baada ya Iryn kuondoka kuna mambo yalitokea lakini bado tuko pamoja na familia yetu inazidi kustawi na mwakani tunatarajia kufunga Ndoa rasmi kama Mungu akitujalia uhai.

Kwa upande wa my son Junior yeye kashakua mkubwa tayari na mwakani tunategemea aanze nursery mapema na atakuwa na 2.5yrs by January. Dogo kawa mtundu sana, ni mkorofi sana kupiga watoto wenzie kwake ni kitu cha kawaida ila huji kuta akiwapiga watoto wa kike.

December Iryn atakuja kama nilivyosema awali na tutadiscus mambo mengi sana ikiwemo kuhusu project ya kufanya kule Dodoma, suala lingine nilimwambia nikimaliza chuo nataka kufanya project zangu sitaki kuwa chini yake tena.

Nilimwambia yeye ni mke wangu kuendelea kunilipa mshahara naona kama dharau, so kama vipi tufungue kampuni ya pamoja au mimi nifanye mambo yangu. Baada ya kumpa hizi taarifa naona hajazipenda na amesema yuko tayari kunisikiliza ila hataki nifanye kazi na mtu mwingine kwani bado ananitegemea sana, akija mwezi ujao ndo tutafikia muhafaka.

Plan za Iryn akimaliza chuo anataka kwenda kuishi Ufaransa na mtoto maana kuna project zake mpya anazo kule. Pia hata yeye anapenda sana kuishi Ufaransa.

Mwisho, sikuwahi kuwaza kuja kuchepuka au kuzaa na mwanamke mwingine nje na mama J, nilianza kuchepuka kutokana na kutopewa tendo kwa wakati maana kama mwanaume uvumilivu ulinishinda na kile kitendo cha kuondoka kwenda kwao kisa Prisca na huku sijatembea naye, ukweli kilinikera sana.

NB: Nitaangalia kama nitawapa muendelezo hata mwakani huko lakini siwapi promise kwa hili, nitaangalia kama kuna code zozote zimefunguka kupitia hii story mpaka sasa na kama upepo ni shwari nitaangalia namna ya kuwapa.

“Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.

Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana.
(EPISODE 07)
Sikia mkuu INSIDER MAN watu wengi wanaogopa kuzaa watoto wengi ksbb ya uchumi. Sasa wewe kwa Iryn mama yao uchumi umesimama. Hapo ungepiga watoto double double hata 8 mkuu wa kiume kwa wa kike,mpaka yeye mwenyewe aseme pooh. Watoto ni faraja sana. Na wana msaada sana huko mbele. Bahati kwako hawatakupa shida kila kitu kiko sawa
 
INSIDER MAN ...achana na mambo ya kumtambulisha Iryn na mtoto Kwa wazazi wakati huu. Mama Yako ni mtu makini sana, anawezakukupa maelekezo yatakayokuweka mahali pagumu sana.

Kumbuka unatarajia kufunga ndoa(kubariki ndoa) muda si mrefu, hizi habari za mtoto zitatibua na kuibua mambo mengine. Kwa maoni yangu, ungekamilisha Hilo zoezi la ndoa kwanza, huku ukisikilizia mambo yanaendaje.

Mie nilisha ambiwa, siku ikitokea taarifa za ujauzito au mtoto wa nje ndio mwisho wa mahusiano na wife. Akasema yuko radhi kumtambulisha watoto wengi wajae fuso ila kama walipatikana kabla ya kufahamiana nae ila sio tukiwa wote.

Inabidi uongeze sasa mdogo wa hao watoto kwa Mama Jr. Naona Iryn ndio anamoto wa kukuzalia mtoto mwingine, angalia asije akasawazisha na kuongoza ligi...

Ni kweli hautaki kuendelea kulipwa mshahara kwenye kazi za Iryn, lakini hauoni kuondoka kwako inaweza kusababisha mambo yakayumba kibiashara mkapoteza wote?

Unaweza kufanya mambo mengine lakini ukaendelea ku oversee hizo biashara.

Kwenye extra episode 06 haujagusia suala la Mama Janeth na mtoto wa Iryn, hajawahi kujua wewe ndio baba wa huyo mtoto?

Kingine unakibarua kizito sana, tena sana cha kukaa mbali na akina Mary, Mdogo wake Jane, mtoto wa Mzee Juma na walimbwende wengine, siku ukijichanganya, ikathibitika pasi shaka umechepuka, Kwa akili za Iryn zilivyo, hasira zake anaweza kumshirikisha Mama Jr kuhusu hizo tabia hata kama na yeye atakua matatani lakini hatakua na cha kupoteza. Usiwaumize mioyo hao wake zako, Iryn akijua unachepuka ni bora ukajifiche Gaza.

Mwisho wa siku maamuzi unayo wewe kiongozi.
Kabisa. Asiachie kazi pale kwa Iryn kwa mawazo ya kujishusha kupata mshahara. Mshahara ni sehemu tu. Yeye asifikirie habari za mshahara,ila afikirie kuiendeleza kampuni ya mkewe Iryn.

Hata kama watafungua kampuni nyingine INSIDER MAN na Iryn bado anaweza kuendelea kuwa manager kwenye kampuni za Iryn mbona hakuna ubaya kabisa?. Mtu amemwamini na kwa namna ya story yeye ndio anaimudu vizuri kampuni. Mimi sioni sababu kwa nini aichie kampuni,inaweza kuyumba.

Jambo la pili usijaribu kwenda kumtambulisha Iryn kwenu kwa haraka namna hii,kama wengi wanavyoshauri,hata kama utaongezea nae watoto,endelea kuifanya siri kwanza. Muda mwingine mpaka hiyo siri iendelee kudumu tu. Kwani kuna haja gani ya kufanya hivyo sasa wakati maisha yanaendelea vizuri tu?. Nina uhakika ukiliweka wazi hili tu kwa mama J,fahamu lazima ukubariene na masharti kuachia kazi kwenye hiyo kampuni pia masharti kuacha kabisa mawasiriano na Iryn. Mimi nasema hata hao wachache unaowaamini wasijue kwanza hii siri kabisa. Endelea kubuy time.
 
Eti bro Watu8 katiba ya kibazazi inasemaje? Amchane mama J kabla hawajaanza process za kubariki ndoa au akaushe mpaka watakapofunga ndoa aje agundue tu mwenyewe kwamba jamaa ana familia nyingine na Iryn?? Ila wanaume mna siri daaahh[emoji119][emoji119]
Akaushe tu mpaka watakavyojua wenyewe,ndio ataanda utetezi. Tena utetezi wake utakuwa simple tu. Kutotaka kukuumiza mama J.
 
Kama ni hivyo asitishe jambo la kubariki ndoa, aweke wazi hili la mtoto na msimamo wake na Iryn baada ya vumbi kutulia ndio itaamuliwa kama ndoa itakua ya wake wawili, Mke mmoja ( Iryn au Mama J).

Nimesharudi suala la mtoto liwekwe kando kwanza Kwa sababu halina madhara makubwa Kwa Sasa. Kutojulikana kwake hakufanyi mtoto akose matunzo, hakufanyi Iryn alalamike Wala hakuna shida yoyote Kwa Mama J na haiathiri utensaji kazi wa insider.

Nakuhakikishia kujulikana Kwa hili jambo Sasa hivi sakata linaweza kuchukua sura mpya Kila kitu kikavurugika.

Watu8 tia neno Mkuu.

Sie tunataka tule ubwabwa Harusi ya kaoteni mwenzetu. Umekwepa mishale mingi tupe uzoefu kidogo
Ni sawa kabisa iendelee tu kuwa siri. Iendelee kuwa siri kama ilivyo kuwa mwanzo,na ikiwezekana siri tu ya kudumu. Kwani kuna shida. Kizuri zaidi Iryn anajimudu kwa kila kitu. Kitendo tu cha kuweka wazi kwa mama J maana yake akubariane na kuachana kabisa ma Iryn. Vinginevyo afanye kukaidi masharti ya mama J
 
Ningekua mimi ndo mama J. Bora usiniambie mpaka mtoto atakavyokua mkubwa maybe miaka 10 huko tukiwa tushakuwa watu wazima zaidi tunafikiria majukumu zaidi.

My dad alimficha mama kwamba ana mtoto. Mama akaja kujua mtoto akiwa 20yrs, akamwambia tu baba amlete mtoto amuone.

Ila sasa hivi mapenzi bado ni moto moto, mimi nashauri usimwambie mama J. Kuhusu kuwaambia wazazi hapo labda wenzangu wakusahauri. Ila mzazi wako anaweza kukwambia mwambie mkeo na tunarudi pale pale.
@INSIDER MAN Fuata ushauri huu tu. Usijaribu kumvuruga mama J kabisa. Hata home usiwaambie. Iryn mfanye mchepuko wako wa siri. Wachache sana wajue. Bahati nzuri hataishi hapa Tz. Endelea kufanya siri milele,wajuage mbele mwamba
 
@INSIDER MAN Fuata ushauri huu tu. Usijaribu kumvuruga mama J kabisa. Hata home usiwaambie. Iryn mfanye mchepuko wako wa siri. Wachache sana wajue. Bahati nzuri hataishi hapa Tz. Endelea kufanya siri milele,wajuage mbele mwamba
Mzee Kwa uzoefu wetu wengine sio kinadharia nashauri amtambulishe kwao Example kwake ni Mzee Pama situation ni the same Kuna mambo haya kwepeki mama j anaweza subiri ila sio Kwa wazazi wake
 
Sipingi mawazo Yako lakini unalichukulia hili jambo kwa wepesi sana, tunaoshauri hapa wengine tumeshapitia mambo mazito maishani ni vile tu hatuwezi kuandika Kila kitu hapa, tunauzoefu na haya mambo chini ya mwenyekiti wetu wa kudumu Watu8

Usifikiri Mama J kuambiwa mapema ni suluhisho la uhakika, anaweza akaambiwa, akavunga amelipokea Kwa moyo mkunjufu bila kinyongo na ndoa ikafungwa lakini atakachokuja kukifanya huko mbeleni anakijua mwenyewe moyoni mwake ( na hii haijalishi ni Mchaga, mmatumbi au kabila Gani)
Kumbuka tayari Mama J ana wasiwasi mzito sana na mashaka juu ya Iryn, Sasa kupata uthibitisho wa hili jambo kutoka Kwa INSIDER MAN itaurarua moyo wake na kuleta chuki isiyo na maelezo.

Unavyoona tunasema ndoa ifungwe kwanza hayo mambo mengine yatajisumbukia huko mbeleni sio kwamba hatumpendi Iryn na mtoto wake, tunaangalia namna ya kupunguza athari na uharibifu zaidi ya Hali ilivyo Sasa.

Linaweza kuibuka varangati hata jamaa yetu shule isisomeke, kazi zikavurugika na hata mawasiliano ya Siri kati yake na Iryn yakaingia dosari kuelekea asimuone Tena Binti Yao.

Kumbuka Iryn nae ni binadamu ana hisia, likiibuka varangati itabidi aiponye nafsi yake na ya mtoto wake hata kama itabidi kumkwepa Insider.


Ndoa italeta Imani Kwa Mama J na kujihakikishia hati miliki na nafasi yake ya main wife. Danadana zingine ataona kama mizengwe ya kutaka kupigwa chini.

Naomba nieleweke pia nilisema hata jambo la kutambulishwa Iryn na mtoto lisubiri kwanza, sijasema wasipelekwe kabisa Kwa wazazi. Mtoto/watoto lazima wajulikane lakini sio Kwa wakati huu.

Kila maamuzi tunayofanya kwenye maisha, yanagharana zake, ziwe chanya au hasi lakini Yana athiri Kwa namna Moja au nyingine maisha yetu.
Kabisa mkuu. Mimi nasema wasipelekwe kabisa hata kwa wazazi. Uzuri Iryn ni muelewa. Hili swala libaki siri hivi hivi liendelee kudumu katika hali ya hii ya usiri
 
Mzee Kwa uzoefu wetu wengine sio kinadharia nashauri amtambulishe kwao Example kwake ni Mzee Pama situation ni the same Kuna mambo haya kwepeki mama j anaweza subiri ila sio Kwa wazazi wake
Kumtambulisha saa hizi ni kuhatarisha mahusiano yake na mkewe. Huwezi kulinganisha umri wa mzee Pama na mkewe na umri wa Inside na mkewe. Kuna mambo mawili yanaweza kutokea kwa umri huo. Mwanamke anaweza kuchana na ndoa au mwanamke anaweza kukubariana kwa nje ili mradi tu ipite,lakini moyoni akawa sio yule wa siku zote.

Hata mapenzi hapo yatakuwa yamekwisha kimoja kwa inside. Atabaki tu hapo ksbb tu yupo kwenye ndoa. Pili anaweza kuweka masharti aache kazi pia asionane kabisa na Iryn.

Aifanye tu iwe siri kama ilivyo mpaka hapo baadae. Umri wa Pama wameshaona mengi,ni rahisi kusamehe,lakini sio umri wa Inside.
 
Habari mkuu,
Kwanza kabisa hongera kwa namna ulivyotuburudisha na kutufunza mambo mengi kuhusu maisha. Hasa, jinsi ya kutengeneza connections na kuziona fursa.

Pili, ninaomba kupata maoni yako kuhusu sehemu ya kununua Ardhi ya kuwekeza kwa hapo baadae ndani ya mkoa wa Dodoma
1. Nzuguni
2. Msalato
3. Chahwa
4. Chamwino
5. Mahomanyika
6. Ntyuka

N.B Mtu yeyote mwenye details za kutosha kuhusu fursa za Ardhi ndani ya mkoa wa Dodoma hasa yale maeneo mapya yanayokuwa kwa kasi, usisite kushare nasi.
Ahsanteni
Nzugu Yes, Chamwino Yes, Ntyuka sipapend, ila kwa kuanzia nzuguni, ihumwa, mtumba huko ni pazuri sanaa maana ndio ulipo mji wa Serikal na maofisi yote ya kimataifa ukiangalia ramani, nitakusaidia mtu wa ardh umcheck akusaidie, na kama uko Dodoma unaweza kufika ofcn kwake utapata control namba nadhani unaweza lipia for 90 days ila huyo anaweza pia kukusaidia kwa ushauri pia
 
Huu msala nitausovu, 2033 nitakuwa na majibu tuombe uzima. [emoji120]
Mwambie Dada yako mkubwa siri yako, utakuja kunishukuru, tena umtambulishe kwa Irene utanielewa tuu maana yangu, wanajua kutetea sana hapo baadae lakn huwa faraja kwa wifi zao, yule dada yako Muhindi mtambule awajue shangazi zake,. Achana na habari za mwaka 2033 kwani una MKATABA NA MUNGU?? Ongea vzr na dada yako, na ikiwezekana awe anakwenda kumsalimia huko sauziafrika.

Sijui kama unanielewa lakni wewe Baba Ariana?
 
Mwanaume una njaa kali, huna pride, u are cheap and easy japo stori ya uongo ila inakera
 
HV hi story haijaisha jmn au Kuna muendelezo mnk naona iko live kila wakt

Any update mr insider man
 
Pia kuna section moja alisema alikutana na mdada mmoja mzuri sana bahati mbaya hakuchukua namba. Yule dada akaj kurudi pale akamuuluzua Insiderma kwa muhudumu na muhudumu akaja akamwambia Insiderman ambaye aliamua kumuachia namba muhudumu ili aje ampatie huyo dada ( Sikumbuki kama ni kidimbwi, Samaki Samaki au wapi).

Hapa napo kwa namna walivyoivana na huyo dada siku ya kwanza tu kukutana nahisi kuna story nzuri napi! Basi tu INSIDER MAN
Coco beach kwenye mihogo
 
Kwanza hii story nimetumia mwez kuimaliza ✍️✍️🙏
Pili nimejfunza mambo lukuki.. Kama kijana nimejfunza kuhandle madem pia nimejfunza mamb mengine yanayohusu tamaaa

Mambo ya kua mvumilivu
Kuwa mkwel na kuheshm vtu hata kama ni vdogo
Namengne meng ciwez kuandka yote
 

Attachments

  • FB_IMG_16995958208479932.jpg
    FB_IMG_16995958208479932.jpg
    58.2 KB · Views: 36
Teh nilitaka nifoke episode ya mwisho siioni kumbe bidhaa ilitoka kitambo

😇😇
Tusubirie
Nilivyompata mrembo wa ajabu nikiwa masomoni marekani😃
 
Mwambie Dada yako mkubwa siri yako, utakuja kunishukuru, tena umtambulishe kwa Irene utanielewa tuu maana yangu, wanajua kutetea sana hapo baadae lakn huwa faraja kwa wifi zao, yule dada yako Muhindi mtambule awajue shangazi zake,. Achana na habari za mwaka 2033 kwani una MKATABA NA MUNGU?? Ongea vzr na dada yako, na ikiwezekana awe anakwenda kumsalimia huko sauziafrika.

Sijui kama unanielewa lakni wewe Baba Ariana?
Kakuelewaa shangazi Ariana
 
Sio kila kitu lazima kusema....
Iryn alijijua ni mchepuko toka mwanzo basi endelea kumficha.
Subiri hata uzeeni huko ndo uje ulipue hilo bomb,
Otherwise kuwa tayari kupoteza mmojawapo, na ukimpoteza mama J hata Irene huwezi kumfaidi sababu hakai bongo na ana mambo yake, utakua unatanga tanga tu mjini Daslam bila stability.
 
Sio kila kitu lazima kusema....
Iryn alijijua ni mchepuko toka mwanzo basi endelea kumficha.
Subiri hata uzeeni huko ndo uje ulipue hilo bomb,
Otherwise kuwa tayari kupoteza mmojawapo, na ukimpoteza mama J hata Irene huwezi kumfaidi sababu hakai bongo na ana mambo yake, utakua unatanga tanga tu mjini Daslam bila stability.
Huu sasa ndo ushauri. Mama J aheshimiwe.
 
Back
Top Bottom