SEASON 02:
CHAPTER 28
βA TRUE STORY BY INSIDER MANβ
PREVIOUS:
Muda huu mama wa2 alitoka nje kibarazani huku mkononi kashika funguo ya gari na alitoa ishara ya kuondoka. Muda huu nilikuwa nahisi kama niko ndotoni, nilikuwa siamini kama ni kweli mimi Insider napelekwa Polisi.
CONTINUE:
Nilikuwa mpole kwakweli sikutaka kuwa mbishi kabisa na nilitii maagizo niliyopewa. Kwa akili ya haraka nilihisi lazima litakuwa suala la Pili wala sio jambo lingine.
Nilianza kuingiwa na wasiwasi pale maana niliona miaka 30 hii hapa inanihusu. Baada ya kuingia kwenye gari tulianza safari ya kwenda kituoni nami nilianza kuongea pale;
MIMI: βMama wa2 mbona unaniitia Police kuna shida gani?β
MAMA WA2: βInsider sikutegemea kama kuna siku utakuja kuniharibia mwanangu, umeshaharibu future ya binti yangu.β
MIMI: βKivipi unasema hivo?.β
MAMA WA2: βSina hamu ya kuongea na wewe tukifika utajua, mshenzi wa tabia. Nadhani humjui baba Pili vizuri miaka 30 inakuhusu.β
ASKARI: βDogo hivi ulikosa mwanamke wa kutembea naye ukaanza kutembea na mwanafunzi?β
Mwingine akadakia;
βMalaya wote wale wa Riverside na Sinza ulishindwa kuwaona na kukimbilia miaka 30?β
MIMI: βMimi siwezi kufanya kitu kama hicho katika maisha yangu, kwanza nina mke na mtoto hata mama wawili anafahamu fika kuwa siwezi fanya ujinga kama huo.β
ASKARI: βWote tunao wadaka huwa wanajitetea kama wewe.β
Sikutaka kuendelea na maongezi maana nilikuwa nimesha changanyikiwa tayari.
Siwezi kwenda deep kwenye hili suala, kwa ufupi ni kwamba;
Pili alianza kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi mwenzake wa shule nyingine na ilikuwaje mpaka wanakutana?. Kwa siku za jumapili mara nyingi huwa wanatoka kwenda kanisani, beach kutembea au wanakuwa na zile joint events mbalimbali ambazo zinawakutanisha na shule mbalimbali.
Kutokana na hayo matukio walikutana na dogo, kisha wakaanza mahusiano ya kimapenzi, kila wakitoka wanakutana sometimes na kufanya yao. Walijenga mazoea kwa muda mrefu mpaka kupelekea Pili kupata mimba.
Baada ya kugundua ni mjamzito alichukua maamuzi ya kuitoa kwa siri kwa kutumia MISO, hatujui nani alimshauri kwa hili jambo. Baadae alianza kusumbuliwa na maumivu makali ya tumbo na kuvuja damu nyingi sana ambayo ilipelekewa kuzidiwa na kuwaishwa moja ya hospital ya karibu kwa matibabu.
Tukio lilitokea ijumaa jioni na mama wawili baada ya kupokea hizi taarifa ilibidi aende huko, na asubuhi alimleta mjini kuendelea na matibabu pale Rabininsia. Hili jambo lilimuumiza sana na alijihapia kumtia adabu mwanaume ambaye anahusika kwa namna moja ama nyingine.
Baada ya Pili kurudi kwenye hali yake ya kawaida ilibidi wamuulize nani anahusika?. Lakini aligoma kumtaja mhusika na baada ya kumbana sana na kuchunguza simu yake ikaonekana mimi ndo ninae mtumia sana hela.
Sasa kutokana na Pili kugoma kumtaja mhusika na mimi kuonekana ndo nilikuwa natuma pesa, moja kwa moja nikaonekana ndo mhusika wa mimba, kisha taratibu zingine kuendelea za kunipata.
Baada ya kufika kituoni niliandika maelezo yangu vizuri kabisa na kwa ustadi wa hali ya juu sikutaka kujichanganya. Kwa upande wangu ni kama nilikuwa nimeharibika kisaikolojia, bado nilikuwa siamini niko Polisi.
Niliomba kutoa taarifa kwa ndugu zangu wa karibu, wakaniruhusu. Niliwaza nimpigie nani? Nikapata wazo nimpigie simu Ghati na Dullah niliona ndio watu sahihi wa kuwaeleza hili jambo, wakanielewa na kunisaidia.
Baada ya kufanya nao maongezi, Dullah ndo alikuwa wakwanza kufika pale kituoni na baadae Ghati alifika na nikawaambia jambo linaloendelea. Kutokana na uzito wa kesi suala la Dhamana kwangu lilikuwa gumu, hivyo ikabidi atafutwe Wakili wa kunisaidia.
Siku ilipita bila mafanikio muda nao ulikuwa umekwenda sana na kesho yake jumapili, Ghati alitafuta wakili mzuri wa kutusaidia kupata Dhamana na pia walifanya kuomba kuonana na Pili. Kitu kingine kilichonisaidia sikufuta zile chats zangu na Pili, zote zilikuwepo.
Baada ya kukaa na Pili walimuomba sana afunguke ukweli ili kuninusuru mimi na walimwambia ukweli kwamba Uncle Insider atafungwa jela miaka 30 kama hutaki kumtaja mhusika.
Pili, alikubali kumtaja mhusika ambaye ndo huyo dogo ambaye anasoma shule huko Bagamoyo. Ikabidi utaratibu wa kwenda huko uanze haraka ili haki yangu ipatikane.
Dogo baada ya kubanwa sana alikubali ni kweli wapo kwenye mahusiano na huwa wanafanya mapenzi mara kwa mara pindi wanapokutana. Baada ya mhusika kukubali taratibu zingine ziliendelea ikiwa pamoja na kuwatafuta wazazi wake.
Usiku ndo nilifanikiwa kutoka kwa kupewa Dhamana yenye masharti ya kutoa ushirikiano pindi nitakapohitajika na Polisi katika muda wote wa hii kesi. Sikuamini kama ni kweli natoka rumande, kule sio kuzuri jamani muwe mnakusikia tu! na usiombe ukaingia.
Ghati alinipambania sana yule dada mpaka askari walimwambia yani wewe jamaa yako katembea na mwanafunzi bado unamoyo wa kumsadia? Hata wao walishangaa sana ni wanawake wachache wenye moyo kama wake.
Kesi iliishaje? Umri wa mhusika βDogoβ ulikuwa ni mdogo miaka 17 na umri wa Pili ni miaka 18. Dogo yuko form 5 na Pili yuko form 6, kesi ikakosa uzito na jambo lingine, Pili alitishia kujiua kama dogo atakamatwa.
Kesi iliisha kwa familia zote mbili kukutana na kulimaliza hili suala pamoja na kumlipa mama wa2 fidia na gharama zote. Baada ya week kupita, Pili alirudi shule kuendelea na masomo yake na matokeo ya NECTA alipata ufaulu wa Divion 1 ya 4, kwasasa yuko India anasomea udaktari.
Tulipokuwa njiani, nilimshukuru Ghati kwa msaada wake mkubwa ulionifanya nitoke rumande, bila kumsahau ndugu yangu Dullah maana nilikuwa naiona miaka 30 bila kupenda. Niliwaomba wanipeleke nyumbani ili nipumzike, lakini Ghati alisema kuwa hilo haliwezekani, akisisitiza twende kwake. Wakati huohuo, Dullah aliniomba tushuke kwenye gari ili tuzungumze.
DULLAH: βKaka huyu dada ni mpenzi wako?β
MIMI: βNo! ni mshikaji wangu.β
DULLAH: βWife yuko wapi au hukutaka kumshirikisha?β
Nilimwambia Dullah kinachoendelea na wife kwa ufupi;
βSema wife wako ni kipengele sana, kazi unayo. Pole sana ndugu yangu umekuwa na matatizo back to back, nakushauri ondoka Dar mapema kajichimbie sehemu.β
MIMI: βNdo mipango yangu kwasasa kaka, kwa haya mambo yanayoendelea sinabudi kuondoka Dar.β
DULLAH: βUyo dada kama vipi ondoka naye tu maana amejitoa sana kwako mpaka mimi nikahisi ni mtu wako. Mwanamke kama huyu anayejitoa kwenye matatizo yako ni asset kaka, nakushauri nenda kwake kama wife hayupo home.β
MIMI: βAhsante sana Dullah kwa msaada wako, umeshakuwa ndugu kwangu tena muhimu.β
DULLAH: βUsiwaze kaka wewe ni damu yangu, chukua 200k hii itakusaidia kimtindo. Najua unahela kuzidi mimi, naomba upokee nimetoa kutoka moyoni.β
MIMI: βDaah! Nashukuru sana Senior msalimie na wife.β
DULLAH: βZitafika! ngoja nichukue bodaboda niwahi kuonana naye ananisubiri.β
Tuliagana pale na Dullah, kisha nikarudi ndani ya gari na nikamwambia Ghati tuondoke, naye aliishia kufurahi kusikia naenda kulala kwake.
Kipindi chote ambacho tuko njiani nilikuwa kwenye mawazo sana, niliwaza hivi ingetokea Pili alikufa ingekuwaje? Si ningeenda Jela mimi?. Niliwaza sana nikaona kuna haja ya kumrudia Mungu huenda haya matatizo yanatokea ni kama alarm ya kunikumbusha njia nazopita sio sahihi.
Pia niliangalia watu waliokuwa wamenitafuta kwenye simu. Nilikuta missed calls nyingi sana akiwemo mama yangu, Hilda na wengine wengi sana.
Mtu ambaye nilimpigia ni Hilda tu na habari nzuri alisema baada ya kuona sipokei simu aliamua kudraft mkataba, hivyo kesho ataanza kwenda kwa wateja kuchukua madeni.
Nilimpongeza sana kwa maamuzi aliyoyachukua maana alionesha kuanza kukomaa hasa kwenye kufanya maamuzi. Kuhusu malipo ya mzigo tulikubaliana pindi nitakapokuwa na figure halisi za gharama zote nitamrudia.
Baada ya kuwasili pamoja na Ghati, tulimkuta mtoto wake akiwa sebleni akicheza. Ni mvulana mwenye umri wa miaka mitatu, mkubwa zaidi ya Junior. Nilijikuta nikikumbuka maneno ya Ghati kwamba mtoto wake hana baba, lakini mtoto mwenyewe alikuwa hana habari, akicheza kwa furaha. Nilimbeba juu na kuanza kucheza naye pale seblen na aliendelea kufurahi, alionesha kuwa mjanja sana.
βNdugu wa huyu mtoto huwa mnawasiliana? Na vipi kuhusu matunzo ya mtoto?β
βTunawasiliana kwakweli huwa wanapiga simu na kuhusu matunzo huwa wanatuma nisiwe muongo, japo huwa siwapigii kuwakumbusha ila wanajitahidi.β
βHabari njema kama wanamtunza.β
βNgoja nikakuandalie maji ya kuoga upunguze uchovu kidogo.β
βSawa ahsante.β
Mimi niliendelea kucheza na dogo pale na baada ya dakika 10 Ghati alitoka amejifunga khanga kiunoni na alinikaribisha nikaoge. Niliinuka kwenda kuoga, nilishangaa sana kuona akinipeleka chumbani kwake maana nilitegemea ingekuwa bafu ya public.
Alihisi woga wangu na alinitoa wasiwasi kwamba hakuna mtu anayeishi naye ndani hivyo niwe huru na nijiachie. Licha ya yote bado sikutaka kumuamini kabisa, wanasema mwanamke haaminiki.
Chumba chake kilikuwa kimepangwa vizuri sana na kilionekana kuvutia. Niliingia bafuni kuoga, na baada ya dakika 20 alikuja tena kunikaribisha kwa chakula cha jioni. Baada ya kumaliza dinner, nilienda moja kwa moja kulala, kwani nilikuwa na usingizi mzito sana, hasa ukizingatia kwamba sikulala kabisa nilipokuwa rumande.
Asubuhi niliamshwa kwa ajili ya kupata kifungua kinywa. Nilibaki nikiwa na mshangao, nikijiuliza mbona kumekucha haraka sana? Ghati alikuwa ameketi kando yangu na aliulizia maendeleo yangu, kisha akasema, 'Twende tukanywe chai.' Aliongea kwa sauti ya upole, iliyojaa heshima na adabu, hadi nikajisemea, 'Kama ni hivi, basi single mothers hawana upinzani.β
Baada ya kupata breakfast nilianza kupitia mails za ofisi kupitia laptop ya Ghati na niliweza kuzipata invoice ya mzigo na risiti za kufanya malipo. Kwa hesabu za haraka kutokana na thamani ya mzigo/Invoice ushuru wa forodha ungekuwa ni 75M, hapo ni nje na gharama za agent.
Tulikuwa na kiasi cha shilingi milioni 34 tu kama cash, hali ambayo ilifanya mambo kuwa magumu sana. Nilikaa nikitafakari kwa muda mrefu hatua gani ya kuchukua, lakini sikupata jibu sahihi, maana siwezi kukopa benki bila uwepo wa mmoja wa wahusika.
Kuhusu salio la cash, wafanyakazi walikuwa bado hawajalipwa mishahara na mwezi wa pili tayari umeshapita. Pia, bajeti ya gharama zingine za ofisi za kila mwezi ilikuwa haijatengwa. Hivyo, ilibidi nifanye juhudi kubwa kutafakari na kutatua changamoto hii.
Nilipitia kipindi kigumu sana, kwani lilikuwa jambo zito kwangu, hasa kuhusiana na jinsi ya kupata kiasi kikubwa cha pesa. Niliwapigia simu Hilda na Lucy kuwaarifu juu ya haja ya kukutana ili tuzungumze kwa kina zaidi kuhusu suala hili.
Mipango yangu ilikuwa ni kuhakikisha ninaiacha kampuni mikononi salama, na kila kitu kikiwa kimewekwa sawa. Kwangu, hili lilikuwa jaribio kubwa na la mwisho, kwani nikishindwa, kuna hatari ya kampuni kuporomoka.
Niliamua kufunga simu ili kutuliza kwanza akili yangu na baada ya hapo nilirudi tena kulala. Hii siku iliisha nikiwa bado kwa Ghati na usiku nilipanga kesho nitaonana na akina Hilda.
*****
Kesho yake asubuhi tulienda kwa mama wa2 kuchukua gari na baada ya kuwasili pale kwake tulikaribishwa ndani seblen, lakini sisi tulisema tunaishia nje.
Mama wa2 alipewa taarifa ya ujio wetu na alitoka nje haraka sana na yeye aliomba sana tuingie ndani maana alisema Pili anataka kuniona. Baada ya kusikia Pili, ilibidi tuingie ndani ili niweze kumsalimia na kumjulia hali yake.
Maendeleo ya Pili yalikuwa ni mazuri kwa ujumla, hata baada ya kuniona alifurahi sana nami nilimsihi akirudi shule akasome kwa bidii na nilimpa ahadi ya kumnunulia simu nzuri, pindi akimaliza shule.
Kwa upande wake alinikumbusha kuhusu mahafali yao na nilimpa ahadi nitakuwepo hiyo siku. Pia, aliniomba sana nimsamehe mama yake kwa yote aliyonifanyia, nami nilimwambia nimesamehe tayari, kisha nikatoka nje kuongea na mama yake.
MAMA WA2: βNisamehe sana Insider, mpaka naona aibu kukuangalia.β
MIMI: βNi kweli kuhupaswa kunifanyia vile, lakini mimi naelewa uchungu wa mzazi ndomana ukafanya maamuzi yale. Mimi nimekusamehe kwa hili, ila umenikosea sana hivi ningeenda jela ingekuwaje?β
MAMA WA2: βNaamini haki haiwezi kumuacha mtu.β
MIMI: βSi kweli, kuna wengi wamefungwa kwa kusingiziwa makosa ambayo hawajafanya. Ni kweli nilikosea sana kumtumia hela, lakini chats zetu zinajieleza wazi, ukizingatia hata mimi haya maisha niliyapitia.β
MAMA WA2: βNi kweli Insider naomba haya tuache tuanze mapya.β
MIMI: βNahitajika kutoa ushirikiano pindi Polisi wakinihitaji huoni ratiba zangu zitakuwa zinaharibika? Hata kusafiri sitoweza.β
MAMA WA2: βKesi tumeimaliza jana, na sasa uko huru. Tuliona kwamba ni mambo ya watoto, na pia kesi ilikosa mashiko. Zaidi ya hayo, Pili alitishia kujiua.β
MIMI: βUmefanya jambo la busara hapa kidogo nina amani.β
MAMA WA2: βKuna Pesa mzazi wa mhusika aliitoa kwaajili yako kwa gharama ulizoingia naomba nikupatie.β
Ile nataka kumwambia aache tu asijali, akawa ameshaondoka tayari na muda huu Ghati alitoka pale nje;
GHATI: βVipi si tayari tunaondoka?β
MIMI: βTunaondoka soon mummy.β
Muda huu mama wa2 alitoka na Pesa zikiwa kwenye bahasha na akanipa pale, lakini niligoma kuzipokea;
GHATI: βWhat? Yaani kuzalilishwa kote kule bado hutaki kupokea hela are you serious?β
MAMA WA2: βHizo pesa zimetoka kwa mzazi wa mtuhumiwa, na amesema nimpe hataki eti.β
GHATI: βNaziomba hizo Pesa dada.β Mama wawili akamkabidhi Ghati.
Kwa upande wangu niliamua kumsamehe mama wawili, niliwaza huenda alifanya kwa hasira, hasa ukizingatia ni mtoto wake wa kwanza. Lakini bado niliona hakupaswa kunifanyia vile kama mtu wake wa karibu, alipaswa kukaa na mimi tukazungumza badala ya kufanya maamuzi ya kunidhalilisha.
Hatutaka kuendelea kupoteza muda pale na tuliwaaga, kisha tukaondoka maeneo haya. Tukiwa njiani Ghati alifungua bahasha na kutoa zile Pesa jumla zilikuwa ni million 3 na aliendelea kunilaumu kwanini nilitaka kuzikataa?.
Mimi na Ghati tuliachana pale Kibo Complex, yeye alikuwa anarudi kwake, nami nilikuwa nakwenda home kuendelea na ratiba zangu. Nilimshukuru sana kwa kunisaidia mpaka natoka na nilimrudishia gharama zake zote alizokuwa amezitumia.
Mchana nilifanya mawasiliano na sister kuhusu jambo la wife. Nilikuwa nina jeuri ya kumwambia kuhusu kinachoendelea sababu anajua mahusiano yangu na Iryn. Nilimpa mkasa mzima wa wife kukagua simu yangu na kuziona picha za Iryn mpaka kuondoka.
Sister kwa upande wake aliomba azione picha
ambazo mama J alizifuma nami nilimtumia na baada ya dakika 2 alinipigia tena;
SISTER: βMdogo wangu unazingua sana, kikao cha mwisho nadhani unakumbuka ahadi uliyoitoa.β
MIMI: βNakumbuka, lakini ni bahati mbaya sana alinizidi ujanja na sikutegemea angeweza kuziona maana nilizificha sana ujue.β
SISTER: βBro! Tatizo lako unashindwa kuwa makini na simu, hapa ndo unakwama sana, nashindwa kujua ni mazoea au unapuuzia tu makusudi. Miaka yote ya ugomvi wako na mama J ni simu, ukiweza kuilinda simu yako ugomvi wenu utaisha.β
MIMI: βDada hilo nakubali na nilikuwa makini sana hapa katikati ndomana unaona hakukuwa na tatizo. Mpaka sasa nashindwa elewa amezionaje picha wakati nilizihide vizuri kabisa?. Si unakumbuka nilikwambia kuhusu zile chats na dada yake? Dada yake yuko nyuma ya hili.β
SISTER: βUna maana gani, dada yake how?β
MIMI: βMama J ana ushamba wa kutumia iphone, nahisi dada yake alimpa mbinu na kufanikiwa kuziona.β
SISTER: βPasscode alizijuaje?β
MIMI: βAnazifahamu, sikubadilisha.β
SISTER: βYouβre so stupid. Kwanza kitendo cha kuwa na picha za malaya zako kwenye simu ni ulimbukeni, mwanaume anayejitambua hawezi kufanya ujinga kama huu. Kumbuka ulisema utazifuta picha zake zote sasa nini kilikusibu ukasahau?β
MIMI: βSiku tuliyorudi kutoka South ndo ananipa hizi taarifa, inaonekana alifahamu toka mapema akawa anasubiri nirudi.β
SISTER: βMpaka anaondoka wewe ulikuwa wapi? Ina maana ulishindwa kuongea naye myamalize?β
MIMI: βNafikiri unamjua vizuri wifi yako kuwa ana hasira?ndomana huwa namuacha kwanza. Asubuhi nilitoka kurudi jioni, nakuta hayupo kaondoka tayari kwenda kwao.β
SISTER: βUnawezaje kuondoka huku hakuna maelewano na mke wako? Unamuonesha dharau waziwazi sio sawa kabisa. You donβt care about her?.β
MIMI: βI do care, tuachane na haya naomba nisaidie hili kama sister.β
SISTER: βHizo picha hazina ushahidi kama mpo kwenye mahusiano, lakini kitendo cha kupiga picha na mwanamke akiwa amevaa bikini na mnaogelea swimming pamoja ni ishara tosha mpo kwenye mahusiano.β
MIMI: βNakusikiliza dada yangu do something nataka navyokwenda Dodoma huu msala uwe umekwisha.β
SISTER: βWifi yangu hajanicheki bado..β
Nilimkatisha;
MIMI: βAtakuwa amemwambia mama maana toka jumamosi mama ananipigia simu na sijampokelea.β
SISTER: βSidhani kama mama anajua angekuwa ameniambia tayari kuhusu hili. Kingine wifi huwa ananza kuniambia mimi kama kuna tatizo, mpaka sasa hakuna aliyepewa taarifa kwa kinachoendelea.β
MIMI: βKwahiyo unasubiri mpaka akuambie?β
SISTER: βKwanini usimfuate kwenye biashara yake ili myamalize?.β
MIMI: βBad idea humjui vizuri yule mchaga, kwasasa hawezi kuongea chochote na mimi wala kunisikiliza.β
SISTER: βOnesha jitihada sio mbaya anaweza kubadili maamuzi yake. Wewe jaribu kufanya hivi mfate ofisini kwake.β
MIMI: βDada naomba nisaidie kwanza kuongea naye ili nijue yuko kwenye mudi gani, hayo yaliyobaki mimi nitaweza kuyafanya.β
SISTER: βOkay! badae nitampigia simu kujifanya namsalimia, akinifungukia kuhusu hili hapa sasa nitaongea naye vizuri na yataisha.β
MIMI: βNakushukuru dada yangu nakuamini sana kwenye hii sector. Ukinifanikishia hili nitakupa zawadi ya Iphone 15 September.β
SISTER: βKwahiyo unanipa rushwa?. Anyway sasa nisikilize kwa makini, kuanzia leo kaa mbali na huyo Iryn, atakuharibia maisha yako.β
MIMI: βNdomana nataka kwenda Dodoma kufanya mambo yangu na nina mpango wa kusajili line mpya nisipatikane kabisa.β
SISTER: βGood! Hata hio kampuni ukiona imekaa kwenye track achana nayo au uwe na mawasiliano ya siri sana na unayemuachia. Jambo jingine hakikisha unahama hapo nyumbani tafuta sehemu nyingine ya kuishi.β
MIMI: βSawa.β
Baada ya kuongea na sister kuhusu suala la kutafuta sehemu nyingine ya kuishi niliona ni wazo zuri sana. Nilianza kujiuliza pale nihamie wapi? Huku nakosa majibu.
β
Nihamie Goba? Hapana kule watu wanalalamika sana maji ni shida na majambazi. Mbweni na Boko kule kumekaa kushoto halafu ni mbali. Kigamboni? Daah! shida ni kuvuka yale maji na pantoni halitabiriki. Makongo kuzuri ila sijawahi kupakubali kabisa, Sasa nihamie wapi?β
Nilifikiri sana nikapata option mbili kati ya Mikocheni na Mbezi Beach. Suala lingine sikutaka wife awe mbali na eneo la biashara yake, chuo na mtoto. Baada ya kujifikiria sana nikaona niendelee kubaki hukuhuku Mbezi beach, ni eneo ambalo limetulia na zuri kwa familia.
Nilifanya mawasiliano na Dalali na kumpa taarifa anitafutie nyumba ya kuishi angalau yenye vyumba vitatu na anirudie pindi akiwa na nyumba za kueleweka.
Jioni nilikwenda kuonana na kina Lucy kwaajili ya mazungumzo kuhusu kupata pesa ya kulipia ushuru wa forodha. Nilianza kwa kumpitia Lucy kisha tuakendelea na safari yetu ya kwenda Masaki, tulimpa taarifa Hilda tukutane Bistro-Barometer.
Tulishauriana ni namna gani tutapata pesa maana jambo lilikuwa ni zito na kila mtu alikuna kichwa;
MIMI: βKwa hesabu za haraka inahitajika si chini ya 75M, cash tuliyonayo inatakiwa tulipie expenses unaona changamoto?β
LUCY: βInsider wewe huna mtu wa kumkopa atusaidie? Naamini mzigo ukifika ndani ya week hio pesa tunaipata.β
Hili jambo lilikuwa chini ya uwezo wangu lakini sikutaka kuhangaika nalo sababu mimi nataka kuacha kazi, ndomana sikutaka kuhangaika sana;
MIMI: βSina wa kumkopa hizo pesa ni nyingi halafu nani akupe hizo pesa? Sehemu sahihi ni bank ila changamoto hatuna Director.β
LUCY: βHivi hatuwezi kwenda ofisini kwa mama kumuulizia?.β
HILDA: βMama hayupo na hapatikani hata Sumaiya analalamika kwa hili.β
HILDA: βSasa guys mimi nina wazo, lakini sijui mnalionaje kwa upande wenu, haya maji tumeyavulia nguo lazima tuyaoge.β
LUCY: βOngea mpenzi tunakusikiliza.β
HILDA: βMnaonaje tukienda kuongea na agent watupe mkopo tufanye malipo? Mizigo yetu yote wanatoa wao na sisi ni wateja wao naamini wataweza kutusaidia.β
LUCY: βKama inakuja hivi na kutoka watakubali?β
MIMI: βAnachosema Hilda kama kina make sense, hii kampuni tunafanya nao sana kazi. Tumewapa wateja wapya ambao wanafanya nao kazi hata mama sometimes anafanya nao kazi kwa mizigo ya kazini kwake, tuongee nao.β
LUCY: βMimi naona wazo la Hilda ni zuri sana twende nalo.β
MIMI: βKesho tutakwenda wote ofisini kwao kuongea nao.β
LUCY: βGuys ngoja niende washroom nakuja.β
Mimi na Hilda tuliendelea kupiga story;
HILDA: βBest yangu Asmah anakula bata kwenye ofisi mpya hana hata stress anazidi kunenepa.β
MIMI: βAsmah yuko vizuri sana kwenye usimamizi, lakini hata wewe naona unajitahidi sana, unanipa moyo kampuni ipo sehemu salama.β
HILDA: βNiliipenda sana chemistry yako na Asmah pale ofisini na jinsi mnavyoishi mpaka sasa kuna mengi najifunza kwenu.β
MIMI: βMhh! Unajifunza nini?β
HILDA: βOfisini wewe na Asmah mnakubalika sana mnapendwa hata watu bado wanaamini Asmah katolewa na Iryn kwaajili yako.β
MIMI: βOngea ukweli usinidanganye, unaamini mimi niko kwenye mahusiano na Asmah?β
HILDA: βKipindi nafika nilihisi hivo lakini baada ya kukaa na Asmah niligundua hampo but ni washikaji.β
MIMI: βNa pale ofisini wanahisi nini!?β
Muda huu Lucy alirudi na akaharibu maongezi yetu;
LUCY: βGuys kuna jipya?.β
MIMI: βYes! Kesho msisahau vitambulisho vyenu.β
Tuliagana pale, Hilda alikuwa anarudi ofisini, mimi na Lucy tukaondoka kwenda Mikocheni. Nilianza kumdrop Lucy na nikaendelea na safari ya kuelekea home.
Baada ya kurudi home nilifanya mawasilino na agent, nikampa taarifa ya kuonana naye kwa kesho asubuhi, naye alinambia tuoanane kuanzia saa 4 asubuhi.
Kwa upande mwingine Dalali alinipigia simu kunipa taarifa kwamba amepata nyumba 3 za kuangalia, kwahiyo ikiwezekana kesho mapema tukaziangalie maana zitachukuliwa, tukakubaliana iwe ratiba ya kesho.
****
Asubuhi na mapema tulifanya mawasiliano tukutane kwenda Posta kwaajili ya kuonana na wakala. Nilianza kukutana na Lucy pale Mwenge kisha tukaelekea Morocco kumpitia Hilda.
Baada ya kuwasili ofisini kwa agent alitukaribisha vizuri na alishangaa sana kuona kamati nzima iko pale. Kutokana na uzito wa jambo ilibidi amshirikishe manager wake kisha tukaanza mazungumzo.
Niliwaambia dhumuni la sisi kuja ofisini kwake ni kupata msaada wa kupata mkopo kwaajili ya kufanya clearing. Niliwambia hali ya kampuni kwasasa, niliwadanganya kwamba mama yuko field na Iryn yuko likizo ndomana hawapatikani.
Tuliomba watupe mkopo kwaajili ya malipo ya forodha na ndani ya mwezi mmoja tutakuwa tumewarejeshea hata kwa riba. Niliamini ndani ya mwezi wahusika watakuwa wamepatikana hata wasipopatikana bado pesa ya kuwalipa ingepatikana.
Kutokana na sisi kuwa wateja wao kwa muda mrefu na bado huwa tunawapa wateja wapya manager alikubali ombi letu na akasema atatusaidia bila ya riba maana sisi ni moja ya wateja wao muhimu.
Hatukuweza kuamini kwamba meneja alikubali kutusaidia tena bila riba. Tulimshukuru sana na bila kuchelewa tuliandikishana mkataba ambao ulitiwa sahihi na kila mmoja wetu. Katika mkataba, hatukuandika kiasi kamili kwa sababu kodi halisi huweza kujulikana tu baada ya mzigo kufika na kukaguliwa. Niliwaambia kwamba, ikiwa sitakuwepo, Lucy na Hilda watakuja kumalizia taratibu.
Kabla ya kuondoka, tulipiga picha ya pamoja katika ofisi, na picha hiyo hadi sasa ipo kwenye ukurasa wa Instagram wa kampuni hii. Dada alitusindikiza, nami nilimshukuru kwa msaada wake na kumwahidi kumpa donge nono.
Furaha zetu ziliongezeka sana kutokana na hili jambo kufanikiwa kwa sababu ilikuwa miujiza. Niliwaambia akina Lucy kwamba mzigo ukifika, watatoa 1/4 kwa ajili ya kuuza jumla kwa wateja wetu, na 3/4 itabaki kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Tulikubalina na Hilda tuendelee kuwapitia wateja wetu wa Posta ili tuwakumbushie madeni na kuchukua oder mpya. Lucy aliaga anaondoka kwenda ofisini ili amuwahi mteja wake.
Mimi na Hilda tulifanya hii mizunguko na baada ya lisaa tulikuwa tumemaliza na matokeo yalikuwa mazuri, hivyo tukaamua kuondoka Posta.
Kipindi tuko njiani Hilda alikuwa akinipongeza kwa maamuzi magumu niliyachukua kwaajili ya kuinusuru kampuni, nami nilimsihi sana kuisimamia kampuni vizuri na asithubutu kuingiwa na tamaa.
Nilimpa ride mpaka masaki na nilimuaga kesho nitaondoka kwenda Dodoma. Kwa upande wake aliishia kusikitika na aliomba nishuke kwenye gari anikumbatie.
Kwa upande mwingine Dalali alikuwa akipiga sana simu maana nilimpa ahadi ya kuonana naye leo. Baada ya kuachana na Hilda nilianza safari ya kwenda Mbezi Beach na tulikubaliana tukitane Rainbow ili tuanze zoezi.
Ndani ya nusu saa, nilifika eneo la tukio ambapo tulikutana maeneo ya sheli ya GBP akiwa na mwenzake. Baada ya hapo tulienda kuzingalia nyumba alizokuwa ameziandaa kwaajili yangu.
Baada ya kuzunguka na kuziangalia nyumba zote niliipenda nyumba ambayo ipo karibu na kota za BOT maana ilikuwa sehemu nzuri na salama kwaajili ya familia. Sikutaka kupoteza muda hivyo nilifanya malipo kabisa na nilitafuta mtu afanye usafi ili nihamie.
Baada ya hapo nilipitia kwa wakala kusajili line mpya ya simu ya kutumia Dodoma. Pia, muda huu mama wawili alinipigia simu, lakini sikupokea simu zake.
Baada ya kurudi home nilimpigia simu sister kumpa taarifa ya kuhama na kumuuliza mrejesho kama alifanikiwa kuongea na mama J, lakini alisema wife hajamfungukia bado anatafuta gia ya kumuingia vizuri.
Nilimpa taarifa kuhusu safari yangu ya Dodoma na alitakia kila la kheri kwenye mapambano yangu mapya na alisema niwe namtafuta kwa mawasiliano zaidi.
Usiku nilimpigia simu wife kumjulia hali na kumpa taarifa za kuhamia makazi mapya, lakini hakupokea simu zangu na niliishia kumpigia simu Elena na kumuuliza maendeleo yao akasema wako salama.
Kesho yake asubuhi na mapema sana nilianza kupanga nguo zangu kwenye bag kwaajili ya safari na baada ya kumaliza nilianza maandalizi ya kuhama. Nilifanya kuwaaga majirani akiwemo mama Joana, aliishia kulalamika kuwa naondoka na mme wake, Junior, nami nilimwambia tumehamia barabara ya chini na nilimkaribisha.
Nilikuwa na watu wa kunisadia kwahiyo jambo la kuhama lilifanikiwa kwa haraka sana na nilihakikisha kila kitu kinakaa mahala pale kama ilivyokuwa awali. Kufikia saa 10 jioni zoezi la kuhama lilikamilika na kila kitu kilikuwa mahala pake kama zamani.
Kwenye makazi mapya, tulikuwa wapangaji wawili pekee. Ninapenda kuwasalimia majirani mara ninapohamia, hivyo nilikwenda kumsalimia jirani na kumueleza kuhusu ugeni wetu. Sikuishia hapo, bali pia nilienda kutoa taarifa kwa balozi wa mtaa kuhusu ugeni wangu, kwani hii ndiyo desturi yangu.
Saa 12 jioni nilianza safari ya kwenda Dodoma na nilichukua bodaboda wa kunipeleka Magufuli stand. Muda wa jioni mabus huwa yanasumbua hivyo, nilisogea pale darajani kwa Yusuph nikapata private inayokwenda Dodoma.
EPISODE 29
Mkuu umeongea point nzito sana. Mikasa ipo Mikali sana tunaogopa codes.. Matukio ya INSIDER ni ya kawaida kwa Wanaume flani flani hivi...ndio maana tunakufa mapema. Juzi tu tumeamua case moja matata...mtu unawatoto tisa na wanawake wakali mbayaππππππ Shetani atusamehe... Shetani tena