Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 03
CHAPTER 22


“A TRUE STOR BY INSIDER MAN”

CONTINUE:


Tulipokuwa bado tunazungumza, simu yangu ikaanza kuita tena pale kitandani. Mke wangu akaichukua na kunipa. Nilipotazama kwenye screen, nikaona ni Erica anayepiga.

Muda wote huo wife alikuwa amenikazia macho, akifuatilia kila hatua nitakayochukua. Hatimaye akavunja ukimya:

“Baba Junior… kwa nini hupokei hiyo simu?”

Nilihisi hali ya joto ikipanda shingoni. Mama J akaanza kuonyesha dalili za wasiwasi. Ndani ya sekunde chache nilikuwa napanga majibu kumi tofauti kichwani, nikichagua lipi litakaloeleweka kwake.

MIMI: “Huyu dada anafanyia kazi Taasisi X, ndiye aliyenisaidia kubadili baadhi ya taarifa za kampuni. Kuna pesa yake anadai, nimesahau kumtumia.”

Mama J hakuridhika maana aliona ninamdanganya, na alikunja uso kidogo.

WIFE: “Lakini apige muda huu? Haiwezekani Baba J.”

Nikavuta pumzi ndefu.

MIMI: “Mdai hajali muda, anajali pesa yake. Kama unataka, chukua hiyo simu ongea naye mwenyewe ili uridhike.”

Kabla hata hajafanya uamuzi, simu ikakata, lakini haikupita hata dakika simu ikaita tena. Nilimpa simu mikononi mwake bila kusita, kwa sekunde kadhaa aliitazama, kisha akaiweka kwenye meza ya pembeni ya kitanda.

Sikuamini kwa kile kilichotokea, ilikuwa ni kama ndoto naota. Niliwaza haraka kama angeamua kupokea simu ya Erica, sijui mazungumzo yao yangekuwaje. Lakini kwa upande wangu sikuwa na hofu sana sababu Erica tayari alikuwa kwenye mpango wa kuachana naye. Hata kama angezungumza chochote, ningekataa. Na pengine hiyo ingekuwa sababu ya mwisho ya yeye kuniacha kabisa.

Baada ya ukimya mfupi, Mama J akasema tujiandae kwa safari. Tulipaswa kwenda Arusha kumwona dada yangu aliyekuwa amejifungua. Hivyo, nikampigia simu dada Tyna nimpe taarifa njema na pia aanze mchakato wa tiketi mbili.

Asubuhi kulipochomoza, tulijiandaa haraka kwaajili ya safari. Kabla ya kutoka, niliandika email ofisini kuomba udhuru rasmi, sikutaka kufanya makosa tena. Tulitumia Uber kuelekea airport, njiani nikamtumia Iryn ujumbe kumjulisha kuhusu dada yangu kujifungua salama. Dakika chache baadaye akanipigia WhatsApp call, ila sikuweza kupokea sababu Mama J alikuwa pembeni yangu. Nikamtumia ujumbe wa kuomba tuchat, nikamwambia niko na wife tunaelekea Arusha.

Tulichat kwa muda mrefu sana hadi tunafika JNIA na alifurahi sana. Kwa upande wake alisema atakapokuja Tanzania, ataanza kwanza Arusha kabla ya kwenda nyumbani kwetu kuwatambua wazazi wangu. Niliposoma ujumbe huo, nilitabasamu kimyakimya, niliona Iryn yuko spidi sana, kaamua kulivalia njuga hili jambo.

Tulipowasili airport, tukamkuta dada Tyna tayari na tiketi mbili mkononi. Baada ya salamu za haraka, akaanza kuropoka bila kujali mazingira.

TYNA: “Insider mdogo wangu, siku hizi una root nyingi za South Africa. Kuna dili gani huko?”

Bahati nzuri Mama J alikuwa bize akiongea na simu yake, hakusikia. Nikamtupia Tyna jicho kali.

MIMI: “Kwahiyo sasa tumeanza kuchunguzana? Huna confidentiality?”

TYNA: “Juzi nimekuona ukishuka na ndege ya Dodoma. Nakuita husikii, nakupigia hupokei.”

MIMI: “Ni kweli niliona missed calls zako, lakini nilisahau kukurudia. Samahani sana.”

TYNA: “South Africa una agenda zipi?”

Nilihisi mazungumzo yanaelekea pabaya. Kama Mama J angesikia, ingekuwa hadithi nyingine. Haraka nikabadili mazungumzo.

MIMI: “Rafiki yako kapata mtoto wa tatu. Wewe bado hata mmoja huna, una mpango gani?”

Tyna alinyamaza ghafla, uso wake ukabadilika, alinitazama kwa sekunde chache, akakosa cha kusema. Kwa wakati huo Mama J alikuwa amemaliza kuongea na simu yake na kuungana naye mazungumzoni. Nikaona hiyo ndiyo nafasi yangu ya kujitoa kimyakimya, hivyo nikaenda kukaa kwenye benchi.

Muda ule pia tukiwa JNIA, nilipokea simu kutoka kwa mama yangu. Alinipa taarifa kwamba yuko njiani kwa Bus kuelekea Arusha. Nikamwambia kwa upole kuwa niko pamoja na mama Junior, hivyo atatukuta tayari tumeshafika Arusha.

Tulichelewa kuanza safari kutokana na hitilafu ndogo iliyojitokeza, jambo lililotufanya tukae pale airport kwa muda mrefu kuliko tulivyotarajia. Hata hivyo, muda ulipowadia, tuliagana na Tyna, alituambia kuwa kesho yake atakuja Arusha pia, kumuona rafiki yake.

Baada ya kuwasili Arusha, tulichukua taxi iliyotupeleka Sakina, kwenye hospital aliyojifungulia dada yangu. Tulipofika, tulipokelewa na shemeji yangu kwa furaha na bashasha kubwa.

Shemeji alitusaidia kushusha mabegi na kuyaweka kwenye gari lake, kisha tukaelekea sehemu ya kusubiri wagonjwa. Tulikaa pale na mazungumzo ya hapa na pale yakaendelea kwa utulivu. Nilianza kwa kumpongeza kwa baraka ya kupata mtoto wa kike, hasa ukizingatia kwamba tayari walikuwa na watoto wawili wa kiume. Huyu alikuwa wa kwanza wa kike, furaha yake ilionekana wazi machoni.

Shemeji aliendelea kusalimiana na mama J kwa heshima, huku mimi nikiwa na shauku ya kujua ni nani anayemhudumia dada yangu wodini. Aliniambia kuwa mama yake ndiye anayemuhudumia, na kwamba alifika Arusha tangu mwezi uliopita kwa maandalizi ya kujifungua. Nilihisi faraja kusikia kuwa dada yangu yuko mikononi mwa mtu wa karibu na mwenye uzoefu.

Katikati ya mazungumzo, simu yangu ilianza kuita, alikuwa ni Iryn. Nilisogea pembeni kidogo ili kupokea simu yake kwa utulivu. Baada ya salamu za kawaida, alinieleza kuwa ametuma kiasi cha dola 2,000 kwenye akaunti yangu ya USD. Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya wifi yake, na akanisisitiza nihakikishe ninamnunulia zawadi nzuri kwa ajili ya mtoto.

Nilimshukuru kwa moyo wote kwa niaba ya familia, lakini nikamwambia kwa unyenyekevu kwamba hakukuwa na haja ya kutuma kiasi kikubwa vile, maana ningeshughulikia mahitaji yaliyokuwepo. Hata hivyo, alisisitiza kuwa anarejesha fadhila, kwani wifi yake alikuwa mstari wa mbele kumhudumia kwa karibu kipindi alipojifungua.

Baada ya kumaliza mazungumzo, nilibaki nikitafakari. Niliwaza kwenda kufanya shopping ya zawadi kwa ajili ya dada yangu na mtoto, lakini nikahisi huenda vitu vingi tayari atakuwa navyo, na vingine ataletewe na marafiki na ndugu. Mwishowe nikaona ni bora nimkabidhi fedha hizo yeye mwenyewe, ili azitumie kwa namna atakayoona inafaa zaidi kwa mahitaji yake na ya mtoto.

Jioni ile nilifanikiwa kumuona dada yangu pamoja na mtoto wake. Nilimsalimia kwa furaha na kumpa hongera kwa kujifungua salama. Alionekana mchovu kidogo, lakini tabasamu lake lilinipa utulivu wa moyo. Kwa bahati nzuri, alikuwa tayari ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yake kuimarika. Bila kuchelewa, tukajiandaa na kuanza safari ya kuelekea nyumbani.

Baada ya kufika, hatukukaa sana. Mimi na shemeji yangu tukaanza safari nyingine ya kwenda stand kumpokea mama yangu mzazi. Njiani tulikuwa tunapiga story mbalimbali, tukikumbuka mambo ya zamani na kucheka ili kunogesha safari na maongezi. Shemeji alionekana kuwa na furaha isiyo kifani kwa kupata mtoto wa kike.

Katika hali ya kumpongeza, ghafla naye akanigeukia na kunipa hongera ya kupata mtoto wa kike-Aria. Maneno yake yalinishtua kidogo, hapo nikahisi wazi kuwa dada lazima alimwambia shemeji kuhusu sakata la Iryn. Sikushangaa sana, maana isingewezekana dada akae muda mrefu South Africa kisha arejee, halafu shemeji akae kimya bila kuuliza chochote. Nilikaa kimya, nikatabasamu tu, na sikujibu maana ni pongezi ambayo sikuitarajia kabisa.

Tulipofika stand, tulienda moja kwa moja kumpokea mama, alikuwa ameshafika tayari akitusubiri. Baada ya kuonana, tuliishia kukumbatiana kwa nguvu kama watu waliokaa muda mrefu bila kuonana. Nilianza kwa kumsalimia na kumpa pole ya safari, na mama akaendelea kusalimiana na mkwe wake.

Nilimsaidia kubeba bag lake na tukaelekea tulikokuwa tume-park gari na njiani tulikuwa tunazungumza;

MAMA: “Kwahiyo mwanangu ukaamua uje kimyakimya huku Arusha hata mama yako nisijue?”

MIMI: “Mama yaishe bhana nitakulipia ndege wakati unarudi.”

Alitabasamu, lakini bado alionekana kunitania kwa upole. Baada ya kuingia kwa gari mama alianza kuulizia maendeleo ya binti yake. Shem alimpa taarifa ya kila kilichokuwa kinaendelea hadi sasa, kisha tukaanza safari ya kurudi nyumbani. Mimi nilikaa siti ya nyuma pamoja na mama yangu, na tulikuwa tunazungumza mambo mengi sana.

Na moja ya maongezi yetu, mama alinipongeza kwa kupita muda mrefu bila kupokea malalamiko kutoka kwa mama J. Alitusifia pale na akasema kwasasa tumeshukua watu wazima, hivyo tufanye utaratibu wa kufunga ndoa haraka iwezekanavyo.
*****

Kesho yake nilikuwa nimepanga kuondoka Arusha na kurudi Dar es Salaam. Asubuhi ile nilipata muda wa kuongea na dada yangu faraghani. Tulizungumza mambo mengi kwa uwazi na kwa utulivu. Kati ya mambo muhimu, nilimpa taarifa kuwa wifi yake kutuma pesa kwa ajili ya mtoto. Nikamuongezea na kiasi changu binafsi, kisha nikamtumia fedha hizo kwenye akaunti yake ili azitumie kadri atakavyoona inafaa.

Ile asubuhi pia, wageni walianza kumiminika kwa wingi nyumbani kumuona dada yangu, hasa marafiki zake na wafanyakazi wenzake. Shemeji yangu alikuwa busy kupita kiasi, akipokea wageni, kuhakikisha kila kitu kanaenda vizuri. Nilimuonea huruma kidogo kwa jinsi alivyokuwa akihangaika siku hiyo, kwa upande wangu nilikuwa nikisaidia pale napohitajika, zaidi nilikuwa nacheza na vijomba vyangu.

Mchana baada ya kupata lunch, niliwaaga wote kabla ya kuondoka na nilikaa pembeni kuongea na wife, yeye alisema ataendekea kuwa Arusha kwa wiki moja. Nilimtumia Pesa kwenye simu ya kumsaidia kwa kipindi atakachokuwa pale na nikaenda kumuaga mama yangu mzazi pamoja na dada yangu kipenzi.

Nilitua Dar es Salaam saa 12 jioni na nikaenda kukaa pale Cafe nikipoteza muda. Mara tu nilipoweka simu yangu online, nikakutana na ujumbe kadhaa kutoka kwa Sumaiya akiuliza niko wapi, maana alikuwa hanipati kwa simu. Nikamjibu kwa kifupi kuwa nilikuwa safarini kutokea Arusha, haikuchukua hata dakika mbili, simu yake ikaingia.

Bila kusita nikapokea na tukaanza kuongea. Sumaiya aliniambia angependa tuonane kama itawezekana, kwa sababu ana mambo muhimu anataka tuzungumze faragha. Nilipiga hesabu za haraka kichwani, sikuona tatizo, nikamwambia nitapitia ofisini kwake kabla sijaenda nyumbani.

Ilichukua kama dakika arobaini kufika pale ofisini kwake. Nilipanda hadi ghorofani na kumkuta bado yuko busy na kazi zake mezani. Aliponiangalia tu, aliacha alichokuwa anafanya na kunitazama kwa jicho la maana.

SUMAIYA: “Nilikuwa na Hilda hapa, ameondoka si muda mrefu.”

MIMI: “Kipindi unanipigia ulikuwa naye?”

Akatikisa kichwa kuonyesha ndiyo.

Nikavuta kiti nikakaa.

MIMI: “Sawa, nenda straight kwenye point. Agenda ni nini?”

Akanitazama kwa tabasamu la kejeli kidogo.

SUMAIYA: “Unajikuta una haraka? Unawahi wapi usiku huu eti?”

Kabla sijaelewa mwelekeo wa mazungumzo, akasimama na kwenda kufunga mlango kwa funguo. Ghafla akaanza kufungua vifungo vya shati lake taratibu huku macho yake yakiwa kwangu. Nilimkazia macho, nikihisi hali si ya kawaida, na sikuelewa anataka kufanya nini.

MIMI: “What are you doing?”

Hakujibu moja kwa moja ila aliendelea kubadilisha nguo, akavua alizokuwa amevaa na kubaki na bikini, kisha akaelekea kwenye kabati na kutoa nguo nyingine. Alianza kuvaa upya pale mbele yangu bila kuonyesha wasiwasi wowote.

SUMAIYA: “Acha uoga Insider ni kitu gani ambacho hukijui kutoka kwa mwanamke? Nabadilika tu hapa, nina sehemu naenda na mishe zangu.”

Nilivuta pumzi ndefu, nikijaribu kubaki mtulivu.

MIMI: “Hujawahi kumiliki akili wewe. Haya sasa niambie ulichoniitia, nitaondoka.”

Akanicheka kwa sauti ya chini.

SUMAIYA: “Mbona una haraka kama bao la kwanza? Wewe mwanaume vipi?”

Ilibidi nicheke pia, maana kama kuondoka nisingeweza sababu alikuwa kashika funguo za mlango. Baada ya kumaliza kuvaa, tukatoka pamoja ofisini na kushuka hadi parking. Tukaingia kwenye gari lake na kukaa ndani, milango ikiwa imefungwa. Hapo ndipo tulianza mazungumzo yaliyokuwa na uzito zaidi kuliko nilivyotarajia.

Habari kubwa ambayo Sumaiya alinipa usiku ule ilikuwa ni kuhusu mama Janeth. Aliniambia mama analalamika kwamba nimeanza kubadilika, si kama zamani. Pia anaamini kuwa kwa namna fulani nimeanza kuharibu mahusiano yake na Iryn. Sumaiya alizungumza mambo mengi aliyokuwa akiambiwa na mama Janeth kumhusu mimi-mambo ambayo kwa kweli yalinizidishia maswali kuliko majibu.

Kitu kilichomuuma zaidi mama, kwa mujibu wa Sumaiya, ni kitendo cha Iryn kuumwa hadi kulazwa hospitalini bila yeye kupewa taarifa mapema. Hapo ndipo nilibaki nashangaa zaidi.

MIMI: “Hapo kosa langu ni lipi? Mimi ndiye nilipaswa kumpa taarifa mama, au akina Iryn wenyewe?”

SUMAIYA: “Ndio hapo sasa hata mimi nashangaa.”

Nilinyamaza kidogo nikawaza, kisha nikamuuliza tena:

MIMI: “Baba yake Iryn alishindwa kumwambia?”

SUMAIYA: “Nahisi hawako kwenye maelewano mazuri siku hizi. Ndiyo maana mama anaonekana kuchanganyikiwa. Lakini Insider, Iryn kwa sasa ni kama hana muda sana na mama Janeth. Kwenye ishu za kampuni, ni kama amekuachia majukumu yote wewe na yeye hashiriki kabisa.”

Maneno yale yalinifanya niketi vizuri kwenye siti ya gari.

MIMI: “Tatizo ni nini hasa? Iryn ni mke wangu, na kwa sasa yuko kwenye malezi. Ni kawaida kuniachia majukumu ya kampuni kwa muda,au mama ana wasiwasi gani?”

Sumaiya akatoa cheko la kimbea, akainama kidogo karibu nami na kunishika sharubu kwa utani.

SUMAIYA: “Ni hivi… mama anasema Iryn kwa sasa amenasa sana kwenye penzi lako. Huenda akafikia hatua hata huwezi kusemwa kitu kuhusu wewe mkabishana. Labda mama ana wasiwasi kwamba Iryn anaweza kukupa hisa za kampuni bila hata kutumia nguvu.”

Nilicheka kwa sauti ya chini, nikitikisa kichwa.

MIMI: “Hata akinipa, kuna shida gani? Iryn anamiliki asilimia sabini ya hisa za kampuni, zilizobaki ni za mama Janeth. Kama Iryn ataamua kunipa sehemu ya hisa zake, zitakuwa ni zake, si za mama. Mama aache wivu wa mambo yasiyo na msingi.”

Sumaiya akanitazama kwa macho ya tahadhari.

SUMAIYA: “Remember nilikwambia mapema wewe piga hela. Hawa watu hawatabiriki kabisa.”

MIMI: “Sumaiya, mimi siwezi kuiba pesa kwenye hii kampuni, siwezi kuwa na tamaa hiyo. Heshima yangu na jina langu haviwezi kuuzwa kwa tamaa.”

Akaniegemea kwenye siti, akavuta pumzi kisha akasema kwa sauti ya utulivu:

SUMAIYA: “Nikwambie kitu… mama ana hasira na hofu tu. Lakini baada ya muda atatulia.”

Nilikaa kimya kwa sekunde chache nikitafakari. Nilijua wazi kuwa nyuma ya maneno ya Sumaiya kulikuwa na mvutano mkubwa wa kifamilia. Usiku ule pale parking, ndani ya gari, nilihisi kama nimeingizwa katikati ya vita ya kimya, na sababu ya hii vita ni mimi.

Niliachana na Sumaiya pale parking, nikashuka na kuita Uber ya kunirudisha nyumbani. Njiani nilikuwa kimya kabisa, macho yangu nje ya dirisha lakini mawazo yakiwa mbali sana. Kichwa changu kilijaa maswali kuhusu mama Janeth.

Nilishindwa kuelewa kwa nini ghafla ameanza kubadilika kwa kasi kiasi kile? Kwa nini aanze kuwa na chuki au wasiwasi juu yangu? Nimekosea wapi? Niliendelea kuunganisha vipande vya maneno ya Sumaiya, nikajaribu kutengeneza picha kamili. Kadri nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kuhisi huenda kuna mambo yanaendelea chini kwa chini ambayo mimi siyajui. Hapo ndipo nikajisemea kimoyomoyo, ni busara kukaa chini na Iryn tuzungumze kwa kina before it’s too late.

Mara tu nilipofika home, niliingia moja kwa moja bafuni kuoga ili kupunguza uchovu wa safari na mawazo yaliyokuwa yamenijaa. Baada ya kutoka, nikachukua simu yangu na kuamua kumpigia Erica. Tangu niko Arusha alikuwa kanitafuta mara nyingi, lakini sikuweza kupata muda wa kuongea naye kutokana na mazingira niliyokuwa nayo. Pia alinitumia messages kadhaa zilizojaa malalamiko kuhusu mambo anayohisi namfanyia.

Nilimpigia mara moja lakini simu haikupokelewa. Nikapiga tena na bado kimya. Nikaona ni bora nimuache kwa muda badala yake, nikawasiliana na Jane kumjulia hali. Ukweli ni kwamba lengo langu kubwa la kumtafuta Jane lilikuwa ni kutaka kuzungumza naye kuhusu ishu yangu na Mary. Nilihitaji mtazamo wa mtu wa karibu, mtu ambaye angenisikiliza bila kunihukumu. Lakini baada ya kuanza mazungumzo naye, ghafla nikahisi sio wakati sahihi kufungua hilo jambo.

Nikameza maneno yangu, nikaamua nitaftute njia nyingine ya kumtafuta Mary mwenyewe.
Baada ya kumaliza kuongea na Jane, simu ya Erica ikaingia. Niliitazama kwa sekunde chache kabla ya kupokea. Kisha nikavuta pumzi na kubonyeza kupokea.

MIMI: “Hello baby.”

ERICA: “What is wrong with you? You don’t even pick up my phone and reply to my messages.”

MIMI: “Baby sorry! Nilipata emergency Arusha dada yangu kajifungua.”

ERICA: “Insider kila siku huishiwi sababu.”

MIMI: “Ni kweli baby, how could I lie to you baby?”

ERICA: “Do you really love me?”

MIMI: “Yes I do. Where’s all this coming from?”

ERICA: “Bhasi mpenzi wangu naomba yaishe. Nilipatwa na wasiwasi tangu uondoke Dodoma hunitafuti na simu zangu hupokei.”

MIMI: “Kwahiyo nisipopokea simu zako ndiyo sikupendi? Na nikipokea ndiyo nakupenda? Eti baby.”

ERICA: “Hapana mpenzi wangu, nakuwa na wasiwasi, halafu mwezi ujao nakuja Dar es Salaam.”

MIMI: “Sawa baby karibu sana utanambia nije nikupokee.”

Tuliendelea na maongezi mengine na alirudi kwenye hali yake ya sikuzote akiwa na furaha kama zote. Baada ya kumaliza maongezi yetu bado nilikuwa nawaza hatima ya huyu mwanamke maana niliona hatua aliyofikia ni mbaya hivyo inabidi nifanye jambo la haraka ili kumuokoa.

Niliwaza kwa makini nikaona ni heri nikatafuta siku ya kukaa naye chini na kumwambia ukweli ili ajue kinachoendelea. Nikapanga siku atakayokuja Dar es Salaam, bhasi ndio siku ambayo atajua ukweli kuhusu maisha yangu.

Kesho yake, siku ya Ijumaa, niliwahi ofisini mapema ili kuweka mambo sawa na kupitia ripoti zote za fedha. Nilihitaji kuhakikisha kila kitu kiko kwenye mstari sahihi, hasa katika kipindi hiki ambacho mambo ya kampuni yanaonekana kuwa na upepo wa chini kwa chini.

Ilipofika mida ya saa tatu asubuhi, mama alikuja pale ofisini. Alinikuta nikiwa nimejikita kwenye majukumu yangu. Tulisalimiana kwa heshima, kisha akaulizia maendeleo ya dada yangu.

MAMA: “Vipi huko Arusha, hali ya dada yako ikoje sasa?”

MIMI: “Anaendelea vizuri mama, hali yake imetulia na mtoto yuko salama.”

Alitikisa kichwa kwa kuridhika, kisha tukaanza mazungumzo mengine ya hapa na pale. Katikati ya mazungumzo, alinipa taarifa kwamba wikiendi hiyo angesafiri na angerudi tena mwisho wa mwezi. Nilipokea taarifa hiyo kwa utulivu, ingawa moyoni nilihisi kama kuna kitu anakiandaa kimya kimya.

Wakati bado tunaongea, Hilda aliingia ofisini. Akaanza kwa kumsalimia mama kwa heshima, kisha akanigeukia mimi. Mama hakukaa akaaga na kuondoka.

Baada ya mama kutoka, zilipita dakika 5 za ukimya, Hilda akaanzisha mazungumzo;

HILDA: “Insider, mama mkwe wako anasemaje?”

MIMI: “Anasafiri weekend hii, atarudi mwisho wa mwezi.”

Kabla hata hatujaendelea, ghafla Lucy akaingia ofisini kwa kasi, akihema kama mtu aliyetoka kufukuzwa. Tukabaki tukimwangalia.

HILDA: “Vipi na wewe, kulikoni?”

LUCY: “Nimeona gari ya mama kona pale, ndiyo maana nimekuja spidi.”

HILDA: “Alikuwepo hapa ila ametoka si muda mrefu.”

Lucy akavuta pumzi ndefu.

LUCY: “Mawazo yangu nikajua anaingia ofisini.”

Nikatikisa kichwa kwa tabasamu la kejeli kidogo.

MIMI: “Acha nidhamu ya uoga.”

Lucy akakaa vizuri kwenye kiti.

LUCY: “Mama katupiga biti juzi hapa hadi ofisi ikatetemeka, alisema tunajisahau sana.”

Nilimwangalia kwa utulivu na kumtoa wasiwasi;

MIMI: “As long as mimi bado nipo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Cha msingi target zenu ziwe zinafika basi, hiyo ndiyo lugha pekee itakayomfanya atulie.”

Baada ya hapo nikaanza kuzungumza na Lucy kuhusu maendeleo ya Iryn, na akanipa habari mpya kuhusu yeye kwenda South Africa;

LUCY: “Kabla sijafungua chuo, nitaenda South Africa kumuona. Nahisi ni muhimu nikamuona maana ni kitambo sijamuona.”

Niliona hilo ni jambo zuri, lakini nilikuwa nakumbuka maneno ya Asmah juu ya Lucy. Tukahamia kwenye mazungumzo mengine kuhusu hali ya mama yake, na akanihakikishia kuwa kwa sasa hali yake ni nzuri, anaendelea vyema.

Mchana nilitoka ofisini kuelekea Makumbusho kukutana na Dullah kwa mazungumzo tuliyokuwa tumepanga awali. Lakini kabla ya kwenda huko, niliamua kupitia Victoria, kwenye ofisi za Ghati. Lengo langu lilikuwa ni kumsalimia na kumjulia hali, sikumpa taarifa ila nilitaka iwe surprise.

Baada ya kufika pale reception, niliambiwa kwamba Ghati hajaja ofisini kabisa kwa siku hiyo. Nilishangaa kidogo, lakini nikakaa pembeni kwenye kiti, nikatoa simu yangu na kuamua kumpigia nimwulize alipo, maana sikumkuta ofisini kama nilivyotarajia. Simu iliita mara ya kwanza bila majibu, nikapiga tena na safari hii akapokea.

GHATI: “Hey baby, sorry nimeshindwa kupokea on time, nimebanwa na majukumu ya ofisi.”

Nilikaa kimya kwa sekunde chache, nikijiuliza majukumu gani ya ofisi wakati nimeambiwa leo hajaja kabisa? Nilitamani kumuuliza papo hapo, lakini nikaamua kunyamaza kwanza.

MIMI: “Kwani uko ofisini?”

GHATI: “Ndio daddy.”

MIMI: “Hapa Victoria?”

GHATI: “Yes, mbona hivo?”

Nikavuta pumzi polepole.

MIMI: “Hamna bhana, wewe endelea na majukumu yako. Mimi nilikuwa nakupa hi tu! Nimekumiss.”

GHATI: “Mimi nipo, thank you kwa kunikumbuka.”

Akakata simu, nikabaki pale nikiwaza ina maana huyu dada wa reception ananidanganya? Au Ghati ndiye anayenidanganya? Mbona anadai yuko ofisini wakati nimeambiwa hajaonekana kabisa?

Nikanyanyuka na kurudi pale reception.

MIMI: “Dada, nimetoka hapa kuzungumza na Ghati. Anasema yuko ofisini au kajifungia huko ndani hajataka kutoka?”

Dada akanitazama moja kwa moja machoni.

DADA: “Kaka, wallahi siwezi kukudanganya. Ghati leo sijamuona kabisa ofisini na haja-sign in. Anakudanganya tu, muulize vizuri, anakupotezea muda wako.”

Sijui dada alijifikiria nini na akaniuliza;

“Samahani ulikuwa na shida gani?”

MIMI: “Hapana mimi nilipita kumsalimia tu, bhasi nitawasiliana naye.”

DADA: “Sawa pole kwa usumbufu.”

Niliamua kuondoka bila kupiga tena simu na nilipofika kwenye gari, nikakaa kimya kwa dakika kadhaa nikikumbuka namna tulivyokuwa tunaongea na Ghati. Alikuwa anajibu kwa mkato, kama mtu asiye na muda wa mazungumzo marefu.

Nikajiuliza tena, kwa nini adanganye yuko ofisini ilhali hayuko? Anaficha nini? Au anataka nisijue yuko wapi? Mwisho nikaamua kuondoka na kuendelea na safari yangu kuelekea Makumbusho.

Tulikutana na Dullah pale Breakpoint Makumbusho. Yeye alikuwa amewahi mapema, akiningoja. Baada ya kufika, niliagiza chakula na bila kuchelewa tukaanza mazungumzo yaliyotukutanisha pale.

DULLAH: “Shemeji wa South Africa anaendeleaje?”

MIMI: “Wale wako poa kabisa, wanaendelea vizuri. Sijui wewe shem wangu Latifah?”

DULLAH: “Yuko salama sana embu nipange Senior, ni jambo gani linakusumbua hadi unashindwa kufikisha taarifa kwa wazazi?”

Nilitulia kidogo kabla ya kujibu.

MIMI: “Kaka, master plan wa kila kitu ni dada yangu. Yeye ndiye alisema nisubiri kwanza, then tutaanza mchakato. Ila nimeshajua sababu ya kuchelewesha ilikuwa ni mimba yake.”

DULLAH: “Kama mimba ilikuwa kikwazo, sasa amejifungua, mtoto hatakuwa kikwazo tena?”

MIMI: “Uko sahihi ila yeye amesema anaandaa mpango juu ya hili, acha nisubiri.”

Dullah akaniangalia kwa uzito, alinishauri kwamba mambo haya yamekaa kiume zaidi, hivyo ni busara nianze kuongea na baba yangu. Kama nitaona napata changamoto, ni heri niwashirikishe wazee wazima ili wao wafikishe taarifa kwa wazazi kwa heshima na utaratibu.

Aliendelea kusisitiza kwamba kipindi tulipokuwa South Africa, aliona wazi kuwa Iryn ananipenda. Hivyo ni busara nikawa mkweli kwenye hili suala kuliko kuendelea kuzungusha au kumdanganya. Alinionya kwamba kuchelewesha ukweli kunaweza kuzaa mgogoro mkubwa zaidi baadaye.

Dullah aliongea mambo mengi ya busara na uzoefu. Kwa kweli alinipa ushauri mzito wa kiuanaume. Hatukugundua muda umeenda vipi hadi ilipofika saa 11 jioni. Tukalipa bill, tukaagana, kila mmoja akaondoka.

Nikiwa njiani kurudi nyumbani, simu ya Ghati ikaingia. Baada ya kuiona simu yake, nilitabasamu maana yalikuwa yamepita masaa matatu, ndio anapiga, haraka nikapokea.

Alianza kwa kuomba msamaha, akijitetea kwamba alikuwa busy sana na majukumu ya kazi ndiyo maana hakuweza kuongea vizuri. Nilijua wazi kuwa ananidanganya, hakuwepo ofisini. Lakini nikaamua kumsikiliza tu, nikimpa nafasi aendelee na hadithi ya uongo wake bila kumkatiza.

Baada ya kukata simu, moyo wangu haukuwa tena mtulivu. Hisia zilianza kunisonga nikahisi huenda kuna mwanaume mwingine nyuma ya pazia. Maswali yalizidi kuongezeka kuliko majibu, nikajisemea lazima nianze uchunguzi wangu haraka iwezekanavyo, usikute Ghati ni mke wa mtu, lakini ananidanganya.

*****
Week ya kwanza ya mwezi Novemba, Jumamosi ya kwanza kabisa, Jane aliandaa hafla fupi kwa ajili ya kijana wake, Johson. Lengo kuu la hafla hiyo lilikuwa ni kuwashukuru ndugu na marafiki walioungana nao katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Johson.

Movie inaanza saa 10 jioni, Camila binti ya Mzee Juma ananipigia simu na kuuliza nilipo. Nikamwambia niko home, akanijibu kuwa anakuja kunipitia ili twende wote Mbweni, nikamwambia sawa. Saa 11 jioni, Camila alifika nyumbani kunichukua, tukaanza safari ya kuelekea Mbweni.

Tulipowasili Mbweni, nje ya fence tunakutana na magari ya kutosha na sisi tukatafuta sehemu nzuri ya kupark. Baada ya kuingia ndani ya fence tulikuta wageni mbalimbali tayari wamekusanyika, wengi wao wakiwa wamekaa nje chini ya hema. Mpangilio mzuri wa meza na viti ulipamba sana eneo lile, ukalifanya livutie machoni. Kulikuwa na mwanga wa kuvutia na hali ya mziki wa taratibu ilisikika kila kona.

Mimi na Camila tukaamua kuingia kwanza sebuleni kusalimia wenyeji kabla ya kujiunga na wengine nje.

Tulipoingia sebuleni, macho yangu yakatua kwa Mary aliyekuwa amekaa kwenye sofa la mbele kabisa. Tukatazamana kwa sekunde chache zilizobeba mshangao. Kwa kweli, sikuwa na wazo hata kidogo kwamba Mary angekuwepo pale. Kwa muda nilikuwa kama nimemsahau kabisa. Hivyo, kumuona pale ilikuwa ni surprise kubwa kwangu.

Niliendelea kusalimia watu waliokuwepo sebuleni. Nilipokaribia upande aliokuwa amekaa Mary ili nimpe salamu, nikakuta tayari ameondoka pale. Nikarudi na kwenda kukaa pembeni ya Camila.

Hatukukaa muda mrefu ndani, tukatoka nje na kuelekea kwenye hema. Meza tuliyokaa ilikuwa na jumla ya viti vinne. Tukiwa katikati ya mazungumzo yetu, ghafla tukawaona Mary na mdogo wake, Prisca, wakiingia ndani wakitokea getini. Nikahisi labda Mary alitoka nje kumpokea mdogo wake, kisha nikajifanya kuendelea na mazungumzo na Camila.

Baada ya takribani dakika kumi, Camila alinikonyeza na kunong’ona kwa sauti ya chini:

“Mpenzi wako anakutazama sana, kwani mmegombana? Mbona kama hana time na wewe?”

Nikajibu kwa haraka,

“Mary siyo mpenzi wangu bhana, unazingua.”

Camila hakukata tamaa, akaongeza,

“Au labda hajapenda mimi kukaa na wewe hapa?”

Nikageuka kuwaangalia upande waliokaa akina Mary. Walikuwa wanne mezani wakipiga stori, akiwemo Vicky. Ghafla nikagonganisha macho na Prisca, alitoa mshangao wa wazi usoni, akasimama pale alipokuwa amekaa na kuanza kuelekea upande wetu.

Alipofika, alitusalimia wote kwa furaha, nikamsaidia kuvuta kiti akakaa. Alionekana kushangaa sana kuniona pale, akasema amefurahi mno kuniona. Lakini bila kupoteza muda, akaanza kunilalamikia kwa nini sipokei simu zake.
 
Bora ambavyo hajui ninachomkubalj insider anafanya uhuni wake huko mama mjengo hajui kabisa. Mpaka mtoto anazaliwa hana habari😁😁😁
Nakuambia, 😂😂😂😂
Wizzo anaenda kukaa Bondeni kumuuguza mke mwenza miezi kadhaa, na mama J hajui.

Ila hii story ukiileta kwa uhalisia unaona kabisaa haiwezekani, japo yeye alisema wazi ni story ya kweli, ila mmmh hapanaa.
 
Nakuambia, 😂😂😂😂
Wizzo anaenda kukaa Bondeni kumuuguza mke mwenza miezi kadhaa, na mama J hajui.

Ila hii story ukiileta kwa uhalisia unaona kabisaa haiwezekani, japo yeye alisema wazi ni story ya kweli, ila mmmh hapanaa.
Inawezekana sana! Dunia ina watu wengi hii
Mm nmeshuhudia kabsa! Tena kwa mshua
 
Ah dadeki, nimebanwa sana. Natamani nimpe mtu kazi awe anapitia hizi epsodes kabla hazijaja hewani. @cocochanel ni DM na namba inayopokea Pesa. Wahuni walikupendekeza kama mshindi
Mkuu nipe mimi hiyo kazi nitaifanya kwa ufqnisi hadi mwenyewe utapenda.
 
Back
Top Bottom