SEASON 03
CHAPTER 20
CONTINUE:
Baada ya kutua Dodoma, nilimpigia simu wife wangu na kumpa taarifa kuwa nimetua salama Dar es Salaam, lakini kwa wakati huo nilikuwa Dodoma mara moja kushughulikia masuala ya kampuni. Nilimueleza kuwa nilikuja kwa ajili ya mambo ya Biashara, ikiwemo kufanya mabadiliko ya taarifa za kampuni na kumuingiza rasmi kama mmoja wa Directors.
Mama J alifurahi sana baada ya kupokea taarifa hizi. Nilihisi furaha yake hata kupitia simu, jambo lililonipa amani ya moyo. Nilimwambia kuwa endapo nitafanikiwa kukamilisha mambo mapema, bhasi nitarejea nyumbani haraka.
Baada ya hapo, nilimpigia simu Sanchi kumjulisha kuwa nimefika Dodoma na pia kumkumbusha kuhusu appointment yetu ya jioni ya kukutana na Mr. Ando, ambapo tungeenda wote. Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana kutokana na uchovu wa safari, niliamua nipumzike kwanza kabla ya kuendelea na shughuli nyingine.
Saa tisa alasiri, niliondoka kuelekea kwa Sanchi kwa ajili ya mazungumzo mafupi kabla ya kwenda kukutana na Mr. Ando. Sanchi alifurahi sana kuniona na kunikaribisha ndani kwa bashasha kubwa. Baada ya kusalimiana, alinipa pole nyingi kwa niaba ya Aria na mama yake, na akaendelea kuniuliza maendeleo yao ya kiafya kwa ujumla tangu nilipoondoka South Africa.
Baada ya salamu, tulianza kuzungumzia masuala ya kampuni. Nilimuweka wazi Sanchi na kumueleza mpango wangu wa kumwajiri rasmi kama Secretary wa kampuni na kuanza kumlipa mshahara. Nilifanya uamuzi huu kwa sababu alikuwa tayari mtu muhimu sana katika ukuaji wa kampuni. Kwa muda mrefu, alikuwa akinisaidia kuwasiliana na wadau kwa niaba yangu, na zaidi ya hapo, alikuwa mzuri sana katika communication na marketing.
Baada ya kumpa taarifa hizi, Sanchi alifurahi sana, japokuwa mara ya kwanza alionekana kusita na kutaka kukataa. Nilimueleza kwa kina mpango wangu wa dhati pamoja na maono makubwa niliyonayo juu ya kampuni hii. Hatimaye, alielewa na kukubali.
Baada ya hapo, tuligeukia mjadala wa kwenda kukutana na Mr. Ando. Sanchi alitaka kujua ni maamuzi gani nilikuwa nimeyachukua kuhusu pendekezo la Ando. Nilimueleza wazi kuwa kumpa hisa za kampuni ni jambo lisilowezekana kwa sasa, kutokana na risk kubwa iliyopo. Badala yake, niliona ni busara tumlipe kwa mfumo wa commission kwa kila kazi atakayoleta.
Sanchi aliunga mkono wazo langu mara moja, akisema hata yeye tangu mwanzo alikuwa na mtazamo huo huo, na akaona ni njia ya kitaalamu zaidi (a more professional approach). Hata hivyo, nilibaki na maswali moyoni kwa sababu Mr. Ando alikuwa anaonyesha interest kubwa sana kwenye kampuni. Nikaanza kuwaza kwa kina, nikaona huenda kuna kitu kikubwa ameona ndani ya kampuni yangu, ndiyo maana alikuwa ananifuatilia karibu na kutaka majibu kila siku.
Ilipofika saa kumi na moja jioni, mimi na Sanchi tuliondoka kuelekea Morena hotel kukutana na Mr. Ando. Tulikutana kwenye restaurant kwa ajili ya kikao chetu kifupi. Safari hii, Mr. Ando alifika kwa wakati, na bila kuchelewa, tulianza mazungumzo ya kibiashara.
Kwa makusudi kabisa, sikuwa na haraka ya kuzungumza. Nilimpa Sanchi nafasi ya kuongoza mazungumzo. Cha kushangaza, Sanchi alianza kuzungumza mambo ambayo hayakuwa exactly kama tulivyopanga, lakini aliyaeleza kwa ustadi mkubwa, kwa mtiririko na kwa hoja zenye mantiki.
SANCHI:
“Mr. Ando, kwanza tunafurahi sana kukutana na wewe kwa mara nyingine tena. Leo tumekuja kuzungumzia lile wazo ulilolitaja kwenye kikao chetu kilichopita. Management ya INSIDER INVESTMENT LTD inatambua na kuthamini nia yako njema ya kuisaidia kampuni hii kukua na kufikia malengo yake ya muda mrefu.
Kampuni hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na sera zake, na kwa muda mfupi tangu ianzishwe, tayari imeanza kutoa mchango chanya kwa jamii na Serikali kwa ujumla. Hadi sasa, tumeajiri vijana wanne ambao wanajipatia kipato na kuchangia katika kutatua changamoto ya ajira nchini.
Aidha, kampuni inalipa kodi zote stahiki za Serikali, ikiwemo PAYE, Withholding Tax, Stamp Duty, Corporate Income Tax, na kwa muda si mrefu tutaanza kufanya kazi kama Government VAT Agent.
Tunaamini mpaka sasa umeona jinsi kampuni yetu ilivyojipanga kitaendaji na kisheria. Baada ya management kukaa na kujadili kwa kina pendekezo lako, tuliona njia sahihi kwa sasa ni kushirikiana kwa mfumo wa commission kwa kila kazi utakayoleta.
Hata hivyo, tukiona unaendelea kuwa mdau wetu wa karibu na wa kudumu, kampuni iko tayari kuja kufikiria suala la kukupa hisa zake hapo baadaye. Kwa sasa, tunaomba tuendelee na utaratibu huu wa commission.
Tunakushukuru sana kwa nia yako njema na tunaamini kampuni ikikua, itasaidia vijana wengi zaidi kupata ajira na kuchangia mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. Tunaomba ukubali pendekezo hili kutoka kwa management.”
Sanchi alizungumza kwa ufasaha mkubwa, bila kigugumizi, akipanga maneno yake kama hadithi inayovutia. Wakati wote alikuwa anaongea, nilibaki nikimtazama tu. Sikutarajia kabisa kumuona akiongea kwa confidence ile.
Mr. Ando, baada ya Sanchi kumaliza, alikaa kimya kwa muda mfupi, akanywa maji kwenye glass, kisha akaanza kuzungumza.
ANDO: “Nilikuwa napitia MEMART yenu, na nimeona share capital ni TZS 500 million. Nataka kufahamu, je, kiasi hiki chote kimeshaingizwa kwenye kampuni?”
MIMI: “Hiyo ni Authorised Share Capital. Thamani ya hisa moja ni TZS 10,000. Kati ya hisa 50,000, hisa 10,000 zimetolewa zenye thamani ya TZS 100 million, lakini ni hisa 5,000 tu ndizo zimelipwa hadi sasa. Hisa 5,000 zilizobaki zitalipwa muda wowote kuanzia sasa.”
ANDO: “Na zile hisa 40,000 zilizobaki mna mpango gani nazo?”
MIMI: “Zitabaki kwenye reserve account hadi pale kampuni itakapokuwa kubwa na kuwa na uhitaji wa kuongeza mtaji. Kwa sasa, kampuni itaendelea kutumia Equity, yaani mtaji pamoja na retained earnings kama source ya finance, tukichanganya kidogo na mikopo pale inapobidi.”
ANDO: “Director mwingine yuko wapi?”
MIMI: “Ni mama yangu.”
Mazungumzo yalikuwa marefu na ya kina, yakichukua takribani saa nzima, huku Sanchi akiwa kinara mkubwa wa majadiliano. Mwisho wa kikao, Mr. Ando alituaga na kuahidi kuwasiliana nasi baada ya kutafakari na kufanya maamuzi.
Baada ya Ando kuondoka, mimi na Sanchi tulianza kucheka na kuzungumza kwa furaha. Nilichukua nafasi hiyo kumpongeza kwa jinsi alivyo-handle mazungumzo kwa ustadi mkubwa. Alifurahi sana, na tukachukua nafasi hiyo kuagiza chakula na kula, maana muda ulikuwa umesogea.
Baada ya kumaliza kula, tuliamua kuondoka. Tuliendelea kupiga story nje kidogo huku tukisubiri usafiri wake. Usafiri wake ulipofika, tuliagana kwa kukumbatiana. Katika wakati huo, bila hata kutarajia, nilijikuta nikimshika makalio yake na kuyapapasa kwa utulivu. Sikuwa nimewahi kufanya hivyo kabla, lakini safari hii ilikuwa tofauti, nadhani ni furaha iliyonizidi siku ile;
SANCHI: “Insider, thank you.”
MIMI: “Ukifika home, nitumie account number yako.”
SANCHI: “Sawa, wewe unaondoka na usafiri gani?”
MIMI: “Nachukua pikipiki pale nje.”
SANCHI: “Bye Insider.”
Baada ya kurejea nyumbani, nilifanya mawasiliano na Iryn. Tangu nitue Dar es Salaam, sikuwa nimemtafuta, japokuwa yeye alikuwa akipiga simu mara kadhaa na kunitumia meseji. Alipopokea simu yangu, tulianza mazungumzo ya kawaida, kisha nikamjulisha kuwa nilikuwa Dodoma.
IRYN: “Hivi baby, huko Dodoma huna mwanamke kweli? Haiwezekani kila ukitoka South Africa lazima upitie Dodoma.”
MIMI: “Hamna baby, ni mambo ya kampuni tu ndiyo yamenileta huku. Pia niko kwenye process za kusajili VAT.”
IRYN: “Vipi, ulifanikiwa kuzungumza na Mr. Commission?”
Nilicheka kidogo niliposikia jina hilo.
MIMI: “Ndio, nimetoka kukutana naye si muda mrefu.”
IRYN: “Mmefikia wapi?”
MIMI: “Tumempa pendekezo letu la commission. Ametuomba tumpe muda wa kulifikiria, halafu atanijulisha akishafanya maamuzi.”
IRYN: “Mungu akutangulie baby. Napenda hustles zako sana tangu enzi ukiwa Uber. Natamani mwanao Aria arithi spirit hiyo.”
MIMI: “Nikifanikiwa kupata hizi deal, nakupeleka Santorini ukale bata.”
Maneno hayo yalimburudisha sana.
IRYN: “Awww… nikija Dar nitakusaidia kwenye marketing. Unanionaje nikianza kutupia vitu vyangu?”
MIMI: “Deal zote tutazipata, ila ujue watakutongoza sana, halafu mimi nina wivu.”
Tulicheka kwa pamoja.
IRYN: “Momo anakusalimia, ananionea wivu eti.”
MIMI: “Msalimie mke wangu mkubwa, mwambie nimemmiss.”
Mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu, tukizungumza mambo mengi sana. Na kubwa Iryn alikuwa kapona tayari na alinambia ameanza kumnyonyesha mtoto. Taarifa ile, ilinifurahisha sana na baada ya kumaliza maongezi yetu hatimaye, tuliagana, nami nikaelekea bafuni kuoga.
Nikiwa bafuni, hali ya ghafla ikanijia na nikaanza kumkumbuka Mary. Hasa kipindi kile kaja Dodoma na kuishi pamoja, nilianza kukumbuka jinsi tulivyokuwa tunadinyana mle bafuni. Nilimkumbuka jinsi nilivyokuwa nikimvuta karibu, nikimuinamisha, na kupeleka moto huku akitoa miguno ya sauti.
Kumbukumbu hizo zilinizidia nguvu, zikaanza kunipa maswali mazito moyoni. Nilishindwa kuamini kama kweli Mary alikuwa ameamua ku-move on kabisa. Kwa jinsi alivyokuwa akinipenda, sikutarajia kumuona akinichunia kwa muda mrefu namna ile. Hofu ilianza kunijia polepole, nikahisi labda kweli ameamua kufanya maisha yake bila mimi. Zaidi ya yote, tukio lile la kumkuta na mwanaume pale kwake liliendelea kunisumbua sana kichwani. Lilikuwa ni jeraha ambalo halikuwa limepona kabisa.
Moyo wangu haukuwa tayari kumpoteza Mary. Kadri nilivyofikiria, ndivyo nilivyozidi kuona kuwa bado kulikuwa na nafasi, au angalau nifanye jaribio la mwisho. Ndipo nikaamua kuwa ni lazima nimtafute Jane. Nilihitaji kuzungumza naye kwa kina kuhusu hili, kwa sababu nilimwona yeye kama mtu pekee ambaye angeweza kutuunganisha tena.
Nilijisemea moyoni, kama bado kuna uwezekano wowote wa kunirudisha kwa Mary, basi Jane ndiye funguo kwasasa.
Kesho yake saa tatu kamili asubuhi, nilienda ofisini kuonana na Erica pamoja na kukamilisha masuala ya kampuni. Nilipofika ofisini kwake, sikumkuta, hivyo nikakaa kwenye benchi nikimsubiri. Baada ya takribani dakika kumi, nilimuona akiingia na kukaa kwenye meza yake. Alipoinua macho na kuniona, alisimama ghafla na kuondoka tena bila kusema neno.
Nilishangaa kumuona anaondoka na nilijiuliza kimoyomoyo, huyu mama anaenda wapi tena? Nilihisi kama napoteza muda, hasa ukizingatia nilikuwa na ratiba nzito siku hiyo.
Haikupita hata dakika, simu yangu ikapokea ujumbe mfupi:
“Insider mpenzi, njoo mpaka parking.”
Nilisimama mara moja na kufuata maelekezo. Nilipofika parking, nilimkuta Erica amesimama pembeni, akinionyesha ishara ya kunisubiri. Tulitazamana kwa sekunde chache kabla sijaamua kuanza mazungumzo.
MIMI: “Hey baby.”
ERICA: “Insider, kwanini unanipa pressure?”
MIMI: “Samahani! Kulitokea emergency nikahitajika kwenda South Africa, nimerudi jana.”
ERICA: “Hata kunijulisha hukuweza? Hata message za WhatsApp hujibu. Ubusy gani huo hata kujibu ujumbe ni shida?”
MIMI: “Baby, naomba uniamini, naelewa unaweza kuona kama nakudharau au nakudanganya, lakini nimekuja Dodoma kwa ajili yako pia. Nimekumiss sana.”
Alikaa kimya kwa sekunde chache, kisha akabadili mada.
ERICA: “It’s okay! Hizo ndiyo documents nilizo-request?”
MIMI: “Yeah.”
Nilimkabidhi mafaili na aliyachukua na kuanza kuyapitia haraka, moja baada ya jingine.
ERICA: “Ziko sawa, sahivi unaenda wapi?”
MIMI: “Naenda kupitia biashara zangu kidogo, halafu nitarudi nyumbani. Ila ningependa baadaye uje home, upajue.”
Aliniangalia kwa aibu kidogo. Erica alikuwa mwanamke ambaye kujiamini kwake kulipungua kila mara nikimtazama moja kwa moja machoni.
ERICA: “Sawa, nitakupigia simu.”
Tuliagana, kisha nikachukua bajaji kuelekea ofisini kwangu. Dakika chache baadaye nilikuwa tayari nimefika, nikamsalimia Sanchi, nikazunguka ofisini kukagua shughuli na kuwasalimia vijana wangu.
Baadaye nilirudi tena kwa Sanchi. Safari hii, alianzisha mazungumzo kuhusu Erica. Unajua kipindi ambacho Erica anakuja ofisini kwangu kufanya ukaguzi, alikutana na Sanchi, ambaye nilimtambulisha kama Secretary wa kampuni. Sasa kipindi ambacho niko South, Erica ananitafuta halafu sipatikani na message zake sijibu, yeye alikuwa anamtafuta Sanchi na kumuulizia taarifa zangu.
Kutokana na experience ya Sanchi kama dada mkubwa, alinusa kuna something fishy kinaendelea kati yetu. Sasa muda ambao tunapiga story alinibana kwa maswali mengi, akitaka kujua kama kuna uhusiano wa kimapenzi kati yangu na Erica . Hatahivyo sikupenda kuingia ndani sana, nikajibu kwa mkato kwamba ni ushirikiano wa kikazi tu, na hakuna chochote.
Sanchi alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anafurahi sana akiwa karibu na mimi. Tulikuwa ni watu wakupiga story nyingi sana na kupanga mipango mbalimbali ya biashara. Nilikaa pale kwa takribani masaa mawili, kisha nikaondoka kwenda kupumzika nyumbani, nikimuaga Sanchi.
Saa kumi jioni, Erica alinipigia simu kunijulisha kuwa alikuwa anatoka ofisini, akaniomba nimuelekeze mahali napoishi. Nilimpa maelekezo, akasema asingechukua muda mrefu kufika.
Baada ya simu ile, nilijikuta nikitabasamu peke yangu. Nilijua tu, jioni ile ingekuwa tofauti, kimoyomoyo nilijisema huyu leo lazima nimle siwezi kumwacha salama “Mbuzi kafia kwa muuza Soup.”
Baada ya dakika ishirini, Erica alifika nyumbani. Nilitoka nje, nikamfungulia geti na kumkaribisha kwa heshima. Alikuwa bado amevaa nguo zilezile za asubuhi kazini wakati tunakutaba. Nilimpokea mkoba wake na kumkaribisha ndani kwa tabasamu nene, hao tukaingia ndani na kukaa sebleni.
MIMI: “Chakula au kinywaji?”
ERICA: “Maji tu yanatosha.”
MIMI: “Nikuagizie chips bhana.”
ERICA: “No thank you, niko full.”
MIMI: “Unywe wine bhasi.”
Akaniangalia na kutabasamu,
ERICA: “You know situmii alcohol.”
MIMI: “I know.”
ERICA: “So! Hapa ndiyo unaishi ndugu Director.”
Nikacheka sana baada ya kusikia akiniita vile,
MIMI: “Ndio mummy, nimefurahi umekuja kutia baraka kwenye nyumba yako.”
Mazungumzo yetu yalianza kuhusu mambo ya kampuni ambapo alinihakikishia kuwa kila kitu kinafanyika kwa kufuata sheria na taratibu, na kwamba suala la kampuni lingekamilika muda si mrefu. Baada ya hapo, mazungumzo yakageukia maisha yake binafsi. Alinihadithia kuhusu familia yake, malezi yake, na mambo mengine mengi. Kwakweli nilimjua kwa undani zaidi kuliko nilivyowahi kumjua hapo awali.
Wakati huo, akili yangu ilikuwa ikitangatanga mbali. Nilikuwa nawaza ngono tu kichwani muda huu, nilikuwa namtamani sana. Erica ni mwanamke aliyebarikiwa sura, na hips ila ana makalio ya kawaida, sasa akikaa hips zake zinajiachia “bwelelee!” -Ahh! I hate this life.
Hesabu zangu zilikuwa ni kumtoa pale seblen na kwenda naye chumbani, nikamuweke wala sikuwa nawaza vingine. Alikuwa akinipigisha story nyingi, lakini mimi hata sikuwa pale, nikaamua kuanza kushambulia;
MIMI: “Baby, twende chumbani tukapumzike.”
ERICA: “Hapana, hapa hapa panatosha.”
MIMI: “Nilifikiri umechoka na kazi.”
ERICA: “Bado nipo sana na wewe, leo ungependa kula nini, nikupikie?”
Tulikwenda jikoni, na tulipofungua fridge, hakukuwa na kitu, akanicheka sana, kisha tukaamua kwenda supermarket kununua mahitaji. Tulirudi baada ya muda mfupi na kuanza kupika pamoja, tukicheka, nikimpa utani na kupiga story mbalimbali. Kwenye suala la kuongea na mwanamke na kumfanya afurahi hapa nina A+ kabisa, ni mtihani mwepesi sana kwangu.
Baada ya kumaliza kupika tulirudi tena kukaa seblen. Erica suala la kwenda chumbani hakutaka hata kulisikia, ni kama alihisi kwamba hawezi kutoka salama. Kwangu mimi haikuwa kikwazo, maana ninaelewa fika kwamba, kwa mara ya kwanza ili uichape lazima msumbuane sana. Taratibu nilimsogelea na kuanza kumuonesha mahaba waziwazi, nikianza kwa kumshikashika baadhi ya maeneo chokozi, huku namwambia maneno matamu ya kumfurahisha.
Mwanzoni, hakuwa ananipa ushirikiano sababu alionesha kutojiamini na alishikwa na aibu. Baadae alianza kunipa ushirikiano hadi kupelekea mahaba kukolea. Ilifika stage akawa anatetemeka sana na kuweweseka sana kadri navyoongeza spidi ya kucheza na maeneo yake muhimu.
Nilimbeba juu juu na kuanza kwenda naye chumbani na hapa akaanza kuongea kwa kutoa sauti ndogo, lakini iliyosikika;
“Please, let’s not go to the bedroom
Lakini, mimi hata sikujali maana nilikuwa tayari nina mizuka yangu imepanda. Changamoto ilikuwa ni kwenye kutoa pichu maana kote nilifanikiwa, ila hapa ilikuwa ni kimbembe maana ni kama akili zake zilirudi kwa kasi ya 5G. Imagine unaona kila kitu live, lakini kuitoa pichu ni mtihani maana alikuwa hataki kabisa. Hadi nafikia hii stage, tayari tulikuwa tumesumbuana vya kutosha, ilikuwa ni kurupushani.
Baada ya kuona tunasumbuana sana, hata mimi munkari ulinikata kabisa, hivyo nilihisi wazi kuwa sikuwa tayari kuendelea na zoezi. Nilifanya maamuzi ya kuacha, nilisimama na kwenda bafuni kuoga. Muda huu nilijikuta nikitafakari kwa kina misingi niliyoiweka kwenye maisha yangu, principles ambazo nimeishi nazo kwa muda mrefu bila kuzivunja hata siku moja.
Kwanza kabisa, sijawahi na sitawahi ku-force sex. Kwangu, mapenzi hayalazimishwi, yanatakiwa yatokane na ridhaa ya dhati ya pande zote mbili. Pili, sijawahi kufanya sex na mwanamke aliyekunywa au ambaye hajitambui. Hilo huwa naliona kama kuvuka mipaka ya utu na heshima, jambo ambalo dhamira yangu hailikubali. Na mwisho, sijawahi kununua malaya wala kumhonga mwanamke ili nipate sex. Sioni fahari yoyote kwenye tendo linalonunuliwa au kulazimishwa na mazingira ya kiuchumi.
Ndani ya moyo wangu, nilijua kuwa maamuzi niliyoyachukua yalikuwa sahihi, hata kama hayakuwa mepesi. Nilimaliza kuoga, nikajifuta taratibu, na nilirudi kwenye hali yangu ya kawaida na kuwa mtulivu.
Baada ya kutoka bafuni, nilirudi sebuleni nikiwa na laptop yangu. Erica alikuwa amelala kitandani. Niliendelea na kazi zangu, nikichambua ripoti mbalimbali, hasa zile za ofisini Masaki. Lakini akili yangu ilikuwa ikivuta taswira ya tukio ya kilichotokea awali.
Ilipita kama nusu saa hivi. Kulikuwa na ukimya mzito ndani ya nyumba. Nikaamua kuchungulia chumbani. Nilimkuta amelala fofofo, usingizi mzito wa mtu aliyechoka kimwili na kiakili. Nilimtazama kwa sekunde chache, kisha nikatoka kimya kimya.
Nikatoka nje kwenda kumuulizia kaka Bony, nikidhani ningempata ili kumsalimia. Kesho yake nilitegemea kuondoka kurudi Dar es Salaam, na kuondoka bila kumuona kaka Bony niliamini isingekuwa jambo la busara. Nilipofika mlangoni kwa apartment yake na kugonga, mke wake ndiye aliyenifungulia. Aliniambia kuwa Bony alikuwa bado hajarejea kutoka kazini.
Nikamuaga kwa heshima, kisha nikarudi ndani kwangu, sebuleni, nikaendelea na kazi zangu. Muda ulikuwa umesogea sana tayari ilikuwa saa mbili usiku.
Baada ya takribani dakika ishirini, nilimsikia Erica akitoka chumbani. Alikuja sebuleni taratibu na kukaa pembeni yangu. Alikuwa bado amevaa pichu, lakini juu alikuwa amevaa bra. Hakuwa anaongea, alikaa tu kimya, karibu nami. Ukweli sikuwa na hamu naye tena na nilizungumza mkono nikamshika kiuno chake laini.
MIMI: “Uko sawa?”
Alinitazama kwa macho yaliyojaa hisia, kisha akatikisa kichwa taratibu kuashiria ndiyo. Alikaa kimya kwa sekunde chache, kama alikuwa anapanga maneno moyoni, kisha akaanza kuzungumza kwa sauti ya chini.
ERICA: “Insider, I’m so sorry. Mimi ni bikra sijawahi kabisa kuingiliwa na mwanaume yeyote. I swear.”
Maneno yale yaligonga masikio yangu kwa uzito mkubwa. Bila kusema neno, nilifunga laptop yangu polepole na kuiweka mezani. Kisha nikamgeukia kabisa, nikamkazia macho, nikimtazama kwa umakini na utulivu.
Kwa mara ya kwanza nilihisi kama ananidanganya, sikuyakubali maneno yake moja kwa moja. Kwa umri wa mwanamke kama yeye, aliyeajiriwa na aliyekuwa kazini, niliona ni jambo gumu sana kuwa bado ni bikra. Nilikuwa mkubwa kwake kwa miaka mitatu, na mawazo yakaanza kunijia, yaani amalize Form 4 salama, amalize Form 6 salama, apite chuo bila matatizo hapa nilihisi kama akili zangu zinachezewa.
Kulipita kama dakika kadhaa tukiwa hatuongei. Mimi nilikuwa nikitafakari kwa kina kauli yake. Baada ya muda, nikamwambia asogee karibu nami, nikamkumbatia taratibu.
MIMI: “Are you sure wewe ni virgin?”
ERICA: “Kweli, sikutanii mpenzi. I swear, lakini ninaigopa mwenzio.
MIMI: “I will do it gently, na uta-enjoy. Huna haja ya kuogopa.”
Aliniangalia, akatabasamu kwa aibu ya kuvutia, na hapo nikajua amekubaliana na kauli yangu. Bila kupoteza muda, nikamnyanyua kwa haraka na kuingia naye chumbani kwa mara nyingine, nikiwa na dhamira ya kumleta Erica katika ulimwengu mpya wa mapenzi.
TO BE CONTINUED