Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 26

“A TRUE STORY BY INSIDER”

Jumatatu ya Pasaka asubuhi nilifanya mawasiliano na yule constructor wa Mzee na nikamwambia baada ya lisaa nitakuwa Mbweni na yeye alisema yuko njiani ndo anaelekea.

Kwa upande mwingine yale materials ya kununua nilimtumia picha Mzee Mollel na alinisaidia kunitajia bei na kunipa connection kwa sehem yanakopatikana, alinitumia namba za baadhi ya masupplier akanambia nikiwapigia simu niwaambie yeye ndo amenikonekti.

Baada ya kufika Mbweni nilikuta kazi zikiendelea na mimi niliwasalimia Mafundi na Jamaa alikuwa amefika tayari.

Sababu alikuwa anajua kinachoendelea pamoja na ujio wangu, hata hakuwa na maswali zaidi alisema nimpe pesa akanunue materials.

“Kwenye kununua materials tutakwenda wote mkuu usiwe na wasiwasi.”

Na muda huu nilifanya kuwasiliana na baadhi ya supplier na tukapata mmoja pale Africana ndo alikuwa na bei nzuri.

Tulikwenda wote na Jamaa mpaka Africana kuna duka kubwa sana pale lipo mataa ya Africana, mkono wa kushoto kama unakwenda Juliana.

Tulifanya manunuzi ya materials mbalimbali na tukarudi Mbweni, vifaa vyote nilisimamimia manunuzi. Jamaa kama alimind hivi kwanza, pia hakuwa akiamini kuona nayajua maduka vile, kumbe nyuma ya Pazia alikuwepo mzee Mollel anayenipa CODE.

Sababu hii siku nilikuwa na miadi na Mama wa2, nilimwaga jamaa na nikaondoka. Nilitoka pale Mbweni kuelekea Mbezi Beach na muda huo ilikuwa saa 6 kasoro za mchana.

Hii siku tulikuwa tunakwenda kumpokea mdogo wake Airport na kuhusu kwenda kuangalia nyumba yake alisema tutakwenda siku nyingine.

Mama wa2 alitumia dakika 30 kutoka ndani na tukaelekea Airport.

“Insider Unaendeleaje.”

“Safi tu, mgeni ataingia sangapi?”

“Saa 8 atakuwa amefika tayari.”

Tuliwasili pale JNIA na tulikwenda moja kwa moja mpaka Terminal 2 ndo tukapark gari. Tuliamua kwenda kukaa kwenye kimgahawa tukimsubiri mgeni.

“Insider leo jioni nataka twende Masaki na wanangu tukatembee.”

“Sawa haina shida mimi nipo free leo.”

“Nilipata taarifa Uber wanasitisha huduma zao vipi kwako utafanyaje?.”

“Kwa wateja wa Card na kampuni bado wanaendelea ila wanaotumia card ni wachache sana, wateja wa cash ndo wengi kwa bongo hapa. Sio mbaya sana lakini maana Bolt bado wapo japo imeniathiri sana.”

“Pole sana ndo changamoto hizo naamini watarudi soon.”

“Ni mambo yanayohusisha serikali acha tuone itakuwaje.”

Suala la Uber kusitisha huduma zao kwa upande wa magari ni kutokana na LATRA kuwataka kupunguza kamisheni zao kutoka 25% mpaka 15%. Madereva wa Tax mtandao wolilamika kwa mamlaka husika kuwa hizi kampuni zinatoza kamisheni kubwa sana. Uber hawakuwa tayari kupunguza kamisheni zao kwani walisema wanatozwa kodi na tozo kibao hivyo wangeendesha biashara kwa hasara.

Tuliendelea kukaa pale na Mama wa2 huku story zikiendelea maana ndege ilichelewa kutoka KIA kwa taarifa ambazo Mama wa2 alizipata.

Saa 9 kasoro ndege iliwasili na na baada ya dakika 15 mamdogo alitoka na wakakumbatiana na dada yake pale. Walionekana kumisiana sana.

Nilimsaidia kubeba bag lake na tulikwenda parking tulikokuwa tumepark gari na tukaanza safari ya kurudi Mbezi Beach.

MAMA WA2: “Insider huyu ndo mdogo wangu wa mwisho anaitwa Joana.

MIMI: “Nimeona pia mmefanana sana, Joana karibu sana Dar es Salaam.”

“Ahsante.”

MAMA WA2: “Huyu anaitwa Insider ni mtu wangu wa karibu sana.”

MIMI: “Mama mkwe hujawai kunambia kuwa una mdogo mzuri hivi.”

Na wote waliishia kucheka muda huu na walikuwa wamekaa siti za nyuma.

Njiani walikiwa busy sana wakiongea mambo yao na tulitumia kama dk40 kufika nyumbani maana hakukuwa na foleni kabisa.

Tuliingia ndani muda ule na mimi nikatoa bag la mgeni nikaingiza ndani.

Baada ya kuingia ndani mamdogo alisalimiana na kina Rachel na Pili na mimi muda huu nilikuwa nawaza msosi maana njaa ilikuwa inanigonga balaa, toka asubuhi nilikuwa sijaingiza chochote tumboni.

Mama wa2 alitukaribisha dining kwaajili ya lunch na mimi ndo nilikuwa wakwanza kufika pale. Nilikuwa nimeshapazoea kwa Mama wa2 ilikuwa kama niko nyumbani tu.

Na wakati tuko dining Mama wa2 aliwaambia bint zake wajiandae kwaajili ya kutoka out. Mama wa2 alikuwa busy sana na mdogo wake hii siku hata nilipomaliza kula nilimshukuru kwa chakula na mimi nikaenda kukaa seblen.

Joana pia alikwenda kujiandaa na wakati huo bint zake walikuwa wako tayari wamejiandaa.

MAMA WA2: “Insider tunakwenda wapi eti?”

PILI: “Mama twende Slip way.”

MIMI: “Kama watoto wanataka kwenda huko tuwapeleke haina shida.”

MAMA WA2: “Bhasi tutakwenda huko.”

Na muda huu akina Pili na Rachel walionekana kufurahia sana kwenda huko.

Baada ya dakika 20 mamdogo alikuwa naye kajiandaa na ametoka hao tukaanza safari na muda huo ilikuwa saa 11 jioni.

Tulitumia dakika 25 kufika eneo lile na hii siku palionekana kuwa busy sana na tulikwenda upande wa chini wa Restaurant.

Tulitafuta sehemu nzuri ya kutosha watu sita na tukakaa, kwenye hii meza mimi pekee ndo nilikuwa mwanaume pale na hii ilikuwa ikinipa ufahari flani hivi.

Kila mtu aliagiza anachotaka kwa upande wangu sikutaka kuagiza chakula maana nilikuwa nimeshiba, niliagiza heineken 3 tu maana sikutaka kulewa hii siku. Kwa upande mwingine mama wawili aliagiza bucket ya Savanna kwaajili yake na mdogo wake.

Story zilikuwa zimetawala meza yetu tukicheka na mimi nilikuwa nimekaa karibu na Pili nampigisha story sana,

Sasa wakati dada analeta vinywaji Pili alishangaa sana kuona dada kaniwekea heineken pale mezani.

PILI: “Uncle Insider na wewe unakunywa kumbe?”

MIMI: “Nakunywa kwaajili yako hapa.”

PILI: “Toka hapa! mimi situmii pombe”

MIMI: “Wewe ni mchaga soon utaanza kutumia, muulize mama yako alianzaje kutumia. Unataka sikuonjeshe kidogo?”

PILI: “Aku sitaki mimi. Kwanza Baba yangu sio Mchagga”

Pili alikuwa kashanizoea kwa muda mfupi hata Mama wa2 alishangaa sana kuona Pili kanizoea haraka vile.

Mida ya saa moja usiku wakati tukiendelea kunywa na kupiga story, Prisca alinipigia simu, nikaamua kutoka eneo lile ili nikaongee naye mbali na pale.

PRISCA: “Hello baby how you doing?”

MIMI: “Niko poa za toka jana.”

PRISCA: “Safi tu, nimekumiss”

MIMI: “Jana ulinambia mnatoka as family nipe ripoti.”

PRISCA: “Insider ungekuwa unanijali ungekuwa ulinipigia simu na ukajua kinachoendelea.”

MIMI: “Aisee, nijue kinachoendelea kwenye mambo ya familia yenu?, naona kama unanikosea.”

PRISCA: “Sasa unataka ripoti ya nini?”

MIMI: “Ripoti niliyotaka mimi nijue ulirudi sangapi, Jana sikutaka kukutafuta maana nilijua utakuwa busy na Familia.”

PRISCA: “Okay we had funny yesterday, inshort we enjoyed.”

MIMI: “Nice na uko wapi kwa sasa?”

PRISCA: “Niko home nimelala on bed. Nimekumiss nataka nikuone.”

MIMI: “Acha uongo unanimisije na upo period?”

PRISCA: “Insider unataka kumaanisha kwasababu niko period siwezi onana na wewe? You only want sex from me that's all you care about.”

MIMI: “Prisca mimi naona hayo ni mawazo yako, ila naomba utambue kitu kimoja. Usifikiri mimi kama napenda sana kumchepuka Mama Junior na ninampenda sana. Unapaswa kunipa vile navyokosa kwa Mama Junior na sio kulalamika, kumbuka ulichagua mwenyewe na hukulazimishwa na kama unaona nakuumiza unaweza kuniacha na maisha yangu.”

PRISCA: “Leo ndo nimeprove upo na mimi kwasababu ya shida zako na huna hata tone la upendo kwangu, Ahsante nashukuru.” Akakata na simu.

Mimi sikutaka kumpigia tena simu niliamua kumpotezea na nikasema hasira zake zitakuwa sababu ya Period.

Wakati nimerudi pale mezani Mama wa2 aliniangalia afu akatabasamu

“Insider naona ulikuwa kujenga matofali”

Na mimi niliishia kucheka tu muda huu.

Tulikaa mpaka saa4 usiku ndo tukatoka pale na muda huu Mama J alikuwa akisumbua sana kwa kupiga simu.

Baada ya kuwashusha akina Mama wa2 alinipa malipo yangu na mimi nikaelekea nyumbani.

Nilimkuta wife yuko seblen anaangalia movie na mimi niliwasalimia na nikaunganisha bafuni kuoga.

Wakati nimetoka bafuni nilimkuta wife yuko kitandani amejilaza kizembe.

MIMI: “Nambie swahiba toka jana hatujaongea kabisa, hujanambia sikukuu ilikwendaje.”

WIFE: “Ilikuwa poa tu, Mama anakusalimia pia amesema uache tabia mbaya. Kwanini hupendi kujumuika na sisi?”

MIMI: “Usijali mwambie nitakwenda msalimia, na vipi kuhusu Mzee ulifanikiwa kuongea naye?”

WIFE: “Ndio alisema mwisho wa mwezi huu atanipa hizo hela.”

MIMI: “Wow nice umetisha sana swahiba, nafanya haya mambo kwaajili yako na hii bajaji tutatumia jina lako.”

WIFE: “Sawa haina shida, twende ukale maana leo nimekupikia vitamu.”

MIMI: “Sawa tangulia nakuja.”

Muda huu nilikaa kitandani maana nilikuwa nafuraha sana kuona jambo limefanikiwa tayari.

**********

Hii week baada ya Pasaka nilikuwa nashinda tu kule kwa Mzee Pama Mbweni. Asubuhi nikishawapeleka wateja wangu Posta naunganisha moja kwa moja mpaka Mbweni. Sikutakaa kaa mbali kabisa na eneo la tukio nilitaka kusimamia kila hatua kwenye ile nyumba.

Kazi ilikuwa inakimbia balaa na kwa upande mwingine mtu wa bustani alikuwa amekuja tukakubaliana bei na nikamwambia miti na maua tutakwenda nunua wote.

Mpaka kufikia jumapili nyumba ilikuwa imekamilika kila kitu kwa ndani na ilibaki vitu vidogo nje vya kumalizia kama kuweka tank na kumalizia pavings. Jumatatu ndo tulimalizia kila kitu na nikatafuta mtu wa kufanya usafi mle ndani, nje na kutengeneza barabara inayokwenda kwenye ile nyumba maana ilikuwa mbovu sana.

Kufikia jumatatu kila kitu kilikuwa kimekamilika vilibaki vitu vichache sana ambavyo sio vya lazima, lakini nyumba ilikuwa tayari kwaajili ya kuhamia.

Katika zile Pesa ambazo alinikabidhi mzee nilibakiwa na kama 3,200,000/= na hapo ndo nikajua jamaa alimpiga mzee japo pia nilipata discount kwenye mizigo ila kulikuwa na balance kubwa sana.

Niliitamani sana hii pesa lakini niliogopa jamaa anaweza kunisnitch kwa Mzee akampa hesabu za vitu na gharama zote afu nikapoteza trust kwa Mzee. Palepale nikachomoa million moja nikasema hii nitaitolea maelezo kwa Mzee ila hii amount inayobaki nitamrudishia.

***********

Kwa upande mwingine Jumapili ndo siku ambayo Pili alikuwa ana rudi shule hivyo Mama wa2 aliomba kampani yangu.

Nilitoka Mbweni kuelekea Mbezi Beach kwa Mama wa2 na saa 7 mchana nilikuwa pale.

Saa 8 mchana ndo tulitoka kuelekea Bagamoyo shuleni. Tulitumia saa moja na nusu kufika Bagamoyo shuleni na Mama wa2 alikwenda kumkabidhi.

Na hii siku walionekana Wazazi wengi wakiwarudisha watoto wao shule.

Baada ya kumuandikisha kuna sehemu tulikaa tukiwa tunaongea na mimi nilimshauri sana Pili asome kwa bidii na akae mbali na wanaume. Ilibidi nimchane ukweli ajitunze Mafisi “wazee wa kula kimasihara” sio watu wazuri Kabisa awe makini.

Pili alionekana kuwa makini sana akisikiliza ushauri wangu na nilitoa laki moja nikampa itamsaidia kama pocket money.

Niliona aibu kumwacha bila kitu afu mama yake alikuwa kanisaidia mkopo wa Pesa nyingi, niliamua kurudisha shukrani kwa njia hiyo.

Pili alishukuru na alifurahi sana, akasema next time nikamchukue na Mama yake pia alimpa Matron namba yangu incase kama kuna lolote wanaweza kunipigia na mimi. Na mama wa2 alininiandikisha mimi kama Uncle wa Pili.

Tuliondoka pale shuleni na kuanza safari ya kurudi Dar na njiani tulikuwa tukiongea mambo mengi sana na Mama wa2.

MAMA WA2: “Insider mwanangu Pili amekuzoea haraka sana, the way ambavyo unaongea naye nilikuwa najiskia faraja sana. Baba yake hajawai hata siku moja kumpa ushauri binti yake nashukuru sana kwa leo.”

MIMI: “Pili ni kama mdogo wangu lazima nihakikishe anafikia malengo yake na kama unajambo lolote usisite kunambia.”

MAMA WA2: “Next time utamfata wakifunga shule.”

Tulitumia lisaa kufika Mbezi Beach nikamwacha kwake na mimi nikarudi zangu home mapema sana.

Usiku mzee alinicheki akanambia kesho nikamchukue Airport ndo anarudi na anatarijia kuingia saa 7 mchana na alinisisitiza sana kuwa ontime, maana tungeenda na kukagua nyumba kule Mbweni.

Asubuhi nilimka mapema na nikafanya usafi wa gari mwenyewe na baada ya kumaliza nilirudi ndani ili nipate kifungua kinywa.

*********

Tarehe 26 ndo siku ambayo mzee alirudi kutoka safari na ilikuwa ni siku ya Muungano. Na mimi mapema sana nilikuwa pale Terminal 3 nikimsubiri.

Nilimcheki dada Tyna akanambia yuko busy atanichek mida kidogo, na muda huu nilikuwa nikipiga story na yule jamaa yangu mlinzi.

Saa 8 kasoro ndo muda ambao mzee Pama aliwasili pale JNIA na nilimpokea na baada ya dakika chache tuliondoka maeneo yale.

Safari yetu ilikuwa ni kwenda moja kwa moja mpaka Mbweni ili afanye ukaguzi wa nyumba. Na tulitumia saa moja na nusu kufika pale

Mzee alifanya ukaguzi wa nyumba na aliridhika kuona jinsi ujenzi ulivyokuwa umekamilika vizuri tena kwa viwango vya hali ya juu. Pia alishangaa kuona nimetengeneza ile Barabara na imekaa vizuri, alishangaa kuona nimetengeneza bustani mpaka nje ya geti na palikuwa pamejengwa vizuri. Mzee pia alinisifu kwa kufanya usafi wa nyumba nje na ndani.

Mzee alimjengea mchepuko wake mjengo mkali sana tena wa kisasa, nyumba ilikuwa kubwa ya vyumba vinne.

MIMI: “Mzee naona unataka kuwa na Familia kubwa vyumba ni vingi sana.”

MZEE: “Nataka anizalie watoto wa3 hata pale tayari ni mjamzito.”

MIMI: “Hongera sana Mzee ni jambo la neema hilo.”

MZEE: “Kabisa, Kijana niseme Ahsante kwa kazi nzuri uliyofanya umenifurahisha sana, materials ni zenyewe hakuna ulichokosea.”

MIMI: “Mzee nilikuwa namsimamia Fundi mwanzo mwisho nilikuwa nakuja asubuhi nashinda na Mafundi jioni narudi nyumbani. Ndomana unaona kila kitu kimeenda vizuri na kwa wakati sahihi.”

MZEE: “Hii nyumba nimejenga kwa siri sana hakuna anayejua kabisa hili suala.”

MIMI: “Sasa suala la watoto vipi hutaki wajuane?”

MZEE: “Hao hakuna shida watajuana tu ila sitaki ifahamike kama mke mdogo anakaa huku italeta shida.”

MIMI: “Sawa mzee hapo nimekuelewa”

Mzee Pama alikuwa ni mzee wa umri wa miaka 60-65 alikuwa anacheza humu ila alikuwa ni dizaini ya wale wazee wajanja au wahuni.

Tulitoka pale Mbweni saa 11 jioni na Mzee alinambia nimpeleke kwake Ununio.

Wakati tumeingia kwenye gari nilifungua drow na nikatoa invoices za manunuzi na nikamkabidhi, na alianza kuzitizama muda ule.

MIMI: “Mzee na hii Pesa ndo ilibakia kwenye manunuzi.”

MZEE: “Kijana kama pesa imebaki ni yako, umefanya kazi kubwa sana. Bila kumsimamia Fundi vizuri angenipiga yule mshenzi.”

Nilimshukuru Mzee na nikawasha gari ili tuondoke eneo lile. Nilimpeleka Mzee kwake ununio na akaniahidi kunitafuta kwani kuna vitu vya kununua vingi anataka nimsaidie kusimamia.

Muda huu nilijikuta nam-miss sana Iryn kwakweli, kwani ndo ilikuwaga mida ya kwenda kwa Iryn kumchukua. Licha ya yote Iryn alikuwa ni moja ya watu wangu wa karibu sana na ilitokea kuelewana sana.

Tulikuwa tunakwenda karibu mwezi bila mawasiliano yoyote na nilikuwa sijui maendeleo yake, kipindi hiki.

Kwasababu mwisho wa mwezi ulikuwa umekaribia nikawaza muda ule niende kwake Kijitonyama. Na lengo langu ilikuwa nijishushe nimwombe msamaha kama kuna sehemu nilimkwaza.

Niliona sometimes ni bora kuwa mjinga ili mambo yako yaende ila kwa upande mwingine niliwaza hivi nikijishusha sana si ataniona mimi bwege? Yaani bila yeye maisha yangu hayaendi? Niliwaza pale ataweza kunisumbua sana huko mbeleni. Pia nilikuwa nawaza ni jambo gani ambalo limemkera mpaka kuchukua maamuzi yale?. Iryn ni mwanamke ambaye ni hatabiriki “UNPREDICTABLE”.

Saa 12 jion nilikuwa pale kwa Iryn Kijitonyama na hata sikumpigia simu niliamua kwenda bila kutoa taarifa, nilitaka iwe saprize.

Nilipark gari nje ya geti na nikafungua geti maana nilikuwa tayari mwenyeji kwenye zile apartments. Niligonga mlango wake na baada ya dakika kadhaa alitoka kufungua.

IRYN: “Ooh Insider karibu na nilikuwa nawaza nikupigie simu toka jana ili uje tumalizane maana namzigo wako.”

MIMI: “Ooh sawa ila mimi sijaja kwaajili ya hilo, nimekuja kukuona na kukujulia hali maana ni muda kidogo toka unitumie ile text ya kuterminate mkataba, pia nilitaka kujua sababu ni nini mpaka ukaamua vile.”

IRYN: “Insider hakuna sababu yoyote na hakuna jambo lolote baya ambalo umefanya, ila nataka kufocus na masuala ya mama kwa sasa.”

MIMI: “Kama hakuna jambo nililokukosea ungenipigia simu na tungekaa chini tukaongea. Iryn mimi ni binadamu sijakamilika kwa asilimia mia, kama kuna sehemu nilikukosea nisamehe. Iryn naomba utambue mimi ni Mwanaume ambaye nakuheshimu sana na bado utaendelea kuwa mtu muhimu sana kwenye moyo wangu.”

IRYN: “Insider hakuna shida mimi naona wewe ndo una wasiwasi.”

MIMI: “Hapana mimi nimekuja kukuomba msamaha pale ambapo sikuwa sawa na nimekukosea. Sijaja hapa kuomba unirudishe kazini, masuala ya kazi ni yako na ni maamuzi yako wewe.”

Na muda huu Iryn hakuongea kitu bali alifunga laptop yake na kuingia chumbani na mimi nilikaa pembeni ya coach. Na baada ya dakika 3 Iryn alitoka akiwa ameshika bahasha ndogo ya kaki

IRYN: “Insider pesa zako hizi nimeweka na fine ya kuvunja mkataba na wewe.”

Na muda huu alinikabidhi ile bahasha na mimi nikasimama nikaipokea ile bahasha pale na nikaiweka mfuko wa nyuma.

MIMI: “Ahsante but nishaelewa tatizo ni nini.”

IRYN: “What do you mean?”

Na muda uleule nikamshika mikono yake miwili na nikapandisha mikono yangu kuzunguka kiuno chake na nikamvuta upande wangu kwa nguvu, kilikuwa kitendo cha ghafla sana. Nikampa ulimi wangu na yeye akanipa wake haraka bila kizuizi na tulichezeshana pale kwa sekunde kadhaa na palepale tulishtuka tukaacha ule mchezo.

MIMI: “I mean hiki ndo ulichokuwa unakitaka, Iryn thank you for everything, I have missed you so much. Mimi naondoka nikutakie maisha mema ila kama utahitaji msaada wangu never hesitate to call me. Byee.!

Nilimwacha pale Iryn katika sintofahamu kwani hakuweza kuongea neno lolote muda ule na alikuwa akiniona nikipotea machoni mwake live.

Na wakati niko kwa gari nilikuwa mtu mwenye furaha sana na kama nilikuwa nimepata Nguvu mpya na nikajisemea pale “When one door closes another opens.”

TO BE CONTINUED
Bila IRYN hii story hainogi aisee
 
EPISODE 8
A TRUE STORY BY INSIDER MAN’

Nilirudi nyumbani huku barabara nzima nikiwa nawaza mambo mawili kichwani. Jambo la kwanza nilikua nawaza Iryn atakua anafanya kazi gani?, nilikua bado najiuliza kazi gani hii ya usiku??, au anafanya illegal?, …mmh hapana yule dada ni mrembo, pia kaniambia ana saloon sidhani kama anafanya hizi dili.

“….Anyway mimi naangalia pesa mambo mengine mimi hayanihusu kabisa, atajua yeye na maisha yake bwana, as long I get paid no problem”

Lakini pia nilikua nafuraha ya kufahamiana na mrembo kama yule niliamini pia ni bahati na nyota.

Upande mwingine nilikua nawaza jinsi ya kudeal na mama Junior maana sikutaka kumuweka wazi juu ya hili suala.

Nilikua bado najiuliza muda ule….

“Hivi kama nitarudi usiku bila kuwa na reason maalum inayoeleweka ,sindo chanzo cha ugomvi na makelele?, au nimwambie tu kieleweke??”. Lakini bado nilikua nakosa maamuzi kwa upande wa Mama J.

Wakati muda ule nikiwa nawaza simu ilianza kuita kucheki naona Dullah….Nikapokea.

“Dullah vipi ndugu yangu hatuonani”

“Tuonane wapi wakati ushaanza kuwa busy na watoto wazuri?”

Nikampa story Dullah jinsi ambavyo nimekutana na Iryn na mpaka kunipa kazi. Dullah akanambia “naona ushaanza kupagawa mapema hivi ndugu yangu hio ni intro tu”

Nikakatisha maongezi na Dullah baada ya kuona mama anapiga simu:

“Mwanangu hujambo?, hivi mama Junior karudi nyumbani?”

“Mama amerudi, haujaongea na mkamwana wako?”

“Sijaongea naye na muda kweli”

“Mhh mama yakweli hayo, maana naona kama haiwezekani”

“Kama amerudi nimefurahi msalimie Mjukuu wangu” (Mama yangu na Junior wamefanana sana, humwambii kitu kuhusu mjuu wake)

Ipo hivi mama yangu na mama J ni marafiki sana, hata mama alivyokua ananiuliza kuhusu mama J kurudi home nilikua najua lazima anafahamu ila ananizunguka tu.

Sielewagi mama J alitumia mbinu gani kuwa close sana mama yangu yaani ni wanapatana balaa, sio kwa upande wa mama tu hata dada yangu pia. Yaani anaweza kuwa na kosa yeye ila mimi ndo nikaonekana mkorofi.

*******

Kesho yake niliwai kuamka ili niwai kumchukua Mama wawili na mwanae, baada ya kumdrop mwanae nikampitia Maggy hao Posta. Japo kuamka asubuhi sometimes ilikua inakera sana unakua kama mtumwa. Lakini ukicheki una mkataba wa kazi na watu huwezi kuleta ufedhuli inabidi uwe mpole tu.

Upande mwingine yule dada wa kule Masaki- Olive alikua kanicheki kwamba kama nitaenda masaki tuonane ili tukubaliane bei, jumatatu nianze kazi ya kuwachukua watoto.

Nikaenda Kariakoo kuchukua Rim za gari na tairi mpya ili kubadilisha muonekano wa gari yangu. Baada ya kutoka hapo nikaelekea “@thewheel” Mikocheni, tukabadilisha tairi na Rim, aisee gari ikawa kali balaa, pale garage kila mtu akawa anaisifia IST yangu (nitawatumia picha chini).

Nikatoka hapo kuelekea Masaki kuonana na dada, nilikua pale saa 9 mchana, tukaongea pale, watoto walikua watatu (3) ambapo wakwanza nitakua namuacha pale Mikocheni karibu na Clouds media, hawa wawili walikua wanakaa Kunduchi- Bahari Beach ila maeneo tofauti.

Tukakubaliana kwa watoto wa Kunduchi atanipa 13,000 kwa kichwa na yule wa mikocheni atanipa 7,000. Japo baada ya week 2 aliongezeka mtoto 1 mwingine alikua anakaa kawe jumla nikawa na watoto 4, ila huyu mtoto wa kawe sikutaka kumtoza niliamua kutoa shukran kwa dada.

Hapo nilikua na uhakika wa kuingiza 165,000/= kwa week na tulikubaliana malipo yawe yanafanyika kwa week.

Baada ya deal kuwa done nikafurahi sana hapo tayari nilikua na uhakika wa kuingiza zaidi ya 2,000,000/= kwa mwezi.

Nilijiona na bahati sana kwa muda mfupi kupata wateja wa uhakika, hapo nilikua na uhakika hata nisipowasha App pesa itaingia tu.

******

Ijumaa ndo siku ambayo nilikua na miadi na Iryn kama tulivyokubaliana, niliamka asubuhi mapema sana 06:00. Kwa siku za weekend nilikua napenda sana kuvaa buti au sando, tshirt na cap kichwani, nikivaa buti/raba bhasi lazima nitembee na sando kwenye buti.

Nikapata trip ya kwenda Pwani “Marian boys school” kuna mzee alikua anampeleka mtoto wake shule.

Nikampigia simu chap

MZEE: “Kijana wangu hujambo nataka kumpeleka kijana wangu Marian schools pwani”

MIMI: “Mzee unakwenda na kurudi?”

MZEE : “Hapana kijana kuna kikao pia nitakuweka sana”

MIMI : “Mzee mimi sina shida kama utanilipa muda wangu”

MZEE : “si nitatumia gharama kubwa sana, maana sijui kikao kitachukua muda gani”

MIMI: “Sawa mzee wangu ila sasa kama unataka twende huko itabidi tusitumiee App, tukubaliane bei maana ukishaingia Pwani Uber haisomi, mpaka nirudi tena Dsm ndo nitaweza pata request. Na uhakika wa request mpaka nirudi Bunju atlist, kama upo tayari nikupeleke”

MZEE: “Sawa kijana wangu nimekuelewa unataka kiasi gani?”

MIMI: “Mzee kwenye App ilikua inaonyesha kiasi gani?”

MZEE: “30,000/=“

MIMI: “Bhasi utanipa 50,000”

MZEE: “Nitakupa 45,000 kijana wangu, uje haraka tuondoke”

MIMI: “Sawa mzee nakuja”

Mzee hakuwa mbali sana na mimi nakoishi yeye alikua anakaa nyuma ya Hospital ya Massana.

Unajua hawa watu ambao walikua wanaishi ushuani nilikua siwachekei kabisa, nilikua najua kabisa wanahela. Huwezi mpeleka mtoto Marian kama hauna hela.

Nikawapeleka mpaka Marian school, mzee akachukua namba yangu mimi nikageuka kurudi Dsm. Nilichoma wese, sasa wakati nakaribia “Bunju mwisho” nikapata request ya kwenda Airport.

Kufika pale nashangaa kumbe alikua ni kigogo wa serikalini.(Naibu waziri wa Wizara X)

“Mzee shikamoo hata nyie huwa mna request kumbe?”

“Kijana unashangaa tena, huu ni usafiri wangu sana”

“Nilijua unapiga simu, dereva anakuja chap kukubeba”

“Dereva naye ni binadamu leo ni weekend pia na haraka acha apumzike najali pia maisha yao binafsi”

“Sawa mzee hata hivyo tunashukuru hata mimi hapa nimepata ridhiki”

“Ni kweli ndo kutegemeana huku, sasa tutapitia pale TFNC kumchukua mke wangu afu tutaelekea Airport”

Tukatoka pale huku tukipiga story na yule Kigogo, akawa anauliza hali ya Maisha huku anamsifia Mama Samia na mimi namuunga mkono. Na mimi palepale sikutaka kuwa mzembe nikaanza kutengeneza connection maana nilisema hizi chance zinatokea mara chache sana.

Tulifika pale TFNC hizi ofisi zipo kule chini Ocean Road, bhasi tukafika pale tukasubiri kama dk 10 mke wake akawa amekuja hao tukaelekea Airport.

Kigogo alinisifia sana gari yangu kuwa safi, akanambia nimepanda Uber nyingi ila hii ni kiboko sana, akaniahidi atakua ananitumia. (Ila hakuwai nitafuta na alipigwa chini kwnye nafasi yake)

Niliwadrop pale Airpot Terminal 2, palepale kuna ndege ilikua inashuka nikapata request ya kwenda Mikocheni.

Baada ya kupiga kazi mpaka sa12 jioni nikasema acha nipumzike ofcoz ubao ulikua unasoma vizuri sana, kwenye ubao ulikua unasoma 95,000 ukijumlisha na ile 45,000 ya Asubuhi nakua na 150,000 tayari. Wakati nimemshusha yule kigogo pale Airport aliniongezea 10,000 ya ahsante nikasema hii nitaoshea gari badae.

“Ipo hivi mimi pesa ya kuoshea gari huwa sitoi kwenye faida zangu bali huwa natoa kwenye zile ahsante ambazo mteja ananipa, kuna wateja wako poa sana akifurahia huduma utakuta anakuachia chenji, sasa hizi nilikuaga nazitunza kwenye droo”

Nikapeleka gari carwash lipigwe usafi maana likikua lishachafuka tayari, nilitaka gari ing’ae kabla ya kumiti na Iryn. Nilitaka akute gari ikiwa safi.

Muda huo ilikua sa12 na madakika tayari, Iryn akanipigia simu kunikumbusha niwe on-time, nikamwuuliza timetable ikoje tunakwenda wapi na wapi?.

“Leo tutakwenda Ledger Plaza na Serena Hotel”, Iryn alijibu hivo.

Muda huo nilikua zangu pale Texas nimechili nimepumzika huku napiga story na wahuni. Texas nilipazoea sababu Uncle wangu alikua anapenda sana kuoshea gari pale.

********

Hatimae muda ulifika, ontime nilikua pale kumchukua dada kama kawaida alikua kawaka sana asee, niliishia kumtamani tu. Aliweka bag lake kwa nyuma ya siti “duffel bag” akaingia kwenye gari akakaa siti ya mbele, tukasalimiana hao tukaanza safari ya kwenda Bahari Beach, Ledger plaza Hotel.

Wakati tuko njian IRYN alinambia atakua ananitambulisha mimi kama dereva wake kwa mabosi zake, nikamwambia sawa haina shida.

Tulifika pale Ledger Plaza nikapark gari mrembo akashuka akachukua bag lake akanambia kaka sitokaa zaidi ya masaa 2, nikamwambia usiwe na wasiwasi bossy wangu. Nikaishia kumtizama mpaka anavyopotea.

Mimi nikashusha kiti nikalala zangu nikiwa pale Parking, sikutaka kutoka ndani ya gari na muda huo ilikua saa 3 tayari.

Kwa muda wa usiku pale Ledger panakuaga pametulia sana, sikutaka kwenda upande wa kule chini maana hata ningeenda wahudumu wangenisumbua tu. Na sikuwa na mpango wa kutumia pesa yangu niliona bora nichill kwenye gari.

Nilikaa pale parking, nilipitiwa na usingizi nakuja kushtuka ilikua ni text ya wife “Unarudi sangapi?”

“Wife leo ntachelewa kidogo samahani sikukupa taarifa nilikua nimebanwa, nimetembea na key zangu usiwe na wasiwasi”

“Okay, takecare” alijibu hivo.

Kuangalia muda ilikua ni saa 5 tayari lakini Iryn hakua na dalili za kurudi nikalala tena. Nilikuja kushtuka pale niliposikia mtu anagonga dirishani, nikashusha kioo fasta

“Huku aki tabasamu, Kaka sorry nimekuweka sana”

“Hapana usiwe na wasiwasi Bossy wangu, upo tayari tuondoke?”

Nilimwona kabadili mavazi sio yale ambayo alikuja nayo, akaweka bag lake nyuma, hao tukaanza safari ya kwenda Serena hotel.

Baada ya kufika Serena hotel, huyo akaingia ndani mimi nikaenda kutafuta parking. Kwa mazingira ya hotel kama zile huwezi kutoka nje kushangaa lazima utakutana na upinzani wa Askari na mimi sikutaka kukaa reception, hivyo niliamua niwe nakaa ndani ya gari tu.

Alitumia masaa 2 pale akanipigia simu nisogee mpaka reception ili tuondoke, kufika pale nikaona kasimama na Mzungu. Akanambia Insider shuka msalimie bossy wangu, mimi nikashuka akanitambulisha pale.

“Mr Robert, huyu anaitwa Insider ni dereva wangu” (kwa kiingereza)

“Nimefurahi kukufahamu Mr Insider naomba uwe makini sana na Iryn”

“Don’t worry Mr Robert, Iryn ni Boss wangu”

Palepale mzungu akatoa €20 akanipa, nikamshukuru, hao tukaondoka nimrudishe kwake. Nikamdrop pale kwake na mimi nikarudi home.

Wakati niko njian nilikua nawaza Iryn anafanya mishe gani hizi? “Huyu dem anajiuza ila atakua ni International maana hata hotel anazoingia ni 5 star”. Upande mwingine nilikua najiuliza mbona anaingia na kibag ndani au anauza sembe??

“Ila mambo yake binafsi mimi hayanihusu, hiyo sio kazi tuliokubaliana lakini siku nitamwuliza.”

Niliingia home saa 9 kasoro mama J alikua kalala, na mimi sikutaka kumuamsha nikaoga nikapanda kulala.

*****
Kwa biashara ya Uber siku za kupiga hela ni weekend nazungumzia ijumaa, jumamosi na jumapili kwa siku za kawaida bhasi jumatatu na alhamis (mwisho wa hii story nitawaelezea)

Kama kawaida niliamka jumamosi nikaaendelea na majukumu yangu ya kutafuta hela, nakumbuka hii siku niliimalizia kisarawe huko. Nilipata customer alikua anakwenda huko akaomba nimsubiri amalize kikao afu nimrudishe Dar.

Mimi kama nalipwa pesa nilikua sijali kabisa cha msingi tukubaliane sina neno. Tulikaa sana pale kisarawe kulikua na kikao mambo ya chama, walimaliza kwenye saa 10 jioni.

Tulirudi mpaka Dar nikamdrop jamaa pale Lumumba, tulichelewa sana kuingia sababu ya foleni pale Mbagala, sababu barabara ilikua inatanuliwa.

Nilivyotoka hapo uelekeo ulikua ni Kijitonyama kuonana na Iryn, saa 2 kasoro ilinikutia getini. Nikampigia simu kuwa nimefika akasema anakuja.

Alivyofika akanipa time table za usiku huo ilikua tunakwenda sehem 3, ratiba haikua ngumu sana kwani tulikua tunakwenda Hyatt, Golden tulip hotel ya Masaki na Palm village.

Yeye akasema tuanze na Golden tulip hotel, kama kawaida yake na kibag chake kakiweka nyuma tukaanza safari. Pale Golden alitumia masaa 2 tutatoka kuelekea Hyatt Posta, mimi kama kawaida yangu nikatafuta parking nikatulia.

Wakati niko parking mlinzi alikuja akanambia siruhusiwi kukaa parking, kama namsubiri mtu bhasi niende reception. Kama mnavyojua pale Hyatt ulinzi ni mkali sana.

Baada ya saa na nusu hivi Iryn akanipigia simu kwamba niende “level 8” ananisubiri, akaniambia niulizie nitaoneshwa iliko, ndo mara yangu ya kwanza naingia Hyatt. Kufika pale namkuta yuko na jamaa (kwa kumtizama alikua ni mtu wa S. Africa).

Level 8 ni restaurant ya pale Hyatt Hotel.

Akanitambulisha kwa jamaa kama dereva wake, Iryn akanambia niagize chakula tule then tuondoke. Mimi niliagiza seafood maana nilikua hata sioni cha kuagiza.

Jamaa akatusindikiza mpaka parking wakakumbatiana na Iryn, jamaa akaja upande wangu akanambia “Takecare of her”, mimi nikatingisha kichwa kama kukubaliana naye.

Tukaondoka, uelekeo ulikua ni Palm village. Iryn akatoa $100 akanipa, akanambia jamaa alinipa hii pesa ya mafuta itakua so busara nikiiweka mfukoni so keep it.

Kwenye gari tulikua tunazungumza kwa nadra sana, wakati tuko pale mataa ya NMB HQ/Puma filling station, tulikua tunatokea Ohio street ili tuingie Alli hassan road, nikaamua kuvunja ukimya, nikamwuliza kwa utani “Iryn wewe ni Mtanzania?”

IRYN: “Huku akicheka, kwani sionekani Mtanzania?”

MIMI: “Kabisa hapa bongo kama umevamia hivi”

IRYN : “Mama yangu alikua Mmursi-Ethiopia ila baba yangu ni Msouth Africa”.

MIMI: “Sasa ilikuaje mpaka ukaja Tanzania?”

IRYN: “Baba ameishi Tanzania toka 1995 kuna kampuni zake alikua anazisimamia huku na mimi nimekulia Masaki na nimesoma pale FK international school”

MIMI: “Ndomana umebarikiwa kwa uzuri Bossy wangu maana watu wa Ethiopia ni hatari”

Maongezi yetu yalipotea ghafla baada ya simu yake kuanza kuita, nilimind sana kimoyo moyo.

Tulifika pale Palm Village nikamdrop akanambia huku sitakaa sana, pale alitumia kama 1hr hivi akawa ametoka, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamrudisha kwake na mimi nikarudi home kulala.

Ile nimefika home namkuta wife hajalala yuko seblen anaangalia movie. Nikamsalimia nikakaa kwenye kiti.

WIFE: “Baba Junior umetoka wapi sahivi?”

MIMI: “Nilikua nimemsindikiza Michael Airpot, anakwenda masomoni Scottland” niliamua kumdanganya tu.

Michael ni jamaa yangu sana mpaka sasa, wakati tumetoka kwenye ile Taasisi X yeye aliamua kwenda kusoma Mastaz huko Ulaya. Wife anamjua vizuri sana hyu jamaa yangu.

WIFE: “Mbona kaondoka haraka hivyo hata kuniaga ameona shida”

MIMI: “Mambo mengi wife si unajua sisi wanaume, umepika nini? Naskia njaa sana” ilibidi nipotezee mada.

Huku wife akiniandalia msosi,

WIFE: “Mwanao anasumbua sana halali, kalala sio muda”

MIMI : “Pole ndo maana ya kuwa mama”

Baada ya kumaliza msosi nikamwambia wife mimi naenda kulala baada ya kuona yuko busy na movie yake.

Nikachomeka simu kwenye chaji nikakutana na message ya Iryn akinitakia usiku mwema, nikareply “Same to you Bossy wangu”.

*********
Jumapili sikwenda church kwanza nilichelewa kuamka, wife akaniamsha akaomba nikamsaidie kununua vitu sokoni.

Sababu dada alikua mgeni ikabidi niondoke naye hata akiwa peke yake awe anayajua mazingira.

Iryn akanipigia simu akanambia leo tutaenda sehemu 1 tu by 21:00 niwe around, tutakwenda Peninsula hotel. Hii Peninsula hotel ipo “Haile selasie road” karibu na Puma Filling station.

Nilitoka zangu home mapema nikaenda poteza muda pale survey, ilivyofika 3 kasoro nikaelekea Kijitonyama. Katika vitu ambavyo Iryn nilikua namsifu ni pamoja na kwenda na muda yaani akikwambia muda wa kufika utamkuta yuko tayari.

Nikamsifia pale, umependeza sana Bossy wangu,
akajibu “thank you, Gentleman”.
Siku ya leo hakua na kibag chake bali alikua na mkoba.

Kwenye upande wa kuvaa au kupendeza dada alikua yuko vizuri sana.

Ndani ya nusu saa tulikua tumeshawasili Peninsula hotel nikamdrop nikamwambia mimi nakwenda Samak samak kupoteza muda. Atakapokuwa tayari bhasi anipigie ili nikamchukue.

Nikachili pale Samaki samaki huku napiga zangu heineken mdogo mdogo. Wakati niko pale Samaki samaki kuna jamaa nilimkuta so nikaamua kumjoin story zikawa zinaendelea mdogo mdogo.

Iryn akanipigia simu nikamchukue yuko tayari nikamwaga jamaa huyo nikamchukua mrembo nikamrudisha kulala.

Wakati niko njiani nilijikuta ni mtu mwenye furaha sana. Nikawa najisemea huyu Iryn anaroho nzuri sana, kama anaweza kunipa $100 alopewa ya mafuta, je angekua mtu mwingine angenipa?? Na bado amenilipa 300,000 yangu.

Nikasema acha niendelee kuwa mpole tu, ni watu wachache sana wenye roho kama yake, mwingine asingenipa kabisa.

Nikawa nakumbuka jinsi anavyo nitambulisha kwa watu wake, nikasema huyu dada ananithamini na anaheshimu kazi yangu. Acha na mimi niheshimu kazi zake naamini ipo siku nitajua mishe zake.


Nilivyorudi home kama kawaida nilimkuta wife yuko seblen na movie yake, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamsalimia, hakujibu ila alikua akiniangalia, na mimi sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani then nikaenda kuoga.

Wakati naoga kumbe wife kachukua key na kwenda kukagua gari, ile natoka bafuni naona mtu kashika lipstick mkononi.

“Nilijua tu lazima una mwanamke maana nilishaona dalili mapema, ukirudi tu breki ya kwanza kuoga. Toka ijumaa unarudi usiku afu unarudi umechoka kumbe kuna mwanamke anakuchosha huko. Hii lipstick ni yanani? Gari nzima inatoa harufu ya mwanamke, Baba Junior nataka maelezo yakueleweka mimi sio mtoto”

Ghafla wife akaanza kubadilika

Tutaendelea:
Ila hapa ulifeli kumficha ....ukwl humuweka mtu huru
 
muda uleule nikamshika mikono yake miwili na nikapandisha mikono yangu kuzunguka kiuno chake na nikamvuta upande wangu kwa nguvu, kilikuwa kitendo cha ghafla sana. Nikampa ulimi wangu na yeye akanipa wake haraka bila kizuizi na tulichezeshana pale kwa sekunde kadhaa na palepale tulishtuka tukaacha ule mchezo.

MIMI: “I mean hiki ndo ulichokuwa unakitaka, Iryn thank you for everything, I have missed you so much. Mimi naondoka nikutakie maisha mema ila kama utahitaji msaada wangu never hesitate to call me. Byee.!

Kuanzia leo nakukaribisha kwenye chama chetu cha ubazazi...

Mwamba sana wewe 😊
 
Nilicho gundua huyu insider hii ni story ambayo bado inaendelea kwenye maisha yake halisi. Hivyo hadi apate Visa ndio anatuletea ndio maana katuambia atatuletea Visa wiki hadi wiki .....ila ni story moja tam sana
dah yaweza kuwa
 
Back
Top Bottom