Pale ambapo mwanamke na mwanamme, wenye sifa za kufunga ndoa, wameishi pamoja kwa miaka isiyopungua miiwili kwa namna ambayo inawatambulisha kama mke na mme watachukuliwa kama wanandoa hadi pale itakapothibitika vinginevyo.
Je mwanamke na mwanaume walioishi pamoja kwa kipindi fulani bila kufunga ndoa wanaweza kuhesabika kuwa wanandoa?
[emoji3578][emoji736]Sheria inatambua dhana ya kuwepo kwa ndoa kati ya mwanamke na mwanaume walioishi pamoja bila kufunga ndoa iwapo mambo yafuatayo yatatimizwa:
• [emoji127] Iwapo watu hao wawili wameishi kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo pamoja.
• [emoji127]Majirani wanaowazunguka wanawachukulia kuwa ni mke na mume.
• [emoji127]Hakuna ndoa inayoendelea kutokana na maisha yao ya awali.
• [emoji127]Wametimiza umri unaokubalika kisheria wa kuoa au kuolewa (umri wa18 au zaidi).
[emoji3578][emoji736]Iwapo mambo hayo manne yametimizwa, mahakama inaweza kuthibitisha kuwepo
kwa ndoa kati ya watu hao wawili.
#KUMBUKA
• [emoji3516][emoji736]Ni mahakama pekee yenye uwezo kisheria kuthibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa dhana ya ndoa. kwa maana hiyo mahakama inaweza kataa kama vigezo tajwa hapo juu havijakamilika, na hii ilianzishwa kwa lengo la kumlinda mwanamke na watoto ili asionewe na akaachwa patupu. lakini kumbuka pia mahakama ikitangaza dhania ya ndoa haiwezi toa talaka lakini itatoa hukumu juu ya malezi ya watoto na mgawanyo wa mali ambazo mahawala hao walichuma pamoja kipindi wanaishi pamoja. lakini ni muhimu mlalamikaji akaleta ushahidi kudhibitisha dhana hiyo ya ndoa
• [emoji3516][emoji736]Ni vigumu kuthibitisha kuwepo kwa dhana ya ndoa iwapo mmoja wa wanandoa amefariki dunia. Wanandoa wanaoishi bila ndoa wanashauriwa kuhalalisha ndoa yao ili kuwa katika mazingira mazuri ya kudai haki hasa pale mmoja wa wanandoa anapofariki. utaratibu wa kuhalalisha ndoa nimewahi kuelezea kipindi cha nyuma, Haya na kulingana na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 kifungu Cha 160.
Kwa upande wangu Insider hapo siwezi kuchomoa sababu
1. Nimelipa mahari mpaka pete nilimvalisha
2. Tunaishi pamoja mwaka wa tatu huu.
3. Tuna mtoto mmoja wa miaka 2
4. Wazazi wana mtambua mama J mpaka kwenye kutoa mahari walikuwepo.
5. Wazazi wake wananitambua mimi kama mkwe
6. Marafiki, ndugu zangu wa karibu wanamtambua kama mke.
7. Tunashare maendeleo kama biashara tunatumia jina la kampuni as Directors, bado magari nimeandika jina lake.
Hapa nakataaje sio mke wangu???