Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 69
A TRUE STORY BY INSIDER MAN

PREVIOUS
MA’ JANETH: “Okay one more thing, una mahusiano gani na Iryn? be honesty with me.”

Mama Janeth alinipiga swali gumu sana ambalo hata sikujua najibuje na mimi niliona limekaa kimtego sana.

CONTINUE….

PART I

Muda huu ubongo wangu ulifanya kazi kwa haraka sana kama AI na niliwaza mambo matatu,

Mosi, mama Janeth anajua kila kitu kuwa nina mahusiano na binti yake, either kaambiwa na Iryn au Mzee Virgil.

Pili, anahisi nina mahusiano na binti yake maana tumekwenda wote Zanzibar na Dodoma kwa mtu mzima lazima ahisi something fishy is going on kwa kuunganisha haya matukio.

Tatu, hajui chochote ila anataka kujua kupitia mimi.

“Niliwaza pia hivi kama anajua na nikamkatalia atanifikiriaje?, nilifikiri pia Iryn hawezi kumwambia mama Janeth kuhusu hili suala letu bado ni mapema sana, ukizingatia leo kanitumia ujumbe wa kuachana. Kuhusu Mzee wake kumwambia niliona sio rahisi kuongea haya mambo kwani mahusino ni suala binafsi na pia wanaume hatunaga sifa za umbea.”

Palepale nikajua mama Janeth hakuna anachojua na huenda Iryn kamficha hili suala na hapa nikapata nguvu ya kumjibu kwa confidence,

MIMI: “Mama mahusiano niliyonayo na Iryn ni kama rafiki yangu wa karibu ambaye tumekuwa kama ndugu.”

MAMA JANETH: “Sounds great I’m happy for you guys hata kama mngekua kwenye mahusiano ningebariki, umefanya kazi kubwa sana kumuweka Iryn sawa hata mimi nilishindwa hili maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana.”

MIMI: “Katika jambo ambalo nilimuahidi Iryn ni pamoja na kumfanya awe na furaha na nilijua suala la baba yake linamuumiza sana hivyo nilimshauri ayamalize na baba yake.”

MAMA JANETH: “Niseme Iryn kwasasa ni yule naemjua zamani amekuwa mchangamfu sana, Ahsante sana kwa hili.”

MIMI: “Usijali mama mimi nimeshakuwa familia tayari.”

Japo mama Janeth alionekana kuna jambo anatamani kunambia ila alikuwa anasita na mimi nimlimsoma mapema na nilihisi alitamani kunambia ukweli kuwa binti yake ananipenda lakini alipotezea.

MAMA JANETH: “Insider mimi naondoka Jumatatu akija dada utanipa feedback, chukua hii bahasha kuna pesa itakusaidia na hii weekend.”

MIMI: “Ahsante sana mama, Mungu akubariki sana.”

Baada ya mama Janeth kuondoka niliisikiliza tena ile voice note ya Iryn kwa makini sana, nikagundua Iryn anaendeshwa na hisia na hatumii akili yake, ni kama anakuwa anakurupuka kwenye kufanya maamuzi na anakosa misimamo. Kwa upande mwingine niliwaza labda Claire kajua nina mke hivyo kamshauri Iryn aniache, pia nilikuwa na wasiwasi sana na Claire.

Kitendo cha Iryn kutokuwa na misimamo kilinikera sana na nilimuona anakua kama mtoto mdogo, nikaamua kumpigia simu kwanza ili nijue tatizo ni nini. Nilimpigia simu na iliita muda mrefu na akapokea,

MIMI: “Hi baby how you doing.”

IRYN: “Just fine.”

MIMI: “Nahitaji kuonana na wewe upo wapi? Ni siku tano sasa sijakuona toka uniage unakwenda kwa Claire.”

IRYN: “Insider umepata ujumbe wangu?”

MIMI: “Ndio nimeupata ndomana nakuuliza upo wapi ili tuonane tuzungumze.”

IRYN: “Nimekwambia nitakutafuta before sijaondoka but for now hapana.”

MIMI: “Umetuma huu ujumbe ukiwa na akili yako timamu au umekosea?”

IRYN: “Ni kitu gani ambacho hujaelewa Insider, I said that lets assume like nothing happened between us, maamuzi niliyoyachukua yananiumiza but yatapita na haya yote ni kwaajili ya familia yako.”

MIMI: “Sawa mimi nimekuelewa sina shida naomba tuonane we nambie ulipo mimi nitakuja.”

IRYN: “Nilikusubiri sana ofisini mpaka nikachoka, voice niliyokutumia imejieleza vizuri kabisa.”

MIMI: “Sawa sikulazimishi kuonana na mimi hata unavyoondoka usinitafute na sihitaji uniage maana unanitafuta unavyojisikia wewe, hivi wewe mwanamke mimi unanichukuliaje? unajua nimekuvumilia mpaka nimechoka sasa, labda unanichukulia mimi kama fala flani.”

IRYN: “Insider what are you talking about? Are you angry with me?”

MIMI: “Wewe ni mtu mzima tena unayejitambua lakini maamuzi yako ni ya kitoto sana, unakosa kuwa na misimamo maana unakuwa sitaki na nataka, unakuwa unaendeshwa na hisia badala ya kutumia akili kwenye maamuzi yako.”

IRYN: “Kwahiyo unataka kusema natumia hisia kwenye jambo la faida kwa familia yako.? Are you serious?.”

MIMI: “Ina maana wakati unaingia kwenye mahusiano na mimi hukulijua hili ndo umelijua leo hii? Ungekuwa ulitumia akili haya ya leo yasingetokea na wala usinge sex na mimi.”

IRYN: “Point yako mimi sina akili?”

MIMI: “Sijasema wewe huna akili but unashindwa kutumia akili uliyonayo kwenye kufanya maamuzi sahihi. Mimi naheshimu maamuzi yako na nimekubali tuachane kiroho safi na nikwambie, naipenda sana Familia yangu na mama Junior atabaki kuwa mke wangu no matter what. “

IRYN: “Thank you Insider I wish you and your family all the best.”

MIMI: “Nilitegemea hili jambo tungediscuss kwa kukaa chini lakini kitendo cha kunitumia voice kwangu ni dharau, afu one more thing naomba usije kukanyaga pale kwangu wala kusikia umemchukua Junior, kwaheri.”

IRYN: “Insider what are…..” Na mimi nikakata simu sikutaka kuendelea kumsikiliza.

Niliendelea kukaa pale ofisini nikiwaza hili suala na nikaondoka kurudi home, lakini nilipitia pale Mikocheni plaza nikanunua Pizza large na soda ya fanta takeaway kubwa nikaendelea na safari yangu ya kurudi home.

Baada ya kufika home niliwakuta wote wamekaa nje kibarazi mpaka bibi na nikawasalimia pale na muda huu mama J alikuwa kanipokea ile Pizza,

MIMI: “Wife nimewaletea leo Pizza mle na Bibi.”

WIFE: “Baba J, bibi na Pizza wapi na wapi?”

MIMI: “Si amekuja mjini azoee na vya mjini kidogo, eti bibi utashindwa?”

Na muda huu wife alikuwa kachukua kipande kimoja anakila,

BIBI: “Vyakula vya kizungu hivyo.”

Niliwaaga pale na mimi nikaingia chumbani kuoga maana mchana kutwa nilikuwa na hekaheka za bandarini. Baada ya kuoga nililala pale kitandani na mama J aliingia chumbani muda huu na tukaanza maongezi pale,

MIMI: “Mke wangu tangu urudi Moshi naona unazidi kuwa mzuri ulikuwa unalishwa nini huko?”

WIFE: “Mimi najiona kawaida mbona ni vile hujaniona kwa muda mrefu.”

MIMI: “Sogea hapa kitandani uwe karibu na mimi unajua nakupenda sana mke wangu, zawadi ya Junior uliyonipa ni heshima kwangu.”

WIFE: “Nashukuru kwa kulitambua hili hata mimi nafurahi kuona kuwa na mwanaume anayejua majukumu yake kama baba, lakini mimi kama mke wako kuna vitu naona haviko sawa baba J.”

MIMI: “Niambie mke wangu ni vitu gani hivyo vinakukera?”

WIFE: “You know Baba J wewe ndo mwanaume wa kwanza kunifahamu na ninakuapia sijawahi kulala nje na mwanaume mwingine na siji kufanya hivyo. Ila tambua kuna mambo huwa unayafanya na yananiumiza sana na wewe unayajua sina haja ya kuyasema. Kumbuka na mimi ni binadamu ninaumia sana kuona unanicheat, naomba tu-focus kwenye malezi ya mtoto kama sisi tutayumba hata mtoto tutampoteza.”

MIMI: “Mke wangu mbona hayo yalikwisha muda mrefu sana na bado unayakumbushia na mengi nilikukatalia sio kweli shida ni nini?”

WIFE: “Roho yangu inakosa sana amani juu ya Iryn nahisi kuna kitu nyuma ya pazia kinafanyika kati yenu. Naheshimu sana kazi yako maana hata mafanikio nina yaona kwa macho, pia nafahamu Iryn ni bossy wako na ni rafiki kwako, lakini napatwa na wasiwasi na huu ukaribu wake kwangu seems like anahide something nisikijue.”

MIMI: “Something what?”

WIFE: “Unajua hata bibi naye amehisi kitu kwa Iryn na amenambia niwe naye makini sana, anaonekana ni rafiki kwangu lakini ni adui yangu namba moja, na sikuzote adui huwa hatoki mbali.”

MIMI: “Mke wangu mimi naona wasiwasi wako tu afu Iryn kuja hapa home ni kwaajili yako na sio mimi, kitu kingine unawasiwasi sababu ya uzuri wake, lakini trust me angekuwa ni mwanamke ambaye hana mbele wa nyuma sidhani kama ungekuwa na wasiwasi huu, hata bibi ana wasiwasi sababu ya uzuri wake.”

WIFE: “Ni kweli unachoongea kumbuka bibi alikuwa binti kama mimi na ana ujuzi wa kutosha na kumsoma mtu tabia, lisemwalo lipo kama halipo basi linakuja.”

MIMI: “Mke wangu siku zote wewe huwa unaniombea mabaya na sio mema hapa ndo huwa sikuelewi, badala uniombee wewe unawish litokee ndo point yako.”

WIFE: “Sina maana hiyo ila naomba kama kuna kitu mnafanya kwa siri bhasi acha, hakuna siri kwenye hii Dunia.”

MIMI: “Mke wangu naomba uwe na amani kama ningekuwa nafanya hayo hata Iryn asinge kuwa anakuja hapa home angeacha kuja kwaajili ya aibu. Mapenzi yana nguvu kubwa sana na hayafichiki hata mimi ningemkataza kuja hapa home, Iryn ni kama familia kwetu na anatuchukulia sisi kama ndugu zake, sioni sababu ya kuendelea kumfikiria vibaya kama hupendi kumwona hapa home ni juu yako sababu anakuja kwako na Junior.”

WIFE: “Sijataka kufika huko na siwezi kumkataza kuja home, mimi nakwenda kupika. Unataka kula nini usiku huu?”

MIMI: “Mimi nitakula chochote mlichopanga kupika.”

WIFE: “Ni muda sana toka niwe Moshi najua kuna chakula unatamani kukila wewe sema tu.”

MIMI: “Nahamu na wali-maini.”

WIFE: “Usijali.”

Wife aliongea maneno ambayo yalinichoma sana na nilijihisi nina hatia sana juu yake maana mambo aliyokuwa anaongea ni ya kweli ni vile alikuwa hana ushahidi. Nilijisikia vibaya sana na nikajisemea moyoni I have to change, family means everything to me.

Baadae tulipata dinna ya pamoja pale mezani na tulikuwa tunapiga sana story na bibi maana ni mtu muongeaji sana kwakweli. Pia nilimwambia mama J kesho tutatoka as family na tutakwenda Ramada Hotel na yeye alisema kwa bibi itakuwa ngumu kwenda na itabidi abaki na dada, tutatoka sisi pamoja na Junior.
•••••••
Jumamosi Asmah aliripoti ofisini kuendelea na kazi na mimi baada ya kuwasili ofisini nilimkuta amekaa reception na laptop yake, tulisalimiana na tukaanza kuongea pale,

MIMI: “Nambie Asmah unaendeleaje na mguu wako?”

ASMAH: “Nashukuru Mungu naendelea vizuri kidogo naweza kutembea.”

MIMI: “Embu tuone maendeleo ya mguu.”

ASMAH: “Insider hapa hapana sitaki matatizo na watu mimi, twende ofisini nikakuoneshe afu kuna jambo itabidi unisaidie.”

Baada ya kuingia ofisini Asmah alikaa kwenye coach na akapandisha juu gauni yake usawa wa kiunoni na nikaweza kuliona paja lake lilikokuwa limeumia na niliishia kusisimuka maana lilikiwa jekundu sana.

MIMI: “Damn! kumbe uliumia sana rafiki yangu mpaka nimesisimuka ujue.”

ASMAH: “Hata hapa afadhali ilikuwa zaidi ya hapa unavyoona.”

Na mimi nilijaribu kulishika na nilijaribu kulibinya na aliishia kulalamika namuumiza. Hata kwenye kutembea bado alikuwa anatembea kwa shida sana yaani ile slow but sure,

ASMAH: “Insider nimerudi kwangu now, dada amesafiri na pia niwe karibu na ofisi.”

MIMI: “Utawezaje mikiki ya kuishi peke yako na hali hii?”

ASMAH: “Ndomana nimeamua kurudi ofisini kidogo nikiwa natembea tembea nakuwa nafanya mazoezi ili nirudi kwenye hali yangu.”

MIMI: “Now huwezi kusex kabisa sindio?”

ASMAH: “Hahaaa ushaanza ujinga wako, naomba unisaidie jambo moja, wewe ndo mtu niliyekuzoea humu ndani.”

MIMI: “Nambie tu ni jambo gani hilo unahitaji msaada?”

ASMAH: “Naomba kila siku jioni uwe unanisaidia kufanya mazoezi ya mguu”

Asmah aliomba niwe namsaidia kumtembeza huko nje pamoja na kumfanyisha mazoezi ya mguu kama kuukunja na kuunyoosha.

MIMI: “Hilo ondoa shaka ila kwa leo nina ratiba binafsi jioni ila tutafanya zoezi moja before sijaondoka.”

ASMAH: “Sawa Ahsante dear.”

Wakati nikiendelea na majukumu yangu ule mchana Camila alinipigia simu na akaomba nimpe kampani ya kwenda Bahari beach jumapili na mimi nikamkubalia kwa masharti ya kwenda kwa Jane baada ya kumaliza mambo yake. Tangu nirudi kutoka Zanzibar nilikuwa sijakanyaga kabisa kwa Jane zaidi ya kuongea kwa simu tu na nilikuwa nimemiss kumuona na kumjulia hali.

Saa 10 jioni ilibidi niondoke kwenda home ili nitoke out na familia kama nilivyokuwa nimeahidi jana, na before sijaondoka nilimcheki Asmah ili zoezi lianze na ndani ya muda mfupi alikuwa ameingia ofisini na akakaa kwenye coach.

Na mimi nilimsogelea tukaanza zoezi, mguu wake aliuweka tumboni kwangu, lilikuwa ni zoezi la kukukunja na kunyoosha mguu. Alikuwa ananipush kwa nguvu then mguu unanyooka afu mimi nikirudi kwake mguu unajikunja vivyohivyo japo alikuwa analalamika sana na mimi nilimwambia aache kutoa kelele.

ASMAH: “Insider ungefunga mlango na funguo sipendi shida na watu.”

MIMI: “Nifunge mlango tena kwani kuna kitu kibaya kinafanyika?”

ASMAH: “Huwajui wanawake wa humu ndani ni wambeya sana.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi kila mtu humu ndani anajua unaumwa na mimi nakusaidia kama rafiki yangu, ila kuanzia kesho uvae tight maana haya mambo ninayo yaona hapa yamefanya Insider aamke toka usingizini na mimi sitaki kufanya jambo lolote na wewe.”

ASMAH: “Siwezi kuvaa tight maana natakiwa kujichua paja mara 3 kwa siku nikivaa itanisumbua sana.”

MIMI: “Sawa pole, bhasi vaa hata zile tight fupi sio mbaya.”

ASMAH: “Okay hata hivyo nashukuru rafiki yangu kwa msaada wako japo mguu kama nimeutonesha tena huna huruma kabisa.”

MIMI: “Si unakumbuka siku ile nilivaa chupi yako kichwani nikawa kama Rambo.”

ASMAH: “Insider unazingua sana kwaheri mimi nipo sana.”

MIMI: “Kesho Jumapili mimi sipo pia, itabidi utafute mtu wa kukusaidia, kingine acha kupanda bodaboda usije ukajitonesha tena.”

ASMAH: “Sawa dear niko makini sana kwa hili.”

Niliondoka maeneo yale na nikarudi home, baada ya kuwasili nilimkuta Bibi amekaa kibarazani na tukasalimiana pale nikaingia ndani na mama J alikuwa pale seblen na Junior.

WIFE: “Nilijua umesahau ulichoahidi jana, una ahadi hewa nyingi sana.”

MIMI: “Mke wangu siwezi kusahau ahadi yangu ndomana nimekuja mapema tuondoke.”

WIFE: “Sisi tuko tayari muda mrefu sana tulikuwa tunakusubiri wewe tu.”

Tulitoka home na tulikwenda Ramada hotel, baada ya kuwasili pale tulitafuta sehemu nzuri tukakaa. Hii siku tulijadili masula ya maisha yetu kwa ujumla na tulipanga mipango yetu mingi sana kwa baadae. Tulikaa mpaka usiku sana na tulirudi home kulala lakini bado nilikuwa nakosa hamu ya kusex na wife.

Jumapili niliamka asubuhi mapema sana ili niwahi misa ya saa moja na baada ya kurudi home nilikuta missed call 3 za Camila. Baada ya kumpigia simu alikuwa ananikumbusha appointment yetu na nikamwambia niko home anipitie ili tuondoke na nitasogea mpaka barabarani.

Baada ya lisaa Camilla alikuwa around tayari na alinipitia pale “Ally sykes Road” mbezi beach na tukaendelea na safari ya kwenda Bahari Beach. Camilla alikuwa anaendesha Mercedes SUV na ilikuwa ngeni machoni pangu na wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story,

CAMI: “Insider hujataka nikujue kwako.”

MIMI: “Wewe lengo lako uje kwangu au nikupe kampani?”

CAMI: “Hata ningekujua kwako sio mbaya maana wewe ni ndugu tayari.”

MIMI: “Kwangu utakufahamu usiwe na wasiwasi.”

CAMI: “Unajua nimechelewa sana kuna watu wananisubiri Bahari Beach ili twende nao site.”

Baada ya kuwasili Bahari beach kuna harrier nyeusi ulikuwa imepark pembeni ya barabara ni kama mtu alikuwa anatusubiri na Cami alitoa ishara kwa ile gari na ikaanza kutufuata kwa nyuma na tulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye plot yao yenye uzio mkubwa.

MIMI: “Hujanambia kuna ishu gani huku mimi nimekupa kampani tu.”

CAMI: “Twende ndani utaona.”

Baada ya kushuka kwa gari Camilla alisalimiana na wale wageni na walikuwa wawili kisha akafungua geti tukaingia ndani na wao walitoa vifaa vyao na wakaanza kufanya vipimo.

CAMI: “Insider hawa ni ma-engineer wanapima eneo kwanza kabla ya kuanza ujenzi.”

MIMI: “Eneo ni kubwa sana mnaplan ya kufanya project gani?”

CAMI: “Mzee anasema anatakaa kujenga hotel, but bado hakuna muafaka. Wewe unaweza kushauri mzee afanye project gani hapa?”

MIMI: “Kwanini Mzee asijenge Apartments? Kwa huku Bahari Beach atapata pesa mingi sana kuliko hata hotel.”

CAMI: “Hata mimi niliona hili.”

MIMI: “Na ukashauri nini?”

CAMI: “Kama nilivyosema bado hakuna muhafaka kama familia.”

Wakati wakiendela na vipimo kwa upande wetu tulikuwa tunapiga story mbalimbali na baada ya lisaa walikuwa wamemaliza kazi yao na wakaondoka, kwa upande wetu tulikaa kwa dakika 10 tukaondoka kwenda Mbweni kwa Jane.

Ilikuwa ni mchana tayari wakati tunatoka pale Bahari beach kwenda kwa Jane na baada ya kuwasili tulikaribishwa seblen. Kwa upande mwingine Jane tumbo lake lilikuwa kubwa sana na alionesha kuchoka sana, ni kama alikuwa anasubiri muda utumie ili ashushe ule mzigo maana ilikuwa miezi 8 tayari ya ujauzito wake.

Tuliongea masuala mbalimbali na Jane ikiwemo afya yake na masuala mengine ya pale home na kabla ya kuondoka nilitoka kwenda kuwasabahi mbwa wangu na niliwakuta wako salama kabisa na nikarudi ndani.

MIMI: “Vicky yuko wapi na muda sijamwona nime-mmiss.”

JANE: “Amelala huko ndani vipi tumuamshe?”

MIMI: “Muacheni apumzike mpaka akalala mchana kweli yuko hoi.”

JANE: “Mhhh! hajasikia sauti yako tu.”

CAMI: “Dada Jane mzee si alikupa taarifa ya hafla pale nyumbani?”

JANE: “Alinambia lakini si unaona nilivyojichokea hapa mdogo wangu.”

CAMI: “Naona utakuwa sawa usijali.”

Baada ya kupata lunch tuliawaaga na wakati tunaondoka Vicky alikuwa kaamka tayari na tukuwa tunaongea pale nje kibarazani.

VICKY: “Insider umekuwa adimu sana why?”

MIMI: “Kila nikija hapa naambiwa haupo sijui umepata bwana wapi.”

VICKY: “Mabwana wenyewe hampo serious bora niendelee kuwa single.”

MIMI: “Mhhh, you’re not ready to mingle?”

VICKY: “Ofcourse No.”

MIMI: “Sisi tunaondoka tulikuja wasalimia.”

VICKY: “Tunashukuru kama unavyotuona hapa, Insider timiza ahadi zako wewe mwanaume ni muongo sana, nitakuchukia.”

MIMI: “Next week jumamosi ukiona kimya nikumbushe.”

VICKY: “Ok byee.”

Tuliondoka na Camila na aliniacha pale Rainbow Mbezi Beach na mimi nikaondoka kurudi home kupumzika.

*********
Jumatatu wakati niko ofisini nilipigiwa simu na Rebby na akanambia kuna mgeni amekuja kuonana na mimi,

MIMI: “Anashida ya ofisi au private?”

REBBY: “Anasema ameagizwa na mama Janeth.”

MIMI: “Ooh nilisahau muelekeze ofisi yangu aje.”

Baada ya dakika nilisikia mlango ukigongwa na baada ya kumkaribisha dada aliingia ndani.

“Good morning sir.”

“Good morning too, wewe ndo umeelekezwa na mama Janeth?”

“Yes it’s me.”

“Ok, it’s my pleasure meeting you today, kuna dada atakufanyia interview usiwe na wasiwasi, do you need anything?”

“No thank you sir.”

Baada ya dakika 10 Asmah alikuja na akawa anamfanyia interview yule dada na baada ya kumaliza alitoa recommendation kuwa yuko vizuri mpaka muonekano wake ulikuwa unavutia.

MIMI: “Hilda leo umeanza kazi na utaanza kupewa mafunzo na majukumu yako yapo Kwenye mkataba na dada hapa atakuelezea kwa ufupi maana utakuwa unaripoti kwake. Mshahara pia utaona kwenye mkataba lakini nje na mshahara kampuni yetu ina offa bima ya afya, bonus, mikopo na masuala mengine mengi utayaona kwenye mkataba wako. Asmah nafikiri ungeanza kumuelekeza kuhusu ofisi yetu na mengine yaendelee mimi natoka kwenda bank.”

ASMAH: “Ok manager haina shida acha niendelee naye.”

Niliondoka ofisini na nilikwenda kwanza Mikocheni kucheki mazingira ya ofisi na nilitumia lisaa pale Mikocheni na nikaenda bank kuweka pesa.
•••••••
Jumanne asubuhi nilipokea simu kutoka kwa Sumaiya na aliomba tuonane mchana muda wa lunch na mimi niliikubalia ofa yake maana ilikuwa ni muda mrefu umepita hatujaonana licha ya ofisi yake kuwa palepale Masaki.

Mchana nilifanya kuwasiliana na Sumaiya na tulikubaliana tuonane Samakisamaki ndo tutapatia lunch yetu pale. Sumaiya alikuwa wa kwanza kuwasili pale na wakati niko njiani alikuwa kanipa taarifa kuwa amefika muda mrefu na ananisubiri.

Baada ya kuwasili maeneo yale niliingia ndani na yeye alikuwa amekaa upande unaotizama barabara, kwa upande mwingine Sumaiya alionekana kupendeza sana na alikuwa amevaa official, surual ya kitambaa, blauzi na chini heels.

MIMI: “Mshikaji umewaka sana hapa kweli ukinambia manager sikupingi.”

SUMAIYA: “Hata wewe naona sio haba gari nyingine mpya unakula sana pesa za Queen.”

MIMI: “Sijawahi kuzipa kipaumbele Pesa za mwanamke mimi sio Marioo.”

Mhudumu alikuwa amefika kutusikiliza na tukaagiza chakula na story zikaendelea,

SUMAIYA: “Jana Queen kaja ofisini kwangu kunisalimia, nikamuuliza vipi dada umekuja kunifukuza na huku? maana kule hukutaka niwe karibu na Insider au ulifikiri mimi nakuibia?, Queen akanambia hapana Sumaiya lengo langu nilitaka uje huku uongeze nguvu.”

MIMI: “Ila Sumaiya bhana hivi wewe na Iryn kwanini hampatanagi?

SUMAIYA: “Sikia sasa maana jana nilimchamba sana afu unanijua mimi siogopagi mtu, nikamwambia Insider ni mtu wa watu afu ana roho nzuri mdomana tunampenda hata mimi namtamani sana na amefanikiwa kuruka mitego yangu yote ila atatanasa tu siku.”

MIMI: “Hahahaa usiweke ligi na Iryn bibie akiamua kukutoa hapo ofisini ni sekunde wewe achana naye fanya yako mama.”

SUMAIYA: “Mama Janeth amekuletea dada mpya tena pisi kali, kazi kwako.”

MIMI: “Umejuaje hili?”

SUMAIYA: “Ooh! Ilitakiwa aje ofisini kwetu ila mama akaona anafaa kuja huko Salon.”

MIMI: “Hivi ulishawahi kwenda kumsalimia Asmah toka apate ajali?”

SUMAIYA: “Hapana ila nilimpigia simu nikamtumia na pole yangu, alinambia akirudi ofisini atanijulisha.”

MIMI: “Yuko ofisini tayari na nimemuacha pale na dada mgeni.”

SUMAIYA: “Itabidi twende wote nikaisalimie na timu yangu.”

MIMI: “Mtoto hajambo?”

SUMAIYA: “Yuko poa nataka nianze kuishi na mwanangu Insider.”

MIMI: “Kwa hili nakuunga mkono ni uamuzi mzuri na baba yake yuko wapi?”

SUMAIYA: “Baba yake yupo ila ni kama hana time na mtoto wake, kwanza alisemaga mtoto sio wake lakini baada ya mama yake kuja kumuona alisema ni mtoto wao. Baada ya hapo akawa hatumi pesa za matumizi sio kwamba hana hela? ni dharau anataka awe anaombwa na kubembelezwa, na pesa zake za masimango sana, mara aniambie akanigonge ndo anipe pesa za matumizi ya mtoto, nikaona huyu mpumbavu hanijui nikaamua kuachana naye napambana na mtoto wangu.”

MIMI: “Aisee! pole sana nenda kamshitaki kama ni damu yake anashindwaje kutoa pesa za matumizi na kweli ni damu yake?”

SUMAIYA: “Kuna wanaume wanatabia za kivulana afu ana 30+ ila anataka umnyekekee na mara ya mwisho ametuma pesa mwezi wa saba na alituma laki mbili tu baada ya kusikia mtoto anaumwa ila hanaga habari kabisa. Nashukuru Mungu kwa hii position niliyopata si haba ndomana nataka nikae na mwanangu, pia mama Janeth ananipiga sana tafu pale napokwama na huyu mwanaume akiendelea na hii tabia atamkosa mtoto.”

MIMI: “Tuondoke dear muda umekwenda nipitie na hapo KFC niwanunulie chakula kina Asmah.”

SUMAIYA: “Ndomana Asmah anakupenda sana unajua kujali sana Insider hata mimi hili nakupa maksi zangu, watoto wakike tunapenda mambo kama haya hata nikikuvulia chupi sijutii.”

Tuliondoka na Sumaiya pale Samakisamaki na tukapitia kwanza KFC kisha tukaendelea na safari yetu ya kwenda Salon. Baada ya kuwasili Salon Sumaiya alipokelewa vizuri na shoga zake na mimi nilimuacha pale reception akiongea na Asmah.

Baada ya nusu saa Sumaiya alikuja na akaaga anaondoka kwenda ofisini kwake ili kuendelea na majukumu yake ya kiofisi na alitoa noti ya $100 na akataka kunikabidhi.

SUMAIYA: “Insider ulinipa dollar ile siku na mimi nakulipa kwa dollar.”

MIMI: “Aisee Sumaiya naona mambo yako ni super mama, huna haja ya kunilipa mimi nilikupa tu maana ulikuwa kwenye wakati mgumu hio kampe mtoto.”

SUMAIYA: “Wow thank you, mimi naondoka but anytime ukinihitaji nijulishe.” Na akanikonyeza afu akaondoka. Na mimi nilibaki nikisikitika maana Sumaiya mpango wake wa kunitunuku ulikuwa haujafa.
•••••••
Ijumaa jioni mama Janeth alikuja ofisini kuangalia maendeleo ya Hilda na ofisi kwa ujumla na alikuja kama surprise. Mama Janeth aliingia ofisini na tukasalimiana pale, aliuliza kuhusu maendeleo ya Hilda pamoja na ofisi na akanambia akimaliza mambo yake tutakwenda wote Mikocheni ili akafanye na visit kule.

Kwa upande mwingine kulikuwa na forms za mikopo ambazo wanafanyakazi waliomba na zilikuwa pending sababu Iryn alikuwa hajazisaini na kwa upande wangu nilikuwa nimemtumia ripoti lakini haikujibiwa. Sasa nilishtuka baada ya kusikia mama Janeth ananambia nimpe azisaini kwa niaba ya Iryn, kwani yeye hayupo na atarudi jumatano hivyo sio busara kuwaacha watu kwa muda mrefu hivi.

Kwa upande mwingine mimi na Iryn hatukuwai kuwa na mawasiliano toka tuzinguane ile siku hivyo nilijua asingeweza kuniaga, kwanza nilimpa maneno makali sana.

MIMI: “Iryn hayupo? sina hizi taarifa.”

MA’ JANETH: “Ameondoka jumatano kwenda Arusha Serengeti, kwani hajakuaga?”

MIMI: “Ndio mama ndomana unaona nimeshangaa na amekwenda na Claire.?”

MA’ JANETH: “Yeah, kumbe unamfahamu yule best yake.”

MIMI: “Alinitambulisha couple weeks ago.”

MA’ JANETH: “Sasa nipe form nisaini ili tuwape hizi pesa.”

MIMI: “Za hapa zipo ila kwa Mikocheni ziko kulekule.”

MA’ JANETH: “Nipe za hapa kwanza nizisaini za Mikocheni nitadeal nazo hukohuko.”

Baada ya hapo tuliondoka kwenda Mikocheni na baada ya kuwasili pale Salon Mama alisalimiana na Lucy na watu wengine wote wa mle ndani na akaendelea na ukaguzi wa kote ndani mpaka nje.

Aliziomba form ili azisaini na baada ya kusaini alisema atafanya kutransfer hizo pesa kwenye akaunti za wahusika na akaniaga anaondoka kwenda Mlimani city kuna mtu anakwenda onana naye, niliongozana naye mpaka parking na akaondoka pale ofisini na mimi nilirudi ndani kuonana na Lucy na story zikaendelea.

LUCY: “Insider Iryn amekwenda Serengeti lini?”

MIMI: “Jumanne umejuaje yuko huko?”

LUCY: “Amepost kwenye Snapchat yake.”

MIMI: “Embu tuone maana mimi sina snapchat.”

Na Lucy alitoa simu yake mfukoni na akaanza kunionesha hizo picha.

LUCY: “Sema Iryn ni mrembo sana kweli kabarikiwa, Insider unamwagia pazuri sana rafiki yangu, hizi picha za Jana alikuwa Granmelia hotel leo naona yuko Serengeti na huyu dada ni nani.?”

Kuna picha alikuwa swimming pool na bikini na niliishia kukumbuka utamu wa coochie yake.

MIMI: “Best yake huyo anaitwa Claire na amerudi juzi tu hapa.”

LUCY: “Sijawahi kumuona kabisa.”

MIMI: “Tuachane na haya kesho mama J wangu atakuja Salon asubuhi nataka wewe udeal naye apendeze.”

LUCY: “Sawa haina shida aje na nimfahamu live wifi yangu.”

Nilimuaga Lucy na nilirudi home mapema kabisa kupumzika na baada ya kufika home niliiona gari ya mama mkwe (Bibi Junior) imepark pale nje uwanjani. Baada ya kuingia seblen nilimkuta amekaa seblen, tukasalimiana na maongezi mengine yakaendelea. Mama mkwe alikuwa amepitia kumsalimia mama yake (Bibi) na pia ayajue makazi mapya, baada ya kupata dinna ya pamoja mama mkwe aliaga na akaondoka.

Jumamosi nilikuwa na mualiko wa kwenda kwa Mzee Juma nyumbani kwake pamoja na familia yangu na mimi nilihisi lazima Mzee anataka kuiona familia yangu. Ilibidi ile asubuhi tuondoke na wife kwenda Salon kwa Lucy akatengenezwe maana nilitaka mama J wangu apendeze vizuri.

Baada ya kufika Mikocheni tulionana na Lucy na ilikuwa ndo mara yake ya kwanza anamuona mama J na wakasalimiana.

“Lucy huyu ndo mama Junior wangu, sasa naomba apendeze na mtafutie wigi zuri atakalolipenda, hakikisha anapendeza sawa?”

“Ondoa shaka manager kwa wifi yangu nitafanya mbinu zote ili apendeze.”

Nilimuacha wife Salon na Lucy na niliondoka kwenda Masaki, baada ya kuwasili pale nilimkuta Hilda pale reception tukasalimiana na nilimuuliza kama Asmah amefika na akanambia yuko ofisini.

Nilikwenda ofisini na Asmah alikuwa busy na laptop yake, na baada ya kuniona alinisalimia na tukaanza maongezi pale,

ASMAH: “Insider jana nimekosa mtu wa kunisaidia mazoezi, kila mtu naye muomba anasema yuko busy.”

MIMI: “Pole sana na Hilda je alikugomea?”

ASMAH: “Insider mtu mwenyewe bado mgeni afu nianze kumsumbua? Hapana kwakweli.”

MIMI: “Leo tutafidia mazoezi ya siku mbili ila after lunch na leo nitaondoka mapema sana.”

ASMAH: “Unakwenda wapi?”

MIMI: “Invitation mama.”

Mchana tulitoka kupata lunch tuliongozana na Hilda na tulikwenda kupata lunch “The Fish Monger Restaurant”, tuliagiza chakula na tukaendelea kupiga story pale juu huku tuki view Masaki vizuri.

MIMI: “Hilda unaishi wapi?”

HILDA: “Kigamboni kibada.”

ASMAH: “Ni mbali sana kumbe, itabidi usogee sogee karibu na ofisi.”

HILDA: “Ndo niko na mpango huu, Asmah yule dada (Sumaiya) uliye kuwa unaongea naye jana alifanya kazi pale Salon?”

ASMAH: “Ndio na alihamishwa kwenda ofisini nyingine, unafahamiana naye maana niliona kama mnajuana.”

HILDA: “Alinifanyia interview kwenye ofisi yake na akanambia nitaletwa huku.”

MIMI: “Unajua sababu ya mama kukuleta Salon?”

HILDA: “No sifahamu kwanini, can you tell me?”

MIMI: “Asmah atakwambia badae.”

Na Asmah aliishia kucheka pale lakini Hilda alikuwa na shauku ya kujua ni sababu ipi hiyo?.

Baada ya kupata lunch tulirudi ofisini na mimi nilimfanyisha mazoezi ya mguu Asmah kwa nguvu sana na aliishia kupiga sana kelele hii siku kuliko siku zote, sikuwa na huruma kabisa. Kwa upande wake alikuwa ameanza kukaa sawa hata mabadiliko yalikuwa yana onekana hasa kwenye kutembea.

Muda ulikuwa umekwenda tayari hivyo niliamua kondoka ofisini nirudi home kujiandaa kwaajili ya kwenda Mikocheni kwa Mzee Juma, kwa upande mwingine wife alikuwa amerudi home muda mrefu na alikuwa akinisubiri mimi tu.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 10 kasoro jioni wakati nawasili home na baada ya kuingia ndani chumbani nilimkuta mama J anachagua nguo za kuvaa. Wife alikuwa amependeza sana asee mpaka nikaanza kumtamani, alikuwa ameng’aa sana kwakweli.

MIMI: “Mke wangu umependeza sana umekuwa mrembo sana.”

WIFE: “Thank you kwa kunipendezesha mume wangu. Nilikuwa najifikiria hapa navaaje bora umewahi kurudi.”

MIMI: “Hata mimi sielewi maana ni kama hafla inafanyika nyumbani tu, mimi nafikiri tuvae casual tu inatosha.”

WIFE: “Kama ni hivyo nitavaa gauni langu refu.”

MIMI: “Wewe cha muhimu upendeze ujue nitakutambulisha kwa mzee wangu na Junior, acha nikaoge ili tuondoke.”

Mimi niliingia kuoga na ndani ya muda mfupi nilikuwa nimemaliza mpaka kuvaa nikamuacha wife chumbani akimuandaa mtoto.

Baada ya dakika 20 wife alitoka na alikuwa kapendeza sana na mimi niliishia kumsifia pale seblen mbele ya bibi. Mama J alikuwa amewaka sana naona hakutaka kunitia aibu, Mama J wangu kabarikiwa kuwa na mahips na ana kasura.

Tulitoka pale home na saa 11 jioni ilitukutia pale nje getini kwa Mzee Juma na kulikuwa na magari makali yamepark ni hatari, mimi na ka ist kangu ni kama nilikuwa nazingua maana nilikuwa peke yangu pale nje.

Baada ya kupark tulishuka kwa gari na pale getini tulikaribishwa na dada ambaye simjui na akatupeleka sehem ya kukaa. Palikuwa ni garden na zilikuwa zimewekwa tents na pamepambwa vizuri sana na kulikuwa kunameza za kutosha na kila meza mnakaa watu wanne (4).

Kwa upande mwingine kulikuwa na watu wengi wamefika tayari na wengi walikuwa wanakunywa na sura zao zilikuwa ngeni kwangu, na kamziki kambali kalikuwa kanasikika na haikuchukua muda alikuja mhudumu kutusikiliza pale,

DADA: “Karibuni wapenzi sijui niwaletee vinywaji gani?, leo hapa kuna kila kinywaji unachotaka kunywa ni nyie tu.”

MIMI: “Niletee heineken 3 kwanza afu kwa huyu dogo kuna nini?”

DADA: “Kuna juice ya minute maid ya embe.”

MIMI: “Mletee hiyo sio mbaya.”

DADA: “Na wifi yangu hapa utataka kunywa nini?”

WIFE: “Niletee wine ya 4-cousin kama ipo.”

Hatujakaa sawa ikaja foili ya kutosha kwenye sahani na tukaanza kuipeleka pale mdogo mdogo huku tunasubiri vinywaji na haikuchukua muda vikawa vimefika.

Watu walizidi kuongezeka na ni wale watu wenye hadhi “status” na muda huu Camila alinipigia simu kuniuliza kama nimefika na nilimwambia niko garden nimekaa na akasema anakuja.

Camila baada ya kufika pale garden tulisalimiana na akakaa kwenye kiti na mimi kwa upande wangu ilibidi nifanye utambulisho mfupi, nilimtambulisha familia yangu pale na yeye alibaki akishangaa, na alimchukua Junior akampakata.

CAMI: “Insider kumbe una familia kabisa na hujawai kuniambia una tabia mbaya sana.”

MIMI: “Sasa mzee wako alivyokwambia unambie nije na familia ulifikiri nakuja na nani?”

CAMI: “Mhh sawa bhana hongera sana na karibuni sana, Mzee alikuwa anakuulizia sio muda mrefu sana.”

MIMI: “Nafikiri nitamuona badae akitoka nje.”

Tuliendelea kupiga story pale na Camila na baada ya dakika 10 nilimuona Mrs. Pama akiwasili, mimi nilikuwa namuona vizuri kabisa ila yeye alikuwa hanioni na alikaa mwanzoni kabisa.

Mzee Juma alitoka nje na akatukaribisha wageni wote pale na nilijua dhumuni la ile hafla ni kuwakutanisha ndugu, rafiki na jamaa zake wote wa karibu na huwa anafanya kila mwaka pale kwake. Pia huwa wanatumia siku kama hii kupeana connections mbalimbali za kibiashara na maisha kwa ujumla na huwa wanachanga pesa kwaajili ya kuwasaidia wenye uhitaji.

Baada ya utambulisho na ukaribisho Mzee Juma alianza kupita kila meza kutusalimia na alikuwa ameambatana na mke wake. Baada ya kufika meza yangu Mzee alifurahi sana kuniona nikiwa pamoja na familia yangu na alimuomba cami ampe Junior na akambeba. Mzee alinitambulisha mke wake maana nilikuwa ndo namuona live kwa mara ya kwanza na alinitambulisha mimi kama kijana wa Mzee Pama.

Na mimi nilimsalimia Mrs Juma na nikafanya utambulisho,

MIMI: “Mzee hii ndo familia yangu na huyu ndo mke wangu na uyo ni mtoto wetu wa kwanza.”

MZEE JUMA: “Nimefurahi sana kukuona na familia hapa, sasa huyu babu atazunguka na mimi si unaona hataki kuniachia?”

MIMI: “Hata ukitaka tukuachie sisi hatuna shida.”

Ilikuwa ni hafla nzuri sana kwakweli na watu waliohudhuria pale 100 walikuwa wanafika, pia niliweza kuwafahamu watu wengi sana kupitia maongezi na niliikwenda kumsalimia mama Pama na nilimtambulisha familia yangu. Mrs Pama alionesha kuufurahia ule utambulisho na aliulizia maendeleo ya Jane kwa ujumla na nikamwambia mwezi ujao atajifungua Mungu akijalia, kwa upande wake alisema atakwenda kumsalimia.

Kwenye mida ya saa 2 usiku tulikaribishwa chakula na ilikuwa ni wewe unajisevia maana kila kitu kilikuwepo pale, kazi inabaki kwako wewe mlaji. Baada ya kupata chakula tulipiga picha ya pamoja na familia ya mzee Juma na baada ya hapo tulianza maongezi pamoja na wife.

Mzee Juma alikuwa anataka kujua maendeleo yangu pamoja na familia yangu kwa ujumla na kama kuna shida yoyote nimjulishe, pia alinishukuru kwa kuendelea kumwangalia Jane kwa ukaribu. Mzee alisema atajitahidi sana kabla ya kuondoka twende kumtembelea Jane kwake, na wakati wa kujifungua atajitahidi awepo maana ukoo wa Pama wanamsubiri mtoto kwa hamu sana.

Tulikaa pale mpaka saa 4 usiku ndo tukaaga na mzee Juma alinambia atahakikisha anafika kwangu ili apafahamu na aliingia ndani akatoka na bahasha ya kaki ndogo na akanikabidhi pale.

MZEE JUMA: “Hii kwaajili ya mjukuu wangu nikirudi mwisho wa mwezi itabidi umlete hapa nicheze naye ni mjanja sana.”

MIMI: “Tunashukuru sana Mzee kwa yote niseme Ahsante kwa niaba ya familia yangu.”

MZEE JUMA: “Mimi naomba muishi kwa amani na ninatarajia kuona mkifunga ndoa kabisa iwe official mambo ya kuishi kwa kuviziana hapana, na mkiwa tayari mnijulishe.”

MIMI: “Mzee hili ondoa shaka wife akimaliza shule tutafunga ndoa na huyu nishamchagua kuwa mke wangu wa milele.”

MZEE JUMA: “Safi sana nafikiri nikirudi next time tutaongea mengi sana, kwaherini.”

Camila alikuwa kafika pale kutupa kampani na tuliongozana huku tunapiga story mpaka parking ndo tukaachana na sisi tukaondoka kurudi home kulala.

Wakati tuko kwa gari wife aliomba ile bahasha maana mzee alisema ni kwaajili ya Junior,

“Baba J naomba hio bahasha maana wewe huchelewi kufanyia mambo yako.”

“Angalia kuna kiasi gani humo?”

Wife baada ya kuhesabu alikuta kuna milioni moja na nikamwambia aiweke tu kwaajili ya matumizi ya mtoto.

Kwa upande mwingine wakati niko pale kwa Mzee Juma, Vicky alikuwa kanipigia sana simu na texts juu, na nilijua anakumbishia outing niliyo muahidi hata baada ya kuwasili home nilisema huyu nitampigia kesho.

Baada ya kurudi home ule usiku ulikuwa mzuri sana kwetu na tuliishia kupeana mambo pale 6x6 na kwa upande wangu hisia zangu kwake zilirudi na niliifurahia ile sex kwakweli na kilikuwa ni kitombo kama cha wale watu ambao hamja fanyana kwa muda mrefu.
________________________________________

PART II

Jumapili sikwenda kanisani kutokana na uchovu wa hafla ya jana usiku maana nilikimbiza chupa sana, lakini kwa upande mwingine wife alikuwa amekwenda church na baada ya kuamka nilikwenda bafuni kuoga na nikikwenda kupata breakfast.

Nilimkuta dada yuko seblen na Junior wakiangalia cartoon na baada ya kuniona alinisalimia pale, ukweli dada ameanza kumlea Junior toka mtoto na tumekuwa tunaishi naye vizuri kama ndugu yetu. Nilikuwa naona kama nina deni kwake na nilisema badae nitaongea na mama Junior kuhusu hili, ili tuone tunamsaidiaje asiishie kufanya kazi za ndani tu.

Baada ya kupata breakfast nilirudi chumbani na nilikuwa nachezea laptop yangu pale na muda huu simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Prisca anapiga na mimi nikapokea, lakini nilisikia sauti ya Ivy ikiongea,

IVY: “Hi shem I have missed you, hauji kuniona kama zamani.”

MIMI: “Nitakuja Ivy nimekumiss pia rafiki yangu.”

IVY: “Utakuja lini? niletee na chocolate.”

MIMI: “Nitakuja da Mary akirudi sawa eeh, da Prisca yuko wapi? mpe simu.”

PRISCA: “Hi Insider za wewe?”

MIMI: “Salama ndo umeanza mbinu mpya za kuongea na mimi, unamtumia Ivy kama ngao.”

PRISCA: “Alitaka kuongea na wewe ndomana, upo Dar hii?”

MIMI: “Nipo mama napambana na maisha bado.”

PRISCA: “Ukipata nafasi naomba tuonane hata tutoke out, nimemiss kampani yako.”

MIMI: “Sawa haina shida nikipata nafasi nitakujulisha byee.”

PRISCA: “Bye Insider have a nice sunday.”

Na mimi nikakata simu japo Prisca alionekana bado kuhitaji kuendelea kuongea na mimi.

Saa 5 asubuhi nilikwenda Mbweni kwa shemeji yangu na nilikwenda na Ist mpya ili nikamringishie Jane. Baada ya kuwasili pale dada alinifungulia gate na alinambia Jane kalala ila Vicky yuko Jikoni anapika. Nilikwenda moja kwa moja mpaka jikoni na nilimkuta Vicky pale akipika na baada ya kuniona alinikunjia sura.

MIMI: “Nambie Vicky wangu leo nimekuja hapa kwaajili yako najua unahasira na mimi ila nimekuja kujitetea.”

VICKY: “Ulikuwa na demu hata kupokea simu zangu ukawa hutaki na kumbuka ulisema jumamosi nikukumbushe kuhusu ahadi yako.”

MIMI: “Jana nilikuwa kwa Mzee Juma na nilikuwa nimebanwa sana hata simu ilikuwa mbali, sorry leo niko na wewe hapa siku nzima na badae tunatoka out.”

VICKY: “Insider wewe mwanaume ni muongo sana.”

MIMI: “Trust me muulize Jane atakwambia, hata yeye ilibidi awepo sema hali yake ndo hivo.”

VICKY: “Sawa nimekuelewa nawapikia soup mbwa wangu.”

MIMI: “Sawa wewe endelea mimi niko seblen nimekaa.”

Mchana Jane aliamka na tukaanza kupiga story pale na kubwa alikuwa anataka kujua ile hafla ya jana usiku kwa Mzee pama ilivyokuwa na mimi nikampa story nzima. Baada ya hapo nilitoka naye nje na nikamuonesha ile ist yangu mpya na yeye aliishia kuitamani pale maana ilikuwa ni nzuri sana.

Nilishinda kwa Jane siku nzima na usiku saa 1 nilitoka out na Vicky na niliamua kumpeleka Kidimbwi Beach. Tuliwasili pale mapema sana na tulitafuta angle nzuri na tulikaa nyuma ya kaunta ukutani kwenye macoach na story zikaendelea.

VICKY: “Insider leo nataka kulewa sana maana nina hamu sana na alcohol.”

MIMI: “Kunywa kawaida tu sio lazima ulewe.”

Na muda huu mhudumu alikuwa amefika kutusikiliza tayari mimi sikutaka kulewa, hivyo niliagiza heineken 3 na yeye aliagiza bucket ya savana. Baada ya dada kutuletea vinywaji tuliendelea kukimbiza taratibu na mimi nilimwomba dada atuletee mishikaki.

Nilishangazwa sana na unywaji wa Vicky kwani alikuwa anakimbiza sana chupa ndani ya nusu saa alikuwa kapeleka savanna 2 tayari na kafungua ya tatu, na hapa nilijisemea Vicky ni mnywaji mzuri, pia ni mzoefu na pombe.

MIMI: “Upo spidi sana bila shaka wewe ni mtaalamu.”

VICKY: “Insider na hamu tu ya kunywa ndomana ni muda sijatoka.”

MIMI: “Kilichokuwa kinakuzuia ni nini?”

VICKY: “Kampani na pia dada Jane ananibana sana wewe hujui tu, wewe anakujua na hana shida ndomana hana wasiwasi.”

MIMI: “Sawa kunywa kistaarabu usilewe.”

Pombe zilivyomchanganya alianza kunikatikia mauno tena ya kifundi na niseme sikutegemea kuona Vicky akicheza, she’s hot anajua kudance aisee hata mimi nilibaki nikishangaa sana, na sikutaka aendelee kunipa mauno yake maana angenipa stim tu na heineken zinatabia mbaya sana.

Tulikaa pale mpaka saa 6 usiku nikamwambia tuondoke japo kwa upande wake hakutamani tuondoke muda huu na mimi ilibidi niforce na alikuwa kapelekea chupa 10 za savana. Baada ya kufika kwa gari alianza kunisumbua tuondoke akalale kwangu alikuwa very serious.

MIMI: “Kuondoka na mimi haiwezekani na usiporudi home unafikiri Jane atanionaje mimi? wewe twende nikurudishe home ila ukifungua chuo nambie tutoke out afu tutakwenda kulala wote sawa?”

VICKY: “Sawa nimekuelewa.”

MIMI: “Wewe hizo savanna zimekupa stim afu umelewa hujitambui, unaweza fanya maamuzi ya haraka kesho ukajutia nataka unavyoamua uwe kwenye akili yako sawa?”

VICKY: “No mimi sijalewa Insider.”

MIMI: “Let’s go home.”

Nilimrudisha kwao na dada wa kazi alikuwa bado hajalala na alitoka kutufungulia gate na baada ya kumkabidhi pale, mimi nikaondoka kurudi home kulala.

********
Tulikuwa tumeanza week ya Nyerere Day sasa ile
Jumatatu nilichelewa kuamka kutokana na uchovu na wakati bado niko kitandani nilikuwa nawaza sana kuhusu Iryn na kubwa nilikuwa na wasiwasi sana na urafiki wake na Claire maana nilijiuliza pale,

“Iryn amebadilika chap sana baada ya Claire kurudi ni nini kinachoendelea nyuma ya pazia kati ya hawa warembo?, ona wamekwenda Serengeti wote, hawa lazima kuna something fishy kinaendelea kati yao maana nilimwona Claire amakaa ki-lesbian sana.”

Niliingia bafuni kuoga na nilikwenda ofisini kama kawaida kuendelea na majukumu yangu ya kila siku na muda huu simu ilianza kuita na alikuwa ni Mzee Juma akinipiga na nikapokea pale. Mzee alikuwa anaomba saa 6 mchana twende wote Mbweni kwa Jane ili aka msalimie kabla haja safiri kwenda ughaibuni na mimi nilimwambia sawa.

Nilitoka saa 5 asubuhi pale ofisini na nilikwenda kwanza Salon Mikocheni na baada ya hapo nilikwenda kwa Mzee Juma.

Baada ya kuwasili pale kwake nilikaribishwa ndani seblen na nikaletewa juice, haikuchukua muda Camila alitoka ndani akiwa amependeza sana na ameshika funguo za gari na alikaa tukaanza kupiga story pale. Baada ya dakika 15 Mzee Juma alitoka na tukaanza safari ya kwenda Mbweni na Dereva alikuwa ni Camila.

Mimi nilikuwa napiga sana story na mzee njiani,

MZEE JUMA: “Kijana ulinambia unaishi Mbezi beach ni ipi?”

MIMI: “Nakaa Tangibovu Mbezi ya chini.”

MZEE JUMA: “Nafikiri tukitoka huko tupitie na kwako tupajue maana ndo njia hiihii.”

Camila akadakia kwa haraka,

CAMI: “Kweli daddy umesema jambo zuri leo tukatembee kwa Insider.”

MIMI: “Karibuni sana na mimi nimefurahi kusikia hizi taarifa.”

Baada ya kuwasili Mbweni kwa Jane tulikaribishwa ndani na tulimkuta mama yake Jane yuko pale seblen. Mzee Juma alimwomba sana mama kipindi kile cha msiba asiondoke mpaka Jane ajifungue kwaajili ya uangalizi, kwani yeye ndo mtu pekee ambaye angemwangalia Jane vizuri na kwa ukaribu kuliko mtu mwingine yoyote.

Jane alikuwa kalala hata Vicky hakuwepo maeneo yale na nilihisi atakuwa kalala nayeye maana kule Kidimbwi alizingua sana. Haikumchukua muda Jane kutoka ndani na alikuwa hoi sana maana tumbo lilikuwa kubwa tayari ana hesabu siku za kujifungua.

Mzee na Jane walitoka nje kwenda garden kuendelea na maongezi binafsi na mimi nilikuwa na Cami pale seblen. Baada ya nusu saa Vicky aliamka na akakaa na sisi pale seblen na alikuwa akinionea sana aibu, hata mimi nilishangaa kuona Vicky akinionea aibu kwa mara ya kwanza na ukizingatia sijamla.

Muda huu ilibidi nimpe taarifa wife kuhusu kuja na wageni home na yeye alisema hayupo na yuko ofisini kwake, na tulikuwa tunachati kwa whatsapp.

WIFE: “Baba J wewe si unajua hapa ofisini dada amepata dharura kwahiyo nifunge ofisi? na mchana wateja ndo wengi wanatoa pesa na kuweka.”

MIMI: “Kutoka hapo mpaka home sio mbali unaweza kufunga hata kwa muda, mzee hakai sana anataka apajue home tu ni vizuri na wewe ukawepo.”

WIFE: “Sawa ukifika Africana nambie nianze kutoka.”

MIMI: “Sawa mke wangu.”

Baada ya kupata lunch tuliaga na tukaondoka maeneo haya na safari ilikuwa kwenda nyumbani kwangu na baada ya kuwasili home nilishuka nikafungua geti na wakaingia ndani.

Manager anaishi sehemu nzuri si haba ndomana nilikuwa najiamini sana kwenda kwangu hata Cami alionekana kuwa na shauku kubwa sana ya kupajua kwangu, baada ya kushuka niliwakaribisha na tukaingia ndani.

MIMl: “Mzee karibuni sana hapa ndo kwangu.”

MZEE JUMA: “Ahsante sana babu yuko wapi.?”

Kwa upande mwingine wife naye hakuwa mbali na alikuwa tayari kafika na juice na korosho kwenye visosi. Niliupendaga sana utaratibu wa Mama Janeth anaoufanya kwa wageni zake na mimi niliiga ule utaratibu kwa wageni wanaokuja home, huwa tunawapa korosho na wife anajitahidi sana kuhakikisha mzigo haukati ndani.

WIFE: “Karibuni sana wageni hapa ni kwenu imekuwa surprise leo.”

MZEE JUMA: “Ahsante sana binti simwoni babu yangu yuko wapi?”

WIFE: “Anacheza na bibi yake chumbani ngoja nikawaite.”

Mzee Juma ni Mchaga naye hata alivyomuona bibi alifurahi sana maana walikuwa wanachapa kichaga sana, pia alifurahi sana kuona nimepata mke wa kichaga na alinipongeza sana.

Tulitumia kama nusu saa pale home tukaondoka na wakati tuko njiani tulikuwa tunaongea sana na Mzee.

MZEE JUMA: “Kijana niseme maendeleo utapata kwa huyu mwanamke na akimaliza chuo mwachie asimamie biashara zenu wewe komaa na ajira.”

MIMI: “Hii ndo mipango yetu Mzee ambayo tumepanga.”

MZEE JUMA: “Safi sana mambo mengine siwezi ongea mbele ya Camila, nikirudi november tutaongea mengi ila nataka kuona unafunga ndoa mapema.”

MIMI: “Sawa mzee hili tunalifanyia kazi nikuondoe shaka.”

Baada ya kuwasili kwake Mikocheni kwa upande wangu sikutaka kuendelea kubaki pale na niliaga nikaondoka na gari yangu kwenda Masaki maana nilikuwa na kazi ya kuandaa ripoti ya wiki nzima iliyopita.

Saa 12 jioni Asmah alikuja ofisini kuniaga anaondoka maana hakuna cha maana anachofanya na mimi nilimwambia anisubiri kidogo nitampa offa ya lift mpaka kwake.

ASMAH: “Insider niko na Hilda tunataka tuchukue bajaji si unajua anakaa Kigamboni?”

MIMI: “Haina shida tutamdrop Kivukoni nimpe lift na yeye.”

ASMAH: “Sawa tuko reception tunakusubiri.”

Baada ya kumaliza kuandaa ripoti nilizituma kwa email ya Iryn na nilijikuta nimeanza kum-miss na niliwaza pale nimpigie simu? lakini niliona sio wakati mzuri na nikasitisha mpango wangu.

Kabla ya kuondoka niliaga timu yangu na tukaondoka na kina Asmah na tullinza kumdrop Hilda Kivukoni Posta na sisi tukaenda kwa Asmah Upanga.

Baada ya kuwasili pale kwake, Asmah alinambia nisiondoke mpaka nipate dinna na mimi nilikaa seblen nikisubiri apike. Wakati tunapata dinna tulikuwa tunaongea masuala mengi kuhusu familia yake na maisha kwa ujumla.

MIMI: “Asmah hivi unawezaje kulala peke yako hivi.?”

ASMAH: “Nimezoea mbona na ninaona kawaida tu mara ya kwanza ndo nilipataga shida.”

MIMI: “Hujawahi kunionesha shem wangu ujue.”

ASMAH: “Insider kipindi kile si nilikwambia tuliachana au umesahau?”

MIMI: “Unataka kusema hujapata mwingine toka kipindi kile?”

ASMAH: “Insider mimi nahisi kama nina mkosi unajua wanaume hawanitongozi kabisa mpaka najishtukia kama nina kasoro.”

MIMI: “Hapana wewe ni mwanamke mzuri sana usiwe na papara utapata wa kuendana na wewe, jinsi ulivyo kwa mwanaume wa kawaida ni ngumu kukutongoza, pia uwe unajichanganya maana wewe ni anti-social sana muda wote umejifungia, hata kutoka out na shoga zako hutaki.”

Asmah ni mwanamke ambaye yuko kivyake vyake ni mtu ambaye hapendi kujichanganya wala marafiki. Wenzake mara nyingi weekend huwa wanajichanga wanakwenda Samakisamaki kufurahi, lakini yeye huwa anakwenda kulala hanaga muda kabisa.

ASMAH: “Insider mimi sio mtumiaji wa pombe ndomana huwa sipendi kuungana nao.”

MIMI: “Kuna Mocktail unaweza kunywa sio ukitoka lazima unywe, hii itakusaidia kukutana na watu wapya.“

ASMAH: “Huwa natoka na mara nyingi nakwenda pale Skewerz na sometimes huwa nakuwa na bro.”

Nilikaa na Asmah mpaka saa 4 usiku na nikaondoka pale kwake kurudi home na wakati niko njiani nilikuwa nawaza nimfanye Asmah awe mchepuko wangu?, lakini nikasema acha nitulie na mama J wangu, japo kuwa na mwanamke mmoja niliona kama nitapwaya sana ukizingatia nilishakuwa nimezoea kuwa na mchepuko.
••••••••
Jumatano Bossy lady alikuja ofisini jioni lakini mimi sikuwepo nilikuwa nimetoka na aliniulizia akaambiwa mimi sipo, hivyo aliendelea kukaa pale ofisini mpaka usiku akaondoka. Hizi taarifa nilipewa na Asmah ile asubuhi baada ya kwenda ofisini ndo alinambia kuwa jana Iryn alikuja ofisini na alishinda pale ofisini akipitia ripoti.

Kesho yake alhamis mimi nilishinda ofisini siku nzima maana kulikuwa na fundi anafanya service za AC rooms zote hivyo nilikuwa namsimamia, na hii siku Asmah aliondoka asubuhi kwenda hospital kuangaliwa maendeleo ya mguu wake na mimi nilimwambia akitoka huko akapumzike.

Saa 2 usiku nilitoka pale ofisini na nilipitia Mikocheni ili nimjulie hali Lucy maana tulikuwa hatuonani mara kwa mara kama zamani na nilikuwa nashinda sana Masaki sababu Asmah hakuwa fiti 100%.

Baada ya kuwasili pale nilimkuta yuko ofisini anapiga hesabu zake na baada ya kuniona tulianza kuongea,

LUCY: “Insider sikuhizi huku hushindi kabisa mpaka tunakumiss, afu naomba maokoto maana unadeni la Jumamosi.”

MIMI: “Kiasi gani unadai kwanza maana hukusema.”

LUCY: “Okay ni hivi Wigi ni laki tano, Makeup laki moja, na huduma zingine laki moja jumla laki saba kwakuwa ni wifi yetu lipia laki sita.”

MIMI: “What? You’ve got to be kidding me, yaani mia sita inapotea kimasihara hivi?”

LUCY: “Wewe ulisema achague anachotaka mimi napata wapi nguvu ya kumzuia wifi yangu kama bossy umesema na unazijua bei zetu.”

MIMI: “Anyway nitalipa hiyo laki moja kuhusu wigi mama J alipewa offa na Iryn achague analotaka ila sikumwambia, wewe ukinitumia ripoti ya mauzo mimi nitajua naandikaje.”

LUCY: “Sawa manager mimi sina usemi.”

MIMI: “Mimi naondoka nataka nikalale mapema hiyo pesa yako nitakupa kesho.”

Baada ya kurudi home nikiwa na wife chumbani kitandani alikuwa ananiambia kwasasa anaona mabadiliko ya Iryn mpaka anahisi kuna kitu kinaendelea kati yetu.

WIFE: “Unajua Iryn ni muda hatuja wasiliana na sio kawaida yake naona ameanza kujitenga na mimi.”

MIMI: “What’s your point?, kwanza mimi ndo nimefurahi maana sipendagi kuona akija hapa home.”

WIFE: “Wewe na Iryn mnasiri kubwa sana ila nitajua tu.”

MIMI: “Daily huwa nasema badala ya kuniombea wewe unaniwazia mabaya tu sijui ndo furaha yako kuona likitokea?”

WIFE: “Sijamaanisha hivyo wewe ndo una wasiwasi.”

MIMI: “Wewe ndo una wasiwasi ndomana hata ile siku nilikuuliza Iryn angekuwa mbovu kama Ebitoke ungekuwa unapiga kelele kama hizi?, nikwambie kitu, wewe umemzidi Iryn kwa vingi tu na si lolote kwako, ifike muda hizi maada ziishe tuwe tunajadili maendeleo ya familia yetu, tusimpe shetani nafasi.”

WIFE: “Sawa Baba J nimekuelewa.”

MIMI: “Tulale kesho asubuhi tuwai kwenda jogging.”

Asubuhi tuliamka kwenda jogging na hii siku kulikuwa na watu wengi sana wakifanya mazoezi barabarani sababu ya holiday “Nyerere day”. Baada ya kurudi nilijiandaa haraka haraka na nikapata breakfast na niliondoka kwenda ofisini, lakini hii siku nilianza na Mikocheni.

Kwa upande mwingine nilikuwa nimem-miss sana Iryn lakini nilisema siwezi mtafuta kwani nitampa kichwa, yeye ndo aliyelianzisha bhasi atalimaliza mwenyewe na kama mbwai iwe mbwai.

Saa 7 mchana niliondoka kwenda Masaki maana Asmah alikuwa kanipigia simu nikifika tu nimjulishe ili tukapate lunch anataka kunipa offa. Na mimi baada ya kufika pale ofisini niliingia ndani na nikawasalimia wote afu tukatoka na Asmah kwenda kupata lunch.

Asmah alikuwa yuko fiti tayari na mguu ulikuwa umepona na alikuwa anatembea vizuri kabisa,

ASMAH: “Insider mimi nina hamu na mishikaki twende Pantaleo.”

MIMI: “Sawa twende mummy mimi sina kauli maana wewe ni bossy wangu.”

Pantaleo Barbeque ipo karibu na Coco plaza “Toure road” ni wataalamu sana wa kuchoma nyama mishikaki nknk. Baada ya kuwasili pale tuliagiza mishikaki kwa chips na tukaendelea kupiga story,

ASMAH: “Insider leo sijisikii kabisa kukaa ofisini pako bored sana, twende Coco beach baada ya kula.”

MIMI: “Kule ofisini unamuamini Hilda?”

ASMAH: “Ame master yuko vizuri sana afu nimewaka mambo sawa tayari.”

Tulikaa pale mpaka saa 10 jioni ndo tukaenda Coco beach kupoteza muda na tulikaa palepale kwa siku zote. Na jamaa baada ya kutuona alikuja chap kutusikiliza ila kwa upande wetu tulikuwa tumeshiba hivyo tukaagiza tuletewe madafu.

MIMI: “Asmah leo nataka nikutoe out but nihakikishie kuwa utakunywa kidogo.”

ASMAH: “Mhhh labda wine nitakunywa ila ni muda sana sijatumia hii.”

MIMI: “Leo nitakupeleka Samakisamaki tukapoteze muda tukifunga ofisi.”

ASMAH: “Sawa haina shida ila itabidi nikabadilike siwezi kwenda nanuka jasho hivi.”

MIMI: “Haina shida ni wewe tu, afu naona siku hizi umeanza kuvaa kaptura waziwazi.”

ASMAH: “Doctor alinambia nisilifunike sana paja niache liwe open muda wote ili hizi alama zipotee kwa haraka lakini nimetembea na gauni ya kujifunika navyorudi lazima nivae.”

MIMI: “Sawa rafiki yangu haina shida itabidi tukirudi ofisini wewe uondoke mimi nitabaki kukusubiri.”

Tulikaa pale Coco mpaka giza ilivyo anza kuingia ndo tukaondoka kurudi ofisini sasa wakati tunaelekea parking kwa upande mwingine jamaa aliniita na akanikimbilia na mimi nikamwambia Asmah atangulie kwenye gari.

Jamaa alinambia Sia alimwachia namba yake ya simu na alimwambia kama ataniona anipe ili nimtafute na mimi nilimwambia anipe hiyo namba. Baada ya kuinakili namba tuliagana na jamaa na mimi nikaelekea kwenye gari na tukaondoka na Asmah pale Coco.

Baada ya kuwasili ofisini Hilda alikuwa pale reception na mimi ndo nilikuwa wa kwanza kuingia ndani na Hilda aliniita,

HILDA: “Manager kuna dada alikuja na amewaulizia wewe na Asmah, nikamwambia mmetoka lunch na akaenda ofisini kukaa, alikuja hata ile juzi.”

MIMI: “Asmah hujamwambia Hilda kuwa Iryn ni nani?”

ASMAH: “Yule ni Bossy wetu Hilda ndomana unaona anaingia ofisini, ile juzi nilisahau kukwambia rafiki yangu.”

HILDA: “Ooh kumbe nilikuwa sijui hata juzi niliona kaingia ofisini kumbe ni bossy.”

ASMAH: “Ndio dear itabidi Insider akutambulishe kwake.”

MIMI: “Haina haja report kaiona na anajua kuna mfanyakazi mpya so usiogope.”

Nilikwenda ofisini na nikachomeka simu chaji na nikatoka nje kukaa kibarazani na haikuchukua muda Asmah alitoka akaniaga anakwenda home kujiandaa then atanijulisha akiwa tayari na akaondoka.

Baada ya dakika 20 Rebby naye alitoka na mkoba wake na akakaa kibarazi kwa pembeni yangu na tukaanza kuzinguna pale,

REBBY: “Manager leo bossy kaja mchana wakati nyie mmetoka lunch na Hilda ndo aliyempa hii taarifa bossy, amekaa hapa mpaka ameondoka na nilihisi alikuwa anakusubiri wewe.”

MIMI: “Hii ni ofisi yake anakuja kuangalia maendeleo na sio kwasababu yangu, vipi mbona mapema sana leo?”

REBBY: “Nimemaliza kazi yangu mapema sana leo acha na mimi niwahi nikaonane na My wangu.”

Na muda huu mlinzi alifungua geti na ilionekana Uber ikiingia ndani,

MIMI: “Usinambie mpaka ume request usafiri upo vizuri sana sikuhizi.”

REBBY: “Mr. analipia acha niwahi.”

Na akaniaga huku anaondoka kwa mwendo wa madaha na mimi nilibaki nikimtizama mpaka anaingia kwa uber na wakapotea maeneo haya.

Niliendelea kukaa pale nje niki-buy time na nikaingia ndani kuangalia simu maana nilihisi huenda Asmah akawa anapiga simu na sipokei, toka aondoke ilikuwa zimekata dakika 40 tayari.

Baada ya kuangalia simu nilikuta missed call za kutosha kutoka kwa Lucy na ikabidi nimpandie hewani na simu iliita kwa sekunde kazaa ndo akapokea,

LUCY: “Insider mambo? upo wapi rafiki yangu? naomba uje hapa ofisini kama upo around nina mzigo wako.”

MIMI: “Mzigo? from who?.”

LUCY: “Iryn kaniachia nikupe inaonekana ni urgent sana wewe njoo uchukue sitaki maswali kama utaona una umuhimu njoo hapa ofisini.”

Niliwaza pale nikaona acha niende japo sikutamani kwenda kabisa,

MIMI: “Ok nakuja ila sikai nachukua huo mzigo nakuondoka.”

LUCY: “Sawa”

Nilitoka Masaki kwa spidi kwenda Mikocheni kwa spidi sana na ndani ya muda mfupi nilikuwa nimewasili pale na nikapark gari nje getini nikaingia ndani kuonana na Lucy na alikuwa ofisini anaandaa ripoti zake.

MIMI: “Lucy naomba huo mzigo niondoke maana nina appointment hapa tena muhimu sana.”

LUCY: “Insider hata salamu hakuna? kaa kwenye coach kwanza tuongee.”

MIMI: “Tulisalimiana kwenye simu au umesahau?”

LUCY: “Okay, Insider Iryn kaja hapa she’s not okay na ameumia sana kujua wewe na Asmah ni wapenzi wa muda mrefu. Na leo amekuja mchana huko Masaki mpaka anaondoka usiku hamjarudi amesema alikuwa anataka kuongea na wewe lakini kwasasa bhasi, hana imani tena na wewe.”

MIMI: “Iryn hana msimamo juzi hapa kanambia kila mtu afanye mambo yake, leo tena anaanza kunionea wivu na Asmah, nimeanza kuamini ule msemo unaosema, ukiona umejua mwanamke anataka nini bhasi jua umekaribia kufa.”

LUCY: “Wewe naye, Insider Iryn anakupenda na point aliyofikia hawezi tena bila wewe, inawezekana anajutia wewe ni mume wa mtu lakini sasa kashakolea ndomana anakosa msimamo juu yako na maamuzi anayofanya yanaishia kumuumiza kihisia zaidi, wewe unachotakiwa kufanya ni kumtengenezea msingi wake.”

MIMI: “Iryn ana act kama mtoto lakini ni mtu mzima, Asmah sio mpenzi wangu kama anavyodai ni vile tunapatana tu na kipindi hiki nimekuwa nampa sana kampani hasa za mazoezi.”

LUCY: “Iryn kachukia na amevimba sana na amesema anajutia sana, ame-apa hato kutafuta tena mpaka anaondoka Tanzania, na hutakuja kumuona tena.”

Muda huu Lucy alifungua drow akatoa bahasha nyeupe ya A4 akanikabidhi.

“Insider bahasha yako hio ya farewell, amesema nikupe maana hawezi tena kuongea na wewe”

MIMI: “Duuh aisee hii ni hatari sana, kama ni hivi bora niache kazi nifanye mambo yangu hata hii barua itakuwa ya kuachishwa kazi na si vinginevyo.”

LUCY: “Hata mimi nahisi hivyo na alisisitiza sana ikufikie leoleo.”

Niliagana na Lucy pale na wakati niko kwa gari nimeshika ile bahasha kwa upande mwingine Asmah alikuwa ameanza kunipigia simu lakini sikupokea maana maneno ya Lucy yalikuwa yamenichanganya sana muda huu.

TO BE CONTINUED

I don't want to end the story on a bad episode.
Hii hapa
 
69 Hii hapa Wildlifer
 
Sema maguire bwana, huo muda unabishana na watu kuhusu uhalali wa mama j kama mke wako si ungeshaleta episode ya mwisho humu tumalize hii biashara? Au unapenda kuona watu wanakutag na kukumention humu wakati wote, lol!
Mwanangu maguire kakukosea nn [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom