Sipingi mawazo Yako lakini unalichukulia hili jambo kwa wepesi sana, tunaoshauri hapa wengine tumeshapitia mambo mazito maishani ni vile tu hatuwezi kuandika Kila kitu hapa, tunauzoefu na haya mambo chini ya mwenyekiti wetu wa kudumu
Watu8
Usifikiri Mama J kuambiwa mapema ni suluhisho la uhakika, anaweza akaambiwa, akavunga amelipokea Kwa moyo mkunjufu bila kinyongo na ndoa ikafungwa lakini atakachokuja kukifanya huko mbeleni anakijua mwenyewe moyoni mwake ( na hii haijalishi ni Mchaga, mmatumbi au kabila Gani)
Kumbuka tayari Mama J ana wasiwasi mzito sana na mashaka juu ya Iryn, Sasa kupata uthibitisho wa hili jambo kutoka Kwa
INSIDER MAN itaurarua moyo wake na kuleta chuki isiyo na maelezo.
Unavyoona tunasema ndoa ifungwe kwanza hayo mambo mengine yatajisumbukia huko mbeleni sio kwamba hatumpendi Iryn na mtoto wake, tunaangalia namna ya kupunguza athari na uharibifu zaidi ya Hali ilivyo Sasa.
Linaweza kuibuka varangati hata jamaa yetu shule isisomeke, kazi zikavurugika na hata mawasiliano ya Siri kati yake na Iryn yakaingia dosari kuelekea asimuone Tena Binti Yao.
Kumbuka Iryn nae ni binadamu ana hisia, likiibuka varangati itabidi aiponye nafsi yake na ya mtoto wake hata kama itabidi kumkwepa Insider.
Ndoa italeta Imani Kwa Mama J na kujihakikishia hati miliki na nafasi yake ya main wife. Danadana zingine ataona kama mizengwe ya kutaka kupigwa chini.
Naomba nieleweke pia nilisema hata jambo la kutambulishwa Iryn na mtoto lisubiri kwanza, sijasema wasipelekwe kabisa Kwa wazazi. Mtoto/watoto lazima wajulikane lakini sio Kwa wakati huu.
Kila maamuzi tunayofanya kwenye maisha, yanagharana zake, ziwe chanya au hasi lakini Yana athiri Kwa namna Moja au nyingine maisha yetu.