Jinsi Crown media ilivyoajiri. Ni somo kubwa kwa Graduates wanaotafuta ajira. Zama zimebadilika

Graduates wengi hawajui wanaishi dunia ya aina gani na hiyo dunia inataka nini kutoka kwao.

Hili likawe somo watu watengeneze folios watu wawaone wanavyovifanya na kuvifahamu.
Majuzi america wame change policy kwenye ajira, now ni skill based employment, education ina nafasi yake but kwneye excutive ila kwenye chini ya hapo wanaangalia ni nn mtu anaweza kufanya.

Anacho kifanya crown ni indication kuwa talent na skills ndio zinapewa kipaombele si vyeti tena
 
Tatizo wanarudi kulekule kwenye kusongamana na kina wasafi na clouds na efm. Hawaoni soko kwa hawa watu wenye umri wa miaka 30 hadi 50. Hawa hawana media yao. Hii Crown kama haijatazama hilo itakwama tu. Na hao wa talent labda wapelekwe kozi maana hawawezi kutegemea talanta zao siku zote. Elimu inahusika sana
 
Elimu ni muhimu sana mkuu mnawaiga USA ambao ninyi mpo kwenye maisha ya kupanda bajaji na boda boda wenzenu wanatumia dk 30 kufika eneo la mbali kwa usafiri wa kisasa...
 
Hii nilisikia .
 
Elimu ni muhimu sana mkuu mnawaiga USA ambao ninyi mpo kwenye maisha ya kupanda bajaji na boda boda wenzenu wanatumia dk 30 kufika eneo la mbali kwa usafiri wa kisasa...
Bado hujaelezea why tusiige. Kwa hiyo ajira zijali vyeti zaidi kwasababu watu wanapanda boda boda? Pathetic man

Na si US tu, dunia inaelekea huko, vyeti vina umuhimu wake lakin kwa sasa dunia inahitaji watendaji zaidi kuliko viongozi. Us , europe even baadhi ya nchi africa zimeshaona hili
 
Course Kama ualimu , habari , na mambo yote ya kukariri yalibidi kupigwa marufuku


Maana watangazi wazuri ni talented
Walimu wazuri ni talented

So course zitolewe Kama short course haiwezekani MTU anakaa chuo miaka 3 anasoma mambo ambayo 90% hatoyatumia katika maisha yake.
 
Kwani kuna shida gani ukiwa na Talent na ni Graduate wa UDSM au UDOM.
 
Same tu me, nilichosomea na nachofanya now ni tofauti ila kupitia knowledge niliyopata skuli nai apply kwenye mitikasi yangu ya sasa..

Elimu ya darasani ina nafasi yake katika maisha si ya kuibeza kabisa..
Serious.. hicho cheti kinawez kukuaminisha sehem ukafanya kazi ambayo haiendani na cheti.. ila wanajua kbs huyu mtu anajitambua, ukiwa hauna kushawishi watu kwamba unajitambua ni ngumu.
 
Elimu ni muhimu sana mkuu mnawaiga USA ambao ninyi mpo kwenye maisha ya kupanda bajaji na boda boda wenzenu wanatumia dk 30 kufika eneo la mbali kwa usafiri wa kisasa...
Ni kweli elimu ni muhimu sana, ila Mkuu Isanga family kumbuka kuwa elimu sio vyeti na elimu ipo kwenye mifumo mingi. Rasmi na isiyo rasmi. Kifupi elimu ni maarifa.

Tatizo vijana wengi hawana maarifa juu ya mahitaji ya dunia ya sasa wao wamekalia mavyeti nyumbani na wanaogopa kufanya mambo kuonesha matunda ya elimu walizoenda kupata chuo.

Matokeo yake, sisi jamii tunaona ni kama hawa vijana hawakupata elimu yoyote chuo bali walienda poteza muda.

Elimu ni lazima uoneshe kwa vitendo sio kwa kutoa vyeti kabatini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…