Jinsi Crown media ilivyoajiri. Ni somo kubwa kwa Graduates wanaotafuta ajira. Zama zimebadilika

Mkuu kila mwalimu ana jambo ambalo anaweza kufundisha watu. Na kila mwalimu anaweza kukaa sehemu yoyote ile akafanya kazi.

Tatizo watu wanafikiri kama chuo alisomea ualimu kwa masomo historia na lugha basi aende kutafuta kazi kwa hayo masomo.

Alafu unakuta huyu mwalimu ni mpiga kinanda mzuri tu kanisani ila bado anasema hana ajira na fani yake ya ualimu hawezi kujiajiri.

Wakati huyu mwalimu anao uwezo wa kufundisha watu mtandaoni namna ya kupiga kinanda, akaandaa lesson plan akafundisha kwa ujuzi wa ualimu alioupata chuo akaeleweka vizuri sana.

Akatafuta sponsors wakamlipa kwa kuweka matangazo. Sio rahisi ila akikomaa kwa mwaka mzima atapata matunda ya kazi yake hiyo.

Vile vile kwa mwalimu yoyote yule, angalia unajua nini kama ni mapishi sawa, kama ni namna ya kufua nguo sawa, kama ni namna ya kusafisha mwili sawa, kama ni mapenzi sawa, wewe fundisha watu mtandaoni kwa taaluma uliyonayo kifupi hakuna mwalimu anayekosa kazi ya kufanya.

Tatizo vijana wengi bongo tumerelax sana. Mtu anataka kama alisomea ualimu wa kiswahili basi akafundishe hicho hicho shuleni utadhani alisoma Unit moja tu ya kiswahili huko chuo.

Wakeup brothers
 
big jo na timu yake ni wabunifu, wanajua soko linataka nini kwa wakati. Ukiwa na journalism ethics inatosha kuwa na exposure kwenye taaluma hiyo ambayo msingi mkubwa ni kipaji na ubunifu
 

I agree with you .
 
Ukitaka habari za tajiri nenda kwa masikini atakuambia kuhusu tajiri!! Ila tajiri hana habari za masikini. Hii ndio Dunia




KAZI ni kipimo cha UTU
 
Ni dhambi sana. Watu wamehangaikamkusoma alafu kazi hawapati
hawana ubunifu na ni wajinga. Vipi usome halafu ukose kazi? Kama umesoma fani ya uandishi andika habari hata bure wape gazeti lolote lenye kuandika maudhui hayo, wahariri wake wataona kazi hiyo na itapewa nafasi na mwisho wa siku utapata ajira hapo. Mitandao ipo, onesha unajua kutangaza watu wa tv watakuona, watayarishaji wa kipindi watakuona
 
Tokea zamani walikuwa na structure ya elimu ambayo ni skill based, hiyo change of policy ni ku fine tune the already stable education system. mwalimu wangu wa peace Corp aliniambia kuwa in America mashuleni darasani ndio utamkuta mwalimu, so Kuna darasa la math, chemistry, physics etc, kama ukitaka kusoma physics pekee unashinda kwenye darasa la somo Hilo, ndio maana vijana walikuwa wanaweza maliza topics kwa muda mfupi na ku graduate wakiwa wadogo, na mahiri.
Huku kwetu mtoto wa darasa la saba ana masomo karibia nane, by the time anakuja ku specialize ni a level, na tayari alishajaza makorokoro kibao ambayo hayatumiii tena,
 
Kassim Majaliwa ni mwalimu, Magufuli ni mwalimu, Nyerere ni Mwalimu.
 
Ndo mana hizi media nyingine zinawaandishi wanafanya vitu so unprofessional, wabongo tunapenda ujinga ujinga tu yani. Kuna wakati unakutana na mwandishi eti anaaweka habari title inasema "Utacheka dokta samia alivyomtania diamond" sasa ni nn???
Upuuzi upuuzi Upuuzi ! Yote hii kwasababu watu wanafikilia wanaweza kufanya vitu bila elimu, nakubali talent ni muhimu lakini Elimu + talent ni muhimu zaidi.
Hii sekta ya media saivi ina vitu vya ajabu sana kwasababu ya hayo mambo ya kukosa professionalism ndo mana sioni ajabu kuona zinafungiwa fungiwa hovyo
 
Naomba msimu 2024/25 tuongeze contents za tiktok challenges and best stories creators. Huwezi jua
 
Maisha ya kimasikini harafu mnasema uige USA haya maisha wenzetu waliishi miaka 200 iliyopita ya kutembeza bakuri ili Nchi iendelee Nchi imejaa majambazi kila kona kwa mali za Umma Waziri Mkuu anazunguka kutangaza watu wasiibe na vyombo vya kuwakamata wezi na kuwawajibisha vipo ila vipo kimya harafu eti tuige sijui USA mkiangalia goggle zenu mnakuja na majibu yeyote...USA Rais anapelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi huku Waziri tu anakingiwa kifua...
 
Wenye vyeti kabatini huku wameshapata cha kufanya mbona wanavidharau sana? ambao hawana ndio wanajua uchungu wa kuto kuwanavyo
 
Mkuu radio/tv presenter siku hizi ni KIPAJI na sio ELIMU wala UJUZI

Mfumo huu hauwezi kuwa applicable kwenye fani kama za Afya, Uhasibu, Udereva nk nk

Kwenye tasnia ya HABARI wasomi wanaajiriwa kufanya kazi nyuma ya screen au mic
Huku mbele ya TV au kwenye mic wanatakiwa watu kama akina Baba levo, Juma lokole, Zembwela, Mbwiga wa mbwiguke...... hakuna mtaala unafundisha kuwa na character kama zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…