Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Huu uzi ni shida[emoji15][emoji15]
 
Tunajua kuwa watu huwa tunapenda kufikia hatua ya penzi hilo kutulewesha, lakini bado tunayo nafasi ya kutoka huko na kuendelea na maisha mengine. Isifikie point tuwe watumwa wa mapenzi.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Nakupa mfano rahisi, em muangalie mtu mwenye uraibu wa kuvuta sigara au mtu alieathirika na upiganiji wa punyeto. Hawa wote wawili wapo kwenye nyakati ngumu kweli kweli, lakini huwa wanafanya maamuzi ya kuacha na wanafanikiwa. Mtu ana pesa mfukoni na sigara anaziona lakini kwa sababu ameamua kuacha sigara hanunui wala kuomba kwa mvutaji mwenzake na mwisho anafanikiwa. Na huyu mpiga punyeto kila anapoingia bafuni anakutana na sabuni, ni yeye kuichukua na kuanza kazi tu[emoji3][emoji3] lakini kwa sababu aliamua kwa dhati kuacha huo mchezo anapotezea na hatimae anafanikiwa. Kwa hiyo hapa kitu cha msingi ni nia ya dhati.

Hapo juu umeandika kuwa wewe ndie ulieachwa, kwa hiyo hupati ushirikiano kutoka kwake, hilo ni suala jepesi kama ukiamua kwa dhati kutoka moyoni. Hali yako ni tofauti na yule mvuta sigara ambae suala la kupata hiyo sigara lilikua ndani ya uwezo wake lakini akaamua kujinyima, au yule mwingine ambae licha ya kukuta sabuni bafuni nae akazipotezea ili kutimiza lengo lake. Jaribu kufikiri kama ungemuacha wewe labda kutokana na tabia zake na angekua anakusumbua ungeweza kweli?

Ushauri wangu ni huu, kubali na uamue kutoka moyoni kuwa it's over. Kama mlikua mnakutana au kulala pamoja kwako badilisha mpangilio wa vitu nyumbani/chumbani.

Acha kusikiliza nyimbo za muziki ambazo mlikua mnasikiliza pamoja maana mara nyingi wapenzi huwa wanakua na nyimbo za uhusiano wao.

Badilisha maeneo ambao mlikua mnaenda pamoja hasa maeneo ya starehe kama kumbi za sinema, beach/hotel au hata club.

Kama ulikua na manukato ambayo ulinunua kwa ajili yake na ukawa unatumia achana nayo.

Kumbuka kuwa wakati wewe unawaza na kuteseka juu yake yumkini yeye amekusahau na ana enjoy na mpenzi mwingine.
Maamuzi ni yako.
 
Daah acha tu nichague kimeo changu, yakinikuta sitolaumu mtu[emoji38][emoji38]
Kwa hizi memories itamchukua muda sana kumsahau jamaa

Wadada mkiambiwa rudini Edeni hamtaki, mnataka mnaowapenda nyie

Ile ya kuchaguliwa hamtaki, mnasikiliza mioyo yenu
 
Hahaha kaka zangu hawana sauti kubwa kama ya kokoto wake (kidding). Mungu atamletea tu mwanaume mwingine mwema
Hahahaaa pole mdada wa kinyaki, life must go on. Atakuja mnyakyusa mwenzako kukupenda, si unajuaga vile kaka zako wanajuaga kupenda? He will spoil you with nyaki love [emoji3590]. Heaven Sent kama kuna kaka ako huko ambaye hana mke jaribu kumfanyia connections binti [emoji23]
 
Hongera kwa kusema ukweli!wewe ndio mwanamke pekee unayeongoza kwa stress humu Jf ila kuanzia leo unaenda kupona kabisa!namba yako ninayo nitakupigia tuongee zaidi
[emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Asee jf banaa
 
Kuna boya hapa linataka kujinyonga demu kasepa na kijiji kasema hamtaki jamaa na status anamuweka jamaa yake mpya toka wiki iliyopita sijui alipewa nini na huyu manzi kupenda hivi ilikua olevel ila hili jamaa na midevu yake linalia kisa penzi
Ukute ni wewe mwenyewe[emoji14][emoji14][emoji14]

Maana jf[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom