Le mobimba
Member
- Dec 1, 2020
- 88
- 154
Daah nimeona Kama unaniongelea Mimi, nakuaga na Huruma Sana hasa mtu akilia shda Kama naweza kumsaidia, namsaidia.. napia naogopa kuwaambia watu ukweli.. coz I hate hurting them..[emoji2960]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daah pole sanaa.. Mkuu.. uko Kama Mimi.. sometimes I hate myself..Mie kwa upande wangu tangu nipo mdogo (kuanzia 10yrs) nilikuwa sipendi kuchangamana na wenzangu, nikitoka shule chumbani hadi kufikia wazazi wangu kuichukia tabia yangu, yaani rafiki zangu wakija kunisalimia nipo radhi nivunge nimelala usingizi ili tu waniachie nafasi ya kuwa peke yangu.
Hii tabia niliendelea nayo hadi secondary school, nilikuwa sipendi kitu chaitwa discussion, ni mwendo wa kupiga msuli mwenyewe.
Pia nimekuwa mchaguzi sana wa marafiki, wale wambea, tantalila nyingi hatuivi zaidi ya salamu, sipendi kusikia mtu ananiletea stori za ooh sijui fulani alikuwa anakusema hivi na hivi, akisikia aliache huko huko.
Kuhusu hisia za upendo ninazo sana iwe kwa rafiki ama mpenzi, na kuhusu kusaidia nachukua tatizo la mtu kama la kwangu, hii imepelekea kudhulumiwa sana na watu niliowaamini na kuwasaidia. Huwa naguswa sana.
Sasa sijui nadondokea wapi?
Da'Vinci
Kabisaa.. naweza nikachat na mtu the whole day, lkn tukiwa Wote.. nakosa cha kuongeani kweli kwenye mitandao ni wachangamfu sana na pia tuko comfortable kuliko kwenye uhalisia.....
[emoji119][emoji119]Hapo nimeona sifa kadhaa; aibu, marafiki wachache, uwezo mdogo wa kujielezea na kuongea mbele za watu ingawa nikiwa mbele ya watu nnao wajua huwa naongea, pia kama nikipatwa na matatizo huwa nasimulia kwa wachache ila baadae huwa najilaumu kwa kuona kwamba hata nilivyosimulia hakuna msaada uliotokea na kwamba ningekaa kimya kisingeharibika kitu, nina asili ya kupenda usafi na vitu viwe ktk mpangilio.
Daah huyu ni mimi kabisaNaongezea sifa zengne tulizo nazo ma introvert...
1-: hatujui kuchagua vitu hasa rangi au umbo....yaani unaweza ukatoka nyumban kwenda dukan kununua labda nguo aina flan rangi flani ile nguo ukaikosa apo Sasa muuzaji anaweza akakuuzia rangi yyte ata usiopenda na ukashindwa ata kukataa...unalipa unasepa uku ukijifariji.
2-:wapekuzi sana wa mambo yaani Kama unamauhusiano na bint utampekua bila yeye kujua adi mambo yasiopekurika mwsho wa sku huwa tunabaki na siri moyoni wala hatuwaambii wale tulio wapekua..
3-: hatupendi kutishwaa....mfano kutishwa utoe kitu fulani ili upate kitu fulani,
4-:hatuwezi kusimulia vtu kwa mdomo...tunaweza tukasoma vtu tukavielewa Ila Kwenye kuvipresent tukashindwa.
5:- huwa tunatamani tuwe tofauti na tulivyo Ila tunajikuta tupo hvyohvyo,usipojijua utabaki unaishi maisha ya kuiga tu.
6-:tunapenda Sana kufanya mapenzi Ila hatupendi tuonekane katk hali hyo...
7-: wapenzi wetu Mara nyingi ni wale marafiki zetu wa karbu sana...tulio wazoea ndo hao hao tunawatongoza.
Type 1 inanihusu Kabisa
Mh aliesamarise aniappdate [emoji21]introverts wote wana sifa hizi
- Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
- Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
- Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
- Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
- Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
Sifa zao nyingine ni pamoja na;
- Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
- Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
- Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
- Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasani si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
- Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
- Wakata tamaa wanapokosolewa.
- Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
Nyinginezo ni;
- Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
- Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.
- Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
- Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
- Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa).
- Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.
- Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.
- Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
Pia, wanafahamika kwa;
- Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
- Wana busara na hekima nyingi
- Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
- Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
- Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
- Ni kundi la watu wanoridhika haraka
- Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa.
- Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
- Kundi linalopenda amani na utulivu
- Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
- Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu.
Wana sifa nyingi sana, nyinginezo ni;
- Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
- Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
- Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
- Wakati mwingine hupenda kujikataa.
- Ni waaminifu na wasema ukweli
- Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
- Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
- Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
- Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
Kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani].
- Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
- Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua.
Hiyo hali inatukumba wengi tu, pole sanaThat's me.. [emoji24] naweza nikawa sad ila natabasam
Una sh ngapi..?Mh aliesamarise aniappdate [emoji21]
Dau lolote unalotaka[emoji16]Una sh ngapi..?
Oooh...apo sawaa,mi nataka kile kipenda rohoo 😉Dau lolote unalotaka[emoji16]
jamaa anaonekana mpole sanaMimi sio introvert, lkn nina rafiki tangy yuko hivyo, nilikutana nae shule. Ilikua shida Sana kumzoea Ila tulienda sawa akawa rafiki mpka leo.
Alikua na aibu na uwezo mdgo Sana wa kujieleza. Nakumbuka kuna binti alikua anampenda sana lkn anashindwa kumueleza. Nikimuuliza anakataa ingawa nilijua hilo. Nilichofanya nilimfuata yule dada, nikamueleza ukweli kua jmaaa anakupenda sana lkn anashindwa kukuanza tu, na yuko hivyo kama unahisia nae mrahisishie muwe wote, kumbe binti nae alikua anamkubali Sana jamaa. Walipoanza mapenzi toka 2013, mpaka leo na wapo kwenye process za kuoana saiv. And lack enough jamaa alikua hajawahi kusex na bint alikua virgin sijui siku ya kwanza kukutana ilikuaje.
Jamaa hata awe na shida vip, hapendi kuomba msaada, yaan mpka mda mwingine naforce tu kumsaidia.
Jamaa alikua hapendi maneno mengi anaboreka Sana. Niliwahi kwenda magetoni kwake na rafiki angu mwingine sasa huyo rafiki mwingine alikua hatulii Mara kabadilisha wimbo, Mara kabadilisha movie kwa laptop, Mara kakosoa hiki, Mara kile. nikaona jmaa anakosa amani nikaamua kuondoka tu ili awe huru.
That is me,yaani nikitoa kitu sehemu nikimaliza kutumia narudisha pale kilipokuwa,uchafu ni adui yangu mkubwa,huwa ni rahisi kuweza kujua kuwa kuna mtu kapekuwa vitu vyangu,napata tabu sana kuishi na mtu asiejielewa,mtu ambaye ni rough,hata kama angekuwa na pesa na mali naweza nisione thamani yake kabisa.But to be honest am proud to be introvert...Hapo nimeona sifa kadhaa; aibu, marafiki wachache, uwezo mdogo wa kujielezea na kuongea mbele za watu ingawa nikiwa mbele ya watu nnao wajua huwa naongea, pia kama nikipatwa na matatizo huwa nasimulia kwa wachache ila baadae huwa najilaumu kwa kuona kwamba hata nilivyosimulia hakuna msaada uliotokea na kwamba ningekaa kimya kisingeharibika kitu, nina asili ya kupenda usafi na vitu viwe ktk mpangilio.
Haya. Msalimie mamilooo huyoNo ule ni mchezo wa asili hauna kocha wala mashabiki utaalamu unapatikana automatic
Oooh safi sana, nimekupata.Yaani mimi mtu ambaye hajanizoea akipata nafasi ya kuwa karibu nami anaweza akahisi nina tatizo kubwa sana nalitafakari, kumbe mwenzie wala naenjoy zangu kufikiria tu
Hahahahahha safi sana aisee, inavutia, inapendeza!!! Watu poa sana hawa introverts.
Nina aibu mbele za watu labla chumbani kwangu nikiwa pekeangu.hizo mambo tuwaachie kina sanguineNaomba kuuliza ivi ma introvert wenzangu mnajua kucheza yaan kudance kwenye party stlye kama vile kwaioto shakushaku au yeyoye ile
Vip kwenye sherehe kama graduation yako ya shule ivi ulifanyaje vp haujawah kutana na tukio lolote lililokutaka ucheze je ulifanyajeNina aibu mbele za watu labla chumbani kwangu nikiwa pekeangu.hizo mambo tuwaachie kina sanguine