Jinsi Introverts wanavyopata tabu kuingiliana na watu wanaowazunguka

Jinsi Introverts wanavyopata tabu kuingiliana na watu wanaowazunguka

Yes offcourse hata mimi ndio nilivyo.
Kwa mfano mtu akiniletea dharau huwa narekodi halafu namvizia baada ya muda mrefu sana wakati kashasahau namfanyia kitu ambacho kitamtesa miaka yote.
Yaani niko very strategic nikimuwekea mtu mtego anakuja kunasa mzima mzima lazima kamasi zimtoke.
Akili mingi.. Tena Kwenye mahusiano ndio tunawachoraga sana wasiotufaham.. siku moja tuu mtu anawekewa File mezani mpaka kuomba msamaha au kutetea haki yake anashindwa.
 
Kuna kipindi fulani wife alikuwa anachonga sana mimi nikawa nipo kimya tu namsikiliza kila siku akajua ameshanikamata tayari.
Dah basi nikamchoka aisee akashangaa siku moja namvutia waya mshenga wetu tumalize mchezo kila mtu afe kivyake aisee macho yalimtoka hakuamini kinachoendelea basi tangu siku hiyo amekuwa na adabu ameshajua kwamba sinyenyekei mtu na sihangaiki na uzuri[emoji3][emoji3][emoji3][emoji38]
Akili mingi.. Tena Kwenye mahusiano ndio tunawachoraga sana wasiotufaham.. siku moja tuu mtu anawekewa File mezani mpaka kuomba msamaha au kutetea haki yake anashindwa.
 
Kwenye makundi ya binadamu i mean intro, extro na ambivert makundi nyota (zodiac signs) yanachangia kiasi kikubwa kudetermine group ambalo una exist.

Mfano nyota ya samaki(pisces ) watu wake wengi ni introvert while nyota ya simba(leo) watu wake wengi ni extrovert.

Na ukitaka kupata mwenza wa maisha consider makundi nyota.. utapata who is compatible to your sign and who is not
Nimekuelewa vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemaliza kila Kitu, kama hizo ndio tabia za ma Introvert huyo ni mimi kabisa na mbaya zaidi nazikuta hizo tabia mpaka katika nyota yangu, Scorpio 10, Nov.

Kikubwa uzi huu umenisaidia kubishana na hali hii kwa kiasi fulani... coz kuna mambo mengi niliyoanza kuyafanya ila kuyamalizia ndio mtiti ulipo kwakua naona kama finishing haitakua kama ile niionayo fikrani so now nimeamua kuyamalizia hivyo hivyo na mrejesho niupatao ni tofauti na nilivyokuwa nadhani mwanzoni. Kumbe nilikua sahihi tuu.

Kero kubwa niipatayo ni watu wangu wakaribu ndugu na marafiki kudhani nipo katika mateso ya maisha yangu. ilhali mimi kama mimi naenjoy tuu. Nilijua nimeamua tuu kupenda kuwa peke yangu kumbe sivyo... but faida za upweke zimenifanya niwe mult talented kwakyweza kufanya vitu vingi vyakisanaa kuanzia kuchora, kuimba, kuigiza, kutengeneza uchongaji, ushonaji na hakuna kitu nimejifunza nikafeli.

Na kitu kingine ni watu kudhani mimi siwezi kukosa deal lakufanya kiasi hata deal zikija wanadhani nitazikataa kutokana na u personal wangu katika kuishi. So nakosa michongo mingi sana mpak nikiwa natangaza ukitokea ila bado naonekana kam natania.

Maapenzini ndio umeua kabisa, katika puyanga zangu mpaka sasa sijawahi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye sikufahamiana nae b4 mahusiano.. hata nijue yeye ndio ananipenda mpaka hajiwezi lazima nimfanye rafiki kwanza nikimuelewa tunalisongesha..

Sasa kama kun jamii hii yetu, je Jamii kwa ujumla ina elimu ya tabia hizi? Jibu hakuna, kwa maana hiyo kuna watu wengi channel zao zimekuwa chenga kutokana na kulazimishwa aishi katika maisha yasiokuwa yake..

Kila niliposoma, hadi kuzoeana na maclassment ilikua inanichukua mwaka mzima, na nikishazoeana nao, mimi ndio nakua kiongozi wa watu wenye mishemishe na kufikia kuweza kuwa kiongozi wao.

Ninachokiona sasa, hata mahusiano ya watu wa jamii hii wengi huwa wametendwa kuliko kuwatenda wenzi wao. Na kibaya zaidi Introvert akisema hataki kutoka moyoni, bora uachane nae labda iko siku atakukumbuka, Hatulagi matapishi kabisa.

Swali langu ni hili... Je kwa baadhi ya tabia za Introvert haziwezi kuwekwa katika kundi la magonjwa ya akili?
Mfano kujiona na kuamini yeye ni mtu muhimu na mwenye heshma zake katika jamii na sometimes hana vhochote akifanyacho.
Mwanzo wa kujitambua ndo mwanzo wa kuutambua ulimwengu...

Wengi leo wanaishi maisha ambayo si yao,kwasababu ya kukosa kujitambua....ndo pale unakuta mtu anafanya jambo Ili tu aendane na mtu fulani au amfurahishe mtu fulani.

Hapana introvert si tatizo la kiakili,ni katka kujitofautisha kitabia miongoni mwa wanadamu,kama ilivyo mfano:-

Makundi yetu ya damu....makundi yetu ya rangi....makundi yetu ya kijinsia....n.k
Lau tungeumbwa wote tuwe tunafanana kwa kila kitu sijui dunia leo ingekuwaje.

Natamani sana elimu yetu ya msingi ingekuwa inafundisha masomobya psychology na ujasiriamali wa kujitegemea...

Faida ya kujitambua utaweza kugundua mengi kwanza kabisa utajua nini unataka/unapenda ktk maisha yako na nn hupendi/hutaki katka maisha yako...hii itakufanya ujitofautshe na wengne....

Kuna baadhi ya vitu/watu watahitaji wawe na wewe lakini kutokana na wewe ushatambua nini unataka huenda ukaishia kuwakwepa au kuwakataa,mwishowe watasema wewe unaringaa.
 
Hii thread nimeipenda sana...
Kwanini tusianzishe LIVE MEETINGS kwenye mikoa tuliyopo kwa ajili yetu sisi Introverts; ili tutiane moyo, tuelimishane, tujengane na tutafute suluhisho za kudumu kwa mambo yanayotusibu katika maisha?
Halafu si vibaya tuanzishe hata telegram group letu jamani.

NB: Mimi sipo social sana, ila napenda ku'volunteer na kuwasaidia watu na jamii kwa ujumla. Pia, mimi kwa sasa nina Confidence katika maswala ya kujieleza na kufanya Presentation mbele za watu.

, lkn nina rafiki tangy yuko hivyo, nilikutana nae shule. Ilikua shida Sana kumzoea Ila tulienda sawa akawa rafiki mpka leo.
Alikua na aibu na uwezo mdgo Sana wa kujieleza. Nakumbuka kuna binti alikua anampenda sana lkn anashindwa kumueleza. Nikimuuliza anakataa ingawa nilijua hilo. Nilichofanya nilimfuata yule dada, nikamueleza ukweli kua jmaaa anakupenda sana lkn anashindwa kukuanza tu, na yuko hivyo kama unahisia nae mrahisishie muwe wote, kumbe binti nae alikua anamkubali Sana jamaa. Walipoanza mapenzi toka 2013, mpaka leo na wapo kwenye process za kuoana saiv. And lack enough jamaa alikua hajawahi kusex na bint alikua virgin sijui siku ya kwanza kukutana ilikuaje.
Jamaa hata awe na shida vip, hapendi kuomba msaada, yaan mpka mda mwingine naforce tu kumsaidia.
Jamaa alikua hapendi maneno mengi anaboreka Sana. Niliwahi kwenda magetoni kwake na rafiki angu mwingine sasa huyo rafiki mwingine alikua hatulii Mara kabadilisha wimbo, Mara kabadilisha movie kwa laptop, Mara kakosoa hiki, Mara kile. nikaona jmaa anakosa amani nikaamua kuondoka tu ili awe huru.
 
Kwenye makundi ya binadamu i mean intro, extro na ambivert makundi nyota (zodiac signs) yanachangia kiasi kikubwa kudetermine group ambalo una exist.

Mfano nyota ya samaki(pisces ) watu wake wengi ni introvert while nyota ya simba(leo) watu wake wengi ni extrovert.

Na ukitaka kupata mwenza wa maisha consider makundi nyota.. utapata who is compatible to your sign and who is not
Oooh, ni vema kuchagua mwenza ambaye uko naye nyota moja au?
 
Nguvu niliyozungumzia ni ile hali ya kuhisi akili na mwili wako uko active yaani haujashoshwa.Hata wewe ukijichunguza vizuri utagundua kuna vitu ukifanya akili au mwili wako inachoka au inapata nguvu.Sasa kiasili kuna mambo yanachosha ubongo wa introvert kwa wepesi,ubongo wa introvert unapenda utulivu.
Vitu kama sauti ya mziki wa juu sana,maneno maneno mengi,purukushani/hekaheka,makelele n.k vinasumbua ubongo wa introvert,ndo hapo tunahitaji mazingira yatakayorudisha nguvu mara inapotoweka.
Natumai umeelewa otherwise atakuja introvert mwingine kukueleza vizuri
Ndugu, nakuelewa vizuri, ili nijue vizuri haya mambo, kuna course au kitabu unaweza kupendekeza? Msaada wako tafadhali. Pia, comments za huko juu, jamaa amegusia kidogo kwamba tarehe na mwezi wa kuzaliwa una mchango katika haya mambo kidogo, je hili likoje?
 
Oooh, ni vema kuchagua mwenza ambaye uko naye nyota moja au?
hapana mkuu haiko hivyo..kila nyota ina nyota ambazo inaendana nazo kwenye suala la mahusiano..hasa hasa nyota ambazo mnashare elements (moto,hewa,maji na udongo)

mfano mwanaume wa nyota ya simba anatakiwa kuwa mwanamke wa nyota ya kondoo ,mshale na mizani

nk
 
Naomba kuuliza ivi ma introvert wenzangu mnajua kucheza yaan kudance kwenye party stlye kama vile kwaioto shakushaku au yeyoye ile
Me nina kipaji cha kudance sana style hizi za kisasa hata trap za kina ayo & teo ila huwa nafanya ndani. Hadharani siwezi kabisa yaaani
 
Hivi kushindwa kusamehe ni tabia ya introvert pia au ni litabia langu tu libaya?. Binafsi huwa sio mtu wa kukasirika kirahisi, mtu anaweza kunifanyia kitu kibaya sana na nikawa namchekea tu. Ila ikitokea siku nikakasirika, hiyo ndo nitolee....hata atembee kwa magoti kutoka kwake hadi nilipo siwezi hata kifikiri kumsamehe.


Huu ni mwezi sasa tangu rafiki yangu wa karibu sana (jinsia ke) anitamkie kauli ambayo sikuipenda (si kauli mbaya sana kiasi hicho na nadhani alisema katika hali ya kunitania), kuanzia siku hiyo nilamfungia vioo. Ametuma meseji kibao akiniomba lakini sijajibu hata meseji moja na sina mpango wa kujibu, amepiga simu sana lakini sipokei na sina mpango wa kupokea. Mpango nilionao ni kumwondoa mbali kabisa na maisha yangu.


Yeye ndiye alikuwa alikuwa rafiki yangu wa pekee wa kike. Tumepitia nyakati nzuri sana na yeye tukiwa kama marafiki wa karibu.


Sasa hivi nimebaki mwenyewe tena, nikiwa alone ni mwendo wa kubadili vifaa tu. Mara nishike simu, mara nishike peni na daftari, mara nitupe peni nichukue penseli, mara nishike pc, mara nishike kitabu.


Ila napenda jinsi nilivyo.
Mzee we upo kama mm yani 😂kuna manzi mmoja ingawa ni mzr akanikoroga nilivyomfungia vioo hakuamn mpaka leo mwez wa 4 anaishia ku view status zangu tu na hapo nisha block weng inshort sipend kelele na mtu anipande kichwan kwa upole wangu
 
Akili mingi.. Tena Kwenye mahusiano ndio tunawachoraga sana wasiotufaham.. siku moja tuu mtu anawekewa File mezani mpaka kuomba msamaha au kutetea haki yake anashindwa.
Kila navyopitia comments naona kama introverts wengi ni mapacha yan mm yan mm nikikwambia no ujue nnasabab kama 3-5 na huwez kujitetea
 
Kila navyopitia comments naona kama introverts wengi ni mapacha yan mm yan mm nikikwambia no ujue nnasabab kama 3-5 na huwez kujitetea
Kuna mdau katoa wazo hat tuwe tunakutana kwa ajili yakushare changamoto zetu naongezea hasa zile zinazoweza kutufelisha kimaisha.

Nilipanga nyumba ambayo tulikua kama wapangaji 9, iliwachukua kama miaka 3 kulijua jina langu tuu... na wakaanza kuniogopa yaani issue zote watatuma watoto waniambie.

Sikua najua kuwa hii ni Nature yangu, kimahusiano naweza sema yale yliyovunjik basi mimi ndio niliyvunja.. na baada ya uzi huu hope utanisaidia sana mbeleni.

kwa watu walionizoea, mimi ni intertainer wao na hawachoki kukaa na mimi isipokuwa huwa nakerekwa na vitu vidogovido.

Sema kwa suala la kujielezea mbele za watu, aisee mi siogopi ila iwe ni issue kweli sio maigizo au blabla... hapo unaweza sema nina aibu au nanata sana. Maana yasiokuwa na maana huwa nayahisi kabla na huwa hivyo kweli na kama kitu sina uhakika nacho hata kama nitapata hasara kutokukifanya bora iwe ivyo.

Nakunatabia moja, naweza kumshauri.mtu ushauri mzuri sana utakaomsaidi katika changamoto zake lakini mimi nikiwa nachangamoto kama zake siwezi kuutumia ushauri niliompa.

Kuna mengi mengi mengi....
 
Kabisa huyo ni Mimi sipendi ligi/vita.ukinikosea uniombe msamaha au usiniombe ukiniongelesha nitaongea tena kwa tabasamu,lakini moyoni mwangu sitakaa nikuamini wala sitakuchukia.naweza nikawa na huzuni sana moyoni ukaniongelesha nikakujibu kwa tabasamu at the same time machozi yakawa yananitoka halafu siwezi kusema kwa nini Niko hivyo basi naishia tu kusema Niko sawa!!!!

Introverts tunaongoza kwa Gubu hatari. Gubu hilo aisee 🤣🤣🤣
 
Mimi maisha yananibadilisha, now ni introvert niliyechangamka.

Kilichobaki ni kutokuweza kuchangamana na watu kabisa, kutumia muda mwingi peke yangu, mtu akiwa hanipi amani namuondoa kabisa kwenye maisha yangu. Kukaa kimya kunazidi kupungua now mtu akinikera Nampa live.

Napata amani zaidi nikiwa peke yangu
 
Mimi sijui nipo kundi gani napenda kujifahamu maana nahisi hakuna mtu anayenielewa nipoje personally.

Sifa au tabia zangu ni kama zifuatazo:
1. Mimi ni mcheshi (mwenyekupenda sifa) kila kitu nataka niwe muongozaji nikiwa mbele za watu napewa heshima na attention kubwa
2.mimi napenda kujichanganya na watu lakini sitaki unifuatilie kabisa ani.
3. Mimi ni creativity personal na watu wananiamini natengeneza simu, umeme majumbani, vifaa vya umeme,shughuli za ujenzi na kupaka rangi kuta bila ujuzi wowote kutoka chuo.
4.nina vipaji vingi nacheza basketball sana tu, napiga guitar,naimba.
5.Sipendi kumfuatilia mtu hata ukija na story zako za kisinichi nakutema hapa sasa najikuta kuambiwa nina dharau
6.nachagua marafiki japo ni rafiki wa kila mtu lakini mpaka niwe na best friend hapo pana kazi sana kila mtu namuona ni sinchi tu.
5.katika aibu sina aibu kabisa aidha kwa KE au ME.
6.katika mahusiano najitoa ufahamu kabisa nikipenda napenda kweli kweli hata iweje natumia kila njia tustand kwenye relation lakini nisipopenda lazima ujutie kwanini ulinifahamu 😂😂😂😂
7.Napenda kuwa systematic kitika kila jambo sio mwepesi kukatishwa njiani yani kuishi out of my willing.

Wana psychologist nipeni madini ni ya mung'unye 😂😂😂
 
Kuna mdau katoa wazo hat tuwe tunakutana kwa ajili yakushare changamoto zetu naongezea hasa zile zinazoweza kutufelisha kimaisha.

Nilipanga nyumba ambayo tulikua kama wapangaji 9, iliwachukua kama miaka 3 kulijua jina langu tuu... na wakaanza kuniogopa yaani issue zote watatuma watoto waniambie.

Sikua najua kuwa hii ni Nature yangu, kimahusiano naweza sema yale yliyovunjik basi mimi ndio niliyvunja.. na baada ya uzi huu hope utanisaidia sana mbeleni.

kwa watu walionizoea, mimi ni intertainer wao na hawachoki kukaa na mimi isipokuwa huwa nakerekwa na vitu vidogovido.

Sema kwa suala la kujielezea mbele za watu, aisee mi siogopi ila iwe ni issue kweli sio maigizo au blabla... hapo unaweza sema nina aibu au nanata sana. Maana yasiokuwa na maana huwa nayahisi kabla na huwa hivyo kweli na kama kitu sina uhakika nacho hata kama nitapata hasara kutokukifanya bora iwe ivyo.

Nakunatabia moja, naweza kumshauri.mtu ushauri mzuri sana utakaomsaidi katika changamoto zake lakini mimi nikiwa nachangamoto kama zake siwezi kuutumia ushauri niliompa.

Kuna mengi mengi mengi....
wanawatuma watoto wakuambie[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom