Mimi huona ni kawaida na hafanyi kwa kuwa ananitaka, bali kila mtu anaweza kufanya hivyo, kifupi nina mtazamo huo. Hii inapelekea nisiwe na hisia zozote za kujiongeza na kuishia kuambiwa naringa. Mimi ninaamini labda anitamkie wazi wazi kabisa ndipo nitaamini kuwa ananipenda, otherwise nitaona ni kawaida tu, maybe anafanya kama rafiki au jirani tu. Kama nakosea kwa mtazamo huu, nibadilike. Pia akijipitisha na ukamtongoza akakubali, vipi kama akikuchoka baada ya muda mfupi kwa kutoona vile alivyodhani upo? Imagine anakubadilikia na anakuambia hakutaki tena, inauma eeeh? Umakini unahitajika!