Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Kama faidika.letsshego ni noma..ukichukua M 3 kwa miaka Minne unakuja kulipa.M 5.6 huko
Bank yenye unafuu kwenye mikopo kwa watumishi ni CRDB tu licha ya kwamba sharti waliloliweka kwamba lazima mshahara wa mtumishi upitie huko miezi miwili huko na kuendelea huko huko baada ya kuchukua sera hiyo imewafanya watumishi wengi washindwe kukopa huko isingekuwa hivyo hiyo benki wangevuna mabilioni na mabilioni toka kwa watumishi
 
Saccos ipo vizuri. Mfano walimu siku wakija kujielewa nakufuta kikundi chao cha hovyo CWT wakaanzisha saccos moja matata alafu wakakopeshana kupitia hiyo saccos nadhani hata mpwayungu village angetamani kurudi kufundisha.
Hao Cwt walikuja na gear ya kusema wataanzisha benki yao ili iwakopeshe walimu kwa riba nafuu sana kuliko benki zote na kwa neema ya Mungu wakaanzisha mwalimu commercial bank na kwa jinsi walivyo watu wa ovyo tofauti ya riba na Nmb ambao ndio wakopeshaji wakubwa wa walimu kwa miaka mingi ikawa na asilimia 2.Hakika nimeamini shetani si lazima awe na mguu mmoja na wala hayuko mbali
 
Kuna benki flani ilikopa madolari huko IMF kwa 5% kwa miaka 10, wao wakakopesha 18%, na wengi wa waliokopeshwa ni watumishi.
Nasikiaga mambo za processing fee, kwani kuna kampuni (kama DP vile) ilayochakata mikopo tofauti na maafisa wa benki?
 
Kabla ya kuomba mkopo tunawatumia wao kutupatia ushauri wa nini nifanye, sio kila mmoja amesoma uchumi.

Cha ajabu ushauri wanaonipatia hata mimi nisiesoma uchumi siwezi kumshauri mtu afanye.

Actually riba ilikua 16% plus hiyo processing fee ilikua almost 4 Million.

Hizi benki zinatakiwa kuwa msaada kwa watumishi kwasababu ndio kundi kubwa zaidi linalozifanya ziwe hai, maana yake zilitakiwa kuweka mikopo isiyoumiza sana, angalau riba 11% per annual.
"Bank si rafiki wa masikini" hii kauli aliwahi kuitoa Mzee wa Msoga katika moja ya hotuba zake. G.Mukoba aliyewahi kuwa kiongozi wa juu wa TUCTA alisema kuwa Wafanyakazi ni tabaka la watu masikini duniani. Alitoa kauli hiyo katika mahojiano ya moja ya vipindi vya television akihojiwa nyumbani kwake mwaka jana 2022.

Ziko sheria za fedha na uchumi zinazosimamia masuala ya mikopo Tanzania. Wakopaji wengi hawana elimu ya mikopo na riba hasa wafanyakazi na ndio maana wanaumizwa zaidi kuliko wafanyabiashara wakopaji. Elimu ya fedha ni kitu ambacho wakopeshaji hawataki wakopaji waipate ili waendelee kufanya "plundering" inayolindwa kisheria.

NB: katika duni hii ya "dog eat dog" mtu masikini/mfanyakazi ni f.a.l.a.
 
Habari za jioni GT...Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mabenki nchini wanawaibia sana watumishi wa umma kupitia kinachoitwa mikopo ya watumishi. Nina rafiki yangu anafanya kazi serikalini. Juzi alienda kukopa pesa benki (NMB)...sasa shida ilianza juu ya mchanganuo wa mkopo, duh, ni hatari.

Kwa kiasi cha Tsh mfano 6M, unatakiwa urudishe almost zaidi ya 10M. Bado kwenye hiyo 6M uliyoomba, wanakata 8% kama processing fee. Hivyo, unajikuta unachukua net take home 5.4M. Kumbuka mkopo huu unakatwa kwa muda wa miezi 96. Yaani, unapewa 5.4M, unarudisha 10.6M. Hii ni sawa na riba ya 100%.

5.4M * 2 = 10.8M. Kwanini wasikopeshwe bure kama walivyo wafanyakazi wa BOT, NMB, NK ambao hawatozwi riba kwenye mikopo yao? Serikali ipo wapi kwenye wizi huu wa mchana?
Ukikopa milioni 20 utarejesha milioni 20.

Wakati mwingine heri Mkopo wa NMB kuliko TRA pale bandarini, unanunua gari la milioni 10 inabidi uandae milioni 12-13 ya Kodi.

Kwa Tanzania kila sehemu ni wizi tupu
 
Serikali kuingilia kati? Benki zinafanya biashara.


Kuna mikopo ya hazina (haina riba). Kuna mikopo fulani una riba ya 6% .


Siyo lazima ukope.
Huwezi kupata mkopo kwa urahisi kwani ukifika tu wanaanza kugawana mabosi za kubakia ndio wanawapatia wachache tena kwa connection na unaweza ambiwa chukua mwisho 5 millions
 
Mkuu yaani acha tuu.
Wanachokifanya kwenye ule mkataba just wanakuambia just usaini sehemu yako na shahidi wako tu. Ile sehemu utalipa kiasi gani wanajaza wao wakati haupo, apo utakachoambiwa ni makato ya mwezi ni kiasi gani.

Ni mtumishi mwenyewe azidishe makato ya mwezi na idadi ya miezi ya mkataba, hapo ndipo anaweza kugungua huu wizi.
Acha kukaza fuvu watu wameeleza vizuri hapo juu kuwa shida wewe umetaka kurudisha pesa Kwa muda mrefu. Hakuna wizi hapo
 
Bank za biashara (commercial bank) ni wafanyabishara sawa na wafanyabiashara wengine wanaonunua(kutoka kwa wholesaler) na kuuza bidhaa. Pesa ndo bidhaa(goods) ambayo bank huifanyia biashara so ni lazima bidhaa hiyo itengeneze faida kumbuka wao wanakopa central bank(BOT) ambako na wao wanalipa riba ili hizi bank zipunguze riba ni lazima anayewauzia hiyo bidhaa yaani BOT ipunguze riba. So msiwalaumu nmb and others na msije mkadanganywa kuwa eti kuna bank hazitozi riba hiyo bank haipo!!!
Bank za kiislam hazina riba
 
Bank yenye unafuu kwenye mikopo kwa watumishi ni CRDB tu licha ya kwamba sharti waliloliweka kwamba lazima mshahara wa mtumishi upitie huko miezi miwili huko na kuendelea huko huko baada ya kuchukua sera hiyo imewafanya watumishi wengi washindwe kukopa huko isingekuwa hivyo hiyo benki wangevuna mabilioni na mabilioni toka kwa watumishi

Ila NMB wanatisha kwa sasa wana riba kubwa sana na ada ya mkopo ni kubwa sana,
 
Back
Top Bottom