Habari za jioni GT...Niende moja kwa moja kwenye mada.
Mabenki nchini wanawaibia sana watumishi wa umma kupitia kinachoitwa mikopo ya watumishi. Nina rafiki yangu anafanya kazi serikalini. Juzi alienda kukopa pesa benki (NMB)...sasa shida ilianza juu ya mchanganuo wa mkopo, duh, ni hatari.
Kwa kiasi cha Tsh mfano 6M, unatakiwa urudishe almost zaidi ya 10M. Bado kwenye hiyo 6M uliyoomba, wanakata 8% kama processing fee. Hivyo, unajikuta unachukua net take home 5.4M. Kumbuka mkopo huu unakatwa kwa muda wa miezi 96. Yaani, unapewa 5.4M, unarudisha 10.6M. Hii ni sawa na riba ya 100%.
5.4M * 2 = 10.8M. Kwanini wasikopeshwe bure kama walivyo wafanyakazi wa BOT, NMB, NK ambao hawatozwi riba kwenye mikopo yao? Serikali ipo wapi kwenye wizi huu wa mchana?
Mkuu napingana na wewe kidogo katika hili.
Zamani nilikuwa nawaza kama wewe kuwa benki wanatuibia sana kumbe kiuhalisi tunanufaika sana kuliko benki.
Hoja ni kwamba umekopa kwa ajili gani? Kuna mikopo mzuri na mikopo mibaya, mkopaji ukiangukia ule upande wa mikopo mibaya lazima uone kama vle benki imekuibia na riba utaiona ni kubwa, ila ukiwa upande wa mikopo mizuri na mkopo wako uwe productive utaona kabisa kuwa benki unawapunja na wamekupendelea kwa jinsi unavyopata faida kuliko wao watakavyofaidika kupitia riba yao.
Mfano ukope hiyo 6M kwa mda wa miaka 8 na wakupe mkononi kiasi cha Tsh 5.4M. Uiingize kwenye biashara ambayo kwa mwaka wa kwanza utapata faida ya angalau 1.5M,
5.4+1.5=6.9.
Mwaka wa pili mtaji wako ni 6.9M, izungushe tena na faida yako kwa mwaka iwe ni 2.1M,
6.9+2.1 =9.0.
Mwaka wa tatu mtaji wako ni 9M, zungusha huu mtaji na faida kwa mwaka huo iwe ni 2.6M,
9+2.6=11.6
Ndani ya miaka 3 kama biashara yako inaenda vema unakuwa umeikamilisha hela ya benki, miaka mingine mitano iliyobaki kukamilisha miaka 8 ya mkopo wako unakuwa unafanya faida yako. Nani hapo mwenye faida kubwa kwenye huo mkopo kati yako na benki?
Mikopo ina faida sana kwa wanaojua kuizungusha pesa ya mkopo. Shida tunakopa kupeleka kwenye vitu ambavyo havizalishi au kwenye biashara mpya ambazo hatuna uzoefu nazo ndio maana mara nyingi tunaishia kuona tunakatwa riba kubwa au kuona mkopo ni hasara.
Mojawapo ya faida kubwa kabisa ambayo mfanyakazi wa umma anayo ni kuwa na sifa ya kukopesheka benki kwa dhamana ya kazi yake tu bila kuweke dhamana yoyote ya mali binafsi. Tatizo wafanyakazi wengi hawana mda wa kutosha kusimamia kwa ukaribu biashara wanazoanzisha ndiyo maana wengi hazifanyi vizuri.