Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Wenyewe vigogo wanahisi watumishi wakimiliki kila kitu watashindwa kufanya kazi(kubweteka).

Hawawezi kutoa mikopo ya namna hiyo mkuu.

Benki zetu hizi ni wezi sana . Mfano hayo mambo ya processing fees , sijui Bima ya mkopo n.k , vyote hivyo ni wizi tu.

Mteje akifanya up-dating halipwi fedha alizokatwa kama Bima ya mkopo uliopita, yaani bora hata NBC wanatoa chochote baada ya ku-update
Ku-update nini mkuu?.
 
Kuna jamaa yangu ni mwajiliwa, tena huku kijijini sitimbwi. Mwaka wa saba huu hajawahi kukopa. Amejenga nyumba mbili tofauti . Moja ipo halmashari flan ni ndogo tu ambayo alianzia maisha nyingine ipo moja ya majiji makubwa huko kanda ya ziwa. Haijaisha ila inaelekea kuisha. HANA MKOPO WOWOTE, SI BANK WALA TAASISI YA MICROFINANCE. Ana mke na watoto watatu. Wazazi wake wanamtegemea yeye.

TUACHE TAMAA YA MAFANIKIO YA HARAKA
 
Acha uongo.
Bank za Kiislamu zote hazina riba.
Sawa mchawi lugha tu ya biashara lakini na imani kwa mnyaaz mungu allah hakuna mkopo usio na gharama ya kuurudisha namaanisha faida kwa mkopeshaji. Kwa hiyo hata mikopo ya benk za kiislam ukichukua mwisho wa siku utarudisha mkopo na faida kwa benki (ambapo wao watakwambia sio riba ila ukweli ndiyo riba yenyewe) kama mikopo ya benk za kiislam ingekuwa na unafuu huo unaosemwaga amana benki ingeshakuwa benk kubwa sana! Kifupi benk ya kiislam nayo mwisho wa siku ili kuendelea kuwepo lazima itengeneze faida ambayo inapatikana kwa kukopesha then mkopo kulipwa na cha juu.
 
Wakuu Kuna hii ya salary advance ...hivi kupewa mpaka ukope kwa benki husika? Maana Kuna jamaa yangu amesitishiwa huduma hiyo na NMB kisa amekopa benki nyingine japo mshahara wake unapita NMB
 
Kwani utachukua mkopo bila kusoma mkataba
nani husoma mikataba. unaletewa mkataba una kurasa mia tatu, utaweza kusoma yote na ukayakumbuka?....mikataba yenyewe ni mifumo ya kiwiziwizi tu. unaletewa document kubwa wakiwa wanajua huwezi ukalisoma lote.
 
Na ukienda kuchukua mkopo wanakufanyia process haraka haraka sana ili usibadili maamuzi

Na hata hawakupi muda wa kusoma mkataba sembuse kukufafanulia. Wanakupa tu usaini haraka haraka.
Nyie wenzetu huwa mnakopa wapi ambapo hawawapi taarifa za mkopo wako.
Ukienda kukopa wanakuuliza kiasi unachotaka kukopa, then wanaingiza kwenye mfumo wao, mfumo unafanya calculations za kiasi chote utakachotakiwa kurejesha na kiasi utakachokatwa kila mwezi katika mda uliochagua.
Baada ya hapo anaprint mkeka wa makato yote, ukionesha kila kitu ikiwemo kiasi unachokopa, makato ya kila mwezi utakayokatwa na jumla ya pesa utakayorejesha, anakupatia mkeka huo pamoja na form zingine za kujaza ili uombe mkopo, ukishajaza unarudisha ndio wanaprocess huo mkopo wako.
Ambao wanasaini bila kujua kiasi wanachotakiwa kurejesha na makato ya kila mwezi huwa wanakopa benki gani?
Halafu siku hizi hata kabla hujaenda kukopa unaweza kujua kiasi cha riba utakayorejesha kwa mkopo unaotaka kukopa. Google "loan calculator" uchague link mojawapo ucalculate riba yako. Mfano ambayo huwa natumia na inaendana kabisa na benki zetu wanavyokokotoa makato yao ni www.aren.co.ke/calculator/loancalc.htm
 
Back
Top Bottom