Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Kama faidika.letsshego ni noma..ukichukua M 3 kwa miaka Minne unakuja kulipa.M 5.6 huko
Bank yenye unafuu kwenye mikopo kwa watumishi ni CRDB tu licha ya kwamba sharti waliloliweka kwamba lazima mshahara wa mtumishi upitie huko miezi miwili huko na kuendelea huko huko baada ya kuchukua sera hiyo imewafanya watumishi wengi washindwe kukopa huko isingekuwa hivyo hiyo benki wangevuna mabilioni na mabilioni toka kwa watumishi
 
Saccos ipo vizuri. Mfano walimu siku wakija kujielewa nakufuta kikundi chao cha hovyo CWT wakaanzisha saccos moja matata alafu wakakopeshana kupitia hiyo saccos nadhani hata mpwayungu village angetamani kurudi kufundisha.
Hao Cwt walikuja na gear ya kusema wataanzisha benki yao ili iwakopeshe walimu kwa riba nafuu sana kuliko benki zote na kwa neema ya Mungu wakaanzisha mwalimu commercial bank na kwa jinsi walivyo watu wa ovyo tofauti ya riba na Nmb ambao ndio wakopeshaji wakubwa wa walimu kwa miaka mingi ikawa na asilimia 2.Hakika nimeamini shetani si lazima awe na mguu mmoja na wala hayuko mbali
 
Kuna benki flani ilikopa madolari huko IMF kwa 5% kwa miaka 10, wao wakakopesha 18%, na wengi wa waliokopeshwa ni watumishi.
Nasikiaga mambo za processing fee, kwani kuna kampuni (kama DP vile) ilayochakata mikopo tofauti na maafisa wa benki?
 
"Bank si rafiki wa masikini" hii kauli aliwahi kuitoa Mzee wa Msoga katika moja ya hotuba zake. G.Mukoba aliyewahi kuwa kiongozi wa juu wa TUCTA alisema kuwa Wafanyakazi ni tabaka la watu masikini duniani. Alitoa kauli hiyo katika mahojiano ya moja ya vipindi vya television akihojiwa nyumbani kwake mwaka jana 2022.

Ziko sheria za fedha na uchumi zinazosimamia masuala ya mikopo Tanzania. Wakopaji wengi hawana elimu ya mikopo na riba hasa wafanyakazi na ndio maana wanaumizwa zaidi kuliko wafanyabiashara wakopaji. Elimu ya fedha ni kitu ambacho wakopeshaji hawataki wakopaji waipate ili waendelee kufanya "plundering" inayolindwa kisheria.

NB: katika duni hii ya "dog eat dog" mtu masikini/mfanyakazi ni f.a.l.a.
 
Ukikopa milioni 20 utarejesha milioni 20.

Wakati mwingine heri Mkopo wa NMB kuliko TRA pale bandarini, unanunua gari la milioni 10 inabidi uandae milioni 12-13 ya Kodi.

Kwa Tanzania kila sehemu ni wizi tupu
 
Serikali kuingilia kati? Benki zinafanya biashara.


Kuna mikopo ya hazina (haina riba). Kuna mikopo fulani una riba ya 6% .


Siyo lazima ukope.
Huwezi kupata mkopo kwa urahisi kwani ukifika tu wanaanza kugawana mabosi za kubakia ndio wanawapatia wachache tena kwa connection na unaweza ambiwa chukua mwisho 5 millions
 
Acha kukaza fuvu watu wameeleza vizuri hapo juu kuwa shida wewe umetaka kurudisha pesa Kwa muda mrefu. Hakuna wizi hapo
 
Bank za kiislam hazina riba
 

Ila NMB wanatisha kwa sasa wana riba kubwa sana na ada ya mkopo ni kubwa sana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…