Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Jinsi mabenki yanavyowaibia watumishi wa umma kupitia mikopo

Serikali ina mambo mengi sana ya kufanya na hili walishawaachia hao watumishi wa umma wapambane nalo kwa utashi wao. Yaani serikali iache kulipa vizuri wabunge na mawaziri ambao kimsingi ndio wenye nchi ije ihangaike na watumishi wa umma ambao wengi wao wana Elimu ya kutosha kupambanua mambo? Hizo riba zipo kisheria na mikataba wanayopewa hao wakopaji ipo wazi Sasa sijui kama huwa wanasoma kabla au shida ya pesa ndio inafanya wasielewe kama wanaibiwa?
Serikali ishue riba Kwa watumishi wote, Cha kushangaza madiwani na wakuu wa wilaya wana riba ZAO na JWTZ nao wanariba ZAO walimu na watumishi wengine riba juu .WAARABU karibuni labda mambo yatabadirika
 
Serikali ishue riba Kwa watumishi wote, Cha kushangaza madiwani na wakuu wa wilaya wana riba ZAO na JWTZ nao wanariba ZAO walimu na watumishi wengine riba juu .WAARABU karibuni labda mambo yatabadirika
Waarabu?
Yaani kama tumeshindwa kuitendeana vema sisi kwa sisi tusitegemee mgeni atatutendea vema!
Wakija nchini wamekuja kuchuma na wachumwaji ndio sisi.
Tafakarii
 
Ukiacha mwenyewe kwa mapenzi yako mwajiri atakwambia lipa deni kwanza, Ukifukuzwa bima italipa, ukifa bima italipa na familia inabidi ipewe gawio la faida, ukifa benki watataka cheti cha kifo ili wakadai malipo bima, vilevile ukifukuzwa watahitaji barua ya kufukuzwa kutoka kwa muajiri. Mwisho wa siku kama muajiriwa wewe kopa tu ufanye yako ajira ni yako si ya familia yako. Ukifa kabla hujazikwa kitengo chako kashapewa mtu vilevile wanaanza kukuteta ofisini jinsi ulivyokua unawasumbua kutoa michango ya harusi. Kiufupi kazini hamna urafiki it's all about unafiki 1st class.
""Ajira ni yako, si ya Familia yako""...mkuu hili ni neno asee, linachoma[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] linakumbusha.

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Daaah! NMB wezi sana, mimi nilifanya process zote nikabakisha kusainiwa na Boss wangu. Nilipochukua kwenda kuusoma mkataba nyumbani nilisikitika sana, hadi leo nina ule mkataba sijawahi kuonekana tena machoni panyule afisa.

Mimi nilitakiwa kulipa riba ya 105% kwa miezi 96.
 
Saccos ipo vizuri. Mfano walimu siku wakija kujielewa nakufuta kikundi chao cha hovyo CWT wakaanzisha saccos moja matata alafu wakakopeshana kupitia hiyo saccos nadhani hata mpwayungu village angetamani kurudi kufundisha.
Sahihi kabisa kiongozi
 
Daaah! NMB wezi sana, mimi nilifanya process zote nikabakisha kusainiwa na Boss wangu. Nilipochukua kwenda kuusoma mkataba nyumbani nilisikitika sana, hadi leo nina ule mkataba sijawahi kuonekana tena machoni panyule afisa.

Mimi nilitakiwa kulipa riba ya 105% kwa miezi 96.
FL ni changamoto sana.

Huoni riba ilikua almost 14% pa?

Ulitaka mkopo wa miaka 8. Kumbuka hiyo ni biashara.
Hiyo benki siyo wezi. Unapewa ulichoagiza.
 
Wenyewe vigogo wanahisi watumishi wakimiliki kila kitu watashindwa kufanya kazi(kubweteka).

Hawawezi kutoa mikopo ya namna hiyo mkuu.

Benki zetu hizi ni wezi sana . Mfano hayo mambo ya processing fees , sijui Bima ya mkopo n.k , vyote hivyo ni wizi tu.

Mteje akifanya up-dating halipwi fedha alizokatwa kama Bima ya mkopo uliopita, yaani bora hata NBC wanatoa chochote baada ya ku-update
Elezea kidogo mkuu nbc wanatoa chochote how
 
Habari za jioni GT...Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mabenki nchini wanawaibia sana watumishi wa umma kupitia kinachoitwa mikopo ya watumishi. Nina rafiki yangu anafanya kazi serikalini. Juzi alienda kukopa pesa benki (NMB)...sasa shida ilianza juu ya mchanganuo wa mkopo, duh, ni hatari.

Kwa kiasi cha Tsh mfano 6M, unatakiwa urudishe almost zaidi ya 10M. Bado kwenye hiyo 6M uliyoomba, wanakata 8% kama processing fee. Hivyo, unajikuta unachukua net take home 5.4M. Kumbuka mkopo huu unakatwa kwa muda wa miezi 96. Yaani, unapewa 5.4M, unarudisha 10.6M. Hii ni sawa na riba ya 100%.

5.4M * 2 = 10.8M. Kwanini wasikopeshwe bure kama walivyo wafanyakazi wa BOT, NMB, NK ambao hawatozwi riba kwenye mikopo yao? Serikali ipo wapi kwenye wizi huu wa mchana?
Lengo lao hamtakiwi kuwa matajiri. mnatakiwa kuwa masikini.
 
Kuna hii comment nimetafuta sana juu huko sijaiona, sijui ni mods au mtoa comment mwenye ndio alieifuta?? Kwa bahati tuliicopy na tutaendelea kuipaste ili waalimu wasiendelee kuumia.



#AKILI_ZA_BANDIA_KUTOKA_KWA_FORMER_LOAN_OFFICER

"Kopa 6M kwa 2yrs monthly repayments itakua almost 285k utawapa benki profit ya 846K. Fee ya mkopo itakua 150K. Utapata kibunda chako, kama msingi wa nyumba weka na nyanyua boma.

Baada ya miaka miwili kupitia kakope tena kiasi kile kile (usifanye top up). Kama hamna mabadiliko ya gharama za uendeshaji figure zitakua zilezile.

NINAMAANISHA NINI

Within 4yrs umekopa 12M, fees 300k na benki profit itakua 1.692M. Na utakua umefanya mambo ya msingi sana, kama nyumba umepaua kabisa.

KICHEKESHO
Kopa 12M kwa 4yrs, monthly repayments itarise itakua almost 322K benki profit itakua 3.453M na fees itakua 300k."

KUMBUKA
#Kopa kwa sababu maalum."

#FormerLoanOfficer
Hivi top up zinaathari gani mkuu??nahitaji kuelewa hapa
 
FL ni changamoto sana.

Huoni riba ilikua almost 14% pa?

Ulitaka mkopo wa miaka 8. Kumbuka hiyo ni biashara.
Hiyo benki siyo wezi. Unapewa ulichoagiza.

Kabla ya kuomba mkopo tunawatumia wao kutupatia ushauri wa nini nifanye, sio kila mmoja amesoma uchumi.

Cha ajabu ushauri wanaonipatia hata mimi nisiesoma uchumi siwezi kumshauri mtu afanye.

Actually riba ilikua 16% plus hiyo processing fee ilikua almost 4 Million.

Hizi benki zinatakiwa kuwa msaada kwa watumishi kwasababu ndio kundi kubwa zaidi linalozifanya ziwe hai, maana yake zilitakiwa kuweka mikopo isiyoumiza sana, angalau riba 11% per annual.
 
Hivi top up zinaathari gani mkuu??nahitaji kuelewa hapa
Ukitop up unachokifanya ni kuongeza muda wa mkataba na kadri mda unavokuwa mkubwa na riba inakuwa kubwa.
Chukulia ulikuwa na mkopo wa 6M kwa miaka miwili ambapo ulitakiwa kulipa 840000 zaidi, baada ya mwaka ukatop up 6M zingine hapa utapaswa kulipa hii 6M ya pili ndani ya miaka mitatu coz wanaesabu kutoka siku ulipochukuwa hela. Kwa hiyo kwa miaka kulipa 1,260,000 zaidi kwa 6M ya pili badala ya 840,000.


Mwenye ujuzi anaweza kuelezea vizuri zaidi.
 
Mie nashauri Kwa mwenye malengo kopa fanya malengo hatuna bima za maisha unaweza ajiriwa ukafa ndani ya miaka miwili na hujafanya kitu

Kujichanga mdogo mdogo ni ngumu sanaa hasa hasa ukitaka kujenga huwezi toboa kirahisi lazima ukope tu
 
Back
Top Bottom