Jinsi maombi yanavyoshusha Imani yako kwa Mungu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Tumezoea kudhani kuwa maombi yanakuza Imani. Ni kweli tumesisitizwa kuomba, lakini asilimia karibu 99 ya Sala zako hazipaswi kuwa Maombi Bali Shukrani.

Kuombaomba na mbaya Zaidi kuombewa kunapumbaza na kushusha Imani.

NINI KITAONGEZA IMANI YAKO?

SHUKRANI.
Unatakiwa kushukuru Muda mwingi Kwa vitu ambavyo huna kana kwamba tayari unavyo.

KWA NINI USHUKURU NA SIO KUOMBA?
Tayari Mungu karibu Kila unachokiomba ameshasema amekupa. Badala ya kuomba shukuru Kwa kupewa Kisha Anza kuchukua hatua za kivitendo bila shaka kana kwamba tayari hicho kitu kipo na unacho.

Mfano, Yesu hakuomba ili mikate5 na samaki 3 vilishe watu 5000 (wanaume). Alishukuru Kwa sababu tayari Kuna andiko linasema Kila chenye Mwili akipa chakula chake Zaburi 136:25.

Kiwango chako Cha imani kinapimwa hivi.

Kuombewa ----Mtoto mchanga kiimani.
Kuomba ------Mvulana au msichana kiimani.
Kushukuru nakusifu ---- Mtu mzima na mkomavu kiimani.

Kama umeelewa, andika Amina.

Muebrania
Mitale na Midimu
 
Mkuu unaweza kuambatanisha vifungu vya biblia vinavyosema kuomba kunadumaza imani?
Labda tafsiri ya neno "prayer" kwa kiswahili ndio inakutatiza. Kuomba (prayer) kunajumuisha haya yote, (ask/request/command, praising & worship na thanks giving).

Kwa upande mwingine imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo (warumi 10:17). Hakuna sehemu biblia inasema imani inakuja kwa kushukuru kama ipo nipatie tafadhali (najua hakuna).

Kama kuomba kunadumaza imani una maoni gani kuhusu mistari hii ya bible;
-Luka 18:1 (yampasa mwanadamu kuomba kila wakati na si kukata tamaa)
-1Thesalonike 5:17 (ombeni bila kuchoka).

NB:
Kuombewa haina maana yoyote ya uchanga kiroho, hata kina Mtume Petro waliombewa na kanisa walipokuwa gerezani.

Tafsiri fupi ya maombi (prayer) ni kuzungumza na Mungu, hivyo kwa namna yoyote ile haiwezi kutafsiriwa kama ni uchanga. Kwenye mambo ya kiroho kuna "ranks" na watu wanatofautiana viwango kulingana na ukomavu wao rohoni (sio umri katika wokovu) bali speed ya ukuaji wa maarifa ya kiroho.
Asante na ubarikiwe sana.
 
Mkuu ni vigumu wengi kukuelewa maana umeingia anga za imani.

Imani ikiwa imemkaa vema mtu wa Mungu, basi yeye anaomba, na haombewi.
Shukrani inabeba imani iliyo kubwa zaidi.
Mtu anaomba na anakushukuru baada ya imani yake kwa lile aombalo kuwa tayari limetekelezwa.

Tatizo kubwa katika imani nikuomba neema, imani yako mtu itekeleze yale yote yanayomtukuza Mungu.
La sivyo imani inaweza mpoteza muumini na akaingia kule asikotarajia.
 
Amina!!
Popote ulipo piga kifua mara3 useme mimi ni muanzisha thread bora kabisa
20222

Kweli kuomba kunapunguza imani, mimi ni shuhuda maana kila unachoomba kwa macho hakitokei kwa wakati unaotaka ama hakitokei kabisa, hio hupunguza sana imani yako kwa Mungu.
Mimi huwa siamini kama Mungu anatakiwa kuombwa maana kama yeye alinijua kabla na anajua yaliyo sirini basi huwa anajua mahitaji yangu.

Tusipo focus na kushukuru na kuabudu unakufuru, yani unakufuru kabisaa
 
Mkuu unaweza kuambatanisha vifungu vya biblia vinavyosema kuomba kunadumaza imani?
Labda tafsiri ya neno "prayer" kwa kiswahili ndio inakutatiza. Kuomba (prayer) kunajumuisha haya yote, (ask/request/command, praising & worship na thanks giving).

Kwa upande mwingine imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo (warumi 10:17). Hakuna sehemu biblia inasema imani inakuja kwa kushukuru kama ipo nipatie tafadhali (najua hakuna).

Kama kuomba kunadumaza imani una maoni gani kuhusu mistari hii ya bible;
-Luka 18:1 (yampasa mwanadamu kuomba kila wakati na si kukata tamaa)
-1Thesalonike 5:17 (ombeni bila kuchoka).

NB:
Kuombewa haina maana yoyote ya uchanga kiroho, hata kina Mtume Petro waliombewa na kanisa walipokuwa gerezani.

Tafsiri fupi ya maombi (prayer) ni kuzungumza na Mungu, hivyo kwa namna yoyote ile haiwezi kutafsiriwa kama ni uchanga. Kwenye mambo ya kiroho kuna "ranks" na watu wanatofautiana viwango kulingana na ukomavu wao rohoni (sio umri katika wokovu) bali speed ya ukuaji wa maarifa ya kiroho.
Asante na ubarikiwe sana.
Asante Sana mkuu. Kuna mambo kadhaa naomba nifafanue.

1🙂 nazungumzia (Maombi) Kwa maana ya asking or begging kitu ambacho tayari Mungu ameshasema amekupa. Kwa Mujibu wa mstari ulioutoa,
Warumi 10:17 Imani chanzo chake ni kusikia. Sasa kama Mungu ameshasema amekupa afya, na huna afya. Unatakiwa ushukuru sio uombe. Maana tayari umesikia Umepewa afya hata kama katika ulimwengu wa mwili haipo.

2: Command sio sehemu ya maombi. Hii ni mamlaka ya kutamka. Huitaji kucommand kma sehemu ya maombi. Hakuna huo mfano kwenye biblia. Command, announcements, decrees, Declarations HIZI unazitamka katika kauli zako na vitu vinatii huombi hapo. Ndio maana hazimo kwenye package ya Sala ya Kwetu. Ile sio Sala ya Bwana, Maana Bwana Yesu ametupa sisi.

3:Imani haiji Kwa kuomba kitu ambacho umeshapewa.Imani huja Kwa Kushukuru Neno la kristo lililotamka hicho kitu limekupa.utashukuru Hadi kiwe.

Ninakushukuru Sana Bwana mkubwa. Tunaweza kuendelea kupeana maarifa.
 
Amina!!
Popote ulipo piga kifua mara3 useme mimi ni muanzisha thread bora kabisa
20222

Kweli kuomba kunapunguza imani, mimi ni shuhuda maana kila unachoomba kwa macho hakitokei kwa wakati unaotaka ama hakitokei kabisa, hio hupunguza sana imani yako kwa Mungu.
Mimi huwa siamini kama Mungu anatakiwa kuombwa maana kama yeye alinijua kabla na anajua yaliyo sirini basi huwa anajua mahitaji yangu.

Tusipo focus na kushukuru na kuabudu unakufuru, yani unakufuru kabisaa
Ubarikiwe.
Mungu anapenda Sana Mtu anayeshukuru. Maana inaonekana Hana wasiwasi na utendaji wake hata kama vitu havijatokea.

Mambo mengi utayapata Kwa Kushukuru kuliko kuomba (Begging).
 
Mkuu ni vigumu wengi kukuelewa maana umeingia anga za imani.
Imani ikiwa imemkaa vema mtu wa Mungu, basi yeye ansomba, na haombewi.
Shukrani inabeba imani iliyi kubwa zaidi.
Mtu anaimba abkushukuru baada ya imani yake kwa lile aombalo kuwa tayari limetekelezwa.

Tatizo kubwa katika imani nikuomba neema, imani yako mtu itekeleze yale yote yanayomtukuza Mungu.
La sivyo imani inaweza mpoteza muumini na akaingia kule asikotarajia.
Kweli mkuu.
 
Mfano unakuta mtu anaomba. Baba usema tutaiambia milima ing'oke nayo itangooka. Naomba uondoe milima hii .

Hili ni KOSA baya Sana.
Neno limesema, utaiambia milima, sio utamuambia Mungu aiondoe milima.

Pia halijasema uombe, limesema uiambie.

Kazi yako kwanza ni kushukuru Kwa hayo maelekezo. Kisha unaongea na mlima wako unaambia uondoke, Kisha kinachobaki ni kushuku hata kama Bado upo, wewe angalia neno.
Na unaishi kana kwamba haupo.
 
Kweli mkuu.
Mzizi wa imani ya mtu iko hapa:

"Ebr 11:1-3
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri."

Na bado ukiwa na imani kubwa na njema na isiyotetereka, mtu maombi yake ni kumtukuza , kumshukuru Mungu.

Maana imani hata ikiwa kiduchu ,inaweza kufanya maajabu.

"“tukiwa na imani kiasi cha punje ya haradali,” tutaweza kuhamisha milima"
(Mathayo 17:20).
Milima yako inaweza kuwa upweke, mashaka, magonjwa, au shida zingine.

Hivyo basi, suala si kuomba au uombewe, suala ni imani yako kwa Yesu Kristo.
 
Kushukuru wakati hujapata hitaji lako huoni hiyo ni kama unamfanyia ridiculous Mungu?
Hivyo ndivyo anavyotaka Sasa mkuu.
Angalia kitu kisichokuwepo kana kwamba unacho. Hiyo ndio Imani. Kuamini unakitu ambacho huna Hadi kinatokea.
Unashukuru inadvance
 
Mzizi wa imani ya mtu iko hapa:

"Ebr 11:1-3

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri."

Na badi ukiwa na imani kubwa na njema nabisiyotetereka, mtu maombi yake ni kumtukuza , kumshukuru Mungu.

Maana imani hata ikiwa kiduchu ,inaweza kufanya maajabu.

"“tukiwa na imani kiasi cha punje ya haradali,” tutaweza kuhamisha milima"
(Mathayo 17:20).
Milima yako inaweza kuwa upweke, mashaka, magonjwa, au shida zingine.

Hivyo basi, suala si kuomba au uombewe, suala ni imani yako kwa Yesu Kristo.
Barikiwa
 
Hivyo ndivyo anavyotaka Sasa mkuu.
Angalia kitu kisichokuwepo kana kwamba unacho. Hiyo ndio Imani. Kuamini unakitu ambacho huna Hadi kinatokea.
Unashukuru inadvance
Hiyo ni imani au pretending?

Huna hela halafu unaigiza kuwa wewe ni tajiri kwa faida ha kumridhsisha Mungu?

Yani una flip uhalisia uwe kinyume uje na taswira mpya ambayo sio ya kweli mbele ya Mungu ambaye huyajua yote yaliyo sirini mwa watu?

Kwa aina hiyo ya imani unayoitafsiri inaweza kukufanya hata yale yanaofahamika kuwa ni mabaya uyaone ni mema as long as utayaamini katika namna tofauti na uhalisia wake

Unaua halafu unajenga imani kuwa pale umeponya.

Mwisho wa siku sijui kama huyo Mungu ataendelea kufurahia aina hiyo ya imani unayomuoneshea mbele yake
 
Imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu.
Mungu amesema Usiue. Sasa Imani ni kutoua.

Imani ndio inakutaka uamini kitu unacho hata kama huna. Na sioaneno unaanza kuchukua hatua KATIKA ya Kutokujua. Ukitaka Hadi ujione ndio uamini hiyo sio Imani ni EVENT.

Ibrahim aliamini akaenda asikokujua.
Ibrahim aliamini atarudi na mtoto wake licha ya kujua anakwenda kumchinja.
Musa aliamini bahari itaachia kabla hajaona iachie na hajwahi kuona tangu azaliwe.
Yesu alishukuru kupata mikate ya kulisha watu 5000 wakati haipo.

Imani ni independent na 5 senses ikiwepo kuona. Ndio maana ukiwa na Imani Kali lazima uonekane chizi. Paulo alionekana mpumbavu tu.

Ushahidi kuwa hicho kitu unacho hata kama hakipo sio kuonekana kw hico kitu Bali ni Hilo neno lililosemauna ho au UTAPEWA ndani ya biblia.

Na ushahidi kwamba utapata hata kama ni pesa. Utaondoka Kwa bidii ukiamini kabisa fursa yoyote itakayojitokeza ndio sehemu ya udhihirisho a neno unaloamini. Ndio maana mtu wa Imani ni mtu wa action.faitj without action Is a deadfaith.
 
Back
Top Bottom