Jinsi maombi yanavyoshusha Imani yako kwa Mungu

Na ni Mungu huyo huyo aliyesema usiseme uongo

Sasa kama wewe ni masikini halafu mnamdanganya kuwa we ni tajiri huoni kwamba hiyo ni dhambi?

Ibrahimu hakuamini atarudi na mtoto wake kwasababu lilikuwa ni agizo LA Mungu na hakujua kama hill no jaribio amepewa

Ukisema aliamini atarudi na Issack maana yake alijua exactly kuwa anaenda kujaribiwa

Na Abraham akishajua kuwa hili ni jaribio maana yake hiyo inakuwa ni cheating amefanya na majibu yanayopatikana hapo hayawezi kuwa sahihi

Na Mungu angejua kuwa huyu Abraham amekwishajua lengo la yeye sio kumuamuru amchinje mwanae basi agizo hilo lisingetumika kama kipimo cha imani
 
Mkuu labda kabla hatujaenda mbali ningependa kujua unasoma biblia gani, ya kiswahili pekee?

Binafsi nasoma ya kiswahili (kidogo sana) na si kwa nia mbaya ila ni kutokana na kuwa kwanza biblia ya kiswahili haikutafsiriwa moja kwa moja toka kwny biblia ya kiebrania(vitabu vinavyoitwa agano la kale) na kigiriki (vitabu vinavyoitwa vya agano jipya). Hii inaifanya inakuwa na baadhi ya maana tata/ambazo hazikukusudiwa kutokana na ufinyu na uhaba wa misamiati wa lugha husika wakati wa tafsiri ilipofanyika.

Pia nasoma ya kiingereza (mainly KJV) na pia nasoma ya kiebrania na kigiriki.

Sasa ukisoma biblia ya lugha moja pekee bila kupitia hizi zingine kuna vitu vingi sana utapishana navyo hasa katika tafsiri.

Kama uko deep kwny hizi nyingine, nijulishe ili tuzame kwny mjadala wako vizuri tukianza na maana ya neno "prayer", kwa nini tunaomba ikiwa Mungu anajua haja zetu, kwa nini maombi ya watu fulani yanajibiwa ila we ukiomba the same prayer hupati jibu? Je ni maombi ndiyo yenye nguvu ama nguvu ni ya muombaji nk nk.
 
Tazama ninawapa amri ya kukanyaga nge na nyoka...

Wala hakuna litakaloshidikaba kwenu. Mathayo 17:20

Kifupi sisi tunaomuamini Mungu tunazo nguvu za Mungu ambazo tunatakiwa tuzitumie kuvuka changamoto maishani.

Hivyo wakati changamoto zijapo wengine tunakosea kuanza tena kuomba Mungu atende vitu fulani..wakati mamlaka hayo amshakupa tayari, ila wewe ndiyo umeshindwa kuzitumia nguvu hizo.

Na sawa uwepo kwenye chumba chenye umeme halafu uanze kulia kuwa kuna giza...unatakuwa kuwasha tu switch ili mwanga utokeze.

Hivyo wakati mwingine tunapitia shida ambazo tulikuwa tunaweza kuzitatua kwa mamlaka tuliyopewa...ila tunapoteza muda kwa kuanza tena kumsihi Mungu atende jambo fulani....yeye naye anasema laiti kama huyu mwanangu angejua kuwa tayari anazo nguvu za suluhisho la tatizo lake, asingepoteza muda kulia kwenye maombi akiniomba.

Speak to your challenges, amuru kwa nguvu za Mungu na milango iliyofungwa itakufungukia. Ukishaomba wewe amini tu, kuhusu utekelezaji wewe muachie Mungu.
 
Kuna kaukweli fulani maana hizi kuombewa na kuomba imekuw fashion kiasi kwamba watu WA Mungu wamebaki kukimbizana kwa wachungaji na manabii waombewe mambo Yao yaende sawa...... By doing that kamwe hawatakaa wawe na Imani thabiti sababu wao hawajiamini kuwa wanaweza kuwa na mahusiano na Mungu straight na Kutatua shida zao zote so wamelemaaa kwenye kuombewa tu but sio kushukuru. Na ndio maana hawapati kile wanachokiomba kila siku ukipita wanapoombea wapate wachumba Leo ukija baada ya MWAKA mmoja unawaona bado wapo vilevile au wamejaa zaidi...... Unajiuliza...... Hupati jibu.... MUNGU tayari anajua huitaji lako..... Jaribu kushukuru Utashangaa kwa yatakayokutembelea
 
Maombi hayana nguvu zozote mnazodanganyana.

Yangekuwa na nguvu basi idadi ya wagonjwa, vita, uonevu, mauwaji na umasikini visingekuwa kwa hali iliyopo hivi leo[emoji16][emoji16].

Kwa jinsi wafia dini mnavyokesha kwenye maombi na upuuzi ufananao na kuabudu eti kumkemea shetan na uharibifu wa dunia, basi hayo maovu na madhaifu yangepungua kama sio kuisha.

Waulizeni babu zenu kabla ya dini za kizushi kuja afrika, hakukuwa na magonjwa kama leo hii, hakukuwa na mmomonyoko wa maadili kma leo hii, hakukuwa na uzandiki kma mlio nao wafia dini, je hayo maombi yenu mnayemuomba hawasikii??

Acheni kupoteza muda kwenye dini za kizushi, Mungu wa dini zote ni mmoja na ndiye huyo huyo shetan ktk majina ya vificho[emoji23].

Bitter truth.
 
Ndio MAANA NABII NA MTUME MWAMPOSA KABLA AJAANZA IBADA UTASIKIA AKISEMA" PAZAA SAUTI YA SHUKRANI ,PAZA SAUTI YA SHUKRANI ,MWAMPOSA YEY ANAFAHAMU SIRI HYO wengi hawajui washukuru VIP na atamke nni mbele za bwana
 
Sahihi kabisa.
Sema imani nyingi zimeingiliwa na watafuta shortcuts .
Mwamposa kbla hajanza ibada yake UTASIKIA AKISEMA PAZAA SAUTI ya SHUKRANI ,paza sauti ya SHUKRANI ,Kweli Ni Mara nyingi Sana mtume mwamposa akihimiza watu kushukuru
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kungekuwa hakuna haja ya kuomba wala kushukuru.

Hizi habari za kuomba na kushukuru kuwepo zinaonesha Mungu huyo hayupo.

Na habari za kuwepo kwake zimetungwa na watu tu.
 
Umeandika point kubwa sana, lakn mtu mwenye imani ya kurisishwa ama kukariri hawezi kukuelewa
 
Mwamposa kbla hajanza ibada yake UTASIKIA AKISEMA PAZAA SAUTI ya SHUKRANI ,paza sauti ya SHUKRANI ,Kweli Ni Mara nyingi Sana mtume mwamposa akihimiza watu kushukuru
Sijawahi kumsikiliza hiyu Bwana, Ila ninachojua wengi wa aina yake Huwa wanachanganya.
Unaweza kuona baada ya kushukuru Tena aliowaaminisha wanamagonjwa na wamefungwa.
Niliwahi kfuatilia mmoja anaitwa Kuhani, anawaaminisha waumini wamelogwa na wako kwenye vyama vya wachawi, anawaambia wakili hivyo.
Wakati huohuo anawaambia wameokoka. hayo tunayaita Satan and not Christ Conscious churches

Kama wanaaminishwa kupata Kwa Kushukuru, watakuwa ni waumini imara Sana wasio na hofu.
 
Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa tu ni kweli kushukuru kuna nguvu kubwa sana lakini baada ya kuomba. Ombeni mtapewa, tafuteni mtapata, pigeni hodi mtafunguliwa.
 
Ibrahim aliamini atarudi na mtoto, hata kama angemchimja na kumchoma. Mungu angemrudisha Kwa manjia elfu aliyonayo.
Ndio maana anaitwa Baba wa Imani.
Ushahidi
Waebrania 11:19
[19]akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Accounting that God was able to raise him up, even from the dead; from whence also he received him in a figure.

Ni sahihi kumwambia maskini ni aseme ni tajiri. Ushahidi wa utajiri wake sio vitu vya kugusika alivyonavyo, ushahidi ni neno la Mungu lililosema hivyo. Imani ni uhakika wa usichonacho, uhakika hup ni neno la Mungu usilolitilia mashaka.
Kila mkristo anayejitambua ni Tajiri kuliko Elon Musk Kwa sababu, unafanyika mtoto wa Ufalme na mrithi wa Vyote alivyonavyo Mungu. Hata kama Hauna Sasa vitakuwa vyako siku akirudi.

Ni dhambi mkristo kukili huna kitu, maana imeandikwa.
Wafilipi 4:19
[19]Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
But my God shall supply all your need according to his riches in glory by Christ Jesus.

Ni KOSA mkristo kukiri udhaifu, maana imeandikwa.
Yoeli 3:10
[10] aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.
... let the weak say, I am strong.

Pia udhaifu wako (kiuchumi, kiroho,kimahusiano ndio kigezo Cha kufanywa imara. Udhaifu ni advantage.) Paulo aliandika katika udhaifu ndipo nakuwa imara.

Kwa Nini watu hawapati au hawaoni. Wengi hatujua maana ya tajiri Kwa mtazamo wa biblia. Ni kuwa na financial freedom hata unaishi chini ya Dola Moja. Pia wanavunja kanuni nyingine mfano. Utajiri wa Mungu inahitaji bidii , ndio maana anasema Wenye bidii watakaa na wakuu
 
Wengi awajui nguvu kuu iliyomo kwenye kushukuru.
Kushukuru ni kuiruhusu positive energy ijae mwilini mwako.
Positive energy ikizalishwa vya kutosha uchochea ukuaji na matokeo uonekana kwenye ulimwengu wa mwili.
 
Wengi awajui nguvu kuu iliyomo kwenye kushukuru.
Kushukuru ni kuiruhusu positive energy ijae mwilini mwako.
Positive energy ikizalishwa vya kutosha uchochea ukuaji
Hata kama huna dini. Hii ni kanuni. Ukiitumia inazaa matunda.
Wakristo wengi wanaahangaika eti wamefungwa kumbe midomo yao ndio imewafunga Kwa kutokushukuru na kubaki wakitazamia kuona Mungu atafanya kitu katikati ya bidii zao. Huku wakiepuka negativity Kwa gharama zote.

Haya ni maarifa, tu watu wanatakiwa kuyatest.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…