Inaendelea,
Nilipompa hiyo rand 20, akainuka na kwenda kutafuta sehemu ya kula (kunywa chai). Alivyoinuka hapo ndio niliweza kuuona uzuri wake. Nakumbuka hadi leo alikuwa amevaa top nyeusi mikono mirefu na jeans ya blue. Alikuwa ametokelezea hatari. Kwa wale waliofika South Africa watakubaliana na mimi, wanawake wa kisauzi wapo njema sana kwenye maumbo. Anyway, demu alikuwa kifaa cha haja. Alikuwa ana umbo lililokatika vyema. Alikuwa na tako zuri, kubwa la wastani, ila kwa bongo ataonekana ana bonge la tako, Sio yale matako makubwa ya kufuru ya wasouth Africa, sura pia ilikuwa sio haba, ngozi chocolate color. Kwa ufupi Khumbu alikuwa mrembo sana. Hadi masela wangu walimkubali kwa kila kitu. Nadhani South Africa inaongoza kwa wanawake wenye matako makubwa. Kwenye matako wanawake wa Dizonga wako njema, wakina Sanchi mnaowaona wana mizigo ni takataka tu ukimpeleka Dizonga.
Basi tukaagana pale yeye akaenda kutafuta chakula na mimi nikavuka barabara nikaenda kununua chai na vitafunio, nikarudi zangu golini.
Nikanywa chai kama kawaida, Chaduma akapita nikamwambia tayari nishakunywa chai. Baadae kidogo demu nikamuona kwa mbali anakuja, ila akawa kama anaangaza angaza kama kapotea hivi maana kuna matents mengi yanayouza viatu vya kike na yamepangana, ila kwa kuwa mie tayari nishamuona nikawa kama nampungia mkono hivi ili anione. Akafika golini, nikampa kiti akakaa. Tukaanza kupiga stori sasa. Nikamwelezea mimi ni nani, nafanya nini na mambo mengine. Na yeye akanielezea anaitwa Khumbu, anakaa township moja inaitwa Inanda, na mambo mengine ya hapa na pale. Tukabadirishana namba za simu, tukapanga tutaonana jioni baada ya mimi kufunga. Baada ya demu kuondoka masela wangu walianza kuniuliza, huyu demu umempata wapi? Wewe kweli una mavumba, umekuja juzi tu tayari umepata demu kisu hivi? Mie nikawaeleza jinsi nilivyokutana na demu muda mfupi uliopita.
Jioni mida ya kufunga Khumbu akawa amekuja pale golini. Nikampa kiti akawa ananisubiria tufunge ili tuweze kuangalia kama tutaondoka wote au amekuja tu kwa ajili ya maongezi zaidi. Jamaa zangu walipomuona amerudi wakawa wananitania “Leo uhakika”. Baada ya kumaliza kufunga ikabidi nianze kuongea naye, halafu alikuja akiwa kabadilisha nguo. Kumbe alienda nyumbani kabisa, hivyo alivyorudi ile jioni alikuwa ametoka nyumbani na amekuja kwa ajili yangu. Jamaa yangu akaniuliza, vipi tunaondoka wote (kwenye gari )au mtakuja kivyenu? Maana kwa kawaida huwa tukifunga tuonaodoka wote kurudi nyumbani kwenye gari yake. Nikamgeukia demu nikamwuliza, vipi twende home basi ili ukapajue. Demu hakuwa na kipingamizi. So tukazama ndani ya gari tukaanza safari ya kuelekea geto. Jamaa yangu akaniambia misosi yetu ya kibongo huko magetoni huyu hawezi kula hivyo acha tupitie KFC tumnunulie kitu cha kwenye mabox, basi gari ikaingia KFC kwenye drive thru, tukachukua kitu cha box tukasepa.
Tukafika geto, demu nikampaki sebuleni, nikaingia jikoni kupika misosi yetu ya kibongo huku yeye akiendelea kula msosi wake wa KFC. Kumbuka mie nalala kwenye kale kastore pamoja na mshikaji mwingine homeboy, mdogo wake na huyu jamaa yetu mwenye gari. Huyu jamaa ninaye lala naye alikuwa mtu wa tungi sana. Mkifunga goli ile jioni yeye anaelekea bar kukutana na wabongo wengine wanywaji, hivyo kurudi kwake mpaka saa 5 au 6 hivi usiku, sometimes anaweza kulala kwa masela wake huko. Baada ya demu kumaliza kula nikamwonyesha chumba ”changu” ili akabadili nguo afanye mchakato wa kuoga. Hivyo akaingia chumbani (store), akajiweka, akavaa kanga akaingia bafuni kuoga. Najua watu wataanza kusema hii ni chai kwa kuona demu wa kisauzi anavaaje kanga, au kapataje kanga. Kwa taarifa yenu Khumbu alikuwa na kanga, na kila siku alipokuwa ananitembelea alikuwa anakuja na kanga. Kanga south Africa zipo, sijui wanazitoa Swaziland, maana waswaziland ndio huwa nawaona wanavaa kanga, anyaway sijui alikuwa ananunua wapi ila kanga alikuwa nazo za kutosha.
Baada ya kumaliza kupika mimi na jamaa yangu na Mburundi tukawa tunakula hapo sebuleni. Utaratibu ilikuwa ni kupika kwa zamu, na kula wote pamoja.
Demu akamaliza kuoga akarudi chumbani. Na mimi baada ya kumaliza kula nikaenda kuoga, nikamaliza kuoga nikaenda chumbani. Ila hapo katikati tayari nishampigia simu mwana kuwa leo nimevusha hivyo kama vipi atalala sebuleni kwenye makochi au aendelee kuruka nyoka mpaka asubuhi.
Itaendelea