Baada ya hapo mapenzi yaliendelea. Khumbu alionyesha kunijali. Kama nilivyosema nimedate na wasouth wengine tofauti na Khumbu ila treatment aliyokuwa ananipa huyu mwanamke ni tofauti sana. Kuna siku nikiwa bado nipo Rossburg, maana baada ya kuanza chuo nilihama huko. Nilimuomba aje mjengoni maana tulikuwa hatujaonana karibia wiki hivi. Nilikuwa nimemmiss kinyama. Akasema atakuja lakini hakutokea. Usiku wake nikawa nampigia hapokei, baadae nilipozidi kupiga simu akazima.
Basi nikajua tu hapa yupo na msela mwingine. Ukimpenda mtu wivu hauwezi kukosekana, so nikawa namtumia msg ili akiwasha simu azikute. Simu haikupatikana mpaka kesho asubuhi. Mawazo yalikuwa mengi sana, ile kufikiria tu demu alikuwa analiwa ilikuwa inaniumiza sana. Siku hiyo sikuweza hata kufanya kazi, nilienda kufungua goli lakini baadae nikarudi mjengoni kupumzika. Kule mjengoni alikuwepo demu wa baba Isa, alikuwepo kama wiki hivi. Huyo demu alikuja na sijui baba ake.
So, nilivyofika nikamkuta demu wa baba Isa yupo sebleni anaangalia tv. Kumbuka apartment ilikuwa ya vyumba vitatu. Sebule, jiko na bafu la kushare. Nilipomkuta demu wa baba Isa nikawa nimemjoin hapo sebuleni. Tukawa tupiga story mbili za hapa na pale. Baadae mie nikaamua kuingia chumbani kupambana na stress zangu, hivyo nikamuacha demu wa baba Isa akiendelea kuangalia TV. Nilipoingia chumbani sikuufunga mlango wangu.
Nikiwa nimejilaza nikaanza kusikia makelele hapo sebleni, nikakurupuka kuelekea sebleni kujua nini kinaendelea. Ile kutoka nikakuta yule demu wa baba Isa hayupo ila kuna demu mwingine wa baba Isa yupo jikoni anatukana kwa kizulu huku anatembea tembea, na kugonga mlango wa baba Isa. Harakaharaka nikajua hapa kuna fumanizi. Mademu wote wa baba Isa nilikuwa nawafahamu maana walikuwa wanakuja kila mmoja kwa wakati wake.
Nadhani kuna mmbea aliamua kuchoma utambi siku hiyo. Basi yule demu aliyekuwa anaangalia tv alikuwa kajifungia ndani, halafu mle ndani kulikuwa na baba ake pia, we acha tu. Sasa picha linakuaje hapa. Yule demu mwingine ndio anagonga mlango kwa nguvu akimtaka mwenzie afungue wapambane. Hapo mie nimeduwaa tu sijui hata cha kufanya.
Huyu anayegonga mlango sijui alifikiria nini, mara nashangaa kaingia jikoni sijui kabeba jiwe, sijui alibeba kitu gani mara vuuu kaingia chumbani kwangu na kukipasua kile kidirisha nilichokuwa nawaambia hapo awali. Basi vipande vya glass vikawa nimetawanyika kila sehemu mle chumbani kwangu. Kile kidirisha ndio kikawa kimebomolewa.
Sasa hapa nikawa namuwazia Khumbu, sijui akija atakubali kulala kwenye hiki chumba kisichokuwa na dirisha, maskini mimi Khumbu akigoma kulala humu nitampeleka wapi? Gharama za kulala guest kwa South Africa nitaziweza kweli?
Inaendelea.............
SEHEMU YA TISA