Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Nilipokabidhiwa hilo geto nikaanza na kumfikiria Khumbu. Nikawa najisemea Khumbu akifika hapa nadhani nitapewa na vya uvunguni bila hata kuomba hahahahaha! Geto lilikuwa na kila kitu.

Kwanza lipo maeneo ya kishua hasa, kama ni bongo basi lipo Masaki, nalinganisha tu na Masaki kwa sababu kwa bongo nadhani Masaki angalau ndio sehemu ya watu wenye kipato cha juu ila ki ukweli suburbs za South africa huwezi kulinganisha na Masaki. Masaki pa ovyo tu.

Gheto lilikuwa limetulia. Lilikuwa na zulia nene laini la sufi. Kulikuwa na makochi ukikaa unadumbukia, very comfortable. Vyumba vyote vilikuwa na vitanda vimetandikwa mashuka safi na mito milaini minne kila kitanda, vyumba vyote ni self na zina makabati yale ya moja kwa moja ya kuhifadhia nguo.

Nilianza kufanya ukaguzi kila chumba kujua labda kuna "mambo" yanahifadhiwa humo lakini kulikuwa hakuna kitu chochote kinachofanana na hicho nilichokuwa nawaza. Ila chumba kimoja kulikuwa na lotion na vikorombwezo vya wadada kuashiria kuwa kuna mtu huwa anakuja. Na pia kulikuwa na mashati na nguo chache za kiume.

Nikaanza kupiga mahesabu ya kumleta Khumbu tuanze kupeana raha za dunia. Maana Khumbu anapenda maisha ya kifahari kama haya.

Ila nikawa najiuliza kama mshikaji hatamaindi akiona nishaanza kuvusha mizigo. Jamaa alikuwa anamfahamu Khumbu na alikuwa anamkubali sana. Kipindi anauza viatu pale workshop alikuwa anapiga sana stori na Khumbu hadi akawa anamfundisha kiswahili.

Pia Khumbu alikuwa anamkubali sana jamaa maana alikuwa hachoki kumwongelea eti jamaa ni mcheshi na ni mtu wa masihara sana. So, nikawa najipa matumaini hata kama atakuja kujua kuwa Khumbu huwa analetwa hapa hatamaindi sana ingawa nilikuwa nimepanga niwe na mleta kwa kificho nisiwe najiachia sana mpaka jamaa akajua.

Itaendelea...
 
Nilipokabidhiwa hilo geto nikaanza na kumfikiria Khumbu. Nikawa najisemea Khumbu akifika hapa nadhani nitapewa na vya uvunguni bila hata kuomba hahahahaha! Geto lilikuwa na kila kitu. Kwanza lipo maeneo ya kishua hasa, kama ni bongo basi lipo Masaki, nalinganisha tu na Masaki kwa sababu kwa bongo nadhani Masaki angalau ndio sehemu ya watu wenye kipato cha juu ila ki ukweli suburbs za South africa huwezi kulinganisha na Masaki. Masaki pa ovyo tu. Geto lilikuwa limetulia. Lilikuwa na zulia nene laini la sufi. Kulikuwa na makochi ukikaa unadumbukia, very comfortable. Vyumba vyote vilikuwa na vitanda vimetandikwa mashuka safi na mito milaini minne kila kitanda, vyumba vyote ni self na zina makabati yale ya moja kwa moja ya kuhifadhia nguo. Nilianza kufanya ukaguzi kila chumba kujua labda kuna "mambo" yanahifadhiwa humo lakini kulikuwa hakuna kitu chochote kinachofanana na hicho nilichokuwa nawaza. Ila chumba kimoja kulikuwa na lotion na vikorombwezo vya wadada kuashiria kuwa kuna mtu huwa anakuja. Na pia kulikuwa na mashati na nguo chache za kiume.

Nikaanza kupiga mahesabu ya kumleta Khumbu tuanze kupeana raha za dunia. Maana Khumbu anapenda maisha ya kifahari kama haya.
Ila nikawa najiuliza kama mshikaji hata maindi akiona nishaanza kuvusha mizigo. Jamaa alikuwa anamfahamu Khumbu na alikuwa anamkubali sana. Kipindi anauza viatu pale workshop alikuwa anapiga sana stori na Khumbu hadi akawa anamfundisha kiswahili. Pia Khumbu alikuwa anamkubali sana jamaa maana alikuwa hachoki kumwongelea eti jamaa ni mcheshi na ni mtu wa masihara sana. So, nikawa najipa matumaini hata kama atakuja kujua kuwa Khumbu huwa analetwa hapa hatamaindi sana ingawa nilikuwa nimepanga niwe na mleta kwa kificho nisiwe najiachia sana mpaka jamaa akajua.

Itaendelea...
Naongeza popcorn mkuu
 
Sawa mkuu, nadhani zimebaki episodi kama mbili tukifikie hicho kipengele.

Mkuu nimempata khumbu, kweli ni pisi kali nimekubali.. Na katoto kake kale kakike.. anyway siwezi kumpost maana hujaridhia.. Jamaa ake yule alikuja kufariki.. naomba niishie hapo[emoji1784][emoji1784] Tupe mambo tupe mambo mkuu@Kondamsafi
 
konda msafi hebu elezea harakaharaka tumalizie hiyo story utasababisha wikend ndoa ziwe chungu wife anachukia napokuwa bize na simu mida ya wkend anataka anifaidi na hali hii ya kimvua Dar ndo inadumisha ndoa hahahaaa just kidding
Hii stori ndefu chief sio ya kuisha leo. Ni stori iliyochukua miaka 6 kama sio 7.
 
@Kondamsafi Pisi ni kali kweli mkuu.. Na Shukrani kwa kutupa kisa cha kweli
 
Back
Top Bottom