Zabron Hamis
JF-Expert Member
- Dec 19, 2016
- 7,093
- 11,377
[emoji851][emoji851][emoji851] hii ndio tabu ya kusoma nyuzi za itaendelea[emoji2959][emoji2959][emoji2959]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah hii kweli inaonyesha kuna watu wanamchambua na hawashindwi kumtaja ila muacheni ajilinde identity yake maana wengine wanamfanya ahisi hofuMkuu, memeber wachache wanakuyumbisha ukatishe story na wewe unakatisha, achana na wachache, eleza kwanini Khumbu alifariki na ulisema utaleta picha yake
Ila konda usitufanyie ivyo sisi fans wako kindakindaki ujue[emoji8]
Safi sana boy ila naskitika kujua kuwa ulitoka south kurud home.Nataman sana south,unamjua mbongo mmoja anaitwa jimmy?Usiku ule baada ya kumaliza gemu wazo la kutaka kumwuliza kuhusu jana yake kuonekana akiwa kwenye gari maeneo ya Point likanijia. Kawaida ya Khumbu alikuwa hapendi mno kuulizwa maswali ya kumtilia mashaka au ya kuonyesha simwamini. Hivyo nilijua nikianzisha hiyo mada tutaishia kugombana. Nikaamua kupotezea.
Maisha yaliendelea na mahusiano yangu na Khumbu yaliendelea mpaka nimemaliza chuo japo hapo katikati kabla ya kumaliza chuo ulitokea ugomvi mkubwa sana uliosababisha tuachane kwa muda.
Kuna siku Khumbu aliniambia amepata kazi benki, bank teller hivyo sasa hivi hatakuwa anapatikana sana kama zamani. Alichokuwa anamaanisha ni kwamba hataweza kuwa anakuja kila nitakampomuhitaji, hivyo siku nikimuhitaji halafu akashindwa kuja inabidi nimuelewe.
Baada ya Khumbu kupata kazi tukawa tunaonana mara moja moja sana. Inaweza kupita hata wiki mbili hatujaonana, sikuona tabu sana maana nilijua kwa sasa ana majukumu ya kikazi. Maisha hayo ya kutokuonana mara kwa mara ndio yaliendelea hadi mwisho wa penzi letu.
Siku moja, ilikuwa siku ya Jumapili, Khumbu alinipigia akaniambia nisitoke nyumbani anakuja kushinda na mimi. Hapo tulikuwa hatujaonana karibia kama wiki mbili hivi, hivyo nilikuwa nimemmiss hatari. Ikumbukwe nilikuwa sina mwanamke yoyote zaidi ya Khumbu hivyo hata siku mbili tu nikiwa sijamuona nilikuwa nammiss hatari, sometimes hisia za Khumbu zikinijia nilikuwa napata mfadhaiko, nakuwa kama mgonjwa. Kwa hiyo kutokuonana na Khumbu kwa wiki mbili ilikuwa mateso sana. Kwanza nilikuwa simuamini kabisa. Nilikuwa najua hizi wiki mbili lazima kuna mtu kama sio watu wanamchakata.
Mida kama ya saa sita akanipigia simu ananiambia yupo getini nikamfungulie. Nikachukua rimoti ya geti nikaelekea getini. Kufika hapo getini nashangaa simuoni ila kuna gari mpya aina Polo Vw ipo hapo getini inataka kuingia. Ikabidi nisogee kabisa hapo getini kuangalia Khumbu yuko wapi. Kikawaida unaweza kufungua geti hata ukiwa umbali wa mita 100, kwa hiyo nilitegemea ningemuona Khumbu kasimama hapo getini hivyo ningemfungulia geti bila ya kwenda kwenye geti, yaani ningebonyeza tu rimoti nikiwa kwa mbali na mgeni wangu angeingia. Nilienda mpaka getini kumwangalia Khumbu pia kuiangalia hiyo gari iliyokuwa pale getini inasubiria kuingia. Kwa mshangao Khumbu ndio alikuwa mwenye ile gari, nilipofika getini alishusha kioo cha gari na kuchungulia ili kunipa ishara ni yeye hivyo nifungue geti aingie.
Aliingia na nikamwonyesha sehemu ya kupaki gari yake. Mmh! Khumbu alikuwa amevaa miwani ile ya kisista du rangi kama ya ugoro hivi, nywele kazibana kwa nyuma. Kavaa blouse mikono mifupi imemshepu kimwili chake vizuri hatari. Chini katupia suruali ya kadeti zile za mabaka mabaka kama za jeshi, hakika alipendeza. Nikamkaribisha ndani huku najiuliza huyu kapata wapi hili gari? Kazi yake ya ubank teller ndio kanunua na gari? Au kuna sponsa?
Daah so sad kusikia Khumbu alifariki. Ilikuaje mkuu konda msafi alikufa kabla au baada ya kuondoka.Jamani naomba niikatishe hii stori. Hii stori ni ndefu sana haitaisha leo wala kesho na inanichukulia muda wangu mwingi sana. Ni stori iliyochukua karibia miaka 6, since 2008 hadi 2012, kwa hiyo unaweza kuona ilivyo ndefu. Kwa wale wenye shauku ya kutaka kujua Khumbu yuko wapi kwa sasa, jibu ni kwamba Khumbu alifariki, hatunaye tena duniani. Mwenyezi Mungu aendelee kumuweka mahali pema peponi. I truly miss her and believe one day I will meet her in other worlds of God.
Mimi nilimaliza chuo nikarudi Bongo, nipo Dar nina familia tayari. Kuna uzi mmoja nilishauleta humu mnaweza kuutafuta kuhusu yaliyonipata niliporudi Dar. Asanteni na kwa herini.
Hapana mkuu, hakuna hata mtu anayenichambua kaka. Kuwa na amani kabisa ndugu yangu. Hata kama wataamua kunichambua na kupata identity yangu hamna watakachopata maana naishi maisha clean kabisa. Naendesha maisha yangu kwa kipato halali kabisa.yeah hii kweli inaonyesha kuna watu wanamchambua na hawashindwi kumtaja ila muacheni ajilinde identity yake maana wengine wanamfanya ahisi hofu
Oowh sawa kabisa ni vizuri kiongoziHapana mkuu, hakuna hata mtu anayenichambua kaka. Kuwa na amani kabisa ndugu yangu. Hata kama wataamua kunichambua na kupata identity yangu hamna watakachopata maana naishi maisha clean kabisa. Naendesha maisha yangu kwa kipato halali kabisa. Sema tokea nimeanza kuandika hii stori imenichukulia muda wangu mwingi sana. Mwanzoni nilidhani ningeimaliza siku moja tu ndani ya masaa machache ila kadri nilivyozidi kuandika nikajikuta natamani kuiielezea vizuri tukio kwa tukio ili kumfanya anayeifuatilia aweze kupata picha nzuri ya tukio. Niliona nikiielezea kwa juu juu itabore na insingefikia lengo langu la kuishare hapa JF. Kawaida nikiamua kufanya kitu nina tabia ya kukifanya kwa ufanisi. Hata nilipokuwa shule nikiwa najibu swali huwa nalijibu kwa kuhakikisha point zote ninazozijua naziandika, sina tabia ya kuandika au kufanya jambo kwa kulipua. Kulingana na nilivyo nimeona hii stori itaendelea kunichukulia muda wangu maana sitataka niiandike kwa kuikimbiza au kurukaruka.
Nilimuoa Masogange mkuu hahahahaha.Mkuu vipi ushaoa tayar na vipi ulimuoa masogange au maana unaonekana unabahati na totoz kali kutoka kwa khumbu mpaka masogange adi kwa mtoto wa karikoo daaah
Mkuu unachosema hapa ni tofauti na calibre yako kwa kile unachotaka kutenda kuhusu huu uzi,kuna ahadi mingi umesema hasa picha ya Marehemu KhumbuHapana mkuu, hakuna hata mtu anayenichambua kaka. Kuwa na amani kabisa ndugu yangu. Hata kama wataamua kunichambua na kupata identity yangu hamna watakachopata maana naishi maisha clean kabisa. Naendesha maisha yangu kwa kipato halali kabisa. Sema tokea nimeanza kuandika hii stori imenichukulia muda wangu mwingi sana. Mwanzoni nilidhani ningeimaliza siku moja tu ndani ya masaa machache ila kadri nilivyozidi kuandika nikajikuta natamani kuiielezea vizuri tukio kwa tukio ili kumfanya anayeifuatilia aweze kupata picha nzuri ya tukio. Niliona nikiielezea kwa juu juu itabore na insingefikia lengo langu la kuishare hapa JF. Kawaida nikiamua kufanya kitu nina tabia ya kukifanya kwa ufanisi. Hata nilipokuwa shule nikiwa najibu swali huwa nalijibu kwa kuhakikisha point zote ninazozijua naziandika, sina tabia ya kuandika au kufanya jambo kwa kulipua. Kulingana na nilivyo nimeona hii stori itaendelea kunichukulia muda wangu maana sitataka niiandike kwa kuikimbiza au kurukaruka.
Na hapa ulipo ishia lengo lako la ku share nadhani halita timia. Mimi naamini uliamua ku share kwa nia njema kabisa.Hapana mkuu, hakuna hata mtu anayenichambua kaka. Kuwa na amani kabisa ndugu yangu. Hata kama wataamua kunichambua na kupata identity yangu hamna watakachopata maana naishi maisha clean kabisa. Naendesha maisha yangu kwa kipato halali kabisa. Sema tokea nimeanza kuandika hii stori imenichukulia muda wangu mwingi sana. Mwanzoni nilidhani ningeimaliza siku moja tu ndani ya masaa machache ila kadri nilivyozidi kuandika nikajikuta natamani kuiielezea vizuri tukio kwa tukio ili kumfanya anayeifuatilia aweze kupata picha nzuri ya tukio. Niliona nikiielezea kwa juu juu itabore na insingefikia lengo langu la kuishare hapa JF. Kawaida nikiamua kufanya kitu nina tabia ya kukifanya kwa ufanisi. Hata nilipokuwa shule nikiwa najibu swali huwa nalijibu kwa kuhakikisha point zote ninazozijua naziandika, sina tabia ya kuandika au kufanya jambo kwa kulipua. Kulingana na nilivyo nimeona hii stori itaendelea kunichukulia muda wangu maana sitataka niiandike kwa kuikimbiza au kurukaruka.
Naona wazo la kibepari la kuandika kitabu limepandikizwa kwa konda ili atuuzie, lakini sio mbaya.Haujaeleza siku unaondoka dizonga ilikuaje, na picha ya khumbu haujaweka halafu Baba isa haujaeleza yuko wapi , na ugonjwa gani ulimuua Khumbu, ulitaka kudakwa na wazee ikawaje malizia hayo maana vinginevo wewe ni mnyanyasaji wa wasomaji wako unatakiwa tukushtaki kwa kukatisha story.