Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

[emoji851][emoji851][emoji851] hii ndio tabu ya kusoma nyuzi za itaendelea[emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
Mkuu, memeber wachache wanakuyumbisha ukatishe story na wewe unakatisha, achana na wachache, eleza kwanini Khumbu alifariki na ulisema utaleta picha yake
Yeah hii kweli inaonyesha kuna watu wanamchambua na hawashindwi kumtaja ila muacheni ajilinde identity yake maana wengine wanamfanya ahisi hofu
 
Mkuu vipi ushaoa tayar na vipi ulimuoa masogange au maana unaonekana unabahati na totoz kali kutoka kwa khumbu mpaka masogange adi kwa mtoto wa karikoo daaah
 
Haujaeleza siku unaondoka dizonga ilikuaje, na picha ya khumbu haujaweka halafu Baba isa haujaeleza yuko wapi , na ugonjwa gani ulimuua Khumbu, ulitaka kudakwa na wazee ikawaje malizia hayo maana vinginevo wewe ni mnyanyasaji wa wasomaji wako unatakiwa tukushtaki kwa kukatisha story.
 
Ila konda usitufanyie ivyo sisi fans wako kindakindaki ujue[emoji8]

Kwanza atueleze Baba Isa alipo huyu jamaa tutamshtaki kutupotezea muda wetu wa kujenga nchi halafu atunyanyase kiasi hiki
 
Oya unazingua mzee maliza story, ujue hapa chamwino watu tuliacha kazi kwa muda tukifatilia huu uzi, mkuu mwenyew anafatilia kwahiyo akisikia kama umeachia njiani atamaind sana, ushauri wangu malizia hata kama kwa week mara mbili ili mkuu tumueleweshe kwasasa unachapa kazi na utakuwa unarusha mara moja moja...
 
Sikutegemea kama uzi wangu best for 2021 so far utaishia kuniudhi kiasi hiki, wewe konda msafi hujui ni kiasi gani umetuletea huzuni kubwa...watu tangu alhamis hatuongei na wenza wetu juu ya huu uzi, alafu unaukata kihuni namna hii....ni kweli kua unachukua muda mwingi wakwako lakini unaweza kusema ...jamaniee...nipeni muda mpaka labdakesho au jumanne...utumie muda huu kuandika vyote,then kuanzia jumanne unakua unapost episode tu,huandiki tena. fikiria hilo, usiwe mbinafsi
 
Daaah jamaa umeharibu Sana aisee ,kama unataka pesa si useme tu tulipie kuliko kutukatil namna hiyo.

Hi story inanipa feelings dizain Niko kwa madiba yaan naiona mitaa ya south ilivyo kupitia feelings alaf gafla unakuja kutukatil kias hicho ,unakosea mwamba
 
Safi sana boy ila naskitika kujua kuwa ulitoka south kurud home.Nataman sana south,unamjua mbongo mmoja anaitwa jimmy?
 
Daah so sad kusikia Khumbu alifariki. Ilikuaje mkuu konda msafi alikufa kabla au baada ya kuondoka.

Kama wana JF bado tunakudai sana.
 
yeah hii kweli inaonyesha kuna watu wanamchambua na hawashindwi kumtaja ila muacheni ajilinde identity yake maana wengine wanamfanya ahisi hofu
Hapana mkuu, hakuna hata mtu anayenichambua kaka. Kuwa na amani kabisa ndugu yangu. Hata kama wataamua kunichambua na kupata identity yangu hamna watakachopata maana naishi maisha clean kabisa. Naendesha maisha yangu kwa kipato halali kabisa.

Sema tokea nimeanza kuandika hii stori imenichukulia muda wangu mwingi sana. Mwanzoni nilidhani ningeimaliza siku moja tu ndani ya masaa machache ila kadri nilivyozidi kuandika nikajikuta natamani kuiielezea vizuri tukio kwa tukio ili kumfanya anayeifuatilia aweze kupata picha nzuri ya tukio. Niliona nikiielezea kwa juu juu itabore na insingefikia lengo langu la kuishare hapa JF.

Kawaida nikiamua kufanya kitu nina tabia ya kukifanya kwa ufanisi. Hata nilipokuwa shule nikiwa najibu swali huwa nalijibu kwa kuhakikisha point zote ninazozijua naziandika, sina tabia ya kuandika au kufanya jambo kwa kulipua. Kulingana na nilivyo nimeona hii stori itaendelea kunichukulia muda wangu maana sitataka niiandike kwa kuikimbiza au kurukaruka.
 
Oowh sawa kabisa ni vizuri kiongozi
 
Mkuu unachosema hapa ni tofauti na calibre yako kwa kile unachotaka kutenda kuhusu huu uzi,kuna ahadi mingi umesema hasa picha ya Marehemu Khumbu
 
Na hapa ulipo ishia lengo lako la ku share nadhani halita timia. Mimi naamini uliamua ku share kwa nia njema kabisa.

Sasa sijui nini kimekukuta. But asanteee kwa muda wako na dhamira njemaa ku share nasi sehemu ya maisha yako.
 
Naona wazo la kibepari la kuandika kitabu limepandikizwa kwa konda ili atuuzie, lakini sio mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…