Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Hapana hiyo biashara nilikuwa naiogopa sana. Hata kuyasogelea hayo makitu nilikuwa sitaki kabisa. Kwenye huu mkasa kuna scnerio ilitokea kidogo wazee wapite na mimi (wazee ni polisi), nitakuja kuelezea nini kilitokea.
Pole sana vipi hadi sasa unaposhusha huu uzi bado ndugu zako wapo Hai, maana naskia wabongo wengi waishio huko wanauliwa kimyakimya kwa dili chafu kama za ujambazi, utapeli na dawa za kulevya.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] usisahau kunitag mkubwa nahamu ya kufiks huko nipige na picha kabisa
 
Inaendelea,
Baada ya kumaliza kumwelezea nini kimetokea kwenye hicho kidirisha. Nikawa roho flani inaniambia, hebu mwulize tu bhana alikuwa wapi? Na kwa nini alikuwa hapokei simu na zaidi ya yote mbona amekuja na begi kubwa kidogo tofauti na kawaida yake? Kama vile alikuwa kichwani mwangu. Tukajikuta tunatizama kama sekunde kadhaa kisha yeye mwenyewe akasema "najua kuna kitu unataka kusema, hebu kiseme".

Nikamwambia ni kweli kuna kitu kinanikereketa na nisipokiuliza roho yangu haitakuwa na amani, bora nikiulize hata kama utakataa kujibu lakini tayari nitakuwa nimeondoa mzigo kifuani. Akasema, uliza. Nikamwuliza, ulikuwa wapi kiasi kwamba ulishindwa kupokea simu na mbaya zaidi ukazima kabisa? Akaniangalia akasema hana jibu la hilo swali. Akaongezea kwa kusema kwani shida yako ni nini? Si nipo hapa na wewe? I'm here with you and I'm all yours, what is your problem? Dah! Nikaona hili jibu ni kiboko, nikiendelea kuchokonoa nitaachwa mchana kweupe bila hata kula mzigo.

Kilichofuatia, niliingia jikoni na kwenda kukaanga mayai. By the way South africa hakuna kitu cheap kama mayai. Huku bongo mayai si ni expensive? Huko mayai ni mengi mno na hayana bei kabisa. Ukiona watu wanagonga mayai usidhani wana hela sana. Mayai ni kifungua kinywa cha kawaida kabisa huko.

Kila nyumba haikosi tray la mayai kwenye friji. So, nikakaanga mayai ya kutosha, nikachukua mkate, chemsha chai nikapeleka sebuleni na kuanza kula. ..South africa hata maziwa ni mengi sana, nayo hayana bei kabisa. Hiyo ilikuwa mida ya lunch, niliona napoteza muda kuanza kupika chakula cha maana. Nilikuwa na hamu naye kinyama.

Nilikuwa nataka tule haraka haraka nianze kumshughulia. Halafu kwa majibu yake ya kutokujali hisia zangu nilianza kupata mawazo mabaya juu yake, nilianza kufikiria namna ya kumla 071 ili labda ataleta heshima. Niliona huyu naona keshaanza kunichukulia poa sana, labda nikimfanyia kitu tofauti heshima itarudi.

Itaendelea
 
Hakuna mahandsome huko?wanaume wao wakoje
 

Kwenye mwendelezo usisahau kukazia hapo.
 
Nimempenda Khumbu yaani yuko na upendo mwingi hadi raha hivi humu JF siwezi mpata kama Khumbu kweli jitokezeni basi jmn [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] waiter nishushie konyagi kubwa, kastori katamu sana Alafu unaposema unamla nikosoma vipengele hivyo machozi kama yanalenga lenga hv sijui kwa nn? Anyways shusha nondo @kondamsafi nitag#
 
#I'm here with you and l'm all yours, what is your problem jamani Khumbu daaaah! Kuelekea Valentine ukiambiwa maneno hayo kwa pisi kama Khumbu yaaani furaha yake si mchezo alafu mtoto anakupa bila purukushani yaani konda msafi kwenye list ya picha na mm chonde chonde usinisahau [emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji481][emoji481]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…