Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanga uwa hawakosekaniJamaa boya sn.. kwani amelazimishwa kusoma uzi huu.. sasa ona ameharibu kila kitu
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
hahahahahhah
Mwendelezo upo mbele mama usilie. Pitia kila page utaupata mwendelezo.Nimejitahidi sana kwenda sambamba toka page ya kwanza yani day one unaanza mpk leo lakini malipo yake ndo haya nashindwa kunyonyesha mtoto kwa umakini kwa sbb ya story hii lakini ndo hivi unaishia njiani. Ptuuuuh
Nimekuelewa mkuu. Shukrani sana.
Konda weka Mambo ya mtandaoKipengele cha 071 naachana nacho rasmi. Naomba nieleweke kuwa hakikufanyika kama nilivyoelezea toka awali. Hivyo sioni sababu ya kuelezea in details ilikuwaje au ni mazingira gani yalimfanya mpaka Khumbu akaridhia kutoa 071.
Sawa baba mchungajiUZI UNA MENGI YA KUJIFUNZA HASA UKIANGALIA MWISHO WAKE.
Msikimbilie kumlaumu konda msafi naye ana majukumu mengine, japo mwisho unahuzunisha khumbu hayupo tena duniani.
Hapa ndo mjue maisha ya starehe yana mwisho wake, vyote ni ubatili mtupu, jiwekeeni hazina mbinguni hamtokaa mjute daima enyi kizazi cha nyoka [emoji236]
Mtoa mada naye anazingua , haiwezekani mpuuzi mmoja haaharibu Hali ya hewa , yaani huyo jamaa pengine ana Kura ya vetoKuna mchawi kashaharibu uzi, anyway mabaharia wenzangu mimi naishia hapa uzi ushapoteza ladha.
Nilio wakwaza naomba mnisamehe bure, yalikuwa maoni yangu kwa Konda msafi, bahati nzuri kayaelewa na kuyafanyia kazi.
Inaonesha Dunia imefika sehem mbaya mno, mambo ambayo ni machukizo kwa Muumba wetu ndo yanapendwa na wengi.
Niwakumbushe tu kuwa Mungu aliiangamiza sodoma na Gomora kwa Dhambi za kutumia Tg, hivyo geukeni sasa mkatubu kwa kulia na kuombohoongrtsleza nanyi mtasamehewa
Kupendana kimasihara..😂😂😂😂 Mupenzi Gdd Tech
Nimecheka sana. Mkuu jikaze tuMatukio yote nayasummarise hapa angalau nitoe lawama maana mnavyonishambulia si kitoto.
Baada ya Khumbu kuja na huo mkoko mpya nikamwuliza ameupataje. Akasema kanunua kwa mkopo. ...Baadae kupitia kwa yule demu wa mshikaji niliyewaambia alihamia, alinipa siri ya huo mkoko mpya wa Khumbu. Aliniambia hiyo ndinga kanununuliwa na Mayor wa Durban. Khumbe hata ile habari ya kuniambia kuwa kapata kazi bank hatutakuwa tunaonana mara kwa mara ilikuwa uongo tu. Alitengeneza mazingira ya mimi kutokuwa namuhitaji kila mara ili Mayor akimuhitaji awe anapatikana. Yaani mimi aniweke kando ili awe huru na Mayor. Hivyo hizo story za kuwa busy na kazi ilikuwa za uongo.
Siku niliyotaka kuingia mikononi mwa police:
Wale jamaa walianza kufungia mzigo humu ndani tulimokuwa tunaishi. Lile gheto la kule mwanzo ulikokuwa unafungiwa mzigo waliacha kulitumia. Hivyo mzigo ukaanza kupimwa humo humo getoni tunapoishi. Binafsi kukaa kwenye nyumba na hayo makitu kilikuwa ni kitu ambacho nilikuwa sikitaki kabisa. Baada ya mambo kuanza kufungiwa humo nikaanza mchakato wa kuhama maana niliona hapa naenda kuhatarisha maisha yangu ya chuo. Nilijua tu kuna siku tutavamiwa humu.
Kufunga hayo madude wanatumia hii mifuko ya plastic tuliyokuwa tunaiita ya rambo. Sasa kwenye kufunga lazima kuwe na vipande vipande vya hiyo miplastic kwenye kukatakata. Na hivyo viplastic ukikutwa navyo hata kama hawajakuta mzigo umekwisha maana wazee wanavijua hivyo vipande vya plastic huwa vinasababishwa na nini.
Sasa hawa jamaa kila wakifunga walikuwa wanavizoa tu hivyo vipande na kuvikusanya na kuviweka kwenye makabati. Walikuwa wanasubiria mpaka yawe mengi ndio wakatupe. Kitendo cha kuishi na hivyo vipande vya plastic kilikuwa kinaninyima amani kabisa, halafu ukiwaangalia hawa masela hata hawajali kabisa. Nilichokuwa nafanya ilikuwa kila asubuhi nikiwa naenda chuo navishindilia kwenye begi naenda kuvitupa mbele ya safari ili angalau tukivamiwa wasikute ushahidi wowote. Maana hawa jamaa zangu walikuwa hawajali kabisa.
Sasa siku moja ilikuwa Jumapili, na sikuwa na mpango wa kwenda kokote. Mule ndani kulikuwa na hivyo vipande vya viplastic. Nikaamua acha nikavitupe ili nishinde home kwa amani. Nikawa nimevishindilia kwenye begi langu la shule. Ila kama Mungu tu ameniambia, Konda msafi be careful. Japo nilikuwa natoka mara moja kwenda kuvitupa, niliamua kuvaa kama vile naenda mbali. Yaani sikutaka kutoka let's say nimevaa bukta na vest kwa sababu najua natoka mara moja na kurudi. Nilivaa nguo kama naenda mjini au chuo. Nikachukua kabisa na kitambulisho changu cha chuo. Nikaweka begi mgongoni, nikatoka ndani, nikashusha ngazi na kuanza kuelekea getini nikiwa na rimoti ya geti. Ile kufungua geti tu nakutoka nje ya geti, mara pah! Kipira cha wazee kimepiga break miguuni kwangu, dah! Roho ikalipuka pah! Nikasema hapa nimekwisha. Wakisema tu fungua hicho kibegi tuone ndani kuna nini nimekwisha. Nikawa naona sasa shule ndio imefikia mwisho. Kipira kimesimama miguuni kwangu. Walikuwa askari weusi. Wakashusha kioo cha gari upande niliokuwepo wakaniambia nisogee karibu. Nikasogea, jamaa walikuwa wawili, kama nilivyosema wote weusi wapo kwenye uniform. Nikawa najitahidi nisionyeshe wasiwasi wowote. Wakaniuliza, unakaa humu ndani? Maana nilikuwa ndio nimetoka tu hapo getini. Nikasema ndio nakaa humu. Wakaniuliza tena, humo kwenye begi kuna nini, nikasema kuna vitabu vya dini, naelekea kanisani kufundisha kipindi cha dini kwa ajili ya watoto. Halafu kile kitambulisho cha chuo nilikuwa nimeking'iniza kifuani. Wakaniuliza wewe ni mwanafunzi, nikasema ndio, nikawapa kile kitambulisho wakakiangalia harafu wakanirudishia. Kisha wakasema tulikuwa tunakusalimia tu, wahi kanisani ukamtumikie Mungu. Wakakanyaga mafuta wakasepa, dah! Aisee! Kwanza nilifikiria sijui nirudi ndani nisiendelee kwenda kuyatupa haya madude. Nikaona acha niendelee na safari ya kwenda kuyatupa maana wasije wakageuka wakaniona tena narudi ndani nikawapa wasiwasi, mbona huyu kasema anaenda kanisani halafu amerudi ndani tena? Basi nikaanza kutembea fasta, hapo naangalia kona yoyote nitakayokutana nayo nipige, nipotee kabisa kwenye hiyo barabara. Kona tu ya kwanza nilipoipata nikaikamata, nikatembea mbele kidogo tu, nikafungua begi na kuyatoa hayo madude fasta na kuyatupa. Nikatembea mbele kabisa huko kuzunguka ili nirudi nyumbani kutokea upande mwingine.
Itaendelea jamani.... nilisema nitasummarise ila nashindwa kusummarise. Huko mbele acha nijifunze kusummarise.
Mchungaji anaufuatilia uzi, na 071 episodes zote kazisoma... Stori anaikubali kimoyomoyoNdugu mchungaji hujalefti tu hapa.
Sasa ulipokuwa unalalama kwamba aache kusimulia ungepata funzo hili..!!??Nilio wakwaza naomba mnisamehe bure, yalikuwa maoni yangu kwa Konda msafi, bahati nzuri kayaelewa na kuyafanyia kazi.
Inaonesha Dunia imefika sehem mbaya mno, mambo ambayo ni machukizo kwa Muumba wetu ndo yanapendwa na wengi.
Niwakumbushe tu kuwa Mungu aliiangamiza sodoma na Gomora kwa Dhambi za kutumia Tg, hivyo geukeni sasa mkatubu kwa kulia na kuomboleza nanyi mtasamehewa.
Baada ya konda msafi kukubali maombi ya ndugu zake wa JF mimi nawaita wazamini kdg.. View attachment 1702352
Hivi hii ndio style ya kukung'uta siafu?Baada ya konda msafi kukubali maombi ya ndugu zake wa JF mimi nawaita wazamini kdg.. View attachment 1702352