Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Kwanza kabisa, mnamo Februari 2024 kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, aliwaamuru wanachama wake kuacha kutumia simu kwa sababu zinaweza kunaswa kwa urahisi na kufuatiliwa na majasusi wa Israeli.
Miezi 2 baada ya agizo la mkuu wao yaani April 2024 wakaagiza hizo pagers ndivyo hata BBC na Reuters zimeripoti.
Miezi 2 baada ya agizo la mkuu wao yaani April 2024 wakaagiza hizo pagers ndivyo hata BBC na Reuters zimeripoti.
BBC na Reuters zimeripoti kuwa pagers zilinunuliwa miezi 5 iliyopita kutoka sasa yaani April
Turudi hadi mwezi April mwaka huu tuone mfuatano wa matukio ulivyokuwa:
Turudi hadi mwezi April mwaka huu tuone mfuatano wa matukio ulivyokuwa:
April 2, 2024
- Marekani ilizuia kampuni ya China ya kutengeneza pagers ya Hytera isiuze pagers zake katika soko la dunia. Hiyo hukumu ilitolewa kufuatia kesi ambayo mwaka 2017 Motorola ilifungua dhidi ya Hytera katika masuala ya intellectual property.
- Sawa hatukatai kuhusu uamuzi wa kesi hiyo ila bado swali linabaki; Kwa nini mahakama ya Marekani itoe hukumu mwezi uleule ambao Hezbollah walikuwa na uhitaji mkubwa wa pagers?
- Ikumbukwe kipindi hicho ndicho ambacho Hezbollah walihitaji sana pagers. Kwa kuwa za China zilikuwa zimepigwa ban ikabidi wanunue za kutoka Taiwan.
April 17, 2024
- Siku 15 tu baadaye yaani April 17 mahakama nchini Marekani ikaondoa ban kwa kampuni ya Hytera na ikaruhusiwa kuanza tena kuuza pagers zake katika soko la dunia. Wakati huo Hezbollah walikuwa tayari wameshanunua mzigo wa pagers kutoka Taiwan. Unaweza kujionea mchezo uliofanyika hapo.
Kwa nini kumekuwa na sintofahamu kuhusu ni nani mtengenezaji wa hizo pagers?
Kwa kuwa taifa la Lebanon lina vikwazo vya kiuchumi mataifa na makampuni mengi yanaogopa kufanya nao biashara direct hivyo huwa wanatumia third party.
Kwa kuwa taifa la Lebanon lina vikwazo vya kiuchumi mataifa na makampuni mengi yanaogopa kufanya nao biashara direct hivyo huwa wanatumia third party.
- Ndio maana unaona suala la mtengenezaji na muuzaji wa pagers limekuwa na danadana nyingi. Kampuni ya Taiwan Gold Apollo inakana kuwa yenyewe haikutengeneza hizo pagers bali iliweka tu logo lakini hawakushiriki kwenye kuunda, kutengeneza wala kuziuza bali wanadai waliipa license kampuni ya Hungary iitwayo BAC kutengeneza pagers, kampuni ambayo nayo haieleweki kwani taarifa zake haziko wazi. Ni wazi kuwa kuna black market fulani ilifanyika.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na Al Jazeera ni kuwa order hiyo ya pagers kutoka Taiwan haikwenda moja kwa moja nchini Lebanon ilipitia Hungary.
Sasa hapo Hungary ndipo inaonekana mchezo mzima wa kupandikiza vilipukizi ulifanywa kisiri na Israel. Kwa nini tunasema hivyo?
Mzigo huo wa pagers ulikaa bandarini kwa miezi mitatu ukisubiri clearence ndipo uende Lebanon. Katika hiyo miezi mitatu ya kusubiria Mossad waliitumia vizuri kupandikiza vilipukizi.
Ikiwa vifaa vya kielektroni vinaweza kufanyiwa mchezo kama huu vikiwa kwenye usafirishaji au supply chain je, kuna usalama wa watumiaji wa vifaa hivyo duniani?