Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti

Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti

Kweli naanza kuamini zile imani ya kuzaliwa upya. Yaani Kihiyo tayari ashazaliwa upya kama Bashite
 
Tofauti ya Kihiyo ni kwamba ushahidi ulitolewa mahakamani Na yeye akashindwa kuthibitishi au kukanusha tuhuma hizo , tuhuma Za RC Bado ziko kwenye public court ambapo Bado suala last kukanusha au kuthibitishi halijafanyika
 
20170310_093137.jpg
AIONE BASHITE
 
Duh, Kwa hiyo unamwambia mheshimiwa nae aondoke kwa staili hii!
Kabisa. Daudi ajiuzulu tu na aanze kujipanga upya kimaisha. Akijiuzulu hakuna gazeti hata moja litakalomwandika. Unakumbuka jinsi ambavyo Rostam alikuwa anaanddikwa magazetini kila kukicha. Alipojiuzulu hakuna gazeti hata moja ambalo linashughulika naye. Daudi bado kijana mdogo (35 years). Anaweza kujipanga upya na akatengeneza maisha yake upya. Pia atakuwa amemsaidia sana Rais maana taswira inayojengeka ni kuwa Rais anampendelea kwa kuwa ni home boy, n.k. Huu ndo wosia wangu kwake.
 
Hiyo ilikuaje iweke tuijue
Nyerere aliwataka wakulima wote wakubwa wakabidhi mashamba yao kwa serikali. Akina Mwamindi na wenzie wakiwa wakulima wakubwa huko Iringa hawakupenda kufanya hivyo...mashamba yao makubwa na walikuwa wakiyategemea.

RC Kleruu alikuwa akitilia mkazo na kufuatilia kuhakikisha akina Mwamindi wanatekeleza agizo..alikua kiherehere sana...

Siku moja alikwenda kwa Mwamindi ..siku hiyo aliamua kuendesha gari yeye mwenyewe..Mwamindi kwa kukerwa na kuchoshwa alipoona RC kaja..akachugua gobole lake..akaaga familia yake..alipotoka nje akamfyatulia risasi RC ikampata begani i think...kisha akamfyatulia nyingine na kumwua.


Akaupakia mwili kwenye gari la RC...na akaivaa kofia ya RC..kofia yaani kofia kama vazi sio cheo...kofia kama ya museven.

Then akaendesha lile gari mpaka kituo cha polisi..yaani chukulia mfano kama pale central jamaa aliendesha akitokea Posta japo kuwa ile njia haitoki..polisi walishangaa kuona mkuu wa mkoa akija kwa njia isiyotoka.

Akapaki gari Kisha akawaendea...akawaambia kachukueni mzigo wenu kule nje...

Mwamindi alinyongwa lakini.

Hiyo ni kwa ufupi...Niliwahi kuisoma hiyo stori kwenye gazeti la Mwananchi.Mkuu atakuelezea zaidi.
 
Wadau tangu tarifa itoke kuwa viongozi wa nafasi ya kisiasa sifa kuu ni kujua kusoma na kuandika, kwanini sasa mahakama ilimvua ubunge bwana kihio aliyeshinda nafasi ya ubunge Temeke mwaka 1995 ikiwa sifa ni kujua kusoma na kuandika?

kwanini walimvua nafasi yake kwa kosa la kudanganya elimu yake kwanini wasingempa adhabu nyingine ikiwa sawa na kufoji vyeti baadala ya kumvua ubunge bado nawaza tu
 
Sasa vyeti vya nini waliangalia ikiwa sifa kuu ya ubunge ni kujua kusoma na kuandika vyeti vya nini ikiwa vyeti ni sifa moja wapo ya kuwa mbunge mbona wabunge hawajakaguliwa sasa kama kuwa na vyeti feki au halali ndio sifa ya ubunge
Hizi danganya toto ili kuwalinda wakuu Wa mikoa, wilaya na mawaziri!
Fek ni feki tu!
 
Back
Top Bottom