Jinsi Muungano unavyoathiri Waislamu wa Tanganyika wakati wale wa Zanzibar wakineemeka

Unamfahamu Christian Ronaldo? Yule mchezaji anayecheza kule Saud Arabia?
 
Muislam wa Zanzibar na Muislam wa bara ni yupi muislam sana?
 
Mbona Budha, Hindu, Pagan, Orthodox na wengineo huwaongelei na wao hawapo humo?
Kwani uislam ni jina?
 
Where is the stone-cold hard data to back up all this mumbo jumbo? Weka data za teuzi zote za Serikali kuanzia miaka 20 au 30 nyuma, na uweke wazi umetumia vigezo gani kujua dini ya mteuliwa: chini ya hapo, there's zero objectivity in your claims.
 

Mdogo mdogo tutaanza kuelewana kuhusu huu muungano feki,ila dhambi ya ubaguzi huwa haiishi ukikosa wakuwabagua utawabagua hadi bata wako unaowafuga.

Kabla hamjamalizana na wakristo sasa mmegeukiana waislamu wa bara na viziwani,mkimalizana huko mtakuja wa pwani na kanda ya kati.

Acheni upuuzi.
 
Hii mada imejaa hoja ila ni za kipuuzi sababu mleta uzi anajisahaulisha kwa makusudi kuwa kabla ya imani yake (ambayo ni jambo binafsi si la kitaifa) yeye ni mwafrika kwanza.

Mleta uzi naomba tu ni kwambie wewe ni miongoni mwa watu wajinga katika hili taifa na unahitaji elimu ya uraia kufungua akili yako na kuielewesha juu ya changamoto halisi za kitaifa na sio huu upumbavu umeandika hapa.

Dini au imani ni swala binafsi na halikuwahi na halitawahi kuja kuwa swala la kitaifa.

Zanzibar kuwa na majority Muslim katika nafasi za kazi na uongozi ni matokeo ya jamii ya wazanzibari kwa wingi wao kuwa waislam kama matokeo ya historia ya kutawaliwa na waarabu ambao ndio wenye imani hiyo kwa asili.

Sasa ulitegemea uende ulaya halafu ukute waislam wameshika serikali au uende Iran ukute majority ni wakristo au wahindu wameshika serikalini.

Zanzibar kuwa majority Muslim katika serikali si matokeo ya maamuzi yao bali ni swala la kimazingira na kihistoria kwa kurithi.

Dini au imani ni swala binafsi si swala la kitaifa na wala si kigezo au sifa ya mtu kushika wadhifa wa kiongozi au kupewa kazi au kupewa chochote.

Kinachokufanya uamini haya uliyoyaleta hapa ni matokeo ya malezi mabovu uliyopitia mikononi mwa wazazi au walezi ambao walipotoka au walikosa exposure ya maisha sasa wanaishi kwa kujihami wakiamini dini au imani inabeba masilahi yao zaidi kuliko sheria za inchi ambazo zinalindwa kikatiba na zimebeba masilahi ya kila mtu bila kujali rangi yake, asili yake, imani yake, jinsia yake, urefu wake, lafudhi yake yaani bila kubagua kwa namna yoyote.

Nakushauri utulize kichwa chako, nenda kasome tena vitabu vya kukujenga kiraia na kukufanya ujitambue wewe ni nani katika hii jamii ya mtu mweusi.

Before haujajinasibisha kuwa wewe ni muislam jiulize ukijikata hapo kuna sehemu damu yako itasema wewe ni muislam, nenda urabuni kule iraq,iran, Saudi Arabia then jaribu kujichanganya na waarabu kuswali nao kwenye misikiti yao ndipo utaelewa ninachoongelea namna utabaguliwa hadi utaelewa kuwa before ya kuwa Muslim, au kabila lako, wewe ni mwafrika kwanza ambaye unatakiwa kufahamu mwafrika ana changamoto gani katika dunia ya leo na anatakiwa kushikamana vipi na mwafrika mwenzake ili kujiweka sehemu nzuri katika global community awe na heshima.

Waafrika hatuthaminiki duniani sababu hizi ndizo akili zetu. Tuna amini katika cheap and weak ideas kuwa ndio msingi wa maisha yetu. Sasa kama wewe unaamini dini ndio itakuletea mafanikio ya kiuchumi, kiafya, kifedha, kifamilia binafsi ila unasahau unazungukwa na wanajamii wenzako ambao hawapo na fikra kama zako na hawashei akili kama yako na mitazamo.

Unategemea utaexist kwa amani?!

Grow up. Learn its never to late to learn.
 
mkuu unaongelea waisilamu gani? kwa sababu serikalini naona majina ya waisilamu waisilamu mm siwaoni
 
usichanganye uwisilamu kwenye ujinga wenu
 
namimi muisilamu wa kilwa kwenye kundi hilo la matajiri nimo?
 
kweli kabisa ukimkuta muisilamu serikali tena akikuona umevaa kisilamu hata kama huna shida nae akisha kuona tu anatamani kujificha chini ya meza, ukiwa nashida ofisini boro umkute mgaratia atakuelekeza shida yako kuliko hawa wisilamu wenzetu lakini mgaratia huyo asiwe mrokole awe mloma msabato
 

Waislamu wameshika uchumi [emoji31] unaota
 

Nakataa wafanyabiashara waislamu matajiri ni wale tu waliopo top 10 ya utajiri tena hao ni kwasababu wana asili ya nje so wamefika kwa kupewa booster na ndugu zao wa nje. Ukitoa hapo big population ya waliobaki ni maskini wa kutupwa. Angalia mikoa na maeneo wanayoishi waislamu mengi ni yenye hali duni na ya kimaskini sana. Uswahili kote asilimia 85% ni waislamu nenda kafanye research. Biashara nyingi nchi hii ni za waktisto na waktisto wengi ndo wanaishi katika standards nzuli za maisha. Angalia mitaa yenu mnayoishi then wacheki wepi wanaishi maisha mazuri na wepi masikini.
 

Uko sahihi.

Kiuchumi, majority ya waislamu wana hali mbaya zaidi
Bora Wakiristo angalau wingi wao katika ajira za serikali unawapa wao na ndugu zao unafuu mkubwa zaidi wa maisha, ikiwemo kukopesheka, bima za afya na pensheni
 
Tutajie hata Mkristo mmoja wa Zanzibar ambaye amewahi shika nyadhifa ya juu Serikalini.
 
Ina maana Wasukuma na Waislam tu ndiyo wana sifa ya kuwa Wenyeviti wa Tume ya haki za binadamu,hapa tumepigwa mnada.
 
Huenda kuna ufahamu mdogo wa hii sheria ya TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA. Makamishna ni watano, halafu kuna Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao lazima watoke pande tofauti za Muungano. Makamishna walioteuliwa ni watatu, hivyo wawili wanaendelea hadi muda wao ukamilike. Fuatilia hao wawili wanakotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…