Jinsi nilivyolazwa nje na wachawi mkoani Njombe

Nasubiria wachawi wa jf waje kusema uchawi ni scam.
 
Acheni kuwa na majibu mepesi kulingana na upeo wa mawazo yenu kwa kila tatizo....kama ubongo wako umechakata ukaona haiwezekani haimanishi kuwa haiwezekani na ndio mwisho....yapo mengi hatuyajui na bahati mbaya sayansi haiwezi kugundua yote....kumbuka kuwa sayansi sio uvumbuzi/kugundua kipya, bali ni kuyaweka wazi yaliyojificha, yaliyopo lakini hatukuyajua.
Mfano ...kugundua mchanganuo wa maji kuwa yana hydrogen na oxygen hakufanyi maji yawe kitu kipya...au copper kusafirisha umeme...umeme umekuwepo tangu ulimwengu unaanza kwa ufupi hakuna kipya ambacho sayansi imeleta zaidi ya maarifa mapya yaani taarifa mpya kwa mtumiaji wa kitu husika.
 
Sahihi mkuu
 
Waambie hao ndugu zako waache ulevi wa kupindukia watafirwa siku moja.
 
First lady wa awamu ya .....
Kijijini kwetu hukoo Lindi kaenda msibani na mabodigadi wake Nini na Nini mke wa presidaa bwana analala ndaniii,kitandani nyie nyie nyieeee....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wamwera nyokooo sanaaaa....asubuhi kajikuta njee Mabodigadi wako Mlangoni wanalinda empty room...
Ilikua balaaaa kiranga komoo!!!
 
Mbona umebwabwaja sana? Wewe sijakukataza kuamini unavyoamini mimi nimeeelezea ukweli. Nyie washirikina ni watu waoga sana. Na mnao fail sana
 
Isije kuwa ni vijiji vya Mahaha,Shishani,Kabila n.k vya Wilayani Magu, Mwanza. Mwaka fulani pale kijijini wananchi waliua fisi kadhaa waliokuwa wanafanya matuko kwa wananchi na mifugo, cha ajabu fisi hao walikuwa wamevaa hirizi.

Sasa kuna watu ukiwaambia mambo haya wanakataa. Wamezaliwa hapa hapa Africa na wanavijua vituko vya Afrika, ila wanajifanya wamezaliwa na kukulia Australia, Canada au sijui wapi mbele huko. Mimi nasema hivi: kama hawaamini kama hayo mambo yapo, waende hapo kijijini Mahaha, wilaya ya Magu, mkoa wa Mwanza kisha wawaambie wakazi wa hapo kuwa wao hawaamini uwepo wa uchawi na wawatake wawathibitishie, majibu watayapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…