Nilipata kazi ludewa nikawa naishi nyumba moja na mzee mmoja anaitwa mtweve wote tukiwa wageni, siku ya kwanza nilikabwa usiku nikahisi nililala vibaya au ni majinamizi ndotoni, ikawa ni hivyo kukabwa daily yaani unakabwa unapambana ndotoni ukishtuka unatweta vibaya niliogopa kumueleza mzee mtweve kwanza nilikua sijamzoea pili ni MTU wa dini sikutaka aniwekee doubt ktk mambo ya Giza, ilifika Siku yake alinyooshwa vilivyo,asubuhi anagonga mlango wangu ananiambia usiku nimekabwa mda mrefu nimekuita sana uje unisaidie ina maana hukunisikia? Nikamwambia sikusikia ndipo namm nikamsimulia ninavyokabwa haipiti Sikh mbili, tulimuelezea boss wetu yy badala ya kuwaona wazee akaenda kulizungumzia kanisani jumapili baada ya kuomba kutoa neno, kilichofuatia usiku ule anasema alikabwa hadi asubuhi na anasema alishangaa kujikuta katolewa chumbani hadi sebuleni ndipo alipoamini uchawi upo, pia njombe uchawi wa mapembe kuruka kama ungo ni mwingi sana, wanawake wa njombe ni wafupiii mm mrefu walikua wananikataa wanasema nitasogeza kizazi but all in all wabena, wapangwa ni wakaribu sana nilikua naletewa debe za viazi mviringo, mikungu ya ndizi, mayai yamejaa sadolin , kuku elf tatu tu, dah nilifutuka vibaya, mashavu yaliumuka hayoo, nyama ya ktimoto mbuzi aisee, ukikuta wazee wanakunywa ugimbi au ulanzi ni lazima uende upige pafu unachotea kopo la Lita mbili umalize usipokunywa unaonekana unaleta nyodo kisa unatokea town lazima ukabwe usiku, Kuna siku walinipa mkangafu umekaa wiki mchachu balaa nikajifanya ngoje niwaridhishe wazee niliubugia nikamaliza nikaongeza saa kurudi home nilipotea nikatokezea kijiji kingine ndo nakutana na watu wanaotoka town ndo kunirudisha, njombe beer yao ni Kilimanjaro na safari,nilipofika bar naagiza beer ikachukuliwa tu kwenye shelf nafunguliwa nikamwambia mhudumu sinywi beer ya moto naomba ya baridi akaniuliza we ni mgeni? Nikamuuliza ugeni wangu unahusiana vp na beer ninayohitaji? akaniambia iguse hii beer dah beer ya bariiiid akacheka anasema huku njombe hakuna haja ya fridge, nilifika stand nilikua nimevaa shati yaani ilibidi nikatafute koti,sweta,jacket,na mzula manake baridi inapuliza hadi mfupa unauma, hyo ilikua mwezi wa tano hivi inaenda wa sita nimeita boda nikamwambia nipeleke lodge isiyonakelele wala Fuji au bar, nikapelekwa lodge moja hivi inaitwa kuokoka ni lazima kuchek mlangoni Kuna bango kubwa hauruhusiwi kuingia na mwanamke asiye kua mkewako, hauruhusiwi kuingia na kilevi chochote, mwisho wa kuingia ni SAA tano ukitoka marufuku kumgongea muhudumu dah nilichoka sana but maambukizi Kule yako juu mno, pia pesa kwenye kilimo na miti, mbao ni nyingi sana Kuna wakulima matajiri sana ukienda ngaranga,Amani mavanga, n.k klia mkulima ana canter,Noah,tractor, Kyle Noah ni za kupelekea mbolea shambani, ninapamiss sana njombe kwa kweli.