Jinsi nilivyolazwa nje na wachawi mkoani Njombe

Jinsi nilivyolazwa nje na wachawi mkoani Njombe

Isije kuwa ni vijiji vya Mahaha,Shishani,Kabila n.k vya Wilayani Magu, Mwanza. Mwaka fulani pale kijijini wananchi waliua fisi kadhaa waliokuwa wanafanya matuko kwa wananchi na mifugo, cha ajabu fisi hao walikuwa wamevaa hirizi.

Sasa kuna watu ukiwaambia mambo haya wanakataa. Wamezaliwa hapa hapa Africa na wanavijua vituko vya Afrika, ila wanajifanya wamezaliwa na kukulia Australia, Canada au sijui wapi mbele huko. Mimi nasema hivi: kama hawaamini kama hayo mambo yapo, waende hapo kijijini Mahaha, wilaya ya Magu, mkoa wa Mwanza kisha wawaambie wakazi wa hapo kuwa wao hawaamini uwepo wa uchawi na wawatake wawathibitishie, majibu watayapata.
Wanaokataaa ndo wachawi wakubwa hao
 
Kuna rafiki yangu nilisoma nae on level alikuwa anafanya Kazi huko akafungua duka la madawa kubwa... Alikutana na mambo kama YAKO aiseh... Yeye akakaza... Kuna mzee mmoja Fundi baiskeli niwenyeji huko... Akamwambia kinajana utarudu kwenu ukiwa umevaa suruali shati na viatu.. hivyo nakuibia siri hiyo, kusanya vitu vyako tembea mapema... Mzee hakupenda kijana mchapakazi ateseke akamwambia ukweli Ili akimbie hatari... Jamaa akakaza shingo bwana.. baada ya miezi kadhaa jamaa alirudi kwao KWa masada wa magari ya mizigo tena alipitia mtwara hadi dar,, dar tena akaomba msaada hadi mkoani kwao akiwa hana hata kitu zaidi ya nguo alizo vaa na viatu...

Cha kusikitisha zaidi siku zilivyo kuwa zina zidi kwenda jamaa akawa kama vile anaishi katika mateso sana... Haikupita mwezi toka afike kwao.. daaah!! Jamaa akajinyonga aiseh!! Daah!! Ili niumiza sana...

Wachina wanafanya uchawi KWa ajili ya maendeleo bongo kurudishana na nyuma... Daah!
Subhanaa lllahhh
 
Shalom wapendwa,

Leo nimekumbuka kisa hiki, kilichonitokea mwenyewe nikiwa katika harakati Mkoa wa Njombe. Narudia tena hii sio stori ya kufikirika imenitokea mwenyewe.

Uchawi hauna faida yoyote ni ujinga uliokomaa, ni utumwa. Walio wachawi wanamani kutoka ila there is no way out there. Ninamiliki maduka ya dawa za binadamu yaliyopo maeneo ya vijijini huko, kazi yangu hua ni kuzunguka na kutafuta watu wa kuuza tu na kufunga mahesabu mwisho wa mwezi.

Siku Moja kuna dada wa ADDO aliyekuwa akiuza moja kati ya maduka alipata dharura na kwakua nilikuwa na nafasi nilimruhusu aende nami nikaenda kumpokea kuuza dawa Ili clients wasikose huduma mpaka atakaporejea. Sasa hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Hiyo siku nimeamka vizuri kabisa nikashinda vema jioni imefika nikafunga hesabu na kulikua na pesa kwenye draw nilizibeba na kwenda nazo nyumbani kwa sababu za kiusalama, nikaacha kiasi kadhaa pia kwenye draw. Baada ya kufikia nyumbani nikaweka pesa vizuri nikawasha data niperuzi kidogo Kisha nikalala.

Naamka asubuhi nimelala nje😂😂😂 kwenye shimo Moja lilikua jirani na nyumba. Kitu kilichonishangaza nililala na boksa nikaamka nje nikiwa na nguo zangu nilizovaa jana😨

Kitendo cha kutaka kurudi ndani nakuta mlango umefungwa kwa ndani, nikawa najiuliza nilitokea wapi? Nikajaribu kupush mlango ukafunguka kuingia ndani nakuta panya sita kitandani wametulia wananiangalia tu😂😂😂 nikarusha kiatu wakapanda darini na kupotea ghafla kukawa kimya.

Impact za tukio lile, pesa nilizorudi nazo jana hakukua na hata kumi iliyokuepo😬 (zilipotea)

Sikuweza kukaa tena kule, nikafunga duka mpaka yule dada aliporudi kusongesa gurudumu. Kwa Sasa nikienda huwa silali kabisa hata iwe late kiasi gani nitarudi mjini.

Kama hujapita Njombe hujaona uchawi bado.
Haya mambo kama hayajakukuta unaweza hisi kama ni Riwaya.

Pole sana Mkuu.
 
nikajifanya ngoje niwaridhishe wazee niliubugia nikamaliza nikaongeza saa kurudi home nilipotea nikatokezea kijiji kingine ndo nakutana na watu wanaotoka town ndo kunirudisha, njombe beer yao ni Kilimanjaro na safari,nilipofika bar naagiza beer ikachukuliwa tu kwenye shelf
😂😂😂💔
 
2020
Mkoa wa ruvuma
Wiliya ya Nyasa
Kijiji Cha ng'ombo
Ukoo x
Mama mmoja aliokotwa kilindini kwenye ziwa Nyasa,alikua anaelea juu ya gogo inasemekana halikuwa gogo bali ni mamba,na yeye alichukuliwa usiku amelala,asubuhi wanagongewa mlango kuwa ndugu yenu tumemuokoa majini,haya mambo ya kulazwa nje na wachawi yapo sana tena sana.
 
2020
Mkoa wa ruvuma
Wiliya ya Nyasa
Kijiji Cha ng'ombo
Ukoo x
Mama mmoja aliokotwa kilindini kwenye ziwa Nyasa,alikua anaelea juu ya gogo inasemekana halikuwa gogo bali ni mamba,na yeye alichukuliwa usiku amelala,asubuhi wanagongewa mlango kuwa ndugu yenu tumemuokoa majini,haya mambo ya kulazwa nje na wachawi yapo sana tena sana.
Huko Nyasa ndo balaa
 
Uchawi upo Kila sehemu ila Kuna kuzudiana,kule hata radi unatumiwa mwezi hata wa 8 ,na mpo kundi LA watu ila ikakupiga wewe tu.
 
Back
Top Bottom