Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maneno ya akili sana hayo. Alisema baba wa taifa hayati nyerereKwa hiyo nikisema mimi ndo nilimpa Mimba mama yako ukazaliwa wewe utakubali? Kuwa wewe ni sehemu ya my sperms?
Mambo ya ujana miaka hiyo...Aiseee sawa kwahio ukabutua mama yake halafu shwaaah!
😂😂😂😂😂OK. Umemaliza? Una kisa kingine? Leta vitu jombii.
uhalisia ni kuwa hukuwa umeingia ndani. Ulilewa sana. Ukawa hujielewi ukawaza umeenda ndani hukwenda ndani. Na pesa ulizochukua Dukani kwako ukaendea Bar. Ukapiga sana maji. Ukarudi na Mang'amung'amu. Ukalala nje. Asubuhi kuamka ukaendelea kufikiria ulilazwa nje na wachawi. Kumbe mchawi wewe mwenyewe tu. Pombe siyo chai.
Kudadek jf kuna wajuaji 😂😂😂 nimecheka sana comment za watu hapaNimeshangaa uĺiwarushia panya viatu wavivae au??
Haukukuta ute ute kwenye makalioMe nililala na nguo Hasubuhi najikuta nipo na boxer ila shati lilibaki suruali ndiyo nilivuliwa ingawa hawakunitoa nje au pengine walinitoa na kunirudisha sijui.daah yule mama Muha wa Kigoma sitamsahau kwa uchawi wake alitutessa sana wapangaji wenzake
Peleka Facebook.Shalom wapendwa,
Leo nimekumbuka kisa hiki, kilichonitokea mwenyewe nikiwa katika harakati Mkoa wa Njombe. Narudia tena hii sio stori ya kufikirika imenitokea mwenyewe.
Uchawi hauna faida yoyote ni ujinga uliokomaa, ni utumwa. Walio wachawi wanamani kutoka ila there is no way out there. Ninamiliki maduka ya dawa za binadamu yaliyopo maeneo ya vijijini huko, kazi yangu hua ni kuzunguka na kutafuta watu wa kuuza tu na kufunga mahesabu mwisho wa mwezi.
Siku Moja kuna dada wa ADDO aliyekuwa akiuza moja kati ya maduka alipata dharura na kwakua nilikuwa na nafasi nilimruhusu aende nami nikaenda kumpokea kuuza dawa Ili clients wasikose huduma mpaka atakaporejea. Sasa hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
Hiyo siku nimeamka vizuri kabisa nikashinda vema jioni imefika nikafunga hesabu na kulikua na pesa kwenye draw nilizibeba na kwenda nazo nyumbani kwa sababu za kiusalama, nikaacha kiasi kadhaa pia kwenye draw. Baada ya kufikia nyumbani nikaweka pesa vizuri nikawasha data niperuzi kidogo Kisha nikalala.
Naamka asubuhi nimelala nje😂😂😂 kwenye shimo Moja lilikua jirani na nyumba. Kitu kilichonishangaza nililala na boksa nikaamka nje nikiwa na nguo zangu nilizovaa jana😨
Kitendo cha kutaka kurudi ndani nakuta mlango umefungwa kwa ndani, nikawa najiuliza nilitokea wapi? Nikajaribu kupush mlango ukafunguka kuingia ndani nakuta panya sita kitandani wametulia wananiangalia tu😂😂😂 nikarusha kiatu wakapanda darini na kupotea ghafla kukawa kimya.
Impact za tukio lile, pesa nilizorudi nazo jana hakukua na hata kumi iliyokuepo😬 (zilipotea)
Sikuweza kukaa tena kule, nikafunga duka mpaka yule dada aliporudi kusongesa gurudumu. Kwa Sasa nikienda huwa silali kabisa hata iwe late kiasi gani nitarudi mjini.
Kama hujapita Njombe hujaona uchawi bado.
Nitakuloga wewe... Sema su nifanye yanguMoto wa bibyako😬
wachawi walijua hilo ndio maana wakamlaza na sweater karibu na shimo nyumbani kwakeKwa baridi la Njombe ukalala nje?
Ulikua kwenye hatari ya kufa kwa hypothermia au kupatwa na shida ya frostbitten but you suffered neither.
Nieleweshe kwanini hukukutwa na chochote kati ya hivyo.
VIPi ulimnyima niniMe nililala na nguo Hasubuhi najikuta nipo na boxer ila shati lilibaki suruali ndiyo nilivuliwa ingawa hawakunitoa nje au pengine walinitoa na kunirudisha sijui.daah yule mama Muha wa Kigoma sitamsahau kwa uchawi wake alitutessa sana wapangaji wenzake
Pale ilikua ni mkesha tunachoma moto kula kande ndizi na matakaPela na chai.Ilitakiwa ujimwage hapo hapo msibani ulale