Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

Umenikumbusha kampuni ya Yahoo walijua kabisa watu hua hawasomi terms and Rules za mitandaoni hua wanakimbilia kubonyeza I agree bila kusoma chochote sasa kuna kipindi katika yale maelezo marefu ya terms and rules waliweka namba na maelezo kwamba mtu aliyesoma hadi mwisho apige hizo namba atapata kiasi fulai cha pesa.... Imagine ni mtu mmoja tu alipata hiyo pesa.

Bantu Lady natumaini hata wewe hujasoma hadi mwishoni 😅
Nimesoma huko juu. Weee hayo mapicha nitasomaje kwa amani, leo nitashtuka mara nyingi sana.
 
Story nzuri ila hilo andiko la Mwanzo umetudanganya ufafanuzi wako
Sir, ndio maana nimesema inawezekana kuna sehemu nitaua sipo sahihi.
Je wewe binafsi unatfsiri vipi andiko hili??
Mwanzo 3:15
[15]nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

[And I will put enmity between thee and the woman, and between thy seed and her seed; it shall bruise thy head, and thou shalt bruise his heel.]
 
One of the satanic rule says you shouldn't kill any animal without a reason, you should kill it either for defence or for food.. najiulizaga kwa nini imekuwa satanic rule? Wakati kimtazamo inaonekana kama jambo la busara?
Ushajiuliza kwanini msalaba japo umegeuzwa kidogo nao ni moja ya masonic symbol
 
Hapa ndipo huwa siwaelewi freemasons, sometime huwa nafikiria hata ustaarabu si hulka ya mwanadamu aliyekamilika huenda ni namna tu freemasons wanataka wawe na namna ya kututhibiti kupitia ustaarabu tuliopandikizwa kama namna sahihi ya kutreat mambo
 
Mkuu hongera huu uzi umenipa elimu na mm kuanzia leo siui nyoka... nikimuona tu namuacha aende zake...
 
Muwe mnaandika kwa ufupi jamani. Sisi wengine tumeshasoma maandiko marefu hivi kwa miaka kadhaa sasa tumechoka Sasa. Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa msomaji mzuti sana wa vitabu na makala. Nilishasoma vitabu ziadi ya 100. Sasa hivi hobby ya kusoma imepungua sijui tatizo nini.
 
Kwasababu zangu binafsi ambazo sitapenda niziseme (but very reasonable) hua siui kiumbe yoyote aliye hai tofauti na mbu. Kiukweli siwapendi na nawaogopa sana nyoka ila hata wao imekua ikiniwea vigumu kuwaua hivyo pindi napokutana nao hua naishia kuwafukuza au kuwapotezea kama wameenda eneo ambalo mimi sifiki au watu wengine. Sehemu Fulani nilipokua nakaa kulikua na kisima kisicho na maji humo ndani kuna nyoka alikua akishi humo hadi akawa na watoto kwakweli iliniwea vigumu kumuua japo wananchi weye hasira kali walikuja wakateketeza ile familia, Fast-forwarding

Siku moja natembea barabarani usiku nikakutana na nyoka mdogo yupo katikati ya barabara kashindwa kuvuka ajili ya mwanga wa maloli yaliyokua yanapita, mimi nikaenda kwa nia njema kabisa nimsaidie avuke upande wa pili cha ajabu nilipomfikia akainua kichwa juu anaigonge/ng’ate, nikawa namkwepa. Kila nikimfukuza aende upande wa pili anakua ananijia aning’ate kwakweli nikashindwa kumsaidia ikabidi nimuache roli likamgonga. Iliniuma kiasi maana nilikua nina nafasi ya kumsaidia ila nilishindwa.

Unadhani kwanini japo nia yangu ilikua ni njema kumsaidia maisha yake lakini aliniona adui na kutaka kunigonga?
Kwa mujibu wa biblia baada ya wanadamu wa kwanza kufanya maasi Mungu alitoa laana kati ya nyoka na mwanadamu kwa kusema “name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” kwa mantiki hiyo watu wengi huchukulia kwamba hiyo laana aliyotoa Mungu kati ya binaadamu na nyoka ndio inafanya mwanadamu na nyoka waviziane kumuua mwingine lakini mimi nasema hiyo sio kweli laana hiyo aliotoa Mungu sio sababu bali ilitumika kama fumbo. Maana kubwa aliyomaanisha mungu ni kwamba ujuzi wa mema na mabaya walioupata wanadamu kwa kula tunda/kuasi ndio unaofanya mwanadamu na nyoka wawindane….nitajaribu kulielezea hili kisayansi zaid ili nieleweke vizuri.

Catecholamine The Adrenaline

Endocrine Glands
ni mfumo wa tezi ambao wenyewe hutoa hutoa homoni moja kwa moja kwenda kwenye mfumo/mzunguko wa damu wa damu. Adrenal Gland ni tezi iliyopo katika mfumo watezi ambayo inapatikana juu ya mafigo kazi kuu ya tezi hii ni kuweka sawa kiwango cha chumvi na kurekebisha kiwango cha musukumo wa damu. tezi hii hutengeneza homoni mbali mbalimbali kama vile cortisol,epinephrine,catecholamine nk pia hutengeneza homoni ya adrenaline, adrenaline hutengenezwa pia katika medulla oblongata kwa kiwango kidogo

Pindi unapokua na hasira au unapoona kitu cha hatari kama vile nyoka tezi hii ya Adrenal hutoa homoni ya epinephrine, husababisha kutengenezwa kwa homoni ya cortisol, ambayo huongeza shinikizo la damu, sukari ya damu, na kukandamiza mfumo wa kinga.Mwitikio wa awali na miitikio inayofuata huchochewa katika jitihada za kuunda nyongeza ya nishati. Ongezeko hili la nishati huamlishwa na epinephrine kujifunga kwa seli za ini na uzalishaji unaofuata wa glucose.

NB: Adrenaline hufahamika pia kama Epinephrine

mzunguko wa cortisol hufanya kazi kugeuza asidi ya mafuta kuwa nishati inayopatikana, ambayo hutayarisha misuli ya mwili mzima kwa majibu/reaction. Homoni za catecholamine, kama vile adrenaline (epinephrine) au noradrenalini (norepinephrine), husaidia reaction ya haraka ya mwili ambayo huhusiana na maandalizi ya misuli kuchukua hatua kali…..Misuli inapofikia hatua hiyo unapofikia katika hatua hiyo moyo na mapafu huongezeka kasi yaani mapigo ya moyo yataenda haraka na mtu mtu atakua anapumua haraka, huziwia tezi ya Lacrimal ambayo hufanya kazi ya kuzalisha machozi na mate ndio maana ukiwa umeona kitu cha hatari mate na koo hukauka…pia kutetemeka mwili. Baada ya haya yote kutokea mwili ndio mwanadamu ataamua akimbie hatari(flight) au apambane na hatari(fight.
View attachment 2446763

Vomeronasal organ (VNO) ni sehemu/mlango/sense organi ya ziada iliyopo juu ndani yam domo kwa juu ambayo hutumika katika kunusa mara nyingi organ hii hupatikana zaidi katika nyoka na mijusi. VNO wa jina lingine inaitwa Jacobson Gland. Katika nyoka Tezi hii ya VNO ina uwezo mkubwa sana wa kunusa Scent za vitu….Kama nilivyoelezea huko juu kwamba mwanada mu ukiona kitu cha kutisha Adreanal Gland ina activate reaction ya Fight or Flight kumbuka kwamba mwili ukishakua kwenye reaction hiyo hormone mbalimbali zinazoachiliwa (Adrenaline) zinasambaa katika damu yako hivyo basi nyoka kwa kutumia tezi ya VNO/Jacobson gland huweza kuunusa mwili wako na kugundua kwamba mtu huyu ni adaui kwangu nae atajihmi maana atakusikia harafu yako ni tofauti ajili ya hormones hizo.
View attachment 2446749
Mwanzo kwenye mada nimeeleza nilivyotaka kung’atwa na nyoka nikiwa nataka kumsaidia sababu ni kwamba alisikia scent ya mwili wangu iliyotokana na homoni mbalimbali zilizoachiliwa katika kutekeleza reaction ya fight or flight….Kawaida ya nyoka kama yupo ndani usipomuona wala kumkanyaga hawezi kukudhuru kabisa lakini pindi utakapomuona tu basi naye atajitahidi ajihami kwani kama hujamuona mwali wako unakua upo sawa kabisa lakini pindi utakapomuona tu mwili wako utabadirika kwani utakua unajua ile ni hatari.

Kwa mantiki hiyo uadui uliopo kati ya nyoka na mwanadamu unatokana na ujuzi wetu wa kujua baya na jema kwani kujua nyoka huyu ni adui sio mwema ndio huactivate Adrenal gland kama tungekua hatujui jema na baya basi kamwe tusingekua na uadui na nyoka ndio maana mtoto mdogo chini ya miaka miwili anaweza kucheza na nyoka mkali na asing’atwe kamwe lakini kama mama yake atatokea na kumuona mtoto akicheza na nyoka basi anaweza sababisha kweli nyoka akamng’ata mtoto maana mama anajua jema na baya so akimuona nyoka na mtoto ni lazima apige kelelemna wakati huo adrenaline itakua tayari ishasambaa mwilini nyoka ataisikia scent na kujua huyu ni adui kelele za mama zitamtia uoga mtoto kisha aanze kulia maana mtoto atahisi labda kuna hatari ndio maana mama yake anapiga kelele. Ile kuhisi hatari kwa mtoto nako ni adrenal nayo inakua inaanza kufanya kazi so hapo inakua ni utashi wa nyoka mwenyewe atakachoamua.
View attachment 2446767
Hivyo Yule nyoka japo mimi nilikua nina nia njema ya kumsaidia lakini nilimfuata mwili wangu ukiwa katika hali ya fight or flight kwani najua Yule ni mbaya kwangu hivyo nyoka hakuangalia dhamira yangu bali alifuata sense yake ya Jacobson gland.
….
Hii ni theory yang tu kutokana na uelewa wangu wasayansi inawezekana sipo sahihi hivyo basi ruhusa kwenu kunikosoa na kusahihisha pale nilipokosea

-Criston Cole
Samahani Mkuu wewe kweli unayo akili? Unataka kumsaidia aduwi yako?
 
harakati za siri I took the liberty of narrating it for you....No scary snake pics

Kwasababu zangu binafsi ambazo sitapenda niziseme (but very reasonable) hua siui kiumbe yoyote aliye hai tofauti na mbu. Kiukweli siwapendi na nawaogopa sana nyoka ila hata wao imekua ikiniwea vigumu kuwaua hivyo pindi napokutana nao hua naishia kuwafukuza au kuwapotezea kama wameenda eneo ambalo mimi sifiki au watu wengine. Sehemu Fulani nilipokua nakaa kulikua na kisima kisicho na maji humo ndani kuna nyoka alikua akishi humo hadi akawa na watoto kwakweli iliniwea vigumu kumuua japo wananchi weye hasira kali walikuja wakateketeza ile familia, Fast-forwarding

Siku moja natembea barabarani usiku nikakutana na nyoka mdogo yupo katikati ya barabara kashindwa kuvuka ajili ya mwanga wa maloli yaliyokua yanapita, mimi nikaenda kwa nia njema kabisa nimsaidie avuke upande wa pili cha ajabu nilipomfikia akainua kichwa juu anaigonge/ng’ate, nikawa namkwepa. Kila nikimfukuza aende upande wa pili anakua ananijia aning’ate kwakweli nikashindwa kumsaidia ikabidi nimuache roli likamgonga. Iliniuma kiasi maana nilikua nina nafasi ya kumsaidia ila nilishindwa.
Unadhani kwanini japo nia yangu ilikua ni njema kumsaidia maisha yake lakini aliniona adui na kutaka kunigonga?

Kwa mujibu wa biblia baada ya wanadamu wa kwanza kufanya maasi Mungu alitoa laana kati ya nyoka na mwanadamu kwa kusema “name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” kwa mantiki hiyo watu wengi huchukulia kwamba hiyo laana aliyotoa Mungu kati ya binaadamu na nyoka ndio inafanya mwanadamu na nyoka waviziane kumuua mwingine lakini mimi nasema hiyo sio kweli laana hiyo aliotoa Mungu sio sababu bali ilitumika kama fumbo. Maana kubwa aliyomaanisha mungu ni kwamba ujuzi wa mema na mabaya walioupata wanadamu kwa kula tunda/kuasi ndio unaofanya mwanadamu na nyoka wawindane….nitajaribu kulielezea hili kisayansi zaid ili nieleweke vizuri.

Catecholamine The Adrenaline

Endocrine Glands ni mfumo wa tezi ambao wenyewe hutoa hutoa homoni moja kwa moja kwenda kwenye mfumo/mzunguko wa damu wa damu.

Adrenal Gland ni tezi iliyopo katika mfumo watezi ambayo inapatikana juu ya mafigo kazi kuu ya tezi hii ni kuweka sawa kiwango cha chumvi na kurekebisha kiwango cha musukumo wa damu. tezi hii hutengeneza homoni mbali mbalimbali kama viel cortisol,epinephrine,catecholamine nk pia hutengeneza homoni ya adrenaline, adrenaline hutengenezwa pia katika medulla oblongata kwa kiwango kidogo….Pindi unapokua na hasira au unapoona kitu cha hatari kama vile nyoka tezi hii ya Adrenal hutoa homoni ya epinephrine, husababisha kutengenezwa kwa homoni ya cortisol, ambayo huongeza shinikizo la damu, sukari ya damu, na kukandamiza mfumo wa kinga.Mwitikio wa awali na miitikio inayofuata huchochewa katika jitihada za kuunda nyongeza ya nishati. Ongezeko hili la nishati huamlishwa na epinephrine kujifunga kwa seli za ini na uzalishaji unaofuata wa glucose.

mzunguko wa cortisol hufanya kazi kugeuza asidi ya mafuta kuwa nishati inayopatikana, ambayo hutayarisha misuli ya mwili mzima kwa majibu/reaction. Homoni za catecholamine, kama vile adrenaline (epinephrine) au noradrenalini (norepinephrine), husaidia reaction ya haraka ya mwili ambayo huhusiana na maandalizi ya misuli kuchukua hatua kali…..Misuli inapofikia hatua hiyo unapofikia katika hatua hiyo moyo na mapafu huongezeka kasi yaani mapigo ya moyo yataenda haraka na mtu mtu atakua anapumua haraka, huziwia tezi ya Lacrimal ambayo hufanya kazi ya kuzalisha machozi na mate ndio maana ukiwa umeona kitu cha hatari mate na koo hukauka…pia kutetemeka mwili. Baada ya haya yote kutokea mwili ndio mwanadamu ataamua akimbie hatari(flight) au apambane na hatari(fight.

Vomeronasal organ (VNO) ni sehemu/mlango/sense organi ya ziada iliyopo juu ndani yam domo kwa juu ambayo hutumika katika kunusa mara nyingi organ hii hupatikana zaidi katika nyoka na mijusi. VNO wa jina lingine inaitwa Jacobson Gland. Katika nyoka Tezi hii ya VNO ina uwezo mkubwa sana wa kunusa Scent za vitu….Kama nilivyoelezea huko juu kwamba mwanada mu ukiona kitu cha kutisha Adreanal Gland ina activate reaction ya Fight or Flight kumbuka kwamba mwili ukishakua kwenye reaction hiyo hormone mbalimbali zinazoachiliwa (Adrenaline) zinasambaa katika damu yako hivyo basi nyoka kwa kutumia tezi ya VNO/Jacobson gland huweza kuunusa mwili wako na kugundua kwamba mtu huyu ni adaui kwangu nae atajihmi maana atakusikia harafu yako ni tofauti ajili ya hormones hizo.

Mwanzo kwenye mada nimeeleza nilivyotaka kung’atwa na nyoka nikiwa nataka kumsaidia sababu ni kwamba alisikia scent ya mwili wangu iliyotokana na homoni mbalimbali zilizoachiliwa katika kutekeleza reaction ya fight or flight….Kawaida ya nyoka kama yupo ndani usipomuona wala kumkanyaga hawezi kukudhuru kabisa lakini pindi utakapomuona tu basi naye atajitahidi ajihami kwani kama hujamuona mwali wako unakua upo sawa kabisa lakini pindi utakapomuona tu mwili wako utabadirika kwani utakua unajua ile ni hatari.

Kwa mantiki hiyo uadui uliopo kati ya nyoka na mwanadamu unatokana na ujuzi wetu wa kujua baya na jema kwani kujua nyoka huyu ni adui sio mwema ndio huactivate Adrenal gland kama tungekua hatujui jema na baya basi kamwe tusingekua na uadui na nyoka ndio maana mtoto mdogo chini ya miaka miwili anaweza kucheza na nyoka mkali na asing’atwe kamwe lakini kama mama yake atatokea na kumuona mtoto akicheza na nyoka basi anaweza sababisha kweli nyoka akamng’ata mtoto maana mama anajua jema na baya so akimuona nyoka na mtoto ni lazima apige kelelemna wakati huo adrenaline itakua tayari ishasambaa mwilini nyoka ataisikia scent na kujua huyu ni adui kelele za mama zitamtia uoga mtoto kisha aanze kulia maana mtoto atahisi labda kuna hatari ndio maana mama yake anapiga kelele. Ile kuhisi hatari kwa mtoto nako ni adrenal nayo inakua inaanza kufanya kazi so hapo inakua ni utashi wa nyoka mwenyewe atakachoamua.

Hivyo Yule nyoka japo mimi nilikua nina nia njema ya kumsaidia lakini nilimfuata mwili wangu ukiwa katika hali ya fight or flight kwani najua Yule ni mbaya kwangu hivyo nyoka hakuangalia dhamira yangu bali alifuata sense yake ya Jacobson gland.
….
Hii ni theory yang tu kutokana na uelewa wangu wasayansi inawezekana sipo sahihi hivyo basi ruhusa kwenu kunikosoa na kusahihisha pale nilipokosea.
-Criston Cole
 
Mkuu kwanini unasema Hivyo???😩
Mungu hakuwa mjinga au Mungu hajakosea kuumba viumbe wengine tuwauwe kwa sababu zake ameumba hao Viumbe Mungu tuwauwe kwani wana madhara makubw akw abinadamu kwa mfano unatakiwa uwauwe nzi,mende,panya,nyoka,ng'e,tandu, Viroboto,simba,mamba,chui na kadhalika hao wote waan madhara kwa binadamu iweje wewe ukajifanya mtu mwema kutaka kumuokoa nyoka yupo barabarani anakwenda zake ? hata kama amesimam katika kati ya njia wewe ungelimuacha agongwe na gari kuliko kujifanya mtu mwema kutaka kumuokoa na khuyo nyoka na kifo cha ajali ya gari. Je angekung'ata kwa bahati mbaya na hakuna mtu wakukusaidia si ungelikuwa wewe leo tunakuita jina la Marehemu aka RIP? Hata kam una roho ya imani kuna vimbe wa kuwaonea imani si hao viumbe nilikutajia hapo juu kwani aho ni viumbe ni aduwi mkubwa wa binadamu Mungu ametuumbia hao viumbe tuwe ni maaduwi zetu kwa sababu zake mwenyewe anazijuwa Mungu. Acha hiyo tabia ya kujifanya mwema kuwaonea viumbe maaduwi zakko utakuja kupatwa na matatizo makubwa shauri yako.
 
Back
Top Bottom